Sunday 13 January 2013

Re: [wanabidii] Mwanamama mwingine abakwa India na mijitu saba


Sasa wanazificha nyuso zao kwa nini wahaini hawa. Pengine wakizionyesha, wengine watawatambua kuwa nao walifanyiwa vitendo hivyo nao kama ilivyo kwa ubakaji ulaya na USA wengi kujitokeza kusema nami ni victim wa huyo mzee/kijana/kiongozi. Imani za dini sasa nazo zinakwenda digitali. Siajabu hao wabakaji ni waswalihina sana, kuingia Jamatini kusali kila buda ufikapo. Huenda eti wanamuadhibu kwa vile hatii dini na mila kwa kuwa yupo pekee bila escort hivyo ni prostitute anatakiwa aadhibiwe hivyo. Dhana potofu hizi zinakuwa jinsi uchumi na maendeleo yakuavyo. haishangazi vitendo vya kubaka mwananke akiwa pekee na na mchumba wake kama kwa yule mwingine. Maana India ni mojawapo ya Asian countries zinaongoza kwa brothels na uuzaji wa vitoto me na ke kwa pedophiles. Jirani anakuibia mtoto anamuuza kwa brothels, wanafungiwa, kubakwa na mmiliki kujipatia kipato. Msichana akikukataa usimuoe au kukukataa tu unamwagia tindikali usoni. Wanawake wameharibiwa nyuso kwa tabia hii ya ubaguzi na uonevu ufanywao na wanaume ktk a male dominated and discriminatory society against women. Pamoja na uonevu mwingine wa kutonyonyesha mtoto wa kike mpaka afe maana alitakiwa azaliwe 'Me' hako kakaja au kukatoa tumboni baada ya kujua kuwa a 'she' child atazaliwa  ambaye atashusha hadhi ya familia.

Mwenzio akinyolewa nawe tia maji. Masuala ya ubakaji yanaongezeka pia TZ. Yapo na baadhia ya NGo zimesaidia kutibu STDs kwa watoto wadogo sana wanafunzi shuleni ambao hufanyiwa vitendo vya ubakaji majumbani au njiani wakienda na kurudi shule na matatizo mengine mengi ktk jamii. Wanafunzi kutembea mwendo mrefu kwenda na kurudi shule (3km+), akina mama kwenda shamba pekee au kutafuta kuni na maji TZ nazo zina matokeo ya namna hii ya ubakaji. Tatizo ni watu kujitokeza kwa kuogopa stigma. Lakini yapo sana na ukitumia njia mbadala za siri kwa wanafunzi na akina mama utayapata na wabakaji ni vibabu/watu wazima. Wasichana wa kazi majumbani kuonewa kubakwa na wababa na akiondoka vijana wake kufuatia-ambapo imeleta ukimwi na vifo ktk familia ya baba, mama, vijana wake wote-yamo pia bongo-mtandao wa ndani ya nyumba.

Mengi yanafichwa na familia na viongozi wa chini na ukiyafuatilia hawapendi unaonekana mmonko. Matokeo ni magonjwa ya zinaa kwa watoto hata wadogo na ukimwi pia. Wazazi hawana HIV lakini katoto kadogo kanacho. Kakichunguzwa kameharibiwa. Vitoto vya kike na vya kiume vinaharibiwa kwa uonevu wa kubakwa.

Kuwaingilia akina mama wazee waishio pekee ktk nyumba usiku. Vimlango vobovu, vijumba vya nyasi vya kuta mbovu. Hawa hushambuliwa na vijana hooligans wavuta bangi vijijini. Twaogopa kusema aibu na uzeeni STDs hazitambuliwi. Akienda hospitali na akiulizwa-hakieleweki. Tujiandae maana huku kwetu si ubakaji tu lakini ni pamoja na kumkata mtu viungo. Mabasi kuchelewa kufika maendeo kutokana na foleni akabaki mwanafunzi 'ke' au mwana mama pekee ndani ya bus na akashushwa porini usiku. Bus likiharibika na konda na dreva kutokuwajibika kurudisha nauli bali kulaza watu porini. Wengine kujifanya kuwasaidia wasichana au watoto waliosafiri pekee wapokelewe na wazazi wakifika kumbe wanamatatizo na kubakwa na wanaojifanya kuwasaidia rooms au nyumbani kwao hadi kesho basi likipona. Mimba za wanafunzi zilikuwa zikitokea namna hii kwa mabasi ya TTC yaliyokuwa yakienda Mtwara kupitia Songea-Lukumburu Mountains tope na utelezi. Shule  ya Mtwara Girls in 1969-1970s ikaamua form 1 wote kwenda na kurudi kwa ndege za EA airways Dar-Mtwara na kupata lift za ndege za JWTZ mpaka wanapokuwa form 2 kutokana na kubakwa na kupata mimba kutokana na utata wa usafiri na kukwama njiani. Elimu endelevu kuonya hasa wasichana na wamama tahadhari za aina yote; sheria ya SOSPA kutekelezwa kwa haraka na kwa haki; mbakaji aliyeua-auawe; aliyekamatwa ni viungo vya binadamu naye aliua auawe sio aachwe analishwa tena na walipakodi, anahonga anatoka-anaendelea na uonevu haitotendea haki ndugu wa marehemu aliyebakwa akafa au kukatwa viungo na kuuawa.

Kwa Wahindi, mwanamke akipata mimba tu nje ya ndoa anapigwa mawe anauawa au ananyongwa kisiri for family honour. Nao hao wahindi waliobaka wauawe.

 



--- On Sun, 13/1/13, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Subject: [wanabidii] Mwanamama mwingine abakwa India na mijitu saba
To: "Wanabidii googlegroups" <wanabidii@googlegroups.com>, "Mabadiliko" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Sunday, 13 January, 2013, 21:43

Reports: 6 held over new India bus gang-rape

Strdel / AFP - Getty Images

Indian police personnel present six arrested men, accused of a gang rape in Punjab state, Sunday.
By Alastair Jamieson, NBC News
Six suspects have been arrested over the rape of a woman on a bus in northern India, just weeks after the gang-rape and murder of a student sparked nationwide protests, reports said early Sunday.
Police say a 29-year-old woman was a lone passenger on a bus to her village in northern Punjab state on Friday when she was attacked, The Associated Press reported.
The driver and conductor allegedly drove her to a desolate location and took her to a nearby building where they were joined by friends and raped her repeatedly, the AP said.
The apparent case follows the rape of a student on a New Delhi bus in December, which sparked protests in India over national attitudes to violence against women and made headlines around the world.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment