Tuesday 22 January 2013

Re: [wanabidii] MKUTANO NA WAANDISHI MAKAO MAKUU YA CHADEMA JANUARI 22, 2012

Statement kwenye point (iii) inakubaliana kuwa chadema nacho kinakufa. Sasa mbona maneno yanayofuata anakanusha tena? Je, ni madhumuni ya mwandishi kusema hicho au kiswahili ni tatizo kwake?
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Zantel Etisalat Tanzania.

-----Original Message-----
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 22 Jan 2013 10:20:14
To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] MKUTANO NA WAANDISHI MAKAO MAKUU YA CHADEMA JANUARI 22, 2012

MKUTANO NA WAANDISHI MAKAO MAKUU YA CHADEMA JANUARI 22, 2012

NDUGU waandishi wa habari,

Kuna mambo mengi yamezungumzwa kuhusu CHADEMA. Nanyi waandishi wa
habari mmekuwa mkitupigia simu, mmoja mmoja kutaka ufafanuzi na
msimamo wa chama chetu kuhusiana na masuala hayo. Leo tumeamua kuwaita
hapa ili kuwapa ufafanuzi mkiwa pamoja badala ya kila mmoja kuuliza
akiwa kwenye chumba chake cha habari.

Kwanza, CCM kupitia kwa viongozi wao waandamizi, akiwemo Nape na
Mwigulu, wanazunguka zunguka huko, kuwaambia Watanzania kuwa CHADEMA
inakufa, tena wanatengeneza hata sababu za kifo, wanasema ni ubaguzi
na kutokana na laana ya Mwalimu Nyerere.

Tunataka kuwaambia hivi: Kwamba CHADEMA haina ubaguzi na hivyo haiwezi
kufa leo wala kesho, mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa
Watanzania. Na bahati mbaya, CCM wanaona CHADEMA kitakufa, wanasahau
kuona kuwa chama chao tayari kinakufa tayari sasa.

Kama suala ni laana ya Nyerere. Laana hiyo haiko CHADEMA; iko ndani ya
CCM kwa sababu tatu.

(i) Mwalimu wakati wa uhai wake, kwa kushirikiana na waasisi wengine,
alijenga misingi ya utaifa wetu, ambapo CCM wameamua kuivunja kwa
maslahi ya wachache. Akiwa bado hai, Mwalimu alitunga hata kitabu
akasema CCM kimeoza na kinakuka rushwa. Akaongeza CCM kuna kansa ya
uongozi na uchaguzi ndani ya chama hicho, ni gulio la wala rushwa.
Maneno hayo ni laana tosha.

(ii) CCM kinapata laana ya Mwalimu kwa sababu kimerasimisha ubaguzi
kwa wanachama wao, viongozi wao na Watanzania kwa ujumla. Ni hawa hawa
CCM wanaoeneza uongo wa hatari, wakiwatisha wananchi kwa kusema
CHADEMA kina ukabila, mwaka 2005 walimzushia Dk. Salim Ahmed Salim
uongo kuwa ni Mwarabu na alihusika na kifo cha aliyekuwa mmoja wa
wasisi wa taifa hili, Abeid Amani Karume. Uchafu ulifanywa na wana CCM
wa kundi la wanamtandao ambao leo ndiyo wanaongoza chama na serikali
na ubaguzi huu dhidi ya Dk. Salim ndiyo uliowafanya washinde.

(iii) CCM kinakufa pia kwa sababu ya laana ya ubaguzi wa kukiuka haki
za raia. Ninyi ni mashahidi namna ambavyo baadhi ya makundi ya
wafanyakazi yamekuwa yakibaguliwq katika kupata stahiki zao. CCM na
serikali yake, imekuwa ikijibu kwa kauli za kejeli na vitisho, ikiwemo
kutekwa na kuteswa kwa viongozi wa wafanyakazi na kisha kutupwa katika
Msitu wao wa Mabwepande na baadaye kulinda wahalifu kwa visingizio
vingi vya kulindana huku wakichezea maisha na uhai wa Watanzania
wenzetu.

Hivi unaweza kuielezea vipi hali ya serikali ya CCM kutowalipa wazee
wastaafu waliokuwa watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kama si
ubaguzi! Wazee ambao wametumikia taifa hili kwa uwezo wao, akili zao
na miili yao, wenzao wote katika nchi nzingine zilizokuwa zikiunda EAC
wakati ule, walishalipwa, isipokuwa hapa Tanzania ambapo chama
kinachotawala kimeamua kufanya ubaguzi wa haki za watu, nani apate na
yupi asipate.

Itakumbukwa kuwa wazee wale kutokana na kuyumbishwa na kubaguliwa
katika kupata haki zao, waliamua kuvua nguo barabarani, pia kwa kiburi
na ukosefu wa heshima ya serikali ya CCM kwa wananchi, wakawachapa
viboko wazee wale! Laana ya wazee hawa inakiua CCM.

Hivyo basi, CCM kinakufa kutoka na laana hiyo na uongo uliosababisha
na kushindwa kutekeleza ahadi zake za maisha bora, ajira kwa vijana na
kuwezesha wanawake.

CCM wajiandae kufuata njia za vyama vya KANU ya nchini Kenya, UNIP ya
Zambia na chama cha ukombozi nchini Malawi.

Ndani ya CHADEMA kuna baraka za Mwalimu Nyerere. Hakuna laana. Ninyi
ni mashahidi kuwa kabla ya Mwalimu kufariki dunia, alikimwagia sifa
CHADEMA kwa kusema ni chama makini.

Tofauti ya CCM na CHADEMA

Kwenye mikutano yao, sasa CCM wamejipatia majukumu wasiyoyamudu ya
kujifanya ni maofisa waenezi wetu na moja ya majukumu waliyoamua
kujipachika na kuyafanya ni kuwaonesha Watanzania, moja ya tofauti
kati yetu na wao, ambazo ni uwezo wa kuchukua hatua na kuwa na sera
sahihi mbadala kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Watanzania.

Kwenye mkutano wao uliomalizika hivi karibuni na kwenye shughuli zao
za kila siku, CCM sasa wameamua 'kuimba' sera za CHADEMA, hasa zile za
elimu bure na kushusha bei ya vifaa vya ujenzi. Mambo ambayo miaka
miwili tu iliyopita walikuwa wakiimba kinyume chake. Bahati mbaya
hawana uwezo wa kuzitekeleza, kwa sababu si mawazo yao na hawana
utashi huo.

Hili la pili la kuchukua hatua…bahati mbaya kwa sababu ya kuelemewa na
kansa ambazo tumezitaja hapo juu, CCM wanaona kuchukua hatua ni
'kufukuzana', maneno ambayo hata jana wakati wakizungumza na waandishi
wa habari wameyarudia. Hawawezi kuona kwa sababu wote ni wachafu,
wanaishi hivyo kwa kukubaliana.

Ndugu wanahabari, hii ni moja kati ya tofauti nyingi zilizopo kati ya
vyama hivi viwili, ambazo zimeifanya leo CHADEMA ndiyo tumaini la watu
wanaodai haki na uwajibikaji, tumaini la watu katika kupigania uhuru
na mabadiliko ya kweli nchini, kimbilio la watu wasafi dhidi ya
ufisadi, wanaopinga ubadhirifu na dhuluma ya CCM, ni tofauti hizo
zinakifanya CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani na mbadala
kinachoaminiwa na Watanzania kukabidhiwa dola.

Tukiwa chama imara na makini kinachoaminiwa na kubeba matumaini ya
Watanzania, tutachukua hatua mbalimbali, dhidi ya makosa tofauti
tofauti, kulingana na uzito wake, kama vile uzembe, udhaifu,
ubadhirifu, ufisadi na usaliti.

Tuwachukulia hatua hata wale ambao wametumwa na CCM kuja kufanya kazi
ya chama hicho kupitia kwa jina la CHADEMA.

Ni uwezo na uthubutu wa kuchukua hatua mbalimbali, ndiyo umekuwa moja
ya sababu kubwa ya Watanzania kuiunga mkono CHADEMA kila tunaponyoosha
mkono kuikemea CCM na serikali yake juu ya ufisadi, ubadhirifu na
uminyaji wa haki za Watanzania.

Zamani, CCM kilipokuwa bado chama cha siasa hasa, ambapo kilikuwa
kinasimamia misingi ya umoja wa kitaifa bila kujali dini ya mtu,
kabila au rangi; kilipokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi
rushwa na ufisadi, yaani CCM ya enzi za Mwalimu Nyerere na waasisi
wengine waadilifu, hakika kilikuwa na uwezo wa kufukuza kila
aliyeonekana kwenda kinyume na misingi yake.

Ni katika kipindi hicho, CCM kiliwavua uongozi na uanachama baadhi ya
waliokuwa viongozi wake. Kwa mfano, Maalim Seif Shariff Hamad, Hamad
Rashid Mohammed, Sudi Yusuf Mgeni, Fortunatus Lwanyantika Masha na
wengineo. Baadaye mwaka 1984 kilimfukuza uongozi (msisitizo uongozi)
aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,
Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, kwa kukiuka misingi yao.

Lakini leo hii, CCM hakiwezi kuchukua hatua hiyo hata kwa katibu wa
tawi. Kwa sababu, hiki si chama cha siasa tena. Hili ni genge la
wahuni, waliojikusanya pamoja na kujiita chama cha siasa. Ni wezi wa
raslimali za taifa, waliotayari kulirejesha taifa kwenye utumwa kwa
maslahi yao binafsi.

Ndiyo maana wameshindwa kuwafukuza mafisadi, badala yake ndiyo
wanaoongoza chama na kuwatawala. Walisema wanataka kujivua gamba (la
nyoka) baadae wakagundua kuwa gamba lao halisi (ufisadi) ni gamba la
kombe, ambalo ili livuke ni lazima kobe afe!

CCM ya sasa, hakiwezi siyo tena kutetea wafanyakazi na wakulima.
Hakitetei tena maslahi ya wanyonge. Kimebeba na kukumbatia ufisadi na
mafisadi wa kila aina, na wabadhirifu wa mali za umma, ambao
wameyafikisha maisha ya Watanzania na nchi yao hapa yalipo.

Lakini CHADEMA inachukua hatua kwa sababu hiki ni chama sikivu na
kinachobeba matumaini ya wananchi. Hivyo, hatuko tayari kumuacha mtu
yeyote ambaye anafanyakazi za CCM ndani ya CHADEMA, kisha kujiita yeye
ni mwana-Chadema. Tutamfukuza.

Huwezi kuzusha uongo kwa viongozi wako na chama chako, kisha ukataka
uachwe. Usijadiliwe. Usiguswe. Tutakujadili na tukibaini kuwa una
makosa, tutakuomba ujirekebishe. Ukikataa, tunakuambia hutufai.
Ondoka. Ukishindwa, tunakufukuza.

CCM kupitia mawakala wao wanasema: CHADEMA kinapokea ruzuku kubwa,
lakini kimepanga ofisi. Hii nyumba ni mali ya Chadema. Lakini mbona
hao mawakala wa 'status quo' hawasemi kuwa CCM haina ofisi? Maana ile
inayoitwa ofisi ya CCM Makao Makuu Dodoma, ni mali ya Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu (CDA).

Huyu Nape hana hata maadili ya uongozi. Alifukuzwa kwenye UV-CCM baada
ya wenzake kumwambia amezusha uongo. Baada ya kuitwa kujitetea,
akasingizia kuwa alilishwa maneno na waandishi wa habari. Kumbe
wenzake walikuwa na mkanda wa hotuba yake aliyoitoa pale Peacock
Hotel. Wakampa aisikilize. Eti ndipo akakiri na kuomba radhi. UV-CCM
chini ya Emmanuel Nchimbi, ikamwambia hutufai. Muongo wee. Ikamfukuza.
Sasa mtu ambaye amethibitishwa na chama chake kuwa muongo, atawezaje
kutusumbua CHADEMA?

Wala tunachofanya hapa siyo kujibu maneno yake, bali tunaweka rekodi
zake sawasawa. Tunataka umma umfahamu vizuri, kwa sababu wasiomjua
wanaweza kuamini maneno yake.

Kauli za Mwigulu Nchemba

Tunataka kuwaambia wahusika wa usalama na ulinzi nchini, hususan Rais
Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid, nini maana ya tafsiri
ya habari za kutunga, lakini za hatari sana za Mwigulu Nchemba;

(i) Kwamba suala la yeye kusema CHADEMA inapanga mauaji, tunataka
kumwambia Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said
Mwema na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othuman Rashid kuwa, kwa
sababu wamekuwa kimya na kukubaliana na uzushi wa hatari wa Mwigulu,
tafsiri yake ni kwamba Jeshi la Polisi limeasi na sasa linafanya kazi
kwa maelekezo ya CHADEMA. Linatekeleza amri za CHADEMA!

Kwa sababu, iko wazi. Watanzania na dunia inajua kuwa mauaji yenye
utata yanayohusishwa na siasa, yamefanywa na Jeshi la Polisi. Ushahidi
upo. Polisi wameua watu Arusha, polisi wameua watu Songea, polisi
wameua mtu Morogoro, polisi wameua mwandishi wa habari, Daudi
Mwangosi.

Orodha ya mauaji ya vitendo vya mauaji vinavyofanywa na Jeshi la
Polisi nchini ni ndefu, kwa malengo ya kisiasa ya CCM. Lakini kama
Mwigulu anasema, hiyo ni mipango ya CHADEMA, maana yake ni kwamba
Jeshi la Polisi linatekeleza mipango ya chama hiki, tafsiri ya haraka
hapo, Mwigulu anamaanisha, "basi jeshi limeshaasi."

Sasa mtu anayetangaza 'uasi' wa jeshi kwa kiwango cha kutekeleza
mipango ya chama cha siasa badala ya kumsikiliza Amri Jeshi Mkuu,
serikali inamnyamazia na kumchekea!

Tumeitaka serikali kufanya uchunguzi huru kwenye matukio ya mauaji
yanayohusishwa na siasa, ikiwemo tukio la kifo cha kada na kiongozi wa
CCM huko Ndago, Singida, lakini wamekaa kimya. Badala yake wanatunga
uongo na kumtuma Mwigulu atangaze na kueneza.

(ii)Tafsiri nyingine ya maneno ya kutungwa hayo kisha anatumwa Mwigulu
kutangaza, ni kwamba vyombo vinavyohusika katika ulinzi na usalama,
vimeshindwa kazi. Ni maneno ya aibu kwa IGP Mwema na Othman Rashid,
kwamba wao wameshindwa kazi zao na sasa wamemkabidhi Mwigulu, ambaye
anaweza kuingia kwenye vikao vya CHADEMA, akarekodi, kisha badala ya
kuwapelekea hao wenzake, ili serikali ya chama chake ichukue hatua,
anazunguka nao kulia kwenye vyombo vya habari! Na wahusika wamekaa,
wanamsikiliza na kumchekea!

Tunaomba tuwaambie, tuko makini sana. Hiki ni chama kinachojiandaa
kushika dola, kuwatumikia wananchi. Tunajua mipango yao katika hayo
maneno ya Mwigulu. Tunaelewa wanachotaka kufanya. Tunafahamu hata
kesho wanataka kufanya nini. Tuko imara. Tunawaambia Watanzania
waendelee kutuunga mkono, katika harakati hizi za ukombozi wa nchi
yetu.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.


Imetolewa leo tarehe 22 Januari 2013 na:

…………………………………………………

Benson Singo Kigaila,

Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo (CHADEMA).

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment