Hilda
Mbunge ni Mkristo na alienda kama Waumini wengine
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 3 Jan 2013 13:18:18 +0000 (GMT)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
Kwani Uislamu si umeletwa na nani hata usilinganishwee hivyo si na Waarabu? Ndio maana wengine huchanganya dini hiyo na waarabu. Ukristu umeletwa na wazungu na lugha ya kusalishia mfano ukatoliki ulipoanza ni kilatini. Wazee wa zamani walipata sana tabu kuzoea kusali kwa kiswahili lakini mataifa yakaja kubadili kusali si kilatini tena kwa lugha zao na vitabu vipo vya kilatini-kiswanili upande mwingine; vya kiingereza; kuna kihaya tupu vitabu vya dini na misa Kihaya. Inategemea upo wapi-Ufaranza utasali kwa lugha yao na Uingereza kuna makanisa ya RC yanasalisha Kilatini na baadhi mix kiingereza na kilatini. Unaweza ukaamua utasali misa ya kilatini tupu hapa TZ au ya Kiswahili au ya lugha ya Kiingereza hapa DSM ktk makanisa mbali mbali yafanyayo hivyo. Sidhani kama ipo hivyo kwa waislamu kusali kwa lugha ya nje ya ya Kiarabu ilivyo ktk Quran. Ni akili finyu za kutokukubali mchanganyiko wetu ulivyo. Kuna tabu gani kuitikia salam ya Mbunge ya " Assalamu Alaikum "- "Alaikum salaam" halafu akasema 'Kristu ! ". Tumaini Letu au Bwana Yesu Asifiwe-Amen!! Kwanza amewaheshimu, amewajali, amewapenda na ndio maana amekubali kuingia kanisani kukaa mpaka misa kuisha naye muislamu. Hata wakati wa mazishi ya mfanyakazi mkristu, au sherehe ya ndoa, kufiwa nduguye na mazishi-waislamu mbona huingia kanisani na kuhudhuria vyote mpaka makaburini au ktk hli la arusi. Vile vile-kuna familia kuna mchanganyiko wa dini huingia kanisani, akikosea anarekebishwa. Wengine hudhania anaweza akaongozana na wengine wanapokwenda mbele kupokea mkate wa Bwana nao wanainuka. Jamaa zao huwaambia hapana wewe usiende lakini alikwenda kupeleka hela yake ya sadaka wakati wa miza hiyo ya sherehe au mazishi. Wapo wanaotaniana tunawaona na kuitikia-Alaikum Muislamu!! Tena husema-Aleko Muislamu!! wengine wakadhani hii ni formal response kumbe sio. Upungufu wa uvumilivu, kutokuzikubali tofauti zetu na kukubali mtu anaweza kukosea au akaanza na salamu aliyoizoea na kisha kuja ya wenye dini hiyo ni kitu cha kawaida. Kuzomewa ni mapungufu ya hao wakristo ambapo dini yao inavundisho kuu la Upendo na Uvumilivu. Inaweza kuwa inatokana na haya matendo ya sasa ya kuchoma makanisa na kupika risasi wakristu. Kwa udini hata shule nyingine wanafunzi wanahama kwani akivaa rosali au tasbihi haitakiwi. Picha ya uniform au T-shirt iwe ya kidini. tatizo kumtaka mtu awe perfect kwa dini yako asikosee hata kidogo bali awe mkristu au muislamu akija katika tafrija yako-Sio proper. Mradi tu hakukudharau kwa makusudi, atajifunza akielekezwa. Muandae vizuri mgeni wako asikosee. Unawajibika nawe pia. --- On Thu, 3/1/13, Lemburis Kivuyo <lembu.kivuyo@gmail.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment