Monday 21 January 2013

Re: [wanabidii] MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!

Boniface,
Ngoja hapa nimsaidie Matinyi kidogo. Muungano wetu si ndoa ya watu wawili tu. Umeshazaa watoto na wajukuu. Sasa hawa pia
lazima uwaweke kwenye equation unapozungumzia manufaa na hasara za muungano. Kati ya hao watoto na wajukuu yumo wewe, mimi na Matinyi, kwa mantiki hiyo Matinyi na wewe na mimi tuna haki kabisa ya kuzungumzia hii ndoa ya watu wawili.
em

2013/1/21 Boniface Magessa <magessabm@gmail.com>
Matinyi,
Sijaona km umenijibu.nimeuliza kuwa ni ndoa ya watu wawili.wao wenyewe kwa hiyari yao kabisa hasa mwanamke ameona hafaidiki na ndoa ile na yeye ndo anajua kitu au vitu anavyoona hafaidiki.lakini yule aliyeko nje anakuja na kumwambia mwanamke yule kwamba avumilie tu eti kufunga ndoa ni HESHIMA! heshima gani wakati naumia moyoni nakonda sina furaha, mwanaume anachukua mali ya familia ovyo na kutapanya na wanawake wengine n.k.?
Waache wahusika waone inavyofaa wao.sio ww usiye chunguni hujui hata mboga inayopikwa!


On Tuesday, January 22, 2013, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:
> Magessa,
>  
> Tatizo lako ndilo tatizo la watu kadhaa hivi sasa hapa Tanzania, na hasa kizazi hiki cha vijana - kwamba wanaishi na kufikiri kama walivyo Waafrika wengine wa nchi zilizokwama ama zinazokwama barani humu. Watu wa namna hii, yaani kama wewe, hamuoni mantiki ya utaifa. Ndiyo maana leo hii tuna viongozi ambao hawawezi kuzungumzia kuhusu maadili ya taifa letu kwa sababu hawajui maana ya DOLA-TAIFA, yaani a nation-state. Kwamba, kilichofanywa na viongozi wetu waasisi ni chao, siyo cha taifa hili, siyo cha Watanzania, siyo chako wewe, siyo changu mimi, siyo chetu.
>  
> Unafikiri tukiendekeza fikra kama hizo tutabaki na taifa? Itakwenda hivyo hivyo kwenye kila kitu, fikra, eneo, kabila, dini, rangi, n.k.
>  
> Ni uduni wetu Waafrika huu. Ni mawazi finyu sana. Wewe unafikiri kama kweli mataifa haya makubwa yangekuwa na fikra hizi yangekuwepo hivi leo? Ndiyo maana baadhi ya wanazuoni wanasema kwamba mwafrika hana dhana ya utaifa kichwani mwake na moyoni mwake; anaona mambo kwa udogo wake kwa kadri inavyowezekana na anafikiri ni sifa. Na hata Wazanzibari wanaopiga kelele wamo kwenye tatizo hili hili; ndiyo maana Muungano una matatizo ambayo ukikaa chini na kuyaangalia unaweza kushangaa. Ni uduni tu huu - wa fikra na kila kitu. Waafrika wengine wanahaha kwa sababu hii na sisi tulibahatika kidogo tu kutokana na aina ya viongozi tulioanza nao, lakini sasa tunaelekea shimoni. Ndiyo maana viongozi wetu wanaona kila kitu kiwe Dar es Salaam ama kwao tu. 
>  
> Ni aibu sana!
>  
> Matinyi.
>  
>  
>  
> ________________________________
> Date: Mon, 21 Jan 2013 23:51:27 +0300
> Subject: Re: [wanabidii] MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
> From: magessabm@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Matinyi,
> Walioungana hawautaki muungano, wewe ambaye hujui hata chanzo cha muungano huo unautetea.why?!watu wanafunga ndoa wawili wakiachana ni wao wenyewe wameshindwana.wewe wawashiwa nini?7
>
> On Monday, January 21, 2013, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:
>> Issa,
>> Ndiyo maana watu wengi wa Bara wanasema kwamba Wazanzibari ni walalamishi. Hebu angalie ulichokisema - unaashiria kwamba Zanzibar imefanywa jimbo wakati ina rais wake, makamu wawili, katiba yake, wimbo wake, bendera yake, nembo yake, mamlaka yake, mahakama yake, bunge lake, na sasa eti na eneo lake la mipaka, na inawakilishwa kwenye kila kitu ndani ya Muungano. Nadhani umeona hoja ya watu wengi wa Bara ambao wameshachoka na haya maneno. Mimi binafsi sijachoka na niko radhi hata tuvutane hata kwa miaka 1,000 lakini tusifuate uongo na unafiki. Hapa Marekani kati ya haya majimbo 50 hakuna hata moja lenye vitu vyote hivi kwa mtindo wa Zanzibar na hawalalamiki kitu. Muungano ni kuungana, siyo kubaki na kila kitu cha kwako.
>> Matinyi.
>>  
>> ________________________________
>> Date: Mon, 21 Jan 2013 11:11:16 -0800
>> From: saidissa100@yahoo.com
>> Subject: Re: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
>> To: matinyi@hotmail.com; wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kaka Matinyi,
>> Mengi yanasemwa pande zote mbili, lakini la muhimu ni hali ipo vipi hivi sasa baina ya washirika hawa wawili?
>> Kweli ni Muungano wa nchi mbili au wa nchi moja na jimbo fulani?
>> ...bin Issa.
>> ________________________________
>> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
>> To: saidissa100@yahoo.com
>> Sent: Monday, January 21, 2013 11:05:39 AM
>> Subject: RE: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
>>
>> Issa,
>> Ina maana wewe humjui "Hapa pangu"? Humjui siyo? Karafuu iko wapi siku hizi? Wale waliotaka kuufutilia mbali utalii washatulia? 
>> Halafu siamini kwamba eti wewe Issa hujui kuwa wimbo mkubwa visiwani hivi sasa ni kwamba Waarabu wataleta misaada kuanzia na Oman, halafu Arab League, OIC, na mataifa mengine, na hoja ni kwamba eti Zanzibar ni ndogo, Wazanzibari ni wachache, kwa hiyo misaada itasaidia zaidi. Huo wimbo mpaka Maalim Seif anauimba, bila hata haya, akija huku na kwingineko. 
>> Lakini pia hili la "sisi" na "ninyi" halifai kabisa. Ni ubaguzi tu. Muungano una malalamiko yake na kama tungekuwa viongozi makini yangetatuliwa, lakini ubinafsi wa viongozi wa Tanzania, siyo Tanzania Bara, ndiyo tatizo. Ninaposema ubinafsi viongozi nazungumzia TANZANIA, yaani Bara na Visiwani.
>> Matinyi.
>>
>>  
>> ________________________________
>> Date: Mon, 21 Jan 2013 10:52:22 -0800
>> From: saidissa100@yahoo.com
>> Subject: Re: [wanabidii] Re: MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
>> To: wanabidii@googlegroups.com; matinyi@hotmail.com
>>
>> Kaka Matinyi,
>> Sasa kaka Matinyi kama kwanza ilikuwa Seif, halafu Karume na sasa Salmin na kesho Shein, hivyo bado hujafahamu tu Wazanzibari wanasema nini?
>> Kama hukubali kuwa matatizo yaliyopo ni kwasababu ya Muungano basi kwanini hatuwezi kuyatatua?
>>>Shida yetu kubwa ni kwamba tuna viongozi wezi, wabinafsi na sisi wananchi hatufanyi kazi.
>> Hili ndilo jambo moja linalotufanya tuukimbie huu Muungano. Wenzetu mmezidi wizi na sio wizi tu lakini hata mkiwapata hao wezi hamfanyi kitu kwasababu ndio nyinyi wenyewe wezi - samahanini kwa lugha jamani, kwani sisemi kuwa nyote ni wezi - ni wakubwa wenu tu.
>> Mzee Vijisenti kakubali kuwa anapesa nje, je, aliulizwa chochote? Yule Mhindi wa Radar yupo Switzerland, je, tumechukuwa hatua zozote za kumrejesha? Sitaki hapa kuzungumzia juu ya hizo pesa zilizofichwa huko huko Switzerland na ambazo serikali haitaki kuzidai kama Balozi wa Switzerland alivyoeleza. Mambo haya sisi Wazanzibari tunahisi yanasaidia kuturejesha nyuma, japokuwa nasi sio Mitume!
>> <
>>
>> --
>> Jobs in Africa - www.wejo
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>  
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>  
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>  
>  
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment