Monday 21 January 2013

RE: [wanabidii] MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!


Wanachozungumzia Watanzania hawa wawili, Salmin na Karume, ni kuuvunja Muungano kwa kuwa hakuna kitu kama hicho kinachoitwa Muungano wa Mkataba. Kwani huu hauna mkataba? Hiyo mifano waliyoitoa siyo miungano ingawa inatumia neno "muungano" na hili ni suala la uelewa tu.

Kwa hiyo wao hawazungumzii MUUNGANO bali wanazungumzia kuuvunja Muungano uliopo.

Tusichanganye mambo. Hakuna Muungano wa nchi mbili zenye madaraka yote ndani na nje ya nchi zao. Hakuna.

Matinyi.

Date: Mon, 21 Jan 2013 09:48:43 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: [wanabidii] MARAIS WA ZAMANI WA ZANZIBAR WATAKA MUUNGANO WA MKATABA!
To: wanabidii@googlegroups.com

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Baba wa Maridhiano ya wazanzibari na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambae ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar, Mhe Amani Abeid Amani Karume leo amekutana na Jaji Joseph Warioba na kuwasilisha maoni yake. Katika maoni yake amesema kwamba wakati wa siku za mwanzoni, Muungano ulikuwa wa heshima na usawa kati ya Zanzibar na Tanganyika lakini kadiri siku zinavyokwenda unachukua sura ya nchi moja -Tanganyika – kuuhodhi Muungano huo dhidi ya Zanzibar. Akasema akiwa Rais kwa kipindi cha miaka 10 ameshuhudia mengi dhidi ya maslahi ya Zanzibar. Alisema hizi ni zama mpya za uwazi na ukweli na kwa hali iliyofikia sasa hakuna njia nyengine zaidi ya kila nchi – Zanzibar na Tanganyika – kurejesha mamlaka yake (sovereignty) kitaifa na kimataifa na kisha nchi hizo mbili kushirikiana kupitia Muungano wa Mkataba kati yao. 

Chanzo: Mzalendo

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, zinaeleza kwamba kiongozi huyo ametoa maoni yake tarehe 13 Januari, 2013 na katika maoni yake ameieleza Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiongozwa na Joseph Warioba kwamba anataka kuona Zanzibar na Tanganyika kila moja ikiwa ni nchi yenye mamlaka kamili ndani na nje na kisha zishirikiane kwa mfumo wa ushirikiano kama ule uliopo baina ya nchi za Afrika kupitia Umoja wa Afrika (AU). Dk. Salmin Amour amesema msingi wa umoja wa nchi za Afrika umetokana na mashirikiano kati ya vyama vya ukombozi chini ya PAFMECA. Akasema Umoja wa Vyama vya Ukombozi vya Afrika Mashariki na Kati (PAFMECA) ulitambua haja ya nchi za Afrika kuungana baada ya uhuru lakini kwa msingi wa kuheshimu mamlaka ya kila nchi (sovereignty) na mipaka yake. Hivyo, akataka mahusiano mapya kati ya Zanzibar na Tanganyika uzingatie msingi huo ambao ndiyo pia uliojenga misingi ya Umoja wa Afrika (African Union). Waliokuwa bado wana mashaka na umoja wa Wazanzibari katika kutaka mamlaka yao kamili naamini sasa watawafahamu Wazanzibari.
Waasisi wawili wazito wa Zanzibar ambao uzalendo wao hauna mashaka, aliyekuwa Katibu Mipango wa ASP, memba wa Baraza la Mapinduzi la mwanzo kabisa mwaka 1964 na Waziri katika Wizara tofauti za Serikali ya Zanzibar na ya Muungano kwa miaka mingi, mwanachama wa CCM mwenye kadi ya uanachama nam. 7, Mzee Hassan Nassor Moyo, na Katibu Mkuu wa mwanzo wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia alikuwa Naibu Waziri katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na katika Serikali ya Muungano na kisha akawa Balozi wa Tanzania nchini Guinea na Ethiopia, Mzee Salim Said Rashid, wamemaliza kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba asubuhi hii. Wote wawili hawakutafuna maneno jinsi Zanzibar ilivyodhulumiwa katika Muungano huu wa kikatiba na wakamalizia kwamba wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani na nje ya nchi itakayofuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika.

Chanzo ni facebook ya ismail juss/MZALENDO

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment