Saturday 12 January 2013

Re: [wanabidii] MAPENDEKEZO YA CHADEMA YAWAAMSHA WANA-CCM ZANZIBAR!

Kwa hali ilivyo Watanzania Bara kumchagua mtanzania kutoka Zanzibar kuwa Rais wa \MUungano lazima kuwe na mtu anayeiongoza sehemu ya Muungano ya bara ili likitokea lolote Tanzania Bara isiwe matatati bila kiongozi. Vinginevyo Rais wa Jamhuru ataendelea kutoka Bara. Tunaweza kulifafanua waTanzania bara wakalielewa na kulihakikisha halitenguki

--- On Sat, 1/12/13, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] MAPENDEKEZO YA CHADEMA YAWAAMSHA WANA-CCM ZANZIBAR!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, January 12, 2013, 11:28 AM

Naunga mkono haki ya wazanzibari kuchagua mgombea wao wa urais. Siungi mkono wazo la urais wa zamu baina ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa sababu wapiga kura wengi wako bara itabidi mgombea wa Zanzibar akubalike bara na si vinginevyo.
em

2013/1/12 Said Issa <saidissa100@yahoo.com>
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, kimeeleza nia yake ya kutaka kuachiwa mamlaka ya kumchagua mgombea urais wa visiwa hivyo, badala ya utaratibu wa sasa unaoshirikisha wenzao wa Tanzania Bara. Pamoja na hatua hiyo, chama hicho pia kinafikiria kurejea mtindo wa kupokezana kiti cha urais wa Tanzania kati ya bara na visiwani kama ilivyokuwa awali, ili kuweka usawa katika Muungano.Hatua hiyo inaelezwa kuwa huenda ikazua mpasuko na malumbano mapya kuhusu suala la urais ndani ya CCM, ambako harakati za baadhi ya wanachama wake wameanza kupiga mbio za kuutaka urais katika uchaguzi mkuu wa 2015.Akizungumza katika mahojiano maalumu visiwani humo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, alisema kwa sasa suala hilo linajadiliwa na kwamba ana matumaini kuwa litapatiwa ufumbuzi.Hatua hiyo imekuja wakati Zanzibar ikiadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi yaliyoung'oa madarakani utawala wa mabavu wa Sultani, huku ikiwa imesalia miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani, utakaofanyika 2015."Ndani ya CCM tuna utaratibu wetu wa kupata viongozi, lakini hilo suala la kuchaguliwa mgombea urais kutoka kwenye vikao vya Dodoma hata sisi limetugusa... Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kulijadili ili tupate ufumbuzi," alisema Vuai na kuongeza:
"Siyo tu kuchaguliwa mgombea urais, hata suala la kupokezana urais na jinsi ya kupata viongozi wengine kama wabunge na wawakilishi tunalijadili kwa kina. Ninaamini tutapata ufumbuzi… Siwezi kusema lini kwa kuwa chama chetu ni kikubwa mno, lakini tunalijadili."
Vuai ametoa kauli hiyo, huku kukiwa na malalamiko ya Wazanzibari wengi kuhusu Muungano, ambapo wengine wanahoji iwapo kuna haja ya kuendelea na utaratibu wa sasa kupata mgombea na Rais wa Zanzibar ambao ni lazima upate baraka za CCM Bara.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema jambo hilo halijafikishwa kwenye vikao rasmi vya chama.
"Kama wao wanalifikiria hilo, acha waendelee, labda ungewauliza kama wameshalifikisha kwetu. Ukiniuliza mimi nitakujibu kuhusu utaratibu tulionao sasa, ila kama wao wana hoja nyingine, basi watazileta kwenye vikao husika zitajadiliwa," alisema Nape....................
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment