Tuesday 22 January 2013

Re: [wanabidii] MAFUNZO KWETU WADADA TENA WALE WANAOSEMA WA KISASA



WRDP-NGO imefanya utafiti wa kuenea kwa Sodomy in TZ. huu ni utafiti wa 1997. Wanafunzi wa kike wanaongoza. Ni tatizo kuu ndani ya ndoa (1%) kwa wahojiwa wote prevalence ni 70%. Ndani ya ndoa mke anatishiwa kuachwa. Msichana anatishiwa kuachwa na boyfriend pia ni kuepuka mimba sio HIV. Imani potofu kuwa HIV haipatikani namna hiyo. Vijana walioajiriwa majumbani kukata majani na kazi nyingine mfano kuuza maduka au kimgahawa na biashara nyingine za familia-waathirika wakuu wa mabosi zao kumuahidi hela nyingi au kumtishia kumfuta kibarua hiyo. Chuki na ushindani kibiashara, kugombania mwanamke/msichana kijana au mwanaume anaandaa mpango wa kumdhalilisha mwanamme mwenzake kwa kuwalipa vijana hovyo na kisha kumtangaza. Hapo atahama kwa aibu kuacha biashara hapo. Kama ni mwanamke anaachana nae maana mama kajua aibu ya huyo kijana/baba. Changudoa na mashoga-wanatumika sana siku hizi na mchezo huo una malipo yake makubwa zaidi. Hivyo wakaka, wababa wakitoka huko huupeleka nyumbani-ni tatizo kuu na linazidi kukua licha ya HIV. Utafiti ulionyesha-wale wote waliofanya hivyo na wasichana au wanawake-HAWAKUWAOA licha ya ahadi kuwa akikubali hivyo atamuoa. Aliyemkuta anafanya hayo au anapenda hayo-hakumuoa.

Mwanaume yule ambaye alibakwa na wanaume wenzake-aliendelea kubaka wanaume na wanawake mtindo huo (Hasa wanaume) sababu kuu nikuwa alikua akipata ahueni (psychological relief) kuwa amemuadhibu mtu kama alivyoadhibiwa yeye. aliyeanza mchezo huo akiwa hajaolewa alipoolewa na mtu mwingine-hakuendelea wala kusema kuwa alikuwa anafanya mapenzi ya aina hiyo na aliyepita kwa kuogopa kuachwa ikiwa aliyemuoa hana mambo hayo toka urafiki wao uanze. jambo lililoonekana mashuleni ni kwamba-watoto wadogo majumbani hulawitiwa na kaka zao au wanaumewengine wanaoishi nao humo ndani ya nyumba (houseboy, mtu mzima akaae humo, vijana ktk nyumba wanaopangwa kuchangia chumba kupunguza attizo la vyumba na malazi kama ni wapangaji). wengine tamaa anadanganywa na muuza chips, hoteli, duka na kupewa visenti. Visichana hubakwa na kufanyiwa hivi na jamaa wa karibu waishio humo. Visichana vya kazi huathirika zaidi na sexually transmitted diseases zinaathiri watoto. Baadae ndio vijana wakiume huwa mashoga.

Asilimia 80 ya mashoga source ya kuwa hivyo ni nyumbani sio mtaani, kazini, shule, mazingira mengine au tatizo la homoni. Chunga wanao na unaowalewa na mazingira uishiyo. Tuendelee kujidanganya tu-tuendako kubaya.

Wasichana dada poa wanalalamikia sana tabia ya wababa kwa sasa kupenda sodomy. Fanya utafiti na wadada hao na wale wafanyao kazi za kipato saluni uone utapata matokeo gani kuthibitisha haya ya WRDP. Chukua mashoga 100 uwahoji watakuambia walianzaje ujue- ndani ya familia ndio chanzo. wanaowapangia nyumba na kuwatunza-70% ni married men na wengine ni waswalihina na waheshimiwa sana au watu wa dini na wanaoheshimika kifamilia na mtaani au kazini. KTK baadhi ya semina za kuwabadili hawa mashoga na changudoa-ndio huko wapatapo mabwana zaidi wa mchezo huo na semina inaendelea!!

Baadhi yao matendo haya ya ulawiti huyafanywa nje sio ndani ya ndoa mke hajui au mume hajui kabisa hata akisikia haamini.

Wanaume wanaobakwa hawapati msaada na hawajitokezi lakini kisaikolojia walionyesha kuathirika sana na ndio wabakaji wakuu. Kwa sasa ajira ilivyo ngumu vijana wakiume huathirika zaidi na ulawiti ili kupata favours kuliko wasichana. Wahamiaji haramu watokao Afrika kwenda ulaya-uarabuni na kupata ajira za siri bila vibali ni victims wa suala hili chafu la laana. SIO Wadada ru wanaohitaji mafunzo haya hata vijana wetu wa kiume kuanzia wanapokuwa watoto tuwape mafunzo haya na stadi za maisha-wajijue, wajilinde, wawe na ujasiri kusema wanapoonewa ndani na nje ya nyumba. Lina na uwe muwazi kwa watoto wake me na ke kuwafahamisha jinsi ya kujilinda na kujitetea. WRDP imesaidia kutibu STDs na kushauri wanafunzi (1997-2003) ambapo wazazi hawakuweza kuambiwa siri hiyo na watoto wao kuwa wanaonewaje ndani ya nyumba.Baadhi ya wazazi wakiambiwa na watoto wao-huwakemea wasiseme kuficha aibu na kuogopa stigma. Wengine-kulinda ndoa (mume anabaka au kulawiti wadogo zake, housegirl au ana kijana shoga (Analinda penzi haondoki na anaambiwa ondoka ukitaka). Kesi za namna hii zinakuwa ngumu kutokana na ushirikiano mdogo wa mama. NGOs zinauzoefu na masuala haya wala hakuja geni hapa. Usiri na ukimya  na usiri wetu ndani ya familia; mlolongo wa masuala ya kimahakama, kuogopa kuachwa, stigma yanaleta utata ktk kumaliza au kuzungumzia haya ambayo yapo sana ktk jamii. Samahani ila tulifanya tafiti na huu mchango wangu na ninaujua mtandao mkubwa wa mashoga ninaweza nikakufahamisha kwao ukapata usichokitegemea.


--- On Wed, 23/1/13, Tracy John Kimambo <tracykwetu@gmail.com> wrote:

From: Tracy John Kimambo <tracykwetu@gmail.com>
Subject: [wanabidii] MAFUNZO KWETU WADADA TENA WALE WANAOSEMA WA KISASA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 23 January, 2013, 0:04

Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu
nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng'ombe,
niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu
likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu
mapenzi. Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake.
Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama
haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa
ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae?

Nilimkubalia kila kitu. Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika
siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo
lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana. Nikapata mimba ya
kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe.

Nikaiba pesa nyumbani nikafanya alivyotaka. Kwa mara ya kwanza
nikatyoa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja
kunioa na atanifichia aibu hii. Nilitegemea sasa tutaanza kutumia
kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo.

Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa
na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na
nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa nawahi kulewa. Akautumia
udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako.
Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!!

Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu
mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi. Mchezo ule ukaendelea.
Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala.
Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu.

Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo
ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali
sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo.
Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena.

Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na
maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika
msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini
mimi? Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!!

Nilijua tayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika
kwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri
nikautumia. Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa
ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo
akajitambulisha nyumbani na alitaka kunioa. Akanio kweli. Maisha
yakaanza.

Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba.
Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa hi kunilaumu. Lakini
niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali. Nikaambiwa kizazi
change kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara.

Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa. Nililia sana
huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa
mahali pangu sahihi. Nimekuandikia barua hii mdogo wangu.

Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya
mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso
kama mimi.

Wasipokusikiliza usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa
siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu.
Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!! Nimekuandikia wewe kwa
kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi
siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa.

Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako AMENITENDA
HIVI!!! TAFADHARI TAFAKARI

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment