Sunday 13 January 2013

Re: [wanabidii] KAKA MATINYI: KOTI LA MUUNGANO LATUBANA SANA - lipanuwe kidogo!

Mr. Matinyi,

Nina uhakika kabisa personal interests za watu wanataka kuzihalalisha kuwa public interests! Hili ni kosa na kama wanajiona wana haki leo, kesho hao hao wataonekana kwa waTz wa wakati huo walikuwa puppets wa matakwa ya watu wasiotakia muungano mema!

Naamini kuwa kwenye muungano kuna give and take na principal hii isipopata wafuasi huko Zenj au Tzn basi ipo kazi, tutaunguza mizizi!

Akili zitumike na busara itawale!
------Original Message------
From: Mobhare Matinyi
Sender: wanabidii@googlegroups.com
To: Wanabidii googlegroups
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] KAKA MATINYI: KOTI LA MUUNGANO LATUBANA SANA - lipanuwe kidogo!
Sent: Jan 13, 2013 22:40

Turejee kwenye ukweli.
 
1. Iwapo kila nchi itajiamulia mambo yake yenyewe, ndani na nje, hapo tunakuwa na nchi mbili zenye mamlaka kamili - yaani kwa Kihaya inaitwa two sovereign states. Huo siyo muungano hata kidogo. Hapo muungano umevunjika.
 
2. Iwapo tunakuwa na confederate, nchi zetu zinaweza kuwa two sovereign states mbili lakini tukabaki kushirikiana kwenye mambo makuu kama sarafu, ulinzi, usalama, na uhusiano wa kimataifa. Hata hivyo, hili silo linaloombwa na akina Seif wanaoutaka huo muungano wa mkataba kana kwamba mingine haina mkataba.
 
3. Kwenye serikali kama alivyokuwa akihubiri Seif zamani, ama wanavyotoa maoni wengine kwenye Tume hivi sasa, kama vyama vya upinzani na wale waliokata tamaa na mfumo wa sasa na wasiotaka kuutaja kabisa mfumo wa serikali moja, ni kwamba hakutakuwa na two sovereign states, bali MOJA tu. Tunaweza hata tukawa na serikali kumi, lakini mambo makuu ndani ya nchi na mambo yote ya nje yatakuwa chini ya serikali ya shirikisho. Hili nalo akina Seif hawalitaki.
 
NB: Pendekezo la Chadema la kuwa serikali ya shirikisho iliyo dhaifu nalo sikubaliano nalo hata kidogo. Hakuna mantiki pale na nchi haiweze kuendeshwa. Inabidi serikali ya shirikisho iwe na nguvu kuliko viserikali viduchu vya Zenji na Bara.
 
4. Serikali mbili zinalalamikiwa na hivi sasa kuna ujinga wa kudhani kwamba serikali ya Muungano ni serikali ya Bara, sasa Wazanzibari wanafanya nini kwenye nafasi za Muungano, kama akina Bilal? Mfumo huu una tatizo sasa kutokana na udhaifu wa viongozi.
 
5. Serikali moja watu watapiga kelele kwamba Zanzibar inamezwa.
 
HITIMISHO: Akina Seif wanataka kila kilichomo kwenye Muungano na kila kilicho nje ya Muungano. Hatima yake ni moja kati ya hizi: Muungano kuvunjika halafu tukaanza kulumbana kwenye mengine AU Muungano kubakia halafu tukaendelea kuzozana. Dawa yake watu tuwe wakweli na tuache tamaa na ubinafsi.
 
Matinyi.
 
Date: Sun, 13 Jan 2013 11:08:01 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: [wanabidii] KAKA MATINYI: KOTI LA MUUNGANO LATUBANA SANA - lipanuwe kidogo!
To: matinyi
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment