Sunday 13 January 2013

RE: [wanabidii] KAKA MATINYI: KOTI LA MUUNGANO LATUBANA SANA - lipanuwe kidogo!

Turejee kwenye ukweli.
 
1. Iwapo kila nchi itajiamulia mambo yake yenyewe, ndani na nje, hapo tunakuwa na nchi mbili zenye mamlaka kamili - yaani kwa Kihaya inaitwa two sovereign states. Huo siyo muungano hata kidogo. Hapo muungano umevunjika.
 
2. Iwapo tunakuwa na confederate, nchi zetu zinaweza kuwa two sovereign states mbili lakini tukabaki kushirikiana kwenye mambo makuu kama sarafu, ulinzi, usalama, na uhusiano wa kimataifa. Hata hivyo, hili silo linaloombwa na akina Seif wanaoutaka huo muungano wa mkataba kana kwamba mingine haina mkataba.
 
3. Kwenye serikali kama alivyokuwa akihubiri Seif zamani, ama wanavyotoa maoni wengine kwenye Tume hivi sasa, kama vyama vya upinzani na wale waliokata tamaa na mfumo wa sasa na wasiotaka kuutaja kabisa mfumo wa serikali moja, ni kwamba hakutakuwa na two sovereign states, bali MOJA tu. Tunaweza hata tukawa na serikali kumi, lakini mambo makuu ndani ya nchi na mambo yote ya nje yatakuwa chini ya serikali ya shirikisho. Hili nalo akina Seif hawalitaki.
 
NB: Pendekezo la Chadema la kuwa serikali ya shirikisho iliyo dhaifu nalo sikubaliano nalo hata kidogo. Hakuna mantiki pale na nchi haiweze kuendeshwa. Inabidi serikali ya shirikisho iwe na nguvu kuliko viserikali viduchu vya Zenji na Bara.
 
4. Serikali mbili zinalalamikiwa na hivi sasa kuna ujinga wa kudhani kwamba serikali ya Muungano ni serikali ya Bara, sasa Wazanzibari wanafanya nini kwenye nafasi za Muungano, kama akina Bilal? Mfumo huu una tatizo sasa kutokana na udhaifu wa viongozi.
 
5. Serikali moja watu watapiga kelele kwamba Zanzibar inamezwa.
 
HITIMISHO: Akina Seif wanataka kila kilichomo kwenye Muungano na kila kilicho nje ya Muungano. Hatima yake ni moja kati ya hizi: Muungano kuvunjika halafu tukaanza kulumbana kwenye mengine AU Muungano kubakia halafu tukaendelea kuzozana. Dawa yake watu tuwe wakweli na tuache tamaa na ubinafsi.
 
Matinyi.
 

Date: Sun, 13 Jan 2013 11:08:01 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: [wanabidii] KAKA MATINYI: KOTI LA MUUNGANO LATUBANA SANA - lipanuwe kidogo!
To: matinyi@hotmail.com; wanabidii@googlegroups.com

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad leo amekutana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kutoa maoni yake binafsi kuhusiana na mtazamo wake juu ya katiba mpya ya Tanzania ambapo amesema koti la Muungano linawabana wazanzibari kwa sasa wanahitaji kubadilishiwa jengine la kiasi chao."Koti la Muungano sasa linatubana sana, na kwamba tunahitaji kushona koti jipya kulingana na hali zetu za sasa", alisema Maalim Seif mbele ya tume ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.Maalim Seif ambaye amekuwa kiongozi wa Kwanza mashuhuri kukutana na tume hiyo katika utaratibu wa ukusanyaji wa maoni amesema katika kipindi cha miaka 49 ya Muungano bado hakujakuwa na nia njema ya kutatua kero za Muungano, hali inayopelekea kuongezeka kwa kero hizo na kuleta usumbufu kwa wananchi hasa wa Zanzibar.
Amesema kutokana na hali hiyo ni vyema muundo wa Muungano ukaangaliwa upya, na kusisitiza msimamo wake wa kuwepo Muungano wa Mkataba ambapo kila nchi itakuwa na mamlaka yake kamili ndani na nje ya nchi na baadae kushirikiana katika mambo ya msingi ambayo yataamuliwa na pande hizo mbili.Maalim Seif ambaye ametoa maoni hayo nyumbani kwake Mbweni Zanzibar amefahamisha kuwa muundo wa Muungano wa serikali mbili uliopo sasa hauwezi kutatua kero za Muungano baada ya kuwepo kwake kwa kipindi cha miaka 49 bila ya kuonyesha mafanikio ya kuridhisha ya kutatua kero hizo.
Amesema katika kipindi hicho tume na kamati kadhaa zimeundwa katika kushughulikia kero za Muungano, lakini mafanikio yake ni madogo, hali inayotia wasiwasi wa kuongezeka kwa kero hizo badala ya kutatuliwa.
Amefahamisha kuwa Zanzibar imekuwa muathirika mkubwa wa Muungano uliopo hasa katika Nyanja za kiuchumi na siasa, baada mshirika wake wa Muungano (Tanganyika) kutoweka, na kutumika jina la Tanzania kwa maslahi ya upande mmoja wa Muungano.Maalim Seif anatarajiwa kukutana na waandishi wa habari hapo kesho katika hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar, ili kuyatolea ufafanuzi maoni hayo na kuyaweka bayana kwa wananchi wote maelezo yake aliyoyatoa katika tume ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Source: ZanzibariYetu



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment