Friday 18 January 2013

Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHA

Thank u!!
 
And hopefully soon, i will master the language
 
for now i translate and follow through the discussions.
 
you have brilliant minds here!!

2013/1/18 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Karibu bwana Gugu, hapa pako moto kwelikweli.... tutafurahia michango yako kwa maendeleo na faida ya wanajukwaa na watanzania kwa ujumla.
K.E.M.S.
 
From: Gugu Ndima <gugundima@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, 17 January 2013, 5:46

Subject: Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHA
Greetings all,
 
I hope u are well, my name is Gugu , I just joined the forum.
 
I read some of your posts, quiet intruiging indeed
 
pleasure to make your acquaintance !
 
I am in South Africa  
 

2013/1/17 Joseph Kulangwa <kulangwa@yahoo.com>
Hahahaaaaaaa chezea Azaveli wewe! Hata kama kuna upungufu ktk CDM watu wanyamaze, hata kama wananyanyaswa watulie! Eti waombe ushauri kwa Mkumbo! Kwa hiyo yoote yanayotokea nchini ya watu kupoteza maisha, kuteswa, ajali mbalimbali, nia ni kuisambaratisha CDM kweli Dokta? Makubwa!

--- On Thu, 1/17/13, Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com> wrote:

From: Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com>
Subject: RE: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, January 17, 2013, 12:50 AM

Mimi kama CCM- Mfu napata taabu kumwamini mtu anayetaka kukibomoa Chadema kwa sababu yoyote hile kwa kipindi hiki. Wapo  ambao walikuwa tayari kutoa roho ya Dr Stephen Ulimboka ilimradi wakibomoe Chadema kwa kukisingizia eti kuwa mfadhili wa mgomo ya madakatri. Wapo waliopanga mipango iliyosababisha kifo  cha kikatiri cha Mwandishi Daudi Mwangosi mipango ambayo lengo lake lilikuwa kukisambaratisha Chadema kwa kumuua Dr Slaa ili fujo zikitokea kumlilia sababu ziwepo za kukifuta Chadema. Leo hii mtu eti afukuzwe Umoja wa Vijana wa Chadema halafu eti hasira zake za kufukuzwa hata kama si kwa haki aziweke juu ya umuhimu wa kuzuia kukisambaratisha Chadema ili wananchi wawe na chama mbadala ya CCM. Huyu kweli anauchungu na wanachi wa nchi hii? Kuita waandishi wa habbari ambao vyombo vyao vilivyo vingi ni vya CCM na kuporomosha maneno ya kejeli na kukosa staha dhidi ya Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Slaa inawezaje ikawa na maslahi kwa Chadema ? Si hata mtoto mdogo atajua huyu anatumikia maslahi ya CCM hata kama anaendelea kujinadi eti M/Kiti wa Umoja wa Vijana Chadema. Si angekaa kimya au ajiunge na CCM  moja  kwa moja? Kimantiki sielewi huyu ndugu yangu anadhani haya aliyoyaporomosha  na kuruhusu yarushwe kila siku na vyombo vya habari vyenye ushabi na CCM yatasaidia sana kweli kukisambaratisha Chadema? Historia muda simrefu itamwonyesha hajaijua vizuri historia!!! Hata TANU ilikuwa na matatizo mengi lakini watu makini walivumilia yote ili ukombozi upatikane!! Ndani ya Chadema  kuna matatizo mengi lakini watu makini wanayavumilia yote ili ukombozi upatikane!!! Nina msikitikia huyu kijana anayeporomosha maneno yakukisaidia CCM kukisambaratisha Chadema bila kujua Chadema sasa  ni kama TANU akitasambaratika kirahisi hivi!!! Mimi  mama  yangu  huko Bukoba alikuwa CCM  damu damu  siku za karibuni ukimuuliza nani ni Nyerere wa  leo  anakujibu Dr Slaa!! Halafu wewe  unaangaika kusambaza hiyo sumu ya ukanda na ukabila ukidhani itakisambaratisha Chdema leo hii? Kama kijana huyu aliona umeonewa  na akina Heche si angeomba ushauri kwa watu makini kama Dr Kitila Mkumbo kuona kitu cha kufanya chenye  kutanguliza masilahi ya Chadema na  ya Watanzania wanaotamani CCM king'olewe hata kama Chadema kina  mapungufu kiasi gani? Inasikitisha lakini inawafurahisha watetezi wa CCM kubaki madarakani milele!!! Mwl. Lwaitama 
Date: Thu, 17 Jan 2013 10:11:04 +0300Subject: Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHAFrom: mngonge@gmail.comTo: wanabidii@googlegroups.com Haki gani?
2013/1/16 gloryk kimenye <glorykkimenye188@hotmail.com>
Mungu atakusimamia Shonza haki yako utaipata tu.
Date: Wed, 16 Jan 2013 00:45:14 -0800From: anthony_masare@yahoo.comSubject: Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHA To: wanabidii@googlegroups.com
huyu dada shonza ni mnafiki mkubwa haya yote aliyosema hapa mbona hakusema akiwa ndani ya chama?amefukuzwa ameaanza kutapatapa tumpuuze mtu kama huyu hana nia njema na chama naamini sasa kweli huyu mtu ni kibaraka (mamuluki)

--- On Tue, 1/15/13, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, January 15, 2013, 10:05 AM

TAMKO LA KUTOA UFAFANUZI DHIDI YA TAARIFA BATILI ZILIZOZALISHWA NAMWENYEKITI WA BAVICHABWANA: JOHN HECHE [WEGESA CHARLES SUGUTA] KUHUSU KUVULIWA UANACHAMA WABAVICHA, NA KUSHABIKIWA NA MH. FREEMAN MBOWE, MWENYEKITI CHADEMA TAIFA Nawashukuru sana wanahabari, kwakuchukua muda wenu kuja kunisikiliza.Natambua mnakiu ya kusikiliza mambo mengiya kuwaeleza kutokana nataarifa zilizosambaa kuhusu hiki kichefuchefukinachosambazwa kwamakusudi na virusi vichache vilivyojivika ngozi yaukombozi. Nimepokea simu nyingi kutoka kwawatu mbalimbali kutoka ndani na nje yaTanzania wakitaka kupata ufafanuzi baadaya kupata taarifa kupitiavyombo vya habari kuwa nimevuliwa uanachama naU-Makamu Mwenyekiti waBAVICHA Taifa.Kama mlivyo ninyi, nami pianimeyasikia hayo kupitia vyombo vya habari, maana sijapata barua au mawasilianoyoyote toka kwaMwenyekiti wa BAVICHA, Ndugu Wegesa Suguta (John Heche)aliyetoa tamkohilo.Kwanza kabisa naomba kuweka wazikwamba sijawahi pewa shutumazozote au mashitaka yoyote yale yanayohusiana nahicho alichokiongea.Niliamua kupuuzia kwa sababunamjua Heche ni mlopokaji, kiongozi asiyejua wajibu wake, anayetumikiawasiomchagua, mtu asiye na malengona mtegemezi wa siasa ili kuendesha maishayake na ya familia yake. Pianilimpuuza kwa sababu najuasio Mwenyekiti aliyechaguliwa kidemokrasia,aliwekwa kwa matakwa ya wakubwazake ambao wanamtumia kwa malengo yaliyokusudiwa, ikumbukwe kuwa vijana watatu,Habibu Mchange, MtelaMwampambwa na Grayson Nyakarungu walienguliwa kimizengweili Hecheashinde, hivyo kwetu sisi yeye ni sawa na Mwenyekiti wakuteuliwa.Hivyo sikumjibu mtu asiyekuwa na sifa sawa na zangu katika harakati za kusakademokrasia ya kweli.Lakini kitendo cha Mwenyekitiwangu, Mh. Freeman Mbowe kujitokezakupitia gazeti mojawapo na kudai madaiyangu ni ya kitoto,kwanza kimenifedhehesha, ni dharau kwa vijana walionionanina sifa naukomavu na kunipa kura nyingi ili niwe Makamu Mwenyekiti waBAVICHATaifa.Pili ni kama anahalalisha kikaobatili, kilichokiuka kanuni na katiba ya CHADEMA ili kuhalalisha matakwa yaoyenye lengo la kuminyademokrasia na uhuru wa kujieleza ndani ya chama.Tatu anahalalisha hoja za vijana,ambazo ndio uhalisia kuwa Hechehakuwa na sifa, na uwezo, hivyo alibebwa na Mh.Mbowe ili akae pale kwa malengo yake.Ndio maana nilisema ukionakifaranga kimepanda juu ya figaujue mama yake yuko chini, hivyo mama yakekifaranga kajitokezakuhalalisha kifaranga chake kupanda juu ya figa.MADAI YAALIYODAI MH. MBOWE KUWA NI YA KITOTONiseme wazi kwamba nimesikitishwamno na madai aliyoyatoa Mwenyekiti wangu wa CHADEMA MhFreeman Mbowe kupitiagazeti la Mtanzamia la tarehe 12/01/2013 kwambamadai yangu ni ya kitoto .Kwanza niweke wazi kabisa kwambanamuheshimu sana Kiongozi wangu huyumkuu ambaye ndiye alipaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikishakwambahaligawi baraza la Vijana na chama kwa ujumla, ahakikishe kunautawala borandani ya chama, na utendaji haki, lakini cha kushangaza ameibuka kumtetea Hechekwa hoja za mwegemeo wa upande mmojabilakuangalia maelezo ya upande wa pili.Niweke wazi kabisa kwamba kaulialiyoitoa dhidi yangu ni yakiushabikimaana kama ni madai yangu kuhusu namna ninavyohujumiwakupitia kwa Katibu Mkuu yeye anayo nakala ya malalamiko [ushahidi upo],lakinihakuna hatua ambayo ameichukua.Namshangaa Mwenyekiti kudai madaiyangu ni ya kitoto sasa sijui nimadaiyapi anayazungumzia ? madai ya kitoto ni yapi? na madai ya kikubwa ni yapi ? naje madai ya kitoto ni haya mimi kuhoji kwaninihatuweki akiba kwenye akauntikwa ajili ya uchaguzi 2015 kamatulivyokubaliana kwenye baraza kuu mara baadaya uchaguzi wa2010.Naombaniwajulishe wanachadema kuwa, nimejitahidi sana kushaurijuu ya1; Uanzishwaji wa chuo chamafunzo ya uongozi kwa makada wa CHADEMA ,badala yake ni matumizi mabaya yafedha za ufadhili wa wadau tofauti nahasa mfadhili mkuu ndugu SABODO. Hiiingesaidia pia kulea ki-mfumo wa maadili ya uongozi kwa vijana wa umoja wawanafunzi wa CHADEMA wa vyuovikuu yani " CHASO" ambapo mimi ni mwasisi wamkakati huu nchini.2; Chama kwa ujumla kutokuwa na jengo letu na hasa makao makuu yetu.Niaibu kwa chama kikubwa kama CHADEMA kuwa na ofisi tulizopanga na kulipa mamilioni ya fedha za ruzuku na misaada kwa manufaa yaMwenyekiti Freeman Mbowena Mkurugenzi wa fedha wanaomjua mmiliki wajengo la makao makuu. Kimsingi mimi natambua chama kina uwezo mkubwawa kuwa na majengo yetu. 3; Kupunguza mshahara wa katibumkuu Ndugu Dk. Slaa ambao ni zaidi yamilioni saba kwa mwezi na marupurupu kibao ili pesa hizo na mamilionizielekezwe kujenga chama mikoani kama kweli tunataka2015 tuingieIkulu.4; Kuhakikisha pesa zilizochangishwa kwenye M4C zinatumika ipasavyo nasi kama zitumikavyo kipindihiki ambapo ni kama tumelewa wingi wa watukwenye mikutano ya hadhara. 5; Kitendo cha Mwenyekiti wa chama kufumbia macho hatua ya ndugu Slaa(katibu mkuu) kujikopesha pesa ya ruzuku ya watanzania zaidi yashilingi milioni mia na arobaini.6; Hatua ya mwenyekiti ndugu Heche kulipwa mshahara na marupurupu hali kanuni za chama haziruhusu huku Mbowe akifumbia macho wakati viongoziwa mikoa na wilaya hawapewi pesa na vifaa vya uenezi.7; Kitendo cha mchumba wa Dk.Slaa, Josephine Mushumbusi kuzungukamikoani na kulazimisha kupokelewa kama mke wa mfalme na kuendesha vikao vya ndani na mikutano ya hadhara yenye kulenga kuwajengawagombea ubunge anaowataka yeye na katibu mkuu kwa mwaka 2015.Ndugu wanahabari, je hizi ndo hojaza kitoto anazodai Mh. Mbowe? Hivyobasi namtaka Mh. Mbowe sasa asikimbiliekujibu hoja kiushabiki.Ajitahidi kuwa na fikra na Busara ili kukisaidia chama kuvuka kwenyedaraja la sasa la pepo kufukuzana. Atambue Baraka anazozitoa wanachama wafukuzwe hovyo na kunyanyaswa ni hatari kwa kuwa anaandaa kundi kubwanje ambalo litageuka mwiba siku za usoni.UHALISIA ULIOPO:Ndugu waandishi wa habari,Naomba kuweka wazi kwamba mimi Juliana Shonza ni Makamu Mwenyekiti halali wa baraza la vijana (BAVICHA). Taarifa zozote zile mlizozisikiakuhusu kuvuliwa kwangu uanachama, naomba kwa nguvu moja kupitiataaluma yenu muwaambie watanzania kwamba wazipuuze. Ni taarifazilizotolewa na kikundi cha kihuni kilicholenga kutimiza matakwa ya wakubwa wao. Kikundi hicho hakina mamlaka ya kikatiba yoyote yale yakunivua uongozi huunilio nao.Kuthibitisha hilo kuwa ni kikundimufilisi, hadi ninapoandika warakahuu kwenu sijapewa barua yoyote ile inayonitaarifu kuwa nimevuliwauongozi wangu. Hii ni wazi wanatambua kuwa wanachemka, wanatengenezamakundi kwa maslahi wanayoyaona yanawafaa.Sikuchaguliwa ili niwe chombo cha kuwatumikia watu, na badala yake nilichaguliwa ili niwatumikie vijana waCHADEMA na watanzania kwaujumla, na pale nilipoona kuna ukiukwaji na kuhoji ndio chanzo chamizengwe na matamko ya Ndugu Wegesa (John Heche).Nimekuwa nikiwasumbua viongozi wenzangu kuhusu kutengeneza kadi za BAVICHA na kusajili wanachama katika mfumo mzuri (database) ili tuwena kumbukumbu ya wanachama wetu lakini yote yameshindikana kwasababuamekuwa akiendeshwa na mfumo dume kandamizi kwa mwanamke, mara nyinginimemshauri kwa ajili ya maendeleo ya Baraza na nimekuwa nakwamishwa na Mwenyekiti na Katibu na hata leo sisi wote ni wanachama kwakufikirika (imagination), kwa kuwa bado hatuna kadi za uanachama kwavijana wa BAVICHA zaidi ya kutambulika na katiba ya chama.KUKIUKWA KWA KATIBANdugu wanahabari, ni wazi kuwakatiba pamoja na mwongozo wa baraza letula vijana bavicha ulikiukwa katikakikao walichokiita kamati tendajiiliyokaa tarehe 05/01/2012 ambayo iliongozwa na Bwana Wegesa Suguta (John Heche) kama Mwenyekiti, hali inayonilazimu kusema wazi, bilakumung'unya maneno kwamba maamuzi yaliyotolewa na kikao hichoyalikwishapangwa na viongozi wa kitaifa hayakuwa halali. Nasisitizakwamba ni ukweli ulio wazi kwamba agenda na maazimio ya kikao hicho yalikwisha amuliwa hata kabla ya kikao hicho kwasababu kubwa mbili:1; Taarifa za kufukuzwa kwetuzilikwisha anza kusikika kwenye mitandaoya kijamii kama vile jamii forum nafacebook mwezi mmoja kabla ya kikao cha kamati tendaji batili.2; Pili ushahidi wa kimazingirakwa maana ya ukiukwaji mkubwa wakikatiba na mwongozo wa Baraza letu la Vijana uliofanyika siku yakikao.Ndugu wanahabari,Ikumbukwe kuwa pamoja na uwepo wa taarifa za kikao mwezi mmoja kablabinafsi nililetewa taarifa hizo siku mbili kabla ya kikao, tena kwanjia ya ujumbe mfupi wa maandishi {sms} na baadae kupigiwa simu na Katibu wa Baraza Bwana Munishi ikinitaka kuhudhuria kikao hichokutokana na kuwa nje ya Dar-es –salaam kwa mambo ya kifamilia zaidiniliwataarifu viongozi wenzangu kwa utaratibu maalumu wa mawasilianoya kiuongozi kwa maana ya kuwatumia barua ya udhuru wa kutohudhuria kikao.Lakini cha kushangaza na kustaajabisha kwa viongozi wenzangu hawaambao kwa namna moja ama nyingine napata ugumu wa kuelewa kama kweliwana sifa za kuitwa viongozi tena wa idara nyeti sana katika ustawi wa chama chetu, kwa makusudi kabisa ama kwa kutumwa kufanya hivyo ama kwautashi wao mdogo wa kiupembuzi yakinifu waliamua kuvunja na kukiukakatiba ya chama na kujipa vyeo vya kiunyampara kwa kuamua kuchukuamaamuzi ya kutuvua uanachama wa kufikirika wa baraza mimi na vijanawenzangu Ndugu Mwampamba na Mchange ambao nao hawakupewa nafasi yakusikilizwa, ambao moja kwa moja tunapoteza sifa yakuwa wanachama wa CHADEMA.Ndugu wanahabari,Naomba sasanijikite katika katiba ya chama changu na mwongozo wabaraza la vijana sura ya sita kipengele cha 6.5 ambacho kinasemataratibu zifuatazo lazima zifuatwe katika kuchukua hatua za kinidhamu. 6.5.2 kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na .4.4 ya katiba, mwanachamayeyotehatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa amakufukuzwa uanachama bila kwanza{a} kujulishwa makosa yake kwamaandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.[b] kupewa nafasi yakujiteteakatika kikao kinachohusika.{c} Mwanachama atajulishwa kwamaandishi uamuzi wa kikao mnamo wikimbili baada ya kusikilizwa.Ndugu waandishi wa habari,Nisemewazi kwamba hakuna kifungukilichofatwa kati ya hivyo niliyoviainisha hapo juu,hakuna baruayeyote niliyojulishwa ya hayo waliyoyaita mashitaka yangu zaidi yakuyasoma na kuyasikia kwenye vyombo vya habari baada ya wao na kikao chaoharamu kuchukua maamuzi yakunivua uanachama wa Bavicha .Sikupewa nafasi yakujitetea maanasikuwepo kwenye kikao, barua yaudhuru wakutohudhuria walikuwa nayo. Na vilevile mpaka leo hiisijajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao hicho batili badaa yake viongozi wenzangu hawa wameamua kuujulisha umma wa Watanzania nawanachadema kwa ujumla pasipo kunijulisha mimi kwanza. Ukiangalia piakifungu cha 6.5.6 cha katiba kinasema KIONGOZI YEYOTE hatachukuliwahatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi.Sasa basi namtaka Bwana Wegesa Suguta awaeleze umma wa watanzania kamaalivyokurupuka kuwaeleza kwamba Shonza amevuliwa uanachama wa Chademani wapi na lini yeye kama Mwenyekiti nilipewa barua ya hayowanayoyaita mashitaka, na ni lini niliwapa majibu ya mashitaka hayo.UHALALI WAKIKAO CHA KAMATI TENDAJINdugu wanahabari, Ikumbukwe kwambakikao cha juu kuliko vyote kwenye ngazi ya chamahusika ni Mkutano Mkuu ambao ndio ulioniweka madarakani kutokananakuwa na imani na mimi na kikatiba ndiohaswa ulipaswa kuniandikiamashitaka, kunijadili, kunihoji na kutoa maazimio ambayo yangepelekwa kamati kuu ambao kimsingi ndiyo yenye mamlaka ya mwisho yakumvua mtuyeyote uanachama wake baada ya kujiridhisha na taarifa na uchunguzikutoka kwenye kikao husika kilichomwandikia mwanachama mashitaka nakumuhoji. Ndugu wanahabari ifahamike wazikwamba kikatiba kuna ngazi mbili tuzinazoweza kumvua mtu uanachama wake ambazoni ngazi ya tawi na ngaziya kamati kuu.Hivyo basi namtaka sasa Bwana Wegesa Suguta auambie umma wa watanzaniakwamba ni lini kamati tendaji ya vijanailigeuka ama kukaimishwamadaraka ya ngazi ya tawi, ngazi ya mkutano mkuu amakamati kuu yakuwana uwezo wakumvua kiongozi uanachama wake?Ndugu waandishi wa habari, Wajumbe wa kamati tendaji kikatiba ni makatibu wa kamati za uratibu zamikoa lakini badala yake Bwana Wegesa Suguta (John Heche) amekuwaakiwaita wenyeviti wamikoa na sababu kubwa ikiwa ni kwamba wengi wawenyeviti hao hawastahili kuwepobavicha kutokana na kwamba umri wao kuwa zaidi ya miaka 35 hivyo kupoteza sifa za kuwa viongozi wa BAVICHAambayo katiba inamtaka mwanabavicha yeyote kuwa namiaka 18-35, hivyobasi kwa kuhofia kupoteza nafasi zao hulazimika kukubaliana na lolotelile ambalo bwana Wegesa Suguta analitaka hata kama wakijua kwamba ni kinyume kabisa na matakwaya katiba na mwongozo wa baraza.Hivyo kumpa Heche mwanya wakuamua lolote lileanalotaka ama kutumwakulifanya. Kutokana na hilo natangaza wazikwamba kikao cha kamatitendaji kilichopita ni batili, chenye wajumbe batili, kimesimamiwa naviongozi batili kwa maana ya mwenyekiti na katibu wake maanawameshindwakuheshimu misingi ya kikatiba katika namna ya demokrasia ya chama chetu hivyo basi nachukua nafasi hii kuutangazia umma wawatanzania na wanachadema kwa ujumla wao kwamba maamuzi ya kamatitendaji yaliyotangazwa na kiongozi kilazana daraja la viongozi wa juubwana Wegesa Suguta ni batili. Ndugu wana habari,Sifa ya Mwalimu ni kuweza kubadilisha hali ya umbumbumbu wa wanafunziwake, Heche kama kiongozi, na Mwalimu kitaaluma (nina wasiwasi naufaulu wake katika huo ualimu) alipaswa kuwa mfano bora kwa vijana wa Chadema kuwaelekeza na kuwafundisha namna ya kuheshimu misingi yakikatiba ambayo kama chama na baraza tumejiwekea na tunapaswa kuifuatani wazi kuwa Heche ameshindwa kuwa mfano bora kwa vijana, hajui kanuniza BAVICHA wala katiba ya CHADEMA, mkurupukaji, mropokaji, mwenyeuwezo mdogo wa kufikiri, dikteta anayetumia mamlaka asiyokuwa nayo(akipewa mamlaka atatuchinja huyu) hivyo hafai kuwa hata Mwenyekiti wa serikali za mtaa, wala kuaminiwa popote kupewa nafasi ya kiuongozi. Niwazi ubongo wake yeye nakatibu baraza bwana Munishi haujapewa toharala kisiasa, ifike mahali wakubali kufundwa unyagoni na manyakanga wakisiasa. KUHUSUKUVULIWA UANACHAMA WA BAVICHA;Ndugu wanahabari,Kuhusu kuvuliwauanachama wa Bavicha ambao moja kwa moja napoteza sifaya kuwa mwanachadema namshangaa kiongozi huyu ambaye sifa yake kuusiku zote ni ukurupukaji kwa kusema kwamba nimevuliwa uanachama wa Bavicha huku akijua wazi Bavicha haijawahi kuwa na kadi za baraza.Katika mwongozo wa baraza lavijana kipengele cha 4.4 KUJIANDIKISHAUANACHAMA 4.4.1 inasema ili kijanaaruhusiwe kujiunga bavicha ni lazimaawe na sifa zifuatazo[a] Awe mwanachama wa CHADEMA[b] Awe na umri kati ya miaka 18 na 35[c] Awe anakubaliana na misingiya mwongozo wa BAVICHA4.4.2 Inasema kijana aliyekidhimatakwa hayo hapo juu, atanunua kadi ya uanachama wa BAVICHAKutokana na kipengele hicho namtaka bwana Wegesa Suguta auambie ummawa watanzania na wanaCHADEMA kadi yake yeye ya baraza la vijana ninamba ngapi na aliichukulia wapi? Aueleze umma wa watanzania kadi yangu ya baraza la vijana ni namba ngapi na niliichukulia wapi?Ndugu waandishi wa habari,Nidhahiri baraza la vijana chadema hatuna kadi ambayo kimsingi ndiyoutambulisho wa mwana BAVICHA endapo akishakidhi sifa zilizoainishwa hapo juu. Na ni wazikwamba vijana wote wa CHADEMA tuna sifa za kuwawana Bavicha lakini si wanachama wa BAVICHA kutokana na kwambanimekuwa nikimwambia mara kwa mara umuhimu wa kuirasimisha nakuianzisha ili iwe taasisi kamili kwa kuwa na kadi za vijana kamamwongozo wa vijana unavyojieleza.UELEWA WANGU KUHUSUKUNDI ANALOLIITA NDUGU WEGESA SUGUTA (JOHN HECHE)NI "MASALIA"Ndugu waandishi wa habari,Hakuna kundi linaloitwa masalia ndani ya Chadema na BAVICHA. Gazeti la MWANAHALISI ndilo lililoandika kuwa vijana wote waliofutwa nakuondolewa kwenye uchaguzi wa BAVICHA mwaka 2011 ni MASALIA ya Zittoyanayopukutishwa Chadema. Kimsingi gazeti hili lilikuwa linafanya kaziyake ya kipropaganda ndani ya CHADEMA ili kukigawa Chama. Lilikuwa linatimiza wajibu wake wa kupika mpasuko ndani ya chama tena kwakuhusisha na viongozi wakubwa ndani ya chadema.Ni aibu kubwa sana na ni hatari kuona kiongozi kama Wegesa Sugutaanakuwa mstari wa mbele kushabikia neno masalia, huku akijua wazi kufanya hivyo ni kuligawa baraza la vijana. Kwa nguvu moja nalaanikitendo hiki cha kipuuzi kinachofanywa na Mwenyekiti huyu wa BAVICHAcha kuchekelea upuuzi uliopikwa na gazeti la MwanaHalisi. Naombaatumie rasilimali za chama kujenga umoja wa vijana imara, tushirikianekuimarisha Bavicha yenye tija kwa chama na sio kusherekea mpasukondani ya baraza la vijana. UELEWA WANGU KUHUSU KITU KINACHOITWA PM7Ndugu waandishi wa habari,Naomba kunukuu maneno ya mtu maarufu sana mitandaoni na kwenye uga wahabari Mzee Mwanakijiji anasema"Uongozi imara sio kutegeana, kunyemeleana na kufukuzana. Uongozi imara ni kushirikiana".PM7 ni jina lenye maana ya "PATRIOTIC MOVEMENT" yaani harakatizakizalendo kwa mujibu wa Ndugu Ben saanane ambaye alitumwa na kiongoziwa juuwa chama kuja kulitekeleza kwa vijana walioenguliwa kwenye uchaguzi wa BAVICHAmwaka 2011 na wanaoonekana kusigana na kiongozihuyo kimawazo. PM7 ni wazoliliobuniwa na kiongozi mmoja wa juu wachama akishirikiana na Ben saanane wakinuia kutega mtego wa kuwanasavijana wanaoonekana wapo tofauti kimawazo nakiongozi huyo wa chama.Kwa kuwa wazo hilo lilikuwahalina manufaa kwa chama, halikutekelezwa.Kiongozi huyo bila kumung'unya maneno ameamua kuwatumia vijana haokuandaa kikao batili cha kamati tendaji ya John Heche ili awafukuze vijana hao. Hii ni hatari sana kuona kiongozi wa chama unageuka simbana kuanza kuwawinda watoto wake ili uwamalize kisiasa kwa sababu zakobinafsi.MAAJABU KATIKAMEDANI ZA SIASA ZA BAVICHA MWAKA 2013 Ndugu waandishi wa habari,1. Hii ni ajabu sana katika kikaocha kamati tendaji batili, Ambaohatukuhojiwa ni watu wawili, mimi Juliana Shonzana kijana mmojaanaitwa Exaud Mamuya. Lakini Mimi Juliana Shonza nimehukumiwa bila hata kusikilizwa wala kupewa mashitaka na chombo chochote katikachama. Wakati huo huo Exaud Mamuya hajahukumiwa kwa madai hakufikakwenye kikao. Hii ni dhahiri huu ni mkakati wa kipuuzi ambaounaendeshwa na watu wapuuzi tena kwa misingi ya kikabila na kikanda.2. Muasisi mwenza wa PM7 na kibaraka wa kiongozi wa juu wa chamaaliyetumika kutoa shutuma chafu kwa Naibu Katibu Mkuu. Kijanaanayefahamika kwa jina la Ben Saanane ameachwa kwa madai yeye amekiri mbele ya hiyo kamati tendaji kwamba ni kweli alinuia kumchafua NaibuKatibu Mkuu wa chama na kukivuruga chama. Wakati tuhuma zakezinafananana za Mchange na Mwampamba.3. Mkakati wa John heche navibaraka wake umejikita kutukuza ukanda ndani ya chama tena wa wazi wazi.Ukanda huu umejidhihirisha kwenyekutoa hukumu batili za tuhuma kama ifuatavyo.Vijana waliohukumiwa wote niwale wanaotokea Mbeya, Mbozi na Kibaha.Wakati Vijana wa Kilimanjaro wameachwa kwa madai wao wametoa ushirikiano.Waliohukumiwa ni:_Mtela Mwampamba-Mbozi, Mbeya_Habib Mchange-Kibaha, Pwani-Juliana Shonza-Mbozi, Mbeya-Joseph Kasambala – Mbeya mjini (kasimamishwa)- GWAKISA Mwakasendo –Rungwe, Mbeya (kasimamishwa)Pamoja na wanachama watatu waliopo Mbeya mjini waliofukuzwauanachama.Waliosamehewa ni:_Ben saanane-Kilimanjaro_Exaud Mamuya-Kilimanjaro.Hii ni dhamira ya wazi kabisa kwamba CHADEMA sasa ni chama cha kikanda, Viongozi wa CHADEMA wanatumika kutangaza ukanda kwawatanzania.Kwa maana hiyo wale wote wasio wa kaskazini ndani ya Chadematusitegemee kutendewa haki.MAMBO NILIYOMSHAURI HECHE NA KUMUONYA: Ndugu waandishi wa habari, Sisikama vijana tusigeuze siasa kuwa ajirawala chombo cha kuendeshea maisha, ni moja ya vikwazo katika kukuzademokrasia ya kweli, maana wengi wanaendekeza njaa na uhitaji wamaisha yao ili kupindisha ukweli. Moja ya maswali yangu kwa Mwenyekiti ni kitendo cha kubinafsisha garialilotoa Naibu Katibu Mkuu kwa ajili ya BAVICHA na badala yakeakalifisadi, akafanya mali yake binafsi na kumuweka Mdogo wake ChachaHeche kuwa dereva wake, nimekuwa nikipinga matumizimabaya yarasilimali hiyo kwa manufaa binafsi, na badala yake gari hiyoifanyekazi iliyokusudiwa, huu ni msingi wa kuonyesha tofauti yetu nawanaotumiarasilimali za serikali (Taifa) kwa manufaa binafsi nay a familia zao.Pia nilimshauri Mwenyekiti awe nakipato halali kama katiba ya chamainavyosema Sura 10 MAADILI YA VIONGOZI ibara ya 10 kifungu cha (6)kinasema Kiongozi anatarijiwa kujitosheleza yeye nafamilia yake kwa mapato halali ili kutokuwa ombaomba kwani tabia hiyo itadhoofishauwezo wake wa kutoa uamuzi sahihi, ili kuwa mfano bora wauwajibikajikwa vijana, kama ambavyo Mwalimu Nyerere alivyosema kipimo cha Utunikufanya kazi, badala yake ametelekeza taaluma ya ualimu, aliyotumia pesa za walipa kodi kwa kusoma na muda wote ni kupiga soga bilauzalishaji na kujipatia kipato halali, na badala yake anategemeamshahara usio halali kuishi, ni wazi Mwenyekiti ni cheo cha kisiasa nahatakiwi kulipwa mshahara, wala kulipiwa nyumba kwa mujibu wa kanuni.Badala yake majibu anafikiri ni kufanya njama na waliopindishataratibu hizo ili alipwe mshahara kwa maslahi yao ya kisiasa. Na tumekuwa tukilipinga hilo kwani tunataka tuwe mfano wa utawala borakwa vitendo na si maneno peke yake.MWISHO:Ndugu waandishi wa habari,Nipokwenye mchakato na wanasheria wangu kushughulikia swala la kumpeleka mahakani Bwana John Heche na gazeti la Tanzania Daima toleonamba 2958 kwa kuniita msaliti wa CHADEMA, natumiwa na CCM na kuwanina mahusiano (natumiwa) na Wassira tena bila kunihoji mimi JulianaShonza. Kwa maana hiyo wamenichafua na kunidhalilisha mbele ya umma wa watanzania.Pili naomba kuweka wazi kwambanatarajia kuomba ufafanuzi wa kikatibajuu ya shutuma zilizotolewa kwenye vyombo vya habari dhidi yangu nabwana Wegesa Suguta (John heche) ili aseme ni aminisho lipi lakuthaminisha na kusakidikisha mtazamo wa maono yake ili bongo zawatanzania zijue ukweli. Mimi Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA natangazarasmi Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni wanachama hai na halali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).Hivyo nawaomba waendelee na kazizao za ujenzi wa chama kwenye majimboyao na taifa kwa ujumla. Nawaomba wananchi na wanachama wote waCHADEMA waendelee kuwa na imani dhidi ya vijanahawa. Kama mlivyomwamini Mwampamba na kumpa kura 32000 na kama mlivyo mwaminiMchange na kumpa kura 10,400 kwenye uchaguzi wa Ubunge mwaka 2010.Vivyo hivyo naowaombamuendelee kushirikiana nao kuhakikisha wanatimizaadhima ya ukombozi mwaka2015. Wenu katika ujenzi wa demokrasia makiniJuliana Daniel ShonzaM/Kiti BAVICHA-Tanzania Bara.-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.comKujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.comInternational Jobs - www.jobsunited.blogspot.com  Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.   
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
-- Gugu Ndima+27 76 783 1516 -- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Gugu Ndima
+27 76 783 1516

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment