Wednesday 16 January 2013

Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHA *

Asante Meena. Sie tulio mbali na ambao kufikiwa kwetu na printed newspapers tunapata shida kweli. But anyways - Nashukuru sana kwa ufafanuzi. Mwananchi mnaheshimika sana - sitegemei mfanye kinyume!
Kim
  
On 1/17/2013 8:21 AM, nevilletz@gmail.com wrote:
Kama alivyosema Xn ilikuwa page five kutokana na umuhimu wake kwa maana ya vugezo vya kihabari!  Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania    -----Original Message-----  From: Ismael Kimirei <kiakimirei@gmail.com>  Sender: wanabidii@googlegroups.com  Date: Thu, 17 Jan 2013 08:10:03   To: <wanabidii@googlegroups.com>  Reply-To: wanabidii@googlegroups.com  Subject: Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti   BAVICHA *    unfortunately sipati printed copy. Natumia online version.      On Thursday, January 17, 2013 8:12:55 AM, nevilletz@gmail.com wrote:  
Mwananchi la jana kasome uone iko ukurasa wa ngapi!  Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania  ------------------------------------------------------------------------  *From: * Ismael Kimirei <kiakimirei@gmail.com>  *Sender: * wanabidii@googlegroups.com  *Date: *Thu, 17 Jan 2013 08:01:28 +0300  *To: *<wanabidii@googlegroups.com>  *ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com  *Subject: *Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu  Mwenyekiti BAVICHA *    Meena,  Uliyoyasema juu ya Dr Slaa yanapendeza. Yanatia moyo. Ila cha  kushangaza - huyo huyo Shonza ndo mmempa ukurasa wa mbele kwenye  gazeti lenu kama alivyoomba wakati wa mkutano na wanahabari - kuwa  mkaitangaze vizuri ile habari. Kwangu mimi ile kitu ameandika  haikustahili hata kuwekwa ukurasa wa pili au wa tatu - ningeiweka  katikati huko au karibu na mwisho.  Kim  On 1/17/2013 7:36 AM, nevilletz@gmail.com wrote:  
Mtu alikuwa mwanachama siku zote, leo kawekwa pembeni ndo anaamua  kusema kuhusu uozo, hapo the motive behind ni kutimuliwa kwake. Bado  ni binti mdogo, atulie atapata nafasi tena siku zijazo. Kwenda  hadharani na kuwasema viongozi wake wakuu wa Chama ni utovu wa nidhamu.    James Ole Millya alipotoka CCM kwenda Chadema hakuwahi kuwatukana  waliokuwa wakuu wake wa chama JK wala Mukama. Alieleza udhaifu wao na  udhaifu wa chama chake.    Dk Slaa ni mtu anayeaminika siyo ndani ya Chadema tu hata nje ya  chama hicho. Hana record yoyote ya ubadhirifu wa fedha tangu  alipokuwa TEC, Mbunge wala KM Chadema.    Akiwa Mwenyekiti wa LAAC alifanya kazi kubwa na hakuwahi kulala wala  kula kwa fedha za Halmashuri walikokwenda kukagua miradi, si mtoa  fedha kwa waandishi wa habari kama ilivyo kwa wanasiasa wengine,  haombi kuandikwa na vyombo vya habari bali vyombo hivyo humtafuta  kutokana na umuhimu wake.    Aliyoyafanya akiwa TEC kuanzisha Caritas Tanzania, miradi ya maji  kule Karatu na hata fedha alizoingiza pale CCBRT ni ushahid toka  kwamba siyo mbadhirifu wala mbinafsi. Mtu wa aina hii siyo rahisi  kuharibu credibility yake!    Kwa kauli za Shonza dhidi ya Dk Slaa, anajianika kwamba yeye ni mtu  wa aina gani!  Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania  ------------------------------------------------------------------------  *From: * Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>  *Sender: * wanabidii@googlegroups.com  *Date: *Wed, 16 Jan 2013 20:37:32 +0000  *To: *<wanabidii@googlegroups.com>  *ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com  *Subject: *RE: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu  Mwenyekiti BAVICHA *    Ndugu Wanabidii,    Haya makubwa, lakini tukubali au tusikubali kama haya hayapo siasa  hakuna. Changamoto ni sisi kuchambua ni zipi mbivu na zipi mbichi.    Cheers    Herment    ------------------------------------------------------------------------  Date: Wed, 16 Jan 2013 14:05:54 -0600  Subject: Re: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu  Mwenyekiti BAVICHA *  From: ngonzy@gmail.com  To: wanabidii@googlegroups.com    Sijui chama hakina taratibu za kushugulikia haya mambo? Yanakera  kweli kuyasoma    2013/1/16 Ireneus Kakuru Mushongi <ireneuskakurumushongi@gmail.com  <mailto:ireneuskakurumushongi@gmail.com>>        Bongo politics...!      Ngoma ya watoto haikeshi... Hivi hamna jinsi yoyote ya kumaliza      matatizo haya?      Mnadhani mnatengeza picha gani kwa mashabiki na wanachama wenu?      Nadhani mwenye timamu hatakuja kuanika mambo haya (yenu)      hadharani tena.      Kuna kubwa gani la kugombania hapa na mnamwakilisha nani?      Kwa hali hii tutarajie ngumi kwenye kikao chochote      kitakachokutanisha makundi haya..      Na huo ndio utakuwa mwisho wa Chdm. Na ushindi mwororo upande wa      pili..      Tafakari..ongozweni na busara, si jaziba matusi na maslahi binafsi..      SIjamwona aliyetumia busara hadi hapo na zaidi tutarajie makubwa      zaidi      UONGOZI UMESHINDWA KUMALIZA HAYA YA WATOTO HAWA NDANI YA CHADEMA      AU NI KWELI NAO NI SEHEMU YA TATIZO?      Siko kwa ajili ya kukosoa au kumfinger point mtu..ila nahisi hii      ni trela na kuna mengi nyuma ya pazia na isipotumika busara, ni      hatari tupu. Safari ya 2015 itabaki ndoto      Kama yale ya Mnara wa Babeli!      Ireneus      On Jan 16, 2013 11:45 AM, "Anthony Masare"      <anthony_masare@yahoo.com <mailto:anthony_masare@yahoo.com>> wrote:            Boxbe <https://www.boxbe.com/overview> This message is          eligible for Automatic Cleanup! (anthony_masare@yahoo.com          <mailto:anthony_masare@yahoo.com>) Add cleanup rule          <https://www.boxbe.com/popup?url=https://www.boxbe.com/cleanup?token%3D0W1YPooSTHaFxyy3tB519K%252BHCpV%252FigMONxLK5PYYn7guXek2LMZ7ER63%252BE5x8Kh%252FCcf6XGgdoJ9IVKmoP2YF5%252BeeR2zLRWsazm0WJ6r7rQsiXVq%252FwMzZo4zdSfX6ZKtuCpRegHBqj%252BK04Bl%252B9kiunA%253D%253D%26key%3DrF%252Fk1CEdZEzePFMmTvh4OamPeDznFfConO%252B3YtzlHcw%253D&tc=13356526385_63802074>          | More info          <http://blog.boxbe.com/general/boxbe-automatic-cleanup?tc=13356526385_63802074>              huyu dada shonza ni mnafiki mkubwa haya yote aliyosema hapa          mbona hakusema akiwa ndani ya chama?amefukuzwa ameaanza          kutapatapa tumpuuze mtu kama huyu hana nia njema na chama          naamini sasa kweli huyu mtu ni kibaraka (mamuluki)            --- On *Tue, 1/15/13, Juma Mzuri /<jumamzuri@gmail.com          <mailto:jumamzuri@gmail.com>>/* wrote:                  From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com              <mailto:jumamzuri@gmail.com>>              Subject: [wanabidii] Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu              Mwenyekiti BAVICHA              To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com              <mailto:wanabidii@googlegroups.com>>              Date: Tuesday, January 15, 2013, 10:05 AM                TAMKO LA KUTOA UFAFANUZI DHIDI YA TAARIFA BATILI              ZILIZOZALISHWA NA              MWENYEKITI WA BAVICHA              BWANA: JOHN HECHE [WEGESA CHARLES SUGUTA] KUHUSU KUVULIWA              UANACHAMA WA              BAVICHA, NA KUSHABIKIWA NA MH. FREEMAN MBOWE, MWENYEKITI              CHADEMA TAIFA                  Nawashukuru sana wanahabari, kwakuchukua muda wenu kuja              kunisikiliza.              Natambua mnakiu ya kusikiliza mambo mengiya kuwaeleza              kutokana na              taarifa zilizosambaa kuhusu hiki              kichefuchefukinachosambazwa kwa              makusudi na virusi vichache vilivyojivika ngozi yaukombozi.                Nimepokea simu nyingi kutoka kwawatu mbalimbali kutoka              ndani na nje ya              Tanzania wakitaka kupata ufafanuzi baadaya kupata taarifa              kupitia              vyombo vya habari kuwa nimevuliwa uanachama naU-Makamu              Mwenyekiti wa              BAVICHA Taifa.Kama mlivyo ninyi, nami pianimeyasikia hayo              kupitia              vyombo vya habari, maana sijapata barua au              mawasilianoyoyote toka kwa              Mwenyekiti wa BAVICHA, Ndugu Wegesa Suguta (John              Heche)aliyetoa tamko              hilo.Kwanza kabisa naomba kuweka wazikwamba sijawahi pewa              shutuma              zozote au mashitaka yoyote yale yanayohusiana nahicho              alichokiongea.                Niliamua kupuuzia kwa sababunamjua Heche ni mlopokaji,              kiongozi              asiyejua wajibu wake, anayetumikiawasiomchagua, mtu asiye              na malengo              na mtegemezi wa siasa ili kuendesha maishayake na ya              familia yake. Pia              nilimpuuza kwa sababu najuasio Mwenyekiti aliyechaguliwa              kidemokrasia,              aliwekwa kwa matakwa ya wakubwazake ambao wanamtumia kwa              malengo              yaliyokusudiwa, ikumbukwe kuwa vijana watatu,Habibu              Mchange, Mtela              Mwampambwa na Grayson Nyakarungu walienguliwa              kimizengweili Heche              ashinde, hivyo kwetu sisi yeye ni sawa na Mwenyekiti wa              kuteuliwa.Hivyo sikumjibu mtu asiyekuwa na sifa sawa na              zangu katika              harakati za kusakademokrasia ya kweli.                Lakini kitendo cha Mwenyekitiwangu, Mh. Freeman Mbowe              kujitokeza              kupitia gazeti mojawapo na kudai madaiyangu ni ya kitoto,                kwanza kimenifedhehesha, ni dharau kwa vijana              walionionanina sifa na              ukomavu na kunipa kura nyingi ili niwe Makamu Mwenyekiti              waBAVICHA              Taifa.                Pili ni kama anahalalisha kikaobatili, kilichokiuka              kanuni na katiba              ya CHADEMA ili kuhalalisha matakwa yaoyenye lengo la kuminya              demokrasia na uhuru wa kujieleza ndani ya chama.                Tatu anahalalisha hoja za vijana,ambazo ndio uhalisia              kuwa Heche              hakuwa na sifa, na uwezo, hivyo alibebwa na Mh.Mbowe ili              akae pale kwa              malengo yake.Ndio maana nilisema ukionakifaranga              kimepanda juu ya figa              ujue mama yake yuko chini, hivyo mama yakekifaranga              kajitokeza              kuhalalisha kifaranga chake kupanda juu ya figa.                MADAI YAALIYODAI MH. MBOWE KUWA NI YA KITOTONiseme wazi              kwamba              nimesikitishwamno na madai aliyoyatoa Mwenyekiti wangu wa              CHADEMA Mh              Freeman Mbowe kupitiagazeti la Mtanzamia la tarehe              12/01/2013 kwamba              madai yangu ni ya kitoto .                Kwanza niweke wazi kabisa kwambanamuheshimu sana Kiongozi              wangu huyu              mkuu ambaye ndiye alipaswa kuwa mstari wa mbele katika              kuhakikisha              kwambahaligawi baraza la Vijana na chama kwa ujumla,              ahakikishe kuna              utawala borandani ya chama, na utendaji haki, lakini cha              kushangaza              ameibuka kumtetea Hechekwa hoja za mwegemeo wa upande              mmojabila              kuangalia maelezo ya upande wa pili.                Niweke wazi kabisa kwamba kaulialiyoitoa dhidi yangu ni              yakiushabiki              maana kama ni madai yangu kuhusu namna              ninavyohujumiwakupitia kwa              Katibu Mkuu yeye anayo nakala ya malalamiko [ushahidi upo],              lakinihakuna hatua ambayo ameichukua.                Namshangaa Mwenyekiti kudai madaiyangu ni ya kitoto sasa              sijui ni              madaiyapi anayazungumzia ? madai ya kitoto ni yapi? na              madai ya              kikubwa ni yapi ? naje madai ya kitoto ni haya mimi              kuhoji kwanini              hatuweki akiba kwenye akauntikwa ajili ya uchaguzi 2015 kama              tulivyokubaliana kwenye baraza kuu mara baadaya uchaguzi wa              2010.Naombaniwajulishe wanachadema kuwa, nimejitahidi              sana kushauri              juu ya                1; Uanzishwaji wa chuo chamafunzo ya uongozi kwa makada              wa CHADEMA ,              badala yake ni matumizi mabaya yafedha za ufadhili wa              wadau tofauti na              hasa mfadhili mkuu ndugu SABODO. Hiiingesaidia pia kulea              ki-mfumo wa              maadili ya uongozi kwa vijana wa umoja wawanafunzi wa              CHADEMA wa vyuo              vikuu yani " CHASO" ambapo mimi ni mwasisi wamkakati huu              nchini.                2; Chama kwa ujumla kutokuwa na jengo letu na hasa makao              makuu yetu.              Niaibu kwa chama kikubwa kama CHADEMA kuwa na ofisi              tulizopanga na              kulipa mamilioni ya fedha za ruzuku na misaada kwa manufaa ya              Mwenyekiti Freeman Mbowena Mkurugenzi wa fedha wanaomjua              mmiliki wa              jengo la makao makuu. Kimsingi mimi natambua chama kina              uwezo mkubwa              wa kuwa na majengo yetu.                3; Kupunguza mshahara wa katibumkuu Ndugu Dk. Slaa ambao              ni zaidi ya              milioni saba kwa mwezi na marupurupu kibao ili pesa hizo              na mamilioni              zielekezwe kujenga chama mikoani kama kweli tunataka2015              tuingie              Ikulu.                4; Kuhakikisha pesa zilizochangishwa kwenye M4C              zinatumika ipasavyo na              si kama zitumikavyo kipindihiki ambapo ni kama tumelewa              wingi wa watu              kwenye mikutano ya hadhara.                5; Kitendo cha Mwenyekiti wa chama kufumbia macho hatua              ya ndugu Slaa              (katibu mkuu) kujikopesha pesa ya ruzuku ya watanzania              zaidi ya              shilingi milioni mia na arobaini.                6; Hatua ya mwenyekiti ndugu Heche kulipwa mshahara na              marupurupu hali              kanuni za chama haziruhusu huku Mbowe akifumbia macho              wakati viongozi              wa mikoa na wilaya hawapewi pesa na vifaa vya uenezi.                7; Kitendo cha mchumba wa Dk.Slaa, Josephine Mushumbusi              kuzunguka              mikoani na kulazimisha kupokelewa kama mke wa mfalme na              kuendesha              vikao vya ndani na mikutano ya hadhara yenye kulenga              kuwajenga              wagombea ubunge anaowataka yeye na katibu mkuu kwa mwaka              2015.                Ndugu wanahabari, je hizi ndo hojaza kitoto anazodai Mh.              Mbowe? Hivyo              basi namtaka Mh. Mbowe sasa asikimbiliekujibu hoja              kiushabiki.              Ajitahidi kuwa na fikra na Busara ili kukisaidia chama              kuvuka kwenye              daraja la sasa la pepo kufukuzana. Atambue Baraka              anazozitoa wanachama              wafukuzwe hovyo na kunyanyaswa ni hatari kwa kuwa              anaandaa kundi kubwa              nje ambalo litageuka mwiba siku za usoni.                UHALISIA ULIOPO:                Ndugu waandishi wa habari,              Naomba kuweka wazi kwamba mimi Juliana Shonza ni Makamu              Mwenyekiti              halali wa baraza la vijana (BAVICHA). Taarifa zozote zile              mlizozisikia              kuhusu kuvuliwa kwangu uanachama, naomba kwa nguvu moja              kupitia              taaluma yenu muwaambie watanzania kwamba wazipuuze. Ni              taarifa              zilizotolewa na kikundi cha kihuni kilicholenga kutimiza              matakwa ya              wakubwa wao. Kikundi hicho hakina mamlaka ya kikatiba              yoyote yale ya              kunivua uongozi huunilio nao.                Kuthibitisha hilo kuwa ni kikundimufilisi, hadi              ninapoandika waraka              huu kwenu sijapewa barua yoyote ile inayonitaarifu kuwa              nimevuliwa              uongozi wangu. Hii ni wazi wanatambua kuwa wanachemka,              wanatengeneza              makundi kwa maslahi wanayoyaona yanawafaa.                Sikuchaguliwa ili niwe chombo cha kuwatumikia watu, na              badala yake              nilichaguliwa ili niwatumikie vijana waCHADEMA na              watanzania kwa              ujumla, na pale nilipoona kuna ukiukwaji na kuhoji ndio              chanzo cha              mizengwe na matamko ya Ndugu Wegesa (John Heche).                Nimekuwa nikiwasumbua viongozi wenzangu kuhusu              kutengeneza kadi za              BAVICHA na kusajili wanachama katika mfumo mzuri              (database) ili tuwe              na kumbukumbu ya wanachama wetu lakini yote              yameshindikana kwasababu              amekuwa akiendeshwa na mfumo dume kandamizi kwa mwanamke,              mara nyingi              nimemshauri kwa ajili ya maendeleo ya Baraza na nimekuwa              nakwamishwa              na Mwenyekiti na Katibu na hata leo sisi wote ni              wanachama kwa              kufikirika (imagination), kwa kuwa bado hatuna kadi za              uanachama kwa              vijana wa BAVICHA zaidi ya kutambulika na katiba ya chama.                KUKIUKWA KWA KATIBA                Ndugu wanahabari, ni wazi kuwakatiba pamoja na mwongozo              wa baraza letu              la vijana bavicha ulikiukwa katikakikao walichokiita              kamati tendaji              iliyokaa tarehe 05/01/2012 ambayo iliongozwa na Bwana              Wegesa Suguta              (John Heche) kama Mwenyekiti, hali inayonilazimu kusema              wazi, bila              kumung'unya maneno kwamba maamuzi yaliyotolewa na kikao hicho              yalikwishapangwa na viongozi wa kitaifa hayakuwa halali.              Nasisitiza              kwamba ni ukweli ulio wazi kwamba agenda na maazimio ya              kikao hicho              yalikwisha amuliwa hata kabla ya kikao hicho kwasababu              kubwa mbili:                1; Taarifa za kufukuzwa kwetuzilikwisha anza kusikika              kwenye mitandao              ya kijamii kama vile jamii forum nafacebook mwezi mmoja              kabla ya kikao              cha kamati tendaji batili.                2; Pili ushahidi wa kimazingirakwa maana ya ukiukwaji              mkubwa wa              kikatiba na mwongozo wa Baraza letu la Vijana uliofanyika              siku ya              kikao.                Ndugu wanahabari,              Ikumbukwe kuwa pamoja na uwepo wa taarifa za kikao mwezi              mmoja kabla              binafsi nililetewa taarifa hizo siku mbili kabla ya              kikao, tena kwa              njia ya ujumbe mfupi wa maandishi {sms} na baadae              kupigiwa simu na              Katibu wa Baraza Bwana Munishi ikinitaka kuhudhuria kikao              hicho              kutokana na kuwa nje ya Dar-es –salaam kwa mambo ya              kifamilia zaidi              niliwataarifu viongozi wenzangu kwa utaratibu maalumu wa              mawasiliano              ya kiuongozi kwa maana ya kuwatumia barua ya udhuru wa              kutohudhuria              kikao.                Lakini cha kushangaza na kustaajabisha kwa viongozi              wenzangu hawa              ambao kwa namna moja ama nyingine napata ugumu wa kuelewa              kama kweli              wana sifa za kuitwa viongozi tena wa idara nyeti sana              katika ustawi wa              chama chetu, kwa makusudi kabisa ama kwa kutumwa kufanya              hivyo ama kwa              utashi wao mdogo wa kiupembuzi yakinifu waliamua kuvunja              na kukiuka              katiba ya chama na kujipa vyeo vya kiunyampara kwa kuamua              kuchukua              maamuzi ya kutuvua uanachama wa kufikirika wa baraza mimi              na vijana              wenzangu Ndugu Mwampamba na Mchange ambao nao hawakupewa              nafasi ya              kusikilizwa, ambao moja kwa moja tunapoteza sifa yakuwa              wanachama wa              CHADEMA.                Ndugu wanahabari,              Naomba sasanijikite katika katiba ya chama changu na              mwongozo wa              baraza la vijana sura ya sita kipengele cha 6.5 ambacho              kinasema              taratibu zifuatazo lazima zifuatwe katika kuchukua hatua              za kinidhamu.              6.5.2 kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na .4.4 ya katiba, mwanachama              yeyotehatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama              kuachishwa ama              kufukuzwa uanachama bila kwanza                {a} kujulishwa makosa yake kwamaandishi na kutakiwa kutoa              majibu              katika muda usiopungua wiki mbili.              [b] kupewa nafasi yakujiteteakatika kikao kinachohusika.              {c} Mwanachama atajulishwa kwamaandishi uamuzi wa kikao              mnamo wiki              mbili baada ya kusikilizwa.                Ndugu waandishi wa habari,Nisemewazi kwamba hakuna kifungu              kilichofatwa kati ya hivyo niliyoviainisha hapo              juu,hakuna barua              yeyote niliyojulishwa ya hayo waliyoyaita mashitaka yangu              zaidi ya              kuyasoma na kuyasikia kwenye vyombo vya habari baada ya              wao na kikao              chaoharamu kuchukua maamuzi yakunivua uanachama wa Bavicha .                Sikupewa nafasi yakujitetea maanasikuwepo kwenye kikao,              barua ya              udhuru wakutohudhuria walikuwa nayo. Na vilevile mpaka              leo hii              sijajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao hicho batili              badaa yake              viongozi wenzangu hawa wameamua kuujulisha umma wa              Watanzania na              wanachadema kwa ujumla pasipo kunijulisha mimi kwanza.              Ukiangalia pia              kifungu cha 6.5.6 cha katiba kinasema KIONGOZI YEYOTE              hatachukuliwa              hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa              maandishi na              mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi.                Sasa basi namtaka Bwana Wegesa Suguta awaeleze umma wa              watanzania kama              alivyokurupuka kuwaeleza kwamba Shonza amevuliwa              uanachama wa Chadema              ni wapi na lini yeye kama Mwenyekiti nilipewa barua ya hayo              wanayoyaita mashitaka, na ni lini niliwapa majibu ya              mashitaka hayo.                UHALALI WAKIKAO CHA KAMATI TENDAJI                Ndugu wanahabari,              Ikumbukwe kwambakikao cha juu kuliko vyote kwenye ngazi              ya chama              husika ni Mkutano Mkuu ambao ndio ulioniweka madarakani              kutokana              nakuwa na imani na mimi na kikatiba ndiohaswa ulipaswa              kuniandikia              mashitaka, kunijadili, kunihoji na kutoa maazimio ambayo              yangepelekwa              kamati kuu ambao kimsingi ndiyo yenye mamlaka ya mwisho              yakumvua mtu              yeyote uanachama wake baada ya kujiridhisha na taarifa na              uchunguzi              kutoka kwenye kikao husika kilichomwandikia mwanachama              mashitaka na              kumuhoji.                Ndugu wanahabari ifahamike wazikwamba kikatiba kuna ngazi              mbili tu              zinazoweza kumvua mtu uanachama wake ambazoni ngazi ya              tawi na ngazi              ya kamati kuu.                Hivyo basi namtaka sasa Bwana Wegesa Suguta auambie umma              wa watanzania              kwamba ni lini kamati tendaji ya vijanailigeuka ama              kukaimishwa              madaraka ya ngazi ya tawi, ngazi ya mkutano mkuu              amakamati kuu yakuwa              na uwezo wakumvua kiongozi uanachama wake?                Ndugu waandishi wa habari,              Wajumbe wa kamati tendaji kikatiba ni makatibu wa kamati              za uratibu za              mikoa lakini badala yake Bwana Wegesa Suguta (John Heche)              amekuwa              akiwaita wenyeviti wamikoa na sababu kubwa ikiwa ni              kwamba wengi wa              wenyeviti hao hawastahili kuwepobavicha kutokana na              kwamba umri wao              kuwa zaidi ya miaka 35 hivyo kupoteza sifa za kuwa              viongozi wa BAVICHA              ambayo katiba inamtaka mwanabavicha yeyote kuwa namiaka              18-35, hivyo              basi kwa kuhofia kupoteza nafasi zao hulazimika              kukubaliana na lolote              lile ambalo bwana Wegesa Suguta analitaka hata kama              wakijua kwamba ni              kinyume kabisa na matakwaya katiba na mwongozo wa baraza.                Hivyo kumpa Heche mwanya wakuamua lolote lileanalotaka              ama kutumwa              kulifanya. Kutokana na hilo natangaza wazikwamba kikao              cha kamati              tendaji kilichopita ni batili, chenye wajumbe batili,              kimesimamiwa na              viongozi batili kwa maana ya mwenyekiti na katibu wake maana              wameshindwakuheshimu misingi ya kikatiba katika namna ya              demokrasia ya              chama chetu hivyo basi nachukua nafasi hii kuutangazia              umma wa              watanzania na wanachadema kwa ujumla wao kwamba maamuzi              ya kamati              tendaji yaliyotangazwa na kiongozi kilazana daraja la              viongozi wa juu              bwana Wegesa Suguta ni batili.                Ndugu wana habari,              Sifa ya Mwalimu ni kuweza kubadilisha hali ya umbumbumbu              wa wanafunzi              wake, Heche kama kiongozi, na Mwalimu kitaaluma (nina              wasiwasi na              ufaulu wake katika huo ualimu) alipaswa kuwa mfano bora              kwa vijana wa              Chadema kuwaelekeza na kuwafundisha namna ya kuheshimu              misingi ya              kikatiba ambayo kama chama na baraza tumejiwekea na              tunapaswa kuifuata              ni wazi kuwa Heche ameshindwa kuwa mfano bora kwa vijana,              hajui kanuni              za BAVICHA wala katiba ya CHADEMA, mkurupukaji,              mropokaji, mwenye              uwezo mdogo wa kufikiri, dikteta anayetumia mamlaka              asiyokuwa nayo              (akipewa mamlaka atatuchinja huyu) hivyo hafai kuwa hata              Mwenyekiti wa              serikali za mtaa, wala kuaminiwa popote kupewa nafasi ya              kiuongozi. Ni              wazi ubongo wake yeye nakatibu baraza bwana Munishi              haujapewa tohara              la kisiasa, ifike mahali wakubali kufundwa unyagoni na              manyakanga wa              kisiasa.                KUHUSUKUVULIWA UANACHAMA WA BAVICHA;                Ndugu wanahabari,              Kuhusu kuvuliwauanachama wa Bavicha ambao moja kwa moja              napoteza sifa              ya kuwa mwanachadema namshangaa kiongozi huyu ambaye sifa              yake kuu              siku zote ni ukurupukaji kwa kusema kwamba nimevuliwa              uanachama wa              Bavicha huku akijua wazi Bavicha haijawahi kuwa na kadi              za baraza.                Katika mwongozo wa baraza lavijana kipengele cha 4.4              KUJIANDIKISHA              UANACHAMA 4.4.1 inasema ili kijanaaruhusiwe kujiunga              bavicha ni lazima              awe na sifa zifuatazo              [a] Awe mwanachama wa CHADEMA              [b] Awe na umri kati ya miaka 18 na 35              [c] Awe anakubaliana na misingiya mwongozo wa BAVICHA                4.4.2 Inasema kijana aliyekidhimatakwa hayo hapo juu,              atanunua kadi ya              uanachama wa BAVICHA                Kutokana na kipengele hicho namtaka bwana Wegesa Suguta              auambie umma              wa watanzania na wanaCHADEMA kadi yake yeye ya baraza la              vijana ni              namba ngapi na aliichukulia wapi? Aueleze umma wa              watanzania kadi              yangu ya baraza la vijana ni namba ngapi na niliichukulia              wapi?                Ndugu waandishi wa habari,              Nidhahiri baraza la vijana chadema hatuna kadi ambayo              kimsingi ndiyo              utambulisho wa mwana BAVICHA endapo akishakidhi sifa              zilizoainishwa              hapo juu. Na ni wazikwamba vijana wote wa CHADEMA tuna              sifa za kuwa              wana Bavicha lakini si wanachama wa BAVICHA kutokana na              kwamba              nimekuwa nikimwambia mara kwa mara umuhimu wa kuirasimisha na              kuianzisha ili iwe taasisi kamili kwa kuwa na kadi za              vijana kama              mwongozo wa vijana unavyojieleza.                UELEWA WANGU KUHUSUKUNDI ANALOLIITA NDUGU WEGESA SUGUTA              (JOHN HECHE)              NI "MASALIA"                Ndugu waandishi wa habari,              Hakuna kundi linaloitwa masalia ndani ya Chadema na              BAVICHA. Gazeti la              MWANAHALISI ndilo lililoandika kuwa vijana wote waliofutwa na              kuondolewa kwenye uchaguzi wa BAVICHA mwaka 2011 ni              MASALIA ya Zitto              yanayopukutishwa Chadema. Kimsingi gazeti hili lilikuwa              linafanya kazi              yake ya kipropaganda ndani ya CHADEMA ili kukigawa Chama.              Lilikuwa              linatimiza wajibu wake wa kupika mpasuko ndani ya chama              tena kwa              kuhusisha na viongozi wakubwa ndani ya chadema.                Ni aibu kubwa sana na ni hatari kuona kiongozi kama              Wegesa Suguta              anakuwa mstari wa mbele kushabikia neno masalia, huku              akijua wazi              kufanya hivyo ni kuligawa baraza la vijana. Kwa nguvu              moja nalaani              kitendo hiki cha kipuuzi kinachofanywa na Mwenyekiti huyu              wa BAVICHA              cha kuchekelea upuuzi uliopikwa na gazeti la MwanaHalisi.              Naomba              atumie rasilimali za chama kujenga umoja wa vijana imara,              tushirikiane              kuimarisha Bavicha yenye tija kwa chama na sio kusherekea              mpasuko              ndani ya baraza la vijana.                  UELEWA WANGU KUHUSU KITU KINACHOITWA PM7                Ndugu waandishi wa habari,              Naomba kunukuu maneno ya mtu maarufu sana mitandaoni na              kwenye uga wa              habari Mzee Mwanakijiji anasema              "Uongozi imara sio kutegeana, kunyemeleana na kufukuzana.              Uongozi              imara ni kushirikiana".                PM7 ni jina lenye maana ya "PATRIOTIC MOVEMENT" yaani              harakatiza              kizalendo kwa mujibu wa Ndugu Ben saanane ambaye alitumwa              na kiongozi              wa juuwa chama kuja kulitekeleza kwa vijana walioenguliwa              kwenye              uchaguzi wa BAVICHAmwaka 2011 na wanaoonekana kusigana na              kiongozi              huyo kimawazo. PM7 ni wazoliliobuniwa na kiongozi mmoja              wa juu wa              chama akishirikiana na Ben saanane wakinuia kutega mtego              wa kuwanasa              vijana wanaoonekana wapo tofauti kimawazo nakiongozi huyo              wa chama.              Kwa kuwa wazo hilo lilikuwahalina manufaa kwa chama,              halikutekelezwa.                Kiongozi huyo bila kumung'unya maneno ameamua kuwatumia              vijana hao              kuandaa kikao batili cha kamati tendaji ya John Heche ili              awafukuze              vijana hao. Hii ni hatari sana kuona kiongozi wa chama              unageuka simba              na kuanza kuwawinda watoto wake ili uwamalize kisiasa kwa              sababu zako              binafsi.                MAAJABU KATIKAMEDANI ZA SIASA ZA BAVICHA MWAKA 2013                Ndugu waandishi wa habari,                1. Hii ni ajabu sana katika kikaocha kamati tendaji              batili, Ambao              hatukuhojiwa ni watu wawili, mimi Juliana Shonzana kijana              mmoja              anaitwa Exaud Mamuya. Lakini Mimi Juliana Shonza              nimehukumiwa bila              hata kusikilizwa wala kupewa mashitaka na chombo chochote              katika              chama. Wakati huo huo Exaud Mamuya hajahukumiwa kwa madai              hakufika              kwenye kikao. Hii ni dhahiri huu ni mkakati wa kipuuzi ambao              unaendeshwa na watu wapuuzi tena kwa misingi ya kikabila              na kikanda.                2. Muasisi mwenza wa PM7 na kibaraka wa kiongozi wa juu              wa chama              aliyetumika kutoa shutuma chafu kwa Naibu Katibu Mkuu. Kijana              anayefahamika kwa jina la Ben Saanane ameachwa kwa madai              yeye amekiri              mbele ya hiyo kamati tendaji kwamba ni kweli alinuia              kumchafua Naibu              Katibu Mkuu wa chama na kukivuruga chama. Wakati tuhuma zake              zinafananana za Mchange na Mwampamba.                3. Mkakati wa John heche navibaraka wake umejikita              kutukuza ukanda              ndani ya chama tena wa wazi wazi.Ukanda huu              umejidhihirisha kwenye              kutoa hukumu batili za tuhuma kama ifuatavyo.                Vijana waliohukumiwa wote niwale wanaotokea Mbeya, Mbozi              na Kibaha.              Wakati Vijana wa Kilimanjaro wameachwa kwa madai wao wametoa              ushirikiano.                Waliohukumiwa ni:              _Mtela Mwampamba-Mbozi, Mbeya              _Habib Mchange-Kibaha, Pwani              -Juliana Shonza-Mbozi, Mbeya              -Joseph Kasambala – Mbeya mjini (kasimamishwa)              - GWAKISA Mwakasendo –Rungwe, Mbeya (kasimamishwa)                Pamoja na wanachama watatu waliopo Mbeya mjini waliofukuzwa              uanachama.                Waliosamehewa ni:              _Ben saanane-Kilimanjaro              _Exaud Mamuya-Kilimanjaro.                Hii ni dhamira ya wazi kabisa kwamba CHADEMA sasa ni              chama cha              kikanda, Viongozi wa CHADEMA wanatumika kutangaza ukanda kwa              watanzania.                Kwa maana hiyo wale wote wasio wa kaskazini ndani ya Chadema              tusitegemee kutendewa haki.                MAMBO NILIYOMSHAURI HECHE NA KUMUONYA:                Ndugu waandishi wa habari, Sisikama vijana tusigeuze              siasa kuwa ajira              wala chombo cha kuendeshea maisha, ni moja ya vikwazo              katika kukuza              demokrasia ya kweli, maana wengi wanaendekeza njaa na              uhitaji wa              maisha yao ili kupindisha ukweli.                Moja ya maswali yangu kwa Mwenyekiti ni kitendo cha              kubinafsisha gari              alilotoa Naibu Katibu Mkuu kwa ajili ya BAVICHA na badala              yake              akalifisadi, akafanya mali yake binafsi na kumuweka Mdogo              wake Chacha              Heche kuwa dereva wake, nimekuwa nikipinga matumizimabaya ya              rasilimali hiyo kwa manufaa binafsi, na badala yake gari hiyo              ifanyekazi iliyokusudiwa, huu ni msingi wa kuonyesha              tofauti yetu na              wanaotumiarasilimali za serikali (Taifa) kwa manufaa              binafsi nay a              familia zao.                Pia nilimshauri Mwenyekiti awe nakipato halali kama              katiba ya chama              inavyosema Sura 10 MAADILI YA VIONGOZI ibara ya 10              kifungu cha (6)              kinasema Kiongozi anatarijiwa kujitosheleza yeye              nafamilia yake kwa              mapato halali ili kutokuwa ombaomba kwani tabia hiyo              itadhoofisha              uwezo wake wa kutoa uamuzi sahihi, ili kuwa mfano bora              wauwajibikaji              kwa vijana, kama ambavyo Mwalimu Nyerere alivyosema              kipimo cha Utuni              kufanya kazi, badala yake ametelekeza taaluma ya ualimu,              aliyotumia              pesa za walipa kodi kwa kusoma na muda wote ni kupiga              soga bila              uzalishaji na kujipatia kipato halali, na badala yake              anategemea              mshahara usio halali kuishi, ni wazi Mwenyekiti ni cheo              cha kisiasa na              hatakiwi kulipwa mshahara, wala kulipiwa nyumba kwa              mujibu wa kanuni.                Badala yake majibu anafikiri ni kufanya njama na              waliopindisha              taratibu hizo ili alipwe mshahara kwa maslahi yao ya              kisiasa. Na              tumekuwa tukilipinga hilo kwani tunataka tuwe mfano wa              utawala bora              kwa vitendo na si maneno peke yake.                MWISHO:                Ndugu waandishi wa habari,              Nipokwenye mchakato na wanasheria wangu kushughulikia              swala la              kumpeleka mahakani Bwana John Heche na gazeti la Tanzania              Daima toleo              namba 2958 kwa kuniita msaliti wa CHADEMA, natumiwa na              CCM na kuwa              nina mahusiano (natumiwa) na Wassira tena bila kunihoji              mimi Juliana              Shonza. Kwa maana hiyo wamenichafua na kunidhalilisha              mbele ya umma wa              watanzania.                Pili naomba kuweka wazi kwambanatarajia kuomba ufafanuzi              wa kikatiba              juu ya shutuma zilizotolewa kwenye vyombo vya habari              dhidi yangu na              bwana Wegesa Suguta (John heche) ili aseme ni aminisho              lipi la              kuthaminisha na kusakidikisha mtazamo wa maono yake ili              bongo za              watanzania zijue ukweli. Mimi Makamu Mwenyekiti wa              BAVICHA natangaza              rasmi Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni wanachama hai              na halali wa              Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).                Hivyo nawaomba waendelee na kazizao za ujenzi wa chama              kwenye majimbo              yao na taifa kwa ujumla. Nawaomba wananchi na wanachama              wote wa              CHADEMA waendelee kuwa na imani dhidi ya vijanahawa. Kama              mlivyomwamini Mwampamba na kumpa kura 32000 na kama              mlivyo mwamini              Mchange na kumpa kura 10,400 kwenye uchaguzi wa Ubunge              mwaka 2010.              Vivyo hivyo naowaombamuendelee kushirikiana nao              kuhakikisha wanatimiza              adhima ya ukombozi mwaka2015.                Wenu katika ujenzi wa demokrasia makini                Juliana Daniel Shonza                M/Kiti BAVICHA-Tanzania Bara.                --              Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com              <http://www.wejobs.blogspot.com>              International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com              <http://www.jobsunited.blogspot.com>                Kujiondoa Tuma Email kwenda              wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com              <http://us.mc1411.mail.yahoo.com/mc/compose?to=unsubscribe%40googlegroups.com>              Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma                Disclaimer:              Everyone posting to this Forum bears the sole              responsibility for any legal consequences of his or her              postings, and hence statements and facts must be              presented responsibly. Your continued membership              signifies that you agree to this disclaimer and pledge to              abide by our Rules and Guidelines.                --          Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com          <http://www.wejobs.blogspot.com>          International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com          <http://www.jobsunited.blogspot.com>            Kujiondoa Tuma Email kwenda          wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com          <mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com> Utapata          Email ya kudhibitisha ukishatuma            Disclaimer:          Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility          for any legal consequences of his or her postings, and hence          statements and facts must be presented responsibly. Your          continued membership signifies that you agree to this          disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.              --      Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com      <http://www.wejobs.blogspot.com>      International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com      <http://www.jobsunited.blogspot.com>        Kujiondoa Tuma Email kwenda      wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com      <mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com> Utapata Email      ya kudhibitisha ukishatuma        Disclaimer:      Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for      any legal consequences of his or her postings, and hence      statements and facts must be presented responsibly. Your      continued membership signifies that you agree to this disclaimer      and pledge to abide by our Rules and Guidelines.          --  Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com  International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com    Kujiondoa Tuma Email kwenda  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha  ukishatuma    Disclaimer:  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any  legal consequences of his or her postings, and hence statements and  facts must be presented responsibly. Your continued membership  signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by  our Rules and Guidelines.      --  Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com  International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com    Kujiondoa Tuma Email kwenda  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha  ukishatuma    Disclaimer:  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any  legal consequences of his or her postings, and hence statements and  facts must be presented responsibly. Your continued membership  signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by  our Rules and Guidelines.      --  Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com  International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com    Kujiondoa Tuma Email kwenda  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha  ukishatuma    Disclaimer:  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any  legal consequences of his or her postings, and hence statements and  facts must be presented responsibly. Your continued membership  signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by  our Rules and Guidelines.      
  --  Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com  International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com    Kujiondoa Tuma Email kwenda  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha  ukishatuma    Disclaimer:  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any  legal consequences of his or her postings, and hence statements and  facts must be presented responsibly. Your continued membership  signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our  Rules and Guidelines.      --  Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com  International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com    Kujiondoa Tuma Email kwenda  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha  ukishatuma    Disclaimer:  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any  legal consequences of his or her postings, and hence statements and  facts must be presented responsibly. Your continued membership  signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our  Rules and Guidelines.      
  

0 comments:

Post a Comment