Wednesday 23 January 2013

Re: [wanabidii] HAIBA YA KINANA NA CCM

Mkinga

Hoja zako zina mashiko sema tatizo nilililoliona ni kwamba tayari umeegemea upande mmoja haukuweka usawa katika uwasilishaji wake. Kwa mujibu wa Robert Kiyosaki wa "Rich Dad Poor" mojawapo wa hoja kubwa anazozikazania ni ile ya umilikiwa biashara na uwekezaji (Owning a business and Investment) akitofautisha kati ya kuajiriwa na kujiajiri upande mmoja na huko kumiliki biashra na kuwekeza upande wa pili. Sasa unapotaka mafanikio ni lazima utafute watu ambao watafanya kazi kwa niaba yako na wewe uendelee kula kuku kwa mrija kwa ile faida inayopatikana. Kama nadharia ya Kiyosaki ipo sawa sawa ni rahisi sana kwa mtu kumiliki kampuni na yeye binafsi kama mmiliki asiwe na taarifa ya kinachofnayika zaidi ya kusubiri fungu lake kwa sababu kuna menejimenti inayofanya kazi kwa ufanisi na kwa niaba ya mmiliki. Sasa kama hili ndilo limefanyika ni rahisi sana kwa mmiliki kutokuwa na ufahamu wa kinachondelea katika kampuni yake kwa shughuli za kila siku.

Kaika hili mimi nawaza tu, je kwenye uchunguzi wa sakata hili, Mmiliki aliweza kulazimisha mambo yafanyike kinyume na uratibu na sheria za nchi? Wanaosimamia Sheria wao wametoa tamko gani juu ya hii kampuni? nafikiri maswali kama haya yanaweza kutupa picha ya namna ambavyo mmiliki kahusika ama kutohusika kwenye sakata hili.


2013/1/23 Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
Hivi karibuni kampuni ambayo kati ya wamiliki wake ni Abrahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, ilihusika na usafirishaji wa pembe za ndovu kinyume na sheria za nchi, kinyume na sheria za kimataifa.
 
Vyombo vya habari viliripoti kuwa Kinana mwenyewe alikiri kuwa kampuni yake ilihusika na usafirishaji wa shehena hiyo haramu lakini kampuni haikujua kuwa shehena ile ilikuwa ya biashara haramu.
 
Kwa mtazamo mpana, kashfa hii na utetezi wa Kinana, kweli unatosha kumsafisha kiongozi mkuu huyu wa chama tawala na kashfa hii? Hivi kampuni wakala wa usafirishaji mizigo husafirisha mzigo wowote bila ya kujiridhisha kuwa mzigo unaosafirishwa ni mzigo uliotajwa kwenye nyaraka za usafirishaji? Mara nyingi katika biashara, mtoa huduma huwa na wateja wake wa muda mrefu na wale wa mara moja. Kutokana na kushamiri kwa biashara haramu ya pembe za ndovu, Je, kampuni hii ya usafirishaji wa bidhaa haramu inayomhusisha kiongozi mkubwa wa chama tawala, imesafirisha mizigo ya aina hii mara ngapi bila ya kukamatwa? Wamiliki wa mizigo hiyo haramu waliichagua kampuni ya mheshimiwa huyu kwa bahati mbaya au kulikuwa na sababu maalum ya kuichagua kampuni hii?
 
Swali jingine la kujiuliza, kumiliki kampuni inayosafirisha bidhaa haramu, japo inawezekana Kinana ni mmiliki tu wa kampuni na asiwe mtendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni, je, hiyo pekee yake inaweza kuwa ni sababu tosha ya kumwona Mh. Kinana ana usafi wa kuongoza chama ambacho kinadai kipo kwenye hatua ya kujisafisha?
 
CCM kama chama cha siasa na chama tawala, kinapojiangalia kwenye kioo cha kujitathmini kinajiona ni chama cha namna gani, wakati viongozi wake wakuu majina yao yanatajwatajwa kwenye biashara chafu? Kwenye mambo kama haya, ndipo tunaposhangaa umakini wa CCM.
 
Bart

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment