Wednesday 16 January 2013

Re: [wanabidii] DR SLAA JUU YA MOU KATI YA SERIKALI NA KANISA

Jamani naomba mwenye nafasi aangalie hii kwenye post namba 606 kuna
ustadhi mmoja anawahubiria waumini wake 1) kwamba sheikh akiuawa na
wao wamwue padre, askofu au kardinali na siyo kuharibu mali. Anadai
Uislamu haufundishi kuharibu mali bali kulipiza kisasi na kwamba huo
ndio uhai wa Uislamu 2) anaelezea pia maana ya mfumo Kristo. Pengine
mkisikiliza mnaweza kugundua kuwa udini umeshakua na kufikia asilimia
kubwa sana. Linki yenyewe ni hii hapa chini (ila nenda post namba
606). Asanteni!
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/383549-kauli-ya-dr-slaa-juu-ya-mou-kati-ya-serikali-na-kanisa-31.html

On 1/15/13, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com> wrote:
> Kama wote tutakuwa wazi kukubali ufafanuzi huu tumshukuru Mungu maana
> baadhi yetu tunapenda kujadili kitu tusichofihamau na ambacho hatutaki
> tukifahamu ili tuweze kusema chochote tunachoweza kusema (speculate) kuliko
> kile tunachokifahamu.
>
>
> 2013/1/15 mngonge <mngonge@gmail.com>
>
>> Asante kwa ufafanuzi mzuri baadhi yetu tulikuwa tunafuatilia na kujua
>> nini kilijili. Baadhi ya watua wanaoingiza hisia za udini katika MoU
>> kati ya mashirika ya kidini na serikali wanaelewa fika. Kwa vile ni
>> mradi wa kujipatia chochote kitu kupitia migongoni mwa waumini wenye
>> uelewa wa chini na kati basi wanaamua kulikologa taifa chini ya
>> mwavuli huo.
>>
>> 2013/1/15 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>:
>> > Wana JF,
>> >
>> > Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika. Ningependa tu
>> > kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo
>> > ilizaliwa:-
>> >
>> > 1) Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na
>> > nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi,
>> > hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye
>> > maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za
>> > mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle
>> > School (Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina
>> > yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au
>> > darasa la nane lilipofutwa rasmi).
>> >
>> > 2) Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa
>> > ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato
>> > wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC,
>> > lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na
>> > Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya
>> > shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za
>> > madhehebu ya dini. Wakati huo mimi Dr. Slaa, ndiye nilikuwa Katibu
>> > Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati
>> > huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka
>> > kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana.
>> > Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo
>> > zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo
>> > lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa
>> > bado inaendelelea.
>> >
>> > 3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi
>> > ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu
>> > ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa
>> > kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na
>> > hivyo mapato ya Serikali.
>> >
>> > 4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na
>> > mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali
>> > ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo
>> > ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la
>> > Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la
>> > Ujerumani) toka Ujerumani.
>> >
>> > 5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata
>> > kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali
>> > ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya
>> > Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina
>> > yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani
>> > Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa
>> > ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini
>> > walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na
>> > elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi
>> > kuwaadhibu wananchi na watoto.
>> >
>> > 6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na
>> > kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi,
>> > Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili :
>> > a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii,
>> > b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na
>> > madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo
>> > hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana
>> > kwa mujibu wa Sheria.
>> >
>> > Hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama
>> > Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal
>> > Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya
>> > Christian Council of Tanzania) . Baada ya Mashauriano tuliunda chombo
>> > hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja
>> > hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu
>> > hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza
>> > kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na
>> > ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila
>> > dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu
>> > ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).
>> >
>> > 7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini
>> > kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali
>> > mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali
>> > lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao
>> > walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za
>> > ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa
>> > Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo. Serikali
>> > ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata
>> > suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda
>> > wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza
>> > ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye
>> > ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma
>> > zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika
>> > na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha
>> > tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na
>> > madhehebu ya Dini.
>> > Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani,
>> > nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na
>> > Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa
>> > huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika
>> > michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo
>> > ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano
>> > yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services
>> > Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza
>> > akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando).
>> >
>> > Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa
>> > na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na
>> > CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU
>> > iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma,
>> > Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu,
>> > wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa
>> > upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa,
>> > Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).
>> >
>> > 8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani
>> > ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote
>> > za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango
>> > kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.
>> >
>> > Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo. Ninarudia
>> > kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya
>> > aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu,
>> > wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa
>> > hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini
>> > kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine
>> > hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa. Nashauri ili JF ibaki
>> > na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research
>> > zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina
>> > awaombe wenye taarifa. Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia
>> > yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na
>> > au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza
>> > tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.
>> >
>> >
>> http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/383549-tamko-la-dr-slaa-juu-ya-mou-kati-ya-serikali-na-kanisa.html
>> >
>> > --
>> > Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>> > International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>> >
>> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>> >
>> > Disclaimer:
>> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that
>> you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> >
>> >
>>
>> --
>> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment