Thursday 24 January 2013

Re: [wanabidii] DIALLO: WATENDAJI SERIKALI WATAKAO SHABIKIA UPINZANI KUSHUGHULIKIWA.

Ndugu Tony, naomba niingilie mjadala.
 
Kanuni za ajira/utumishi wa umma zinatoa katazo kufanya siasa ofisi za serikali na pia kwa mtumishi wake kutumia nafasi yake, kama vile mwalimu kufundisha wanafunzi mambo ya kichochezi. 

Hivi hili katazo lipo kwa watumishi wa umma wa kada za kati na chini tu? Mbona kila mara twawaona mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wakitumia nafasi zao na mali za umma kufanya siasa? Tena hadi ilifika kipindi ikulu ikawa ukumbi wa mikutano ya chama cha siasa!! Si ajabu kuona mkuu wa wilaya ndani ya STK akiwa na shati la kijani akielekea Kizota! Si ajabu pia kumwona waziri akiwa ndani ya W U akielekea kupiga kampeni za Kafumu!


 
Eneo la shule, chuo, ni maeneo yaliyokatazwa shughuli za kisiasa. Mifano ipo mingi ya kuthibitisha: mwalimu anapoacha kufundisha hesabu au fizikia na kuanza kuhubiri ubaya wa chama fulani au serikali na uzuri wa kingine wakati sio mwalimu wa somo la siasa.

Kwa upande mwingine, kwa mfano mhadhiri wa sayansi za siasa pale UDSM anavyofundisha misingi na kanuni bora za demokrasia na siasa (ambazo pengine hazizingatiwi kwa hapa kwetu), hayo nayo yatakuwa mambo ya uchochezi? Au yasifundishwe kwa kuwa pengine haya apply kwa mazingira yetu?


Ndugu Diallo kakosea, kwani hata muongozo wa utumishi wa umma wa mwaka 2009 unasema - katika section B, kipengele B.9 - kwamba maamuzi na mapendekezo yoyote kutoka kwenye chama tawala, ambayo chama kinataka serikali iyafanye yanapaswa yawasilishwe kwenye wizara husika kupitia kwa ofisi ya waziri mkuu. Sasa ndugu Diallo angefanya hivyo, kusingeleta mzozo.

Wasaalam.

------Original Message------
From: Bart Mkinga
Sender: wanabidii@googlegroups.com
To: wanabidii@googlegroups.com
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] DIALLO: WATENDAJI SERIKALI WATAKAO SHABIKIA UPINZANI KUSHUGHULIKIWA.
Sent: Jan 24, 2013 11:34

Mfanyakazi kama Mtanzania yeyote ana haki ya kuwa mwanachama au mpenzi wa chama chochote cha siasa alimradi hakiuki masharti ya ajira yake. Hakuna sharti linalosema asiwe shabiki, mwanachama au mpenzi wa chama cha siasa, anachozuiwa ni kufanya siasa kazini.   Viongozi wengi wa CCM, na hasa hawa wenye Udokta au PhD hizi za 'Elimu kwa njia ya posta', wanaitwa 'doctors' lakini fikra na matendo yao havina uhusiano wowote na upeo unaostahili wa PhD holders. Siasa zile za chama kushika hatamu ziliwaharibu, na walio wengi japo wanatamka kuwa tupo kwenye mfumo wa vyama vingi lakini akili zao bado ni za chama kimoja, chama dola. Hawa wanasubiria tu muda wao upite, hawawezi kubadilika. Wanayoyaona hawaamini maana daima waliamini kuwa CCM ni kila kitu, CCM ni serikali, CCM ni mahakama, CCM ni jeshi na CCM ni polisi. Hao ni kuwaombea, wapishe kwa amani, wakapumzike ili mawazo mapya yapate uwanja ulio safi unaoweza kuruhusu fikra mpya kuchipuka, kustawi na kisha kutoa matunda.   Bart
From: Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, January 24, 2013 5:47 AM
Subject: Re: [wanabidii] DIALLO: WATENDAJI SERIKALI WATAKAO SHABIKIA UPINZANI KUSHUGHULIKIWA.

But why is he worried now? Anadhani njia kuelekea 2015 is rough for him now? Alichomaanisha ilikuwa intimidate za kitoto. Civilized community haziongozwi kwa vitisho, bali kwa kukumbushwa pale ambapo anadhani people are going the wrong way. Angetumia a sensible language, nadhani hii thread isingekuwepo. Lutinwa Sent from Samsung Tab 10.1 On Jan 24, 2013 3:51 AM, "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:
Vin,


Kifungu kipi unataka. Mfanyakazi wa serikali anajua, masharti ya kazi PSG, inazuia nini au kuruhusu kitu kipi. Wajibu ni wa kwako kusma.

Wanajaribu kuingiza kifungu cha 19 (1) cha sheria za vyama kinachokataza kulazimisha mtu kujiunga na chama cha siasa. Diallo hasemi hivyo, anataka watumishi wafuate sheria na kanuni za kazi, basi.

Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile Black
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




--
Sent from Gmail Mobile

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment