Friday 25 January 2013

Re: [wanabidii] DIALLO: WATENDAJI SERIKALI WATAKAO SHABIKIA UPINZANI KUSHUGHULIKIWA.

Chifu Yachama,

Maneno yote hayo ya nini? 
Sina utamaduni wa kujibizana na mtu anayezungumzia maneno kama yako.

Wasalaam.

On Friday, January 25, 2013, Yachama Gabriel wrote:
Unataka kufanyiwa kila kitu, uzembe, uende kutafuta website ya serikali, idara ya utumishi, utazipata. Kupenda kutafuniwa ni uzembe. Unataka uelekezwe kila kitu halafu uanze kubisha kama vile unajua, kwavile hutapata taarifa kamili. Tafuta, soma mwenyewe na ndipo uje kubishana hapa ukiwa fully informed.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Zantel Etisalat Tanzania.

From: Mathew Bukhi <bukhimathew@gmail.com>
Date: Fri, 25 Jan 2013 21:26:50 +0300
Subject: Re: [wanabidii] DIALLO: WATENDAJI SERIKALI WATAKAO SHABIKIA UPINZANI KUSHUGHULIKIWA.

Chifu Bariki,

Kwanza ni Bukhi na si Bhuki.

Vyema. Naomba sana unisaidie hizo sheria na taratibu zinazoruhusu mfumo wa chama dola katika vyama vingi.
Nitashukuru, hata ukinitajia tu, nitazitafuta mwenyewe.

Wasalaam.

On Friday, January 25, 2013, Bariki Mwasaga wrote:
Bhuki

Ni Sheria na Taratibu zilizopo zinawaruhusu watumie kwani wako katika nafasi hizo kwa mujibu wa Sheria zilizopo siyo makosa yao hata kidogo.

2013/1/25 Mathew Bukhi <bukhimathew@gmail.com>
Chifu Bariki,

Mimi sijakataa hao wakuu kufanya siasa. Wasiwasi wangu ni juu ya kutumia mali za umma katika kufanya kwao siasa. Na hiyo ndiyo moja ya hoja iliyoletwa; kwamba watumishi wa umma wasitumie nafasi zao (ofisi na mali za umma walizokabidhiwa) kufanyia siasa za vyama.

Mimi sioni kuwa ni sahihi kwa waziri kutumia gari la umma kwenda kwenye shughuli za chama. Lakini hili jambo limeshakuwa ni kawaida; hivyo kubadilisha fikra hizo kunahitajika juhudi za ziada.

Bukhi.

On Friday, January 25, 2013, Bariki Mwasaga wrote:
Bukhi,

Rais, M/Rais, Wazir Mkuu, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawa ni Watumishi wa Umma lakini ambao wanaangukia kwenye wigo wa Siasa hivyo wao kufanya Siasa, Sheria na Kanuni zinawaruhusu sana tena sana kwani ndiyo utumishi wao ulipo. Lakini mtu kama mimi siruhusiwi kufanya Siasa kama wanazofanya wao, Siasa yangu mimi ipo nje ya eneo langu la kazi. Pia kama nimefikia kiwango fulani cha uongozi basi hata kule kujionesha inanibidi niache. Ndiyo maana leo hii wako watumishi wa Umma ambao ni Madiwani (wanasiasa) kwenye Halmashauri tofauti na zile wanazofanyia kazi kwasababu Sheria inaruhusu. Mtumishi huyo huyo akifikia ngazi ya Ukurugenzi/Ukatibu Tawala wa Wilaya/Mkoa ama Ukatibu Mkuu inabidi siasa za wazi aziache kwani kwa nafasi yake itaathiri utendaji wake kutokana na mitazamo ya wale anaowahudumia. Ndiyo maana leo hii mtumishi wa umma akitaka kugombea ubunge ni sharti aachie ngazi kwenye utumishi wa umma (Permanent and Pensionable). Hawa Wakuu uliowataja siyo Watumishi wa Umma wa ajira ya kudumu na mafao. Utumishi wao unatokana na uteuzi ambao muda wowote unaweza kutenguliwa ama kufutwa wakati wowote.

2013/1/24 Mathew Bukhi <bukhimathew@gmail.com>
Ndugu Tony, naomba niingilie mjadala.

Kanuni za ajira/utumishi wa umma zinatoa katazo kufanya siasa ofisi za serikali na pia kwa mtumishi wake kutumia nafasi yake, kama vile mwalimu kufundisha wanafunzi mambo ya kichochezi. 

Hivi hili katazo lipo kwa watumishi wa umma wa kada za kati na chini tu? Mbona kila mara twawaona mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wakitumia nafasi zao na mali za umma kufanya siasa? Tena hadi ilifika kipindi ikulu ikawa ukumbi wa mikutano ya chama cha siasa!! Si ajabu kuona mkuu wa wilaya ndani ya STK akiwa na shati la kijani akielekea Kizota! Si ajabu pia kumwona waziri akiwa ndani ya W U akielekea kupiga kampeni za Kafumu!

Eneo la shule, chuo, ni maeneo yaliyokatazwa shughuli za kisiasa. Mifano ipo mingi ya kuthibitisha: mwalimu anapoacha kufundisha hesabu au fizikia na kuanza kuhubiri ubaya wa chama fulani au serikali na uzuri wa kingine wakati sio mwalimu wa somo la siasa.

Kwa upande mwingine, kwa mfano mhadhiri wa sayansi za siasa pale UDSM anavyofundisha misingi na kanuni bora za demokrasia na siasa (ambazo pengine hazizingatiwi kwa hapa kwetu), hayo nayo yatakuwa mambo ya uchochezi? Au yasifundishwe kwa kuwa pengine haya apply kwa mazingira yetu?

Ndugu Diallo kakosea, kwani hata muongozo wa utumishi wa umma wa mwaka 2009 unasema - katika section B, kipengele B.9 - kwamba maamuzi na mapendekezo yoyote kutoka kwenye chama tawala, ambayo chama k
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
Sent from Gmail Mobile

0 comments:

Post a Comment