Thursday 24 January 2013

Re: [wanabidii] DIALLO: WATENDAJI SERIKALI WATAKAO SHABIKIA UPINZANI KUSHUGHULIKIWA.

Kama tumekubaliana kutoka nje ya mada, basi mi nasema Degree ya nje ya darasa (ya posta kama wengine wanavyoita) ni bora zidi kuliko ya kufundishwa. Kama mtu ameweza akakaa mwenyewe akafungua vitabu na kuproduce paper, huyo ndo anaweza kazi. Kitu si degree ya wapi (mjengoni au chini ya mti), bali huyo mtu mwenye degree yoyote ile halali ana deliver?
Vin

2013/1/24 Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Bart,

Sitaki kujadili PhD ipi ni nzuri kati ya posta au ndani ya kuta nne! Kwanza PhD ya posta haiwezi kuwa na hithibati na hata mimi nazipinga sana hizo. Lakini ukumbuke kuwa mfumo wa kutoa elimu umebadilika hapa duniani na kwa maoni yako hata digrii za OUT au UNISA (south afrika), sio digrii kwako ni ile ya "brick and mortar"! Angalia chuo alichosoma huyo unayemsema ulinganishe na cha kwako ndipo useme mapungufu yake. Hata hivyo hii sio mada yetu.

Siwezi kupingana na  mengine yote uliyoyasema kuhusu utumishi ila nikuombe usome kanuni za utumishi kazini toleo la 1995, na waraka wa watumishi wa 1998. Nakubaliana nawe mwananchi yeyote isipokuwa wafanyakazi wa vyombo vya usalama, hususani Jeshi na Police,  unaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama chochote.

Pia sheria ya vyama vya siasa kif.19 (1), hairuhusu kumzuia au kulazimisha mwananchi asiingie chama cha siasa isipokuwa niliowataja hapo juu. Diallo hawezi kuzuia waalimu au mfanyakazi yeyote wa serikali isipokuwa walio na katazo, kujiunga na chama chochote cha siasa.

Kanuni za ajira/utumishi wa umma zinatoa katazo kufanya siasa ofisi za serikali na pia kwa mtumishi wake kutumia nafasi yake, kama vile mwalimu kufundisha wanafunzi mambo ya kichochezi. Eneo la shule, chuo, ni maeneo yaliyokatazwa shughuli za kisiasa. Mifano ipo mingi ya kuthibitisha: mwalimu anapoacha kufundisha hesabu au fizikia na kuanza kuhubiri ubaya wa chama fulani au serikali na uzuri wa kingine wakati sio mwalimu wa somo la siasa.

Chama chako Bart kinajulikana kwa kuzuia wananchi wasitii sheria kanuni na taratibu, sioni ajabu kumwijia juu Diallo. Mlishatamka kuwa kazi yenu ni kufanya nchi isitawalike! Ni tamko lenu na hivyo hamtafurahia kuona taratibu au kufuata kanuni za utumishi sehemu za kazi.

Nimalizie kwa kusema kama alivyosema Mgonga, ushabiki umejaa kwenye mada hii na wote wanaosema kumpinga Diallo kwa bahati mbaya ni Chadema. Diallo atapata a fair advice toka kwa wana CCM wenzake, iwe hapa jukwaani au huko aliko. Hapa ni sawa na dua la kuku halifiki mwewe. Ushabiki unapunguza fairness na kuondoa maarifa.


------Original Message------
From: Bart Mkinga
Sender: wanabidii@googlegroups.com
To: wanabidii@googlegroups.com
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] DIALLO: WATENDAJI SERIKALI WATAKAO SHABIKIA UPINZANI KUSHUGHULIKIWA.
Sent: Jan 24, 2013 11:34

Mfanyakazi kama Mtanzania yeyote ana haki ya kuwa mwanachama au mpenzi wa chama chochote cha siasa alimradi hakiuki masharti ya ajira yake. Hakuna sharti linalosema asiwe shabiki, mwanachama au mpenzi wa chama cha siasa, anachozuiwa ni kufanya siasa kazini.   Viongozi wengi wa CCM, na hasa hawa wenye Udokta au PhD hizi za 'Elimu kwa njia ya posta', wanaitwa 'doctors' lakini fikra na matendo yao havina uhusiano wowote na upeo unaostahili wa PhD holders. Siasa zile za chama kushika hatamu ziliwaharibu, na walio wengi japo wanatamka kuwa tupo kwenye mfumo wa vyama vingi lakini akili zao bado ni za chama kimoja, chama dola. Hawa wanasubiria tu muda wao upite, hawawezi kubadilika. Wanayoyaona hawaamini maana daima waliamini kuwa CCM ni kila kitu, CCM ni serikali, CCM ni mahakama, CCM ni jeshi na CCM ni polisi. Hao ni kuwaombea, wapishe kwa amani, wakapumzike ili mawazo mapya yapate uwanja ulio safi unaoweza kuruhusu fikra mpya kuchipuka, kustawi na kisha kutoa matunda.   Bart
From: Lushengo Lutinwa <lutinwa@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, January 24, 2013 5:47 AM
Subject: Re: [wanabidii] DIALLO: WATENDAJI SERIKALI WATAKAO SHABIKIA UPINZANI KUSHUGHULIKIWA.

But why is he worried now? Anadhani njia kuelekea 2015 is rough for him now? Alichomaanisha ilikuwa intimidate za kitoto. Civilized community haziongozwi kwa vitisho, bali kwa kukumbushwa pale ambapo anadhani people are going the wrong way. Angetumia a sensible language, nadhani hii thread isingekuwepo. Lutinwa Sent from Samsung Tab 10.1 On Jan 24, 2013 3:51 AM, "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:
Vin,


Kifungu kipi unataka. Mfanyakazi wa serikali anajua, masharti ya kazi PSG, inazuia nini au kuruhusu kitu kipi. Wajibu ni wa kwako kusma.

Wanajaribu kuingiza kifungu cha 19 (1) cha sheria za vyama kinachokataza kulazimisha mtu kujiunga na chama cha siasa. Diallo hasemi hivyo, anataka watumishi wafuate sheria na kanuni za kazi, basi.

Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile Black
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment