Sunday 6 January 2013

Re: [wanabidii] Deogratius Kisandu : UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI

Kwangu mimi, Kisandu si mwanachama ambaye kuondoka kwake CHADEMA liwe ni jambo kubwa sana la kujadiliwa. Alikuwa mwanachama wa kawaida na alikuwa na nafasi ya uongozi wa kawaida (siyo nafasi ya juu) katika chama kiasi cha kutoathiri kwa vyovyote vile utendaji wa CHADEMA.
 
Sioni hata kama kulikuwa na umuhimu hasa wa kuwaita waandishi wa habari kuelezea sababu za kuondoka kwake. Viongozi wa vyama vya siasa ni muhimu kuwa na hekima, hakuna ulazima wa kutoa tuhuma dhidi ya viongozi waliokuwa nao kwa muda mrefu kila wanapohama. Hata kueleza tu kuwa nimeamua kuhama chama hiki na kwenda chama kile kwa vile ninaamini chama ninachohamia kinaendana na mtizamo na imani yangu inatosha. Unapoanza kutoa msululu wa tuhuma ndefu dhidi ya viongozi au chama ulichotoka inakufanya upuuzwe na kuonekana kupungukiwa na hekima. Miaka yote umekaa kwenye chama hicho, hukuyaona yote unayoyasema mpaka siku ulipoamua kuhama? Kiongozi mahiri ni yule ambaye popote awapo hujitahidi kushirikiana na wenzake katika kutatua na kupata ufumbuzi wa yale anayoamini kuwa hayapo sawa. Na kama ukiona yale uyatakayo hayatekelezwi, unaondoka bila ya kulazimika kuweka tuhuma msululu dhidi ya wale uliokuwa nao kwa muda mrefu. Wanasiasa vijana pevukeni na jifunzeni kuwa na hekima.
 
Kuhama chama, kujiunga na chama au kutokuwa mwanachama wa chama chochote si kosa, na ni haki ya kikatiba. Lakini kuhamahama chama kila mara kunasababisha maswali mengi juu ya hekima ya mhusika maana kuwa na haki ni tofauti na kuwa na hekima. Ukipenda unaweza kuhama chama kila mwezi, ni haki yako lakini ukifanya hivyo utaonekana au huna hekima au kichwani kuna walakini.
 
Bart.
From: Bakari Maligwa Mohamed <maligwa1968@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, January 5, 2013 1:20 PM
Subject: Re: [wanabidii] Deogratius Kisandu : UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI
...Ibara ya 20(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 (Toleo la 2005) inatanka kwamba, "Itakuwa marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote...." kwa maana hiyo, Deogratius Kisandu alijiunga CGADEMA kwa hiyari yake na vilevile amejivua uanachama wa CHADEMA kwa hiyari yake; na amejiunga NCCR -MAGEUZI kwa hiyari vilevile! Tatizo lipo wapi? Huo ndio uhuru wa kuwa na maoni (Ibara ya 18(a) ya Katiba ya JMT, 1977 Toleo la 2005).
 
Kisandu hana makosa; na hakuna anayeweza kuhoji uamuzi wake wa kuachana na CHADEMA na kujiunga na NCCR - MAGEUZI au vinginevyo. Kama kuna mtu anayetaka kuhoji uamuzi wa Deogratius Kisandu atakuwa amekiuka haki ya msingi ya Kisandu kwa mujibu wa Katiba ya JMT ya 1977 (Toleo la 2005). Kila mtu yupo huru kufanya maamuzi yanayomuhusu yeye (binafsi) na asiingiliwe na mtu kwa uamuzi wake. Nadhani tuna wajibu wa kukomaa "kidemokrasia" na kukubali maamuzi ya watu wengine.
 
Hakuna kulazimishana kujinga na chama chochote; uamuzi wa mtu (binafsi) ndio msingi wa haki ya mtu kuchagua chama cha kujiunga. Hoja ya kwamba Depgratius Kisandu ni "mgonjwa" au vinginevyo ni "muflisi." Haki ya mtu kuamua anavyotaka bila kulazimishwa ni muhimu kuzingatiwa; na hivyo ndivyo ilivyo "haki ya mtu binafsi katika kuamua hatma yake bila kuathiri haki ya watu wengine."

From: Elias Msuya <emsuya2001@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, January 5, 2013 11:32 AM
Subject: Re: [wanabidii] Deogratius Kisandu : UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI
Tony,
Mwandishi kuwa shabiki maana yake nini? Kwa hiyo Meena angemuunga mkono Kisandu ndiyo ungeona yuko fair? Naomba ufafanuzi wako.


--- On Sat, 1/5/13, Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Deogratius Kisandu : UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Saturday, January 5, 2013, 12:27 AM

Mr Meena, Kawa mgonjwa kwa kuamua kutoka chadema au kwa kuwa sababu moja inayomtoa huko ni kugombea urais? Mgonjwa kwa lipi? Nchi hii imekwisha; wana habari wanakuwa na upande waziwazi a ushabiki wa kisiasa wakati wanadai ni mhimili wa 4 wa nchi! Wakituaminisha hawana ushabiki wa chama cha siasa. Mnaonaje majaji nao wakawa wanasiasa? Au wanahabari nao mnaungana na wabunge/madiwani kuwa kwenye mhimili wenye kufuata itikadi fulani? Ni wakati sasa wanahabari wasidai uhuru wa mawazo na kudai kuwa hawafungamani na upande wowote wa vyama. Kuna mtu mmoja anafanya utafiti kuangalia habari zinazoandikwa na vyombo vya habari Tanzania ni kwa kiwango gani zipo huru au zinaegemea upande upi zaidi. Tusubiri matokeo ambayo yanatarajiwa mwisho wa mwaka huu. Utafiti huo utatusaidia sana kuelewa Katiba yetu itakaaje kwenye suala la uhuru wa vyombo vya habari na waandishi wenyewe. ------Original Message------ From: nevilletz@gmail.com Sender: wanabidii@googlegroups.com To: wanabidii@googlegroups.com ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com Subject: Re: [wanabidii] Deogratius Kisandu : UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI Sent: Jan 5, 2013 10:15 More than sick! Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania From: Paschal Leon <paschalleon@yahoo.com> Sender: wanabidii@googlegroups.com Date: Fri, 4 Jan 2013 21:19:49 -0800 (PST) To: <wanabidii@googlegroups.com> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com Subject: Re: [wanabidii] Deogratius Kisandu : UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI THIS KISANDU MUST BE SICK; VERY SICK --- On Fri, 1/4/13, KULWA MAGWA <magwakulwa12@gmail.com> wrote: From: KULWA MAGWA <magwakulwa12@gmail.com> Subject: Re: [wanabidii] Deogratius Kisandu : UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI To: wanabidii@googlegroups.com Date: Friday, January 4, 2013, 8:17 PM Mhhh makubwa haya tusubiri tuone hili picha litaishaje! 2013/1/5 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UAMUZI WANGU WA KUJIUNGA NA NCCR – MAGEUZI Ndugu wanahabari, Mimi ninaitwa Deogratius Kisandu, nimehitimu katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa huko Lushoto (SEKUCO) nina Shahada ya Elimu Maalum, Siasa na Utawala. Nilikuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA katika nafasi za; Katibu wa Wilaya ya Lushoto na Katibu wa Vijana wa Mkoa wa Tanga (Bavicha). Mwaka 2010 niligombea ubunge katika jimbo la Lushoto, nilishika nafasi ya pili kwa kupata kura 5000+ dhidi ya mgombea wa CCM aliyepata kura 14000+ . Ndugu wanahabari,  Kwa muda mrefu nikiwa ndani ya CHADEMA, tumekuwa katika maelewano mabaya na hata pengine kujengewa chuki na fitina pale nilipojaribu kuhimiza viongozi wenzangu kufuata katiba ya Chama chetu. Mwishoni mwa mwaka jana (2012) niliamua kujivua uanachama ndani ya CHADEMA na kuahidi kujiunga na Chama kingine.Vile vile nilisema siku hiyo nitaeleza sababu za msingi zilizonifanya nijivue uanachama na kukabidhi kadi ya Chama hicho. 1. Mnamo mwaka 2012 nilitangaza nia yangu ya kugombea urais kupitia CHADEMA. Msimamo huo umenijengea chuki na uhasama kwa viongozi wakuu wa CHADEMA akiwemo muasisi wa Chama hicho Mzee Edwin Mtei, kupinga vijana kuonesha dhamira zao. Nimejiridhisha kwamba, CHADEMA ina watu wake inaowataka wagombee urais na hususan wa Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network. Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell. -- Jobs in Africa - http://www.wejobs.blogspot.com/ International Jobs - http://www.jobsunited.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment