Sunday 6 January 2013

Re: [wanabidii] COSTA YAGONGANA NA LORI USO KWA USO GAIRO

Hildegarda
 
Samahani umetumia neno "kusarandasaranda" hivi maana yake ni nini? Nisamehe bure.
 
K.E.M.S.
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, 5 January 2013, 10:57
Subject: Re: [wanabidii] COSTA YAGONGANA NA LORI USO KWA USO GAIRO

Jinsi uchumi unavyozidi kukua na bandari yetu kutumika na nchi jirani na watu kununua malori kuja bandarini DSm ndivyo ajali zitakavyozidi kama wizara ya miundo mbinu haitojifunza na kuiga wenzetu ulaya, na kama tutaendelea kukimbizana barabarani bila kuzingatia usalama wetu. Mtu unapanda basi la abiria BP juu huna raha mpaka ushuke. Dreva anaovertake hovyo akiambiwa unaambiwa shuka utarudishiwa nauli yako. Anaovertake kilimani au bondeni hata kwenye kona asiambiwe na baadhi ay abiria watakuzomea kama unatoa maonyo kila unapoona uzembe. anaendesha gari huku anaongea na simu na kubofya simu kutuma message. Tabia hizi sijui tutajirekebisha lini? Na bado yapo mabasi ya abiria ambayo ni malori wamekarabati na kuweka viti vya vyuma ambavyo vimebanana na ukikaa vinaumiza makalio jinzi vilivyo hard. Na vyuma vyake ikitokea ajali vinaingia watu mwilini na kuwamaliza. Mlio wa lori unasikika kabisa bus linavyotembea na yanayumba hasa. Lakini yapo.

Hata kujazana katika boat-inaendelea mpaka watu kusimama katika mtumbwi na wapo ndani ya ziwa au bahari wanasimama na kushika mlingoti kupanua miguu kuegemeza pande mbili kubalance mtumbwi.

Ikiwezekana GVt iige wenzetu Ulaya-mbona wanasafiri na kuona? Watengenezi na kuweka barabara ya kutoka Mbezi Kimara-Majowe-Wazo hill au ya kutoka Mlandizi-Wazo-Bagamoyo ili malori yatokayo bara yaendayo wazo yasiingie mjini msongamano na kukanyaga waliopanga biashara Tegeta -wazo maana ajali za malori kupiga hodi majumbani haziishi. Itoke gari Mbezi Temboni-Mlonganzila-Pugu Road-Ukonga Kipunguni-Kurazini-Bandarini. yasipite Ubungo-Bugurini-Tanzara-Kurasini. Hii itapunguza msongamano ya ajali maana magari kutoka bandarini yana mizigo na petroli na daladala zinasarandasaranda kuovertake wawahi njia wanapigana pasi na malori ya mafuta. Ipo siku lori la mafuta litagongana nan gari kupinduka na kulipuka nan tutapoteza binadamu wengi, majumba kuwaka moto na msururu wa magari katika foleni kuteketea. Budi tuige Ulaya highway ya malori na magari mengine ya mizigo ni njia yao wao tu ya kwenda upande mmoja haikutani na ya kurudi. Vivyo hivyo ya magari mengine ya abiria mstari wake na ya aina nyingine mstari wake, pikipiki na bajaji mstari wake hakuna kuingia barabara ya magari na kusarandasaranda magari bodaboda kugonga watu wakatizao kwa kwenda zigzag.Wafuate alama ya bodaboda ndio wapite njia hiyo wao, baiskelina bajaji. Mbona wenzetu wameweza na shule maafisa miundombinu wamesomea huko ulaya? Tubadilike tupunguze ajali hata hizi za moto na ujenzi mbanano moto unalipuka mara 3 tukirudia kujenga tunabananisha zaidi majengo; mafuriko yanakuja na kutuzamisha kisha tunarudia kujenga humo humo. Unajenga kuta huachi njia ya maji kwa kuweka tunnels unajaza concrete chini kubwa na maji yanajaa barabarani na kuongeza foleni ya masaa 5 badala ya mwendo wa saa moja. Na unaelewa kabisa unajenga kwenye mapito ya maji au bondeni na unaziba njia ya maji na kuleta madhara hata kwa jirani. Lini tutabadilika kimatendo?


--- On Fri, 4/1/13, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] COSTA YAGONGANA NA LORI USO KWA USO GAIRO
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, 4 January, 2013, 14:38

Taarifa zinasema kuna costa iliyokuwa na abiria imegongana uso kwa usona Lori maeneo ya Gairo katika kijiji kinachoitwa Ngirori .Katika ajali hiyo dereva wa Costa amevunjika miguu yote miwili .-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.comInternational Jobs - www.jobsunited.blogspot.comKujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatumaDisclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment