Sunday 9 December 2012

[wanabidii] Wagonjwa sasa walazimika kwenda na shuka Muhimbili

"Hali ya huduma kwa wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam si shwari, sasa wagonjwa wanalazimishwa kwenda na shuka. 
Inaelezwa kuwa hatua hiyo inatokana na kile kinachoelezwa kuwa ni hali ngumu ya kiuchumi inayosababisha uhaba wa vifaa zikiwemo shuka.
Uchunguzi wa NIPASHE Jumapili ulibaini kuwepo idadi kubwa ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kutoka mikoani, wakilala kwenye vitanda vyenye 
magodoro yasiyotandikwa shuka. Mbali na kukosa shuka, magodoro hayo yalikuwa machafu, hali inayoelezwa kuwa kinyume cha kanuni za afya na matibabu".

Nchi hii kama hatujachinjana hapa mambo hayatokaa sawa, kwasababu huu mchezo sio mzuri hata kidogo. In fact, huu ni ujinga. 
Juzi tulikuwa na pesa za kupeleka kikosi kizima DR Congo kumuokoa Bw. Kabila, leo hata senti 5 hatuna za kununua shuka hospitalini!
Oh my God! 

...bin Issa

0 comments:

Post a Comment