Wednesday 5 December 2012

[wanabidii] TAHADHARI DHIDI YA BARUA ZA KUGUSHI ZA KUPANGIWA VITUO VYA KAZI ZINAZOTOLEWA KWA WATAALAMU WA KADA ZA AFYA

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekuwa ikiwapangia vituo vya kazi wahitimu wa Kada za Afya tangu mwaka 2005/2006.    Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na Matapeli wanaowarubuni na kuwaibia fedha baadhi ya waombaji wa kazi kwa lengo la kuwapangia vituo vya kazi vya Uuguzi na Wahudumu wa Afya.

Wizara inapenda kuwaarifu wananchi hususan wahitimu wa Kada mbalimbli za Afya kuwa:-

1.      Kwa mwaka 2012/2013 Wizara bado haijapata Kibali cha kuwapangia Vituo vya kazi.  Kibali hicho kitakapotolewa wananchi watatangaziwa utaratibu wa jinsi ya kuomba kupitia Runinga, Magazeti, Radio na Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz).

2.      Wizara itabadili mfumo wake wa utoaji wa barua za kupangiwa vituo vya kazi ambapo kuanzia sasa waombaji hawatapewa barua za kupangiwa vituo vya kazi bali majina ya waombaji na vituo walivyopangiwa yatatolewa kupitia Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz) na wahusika watatakiwa kwenda kuripoti katika vituo walivyopangiwa baada ya kuona majina yao kupitia mtandao.

3.      Upangaji wa vituo vya kazi hauwagharimu fedha yoyote.  Hivyo, waombaji wote msitoe fedha yoyote kwa ajili ya ahadi kuwa utapata ajira na mnatakiwa kuwa makini na matapeli hao.

Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
03 DESEMBA, 2012

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment