Sunday 23 December 2012

[wanabidii] Re: RAIS J.M.KIKWETE ANATAKIWA AMPISHE DR.SLAA IKULU

Mtu akileta hoja mbadala sio lazima awe CCM au CUF anaweza kuwa hata
chama kama mimi , pia nimeuliza kuhusu Kunyimwa kura nyumbani kwake
pale kinondoni makao makuu ya CHADEMA maana hata diwani anatoka chama
tofauti mbunge chama tofauti hili suala linaleta ishara gani ?

Pili suala la utendaji usihukumu JK tu , Dr slaa ana halmashauri
kadhaa , ana majimbo kadhaa ya ubunge na madiwani , je huko kote
amefanya nini au wamefanya nini ? watuambie na hata wewe mwenyewe
ndugu lawala au vincent mnaweza kutusaidia kutupatia walichoahidi na
kutekeleza au vinavyoendelea kutekelezwa sio blaa blaa .

Wenzenu juzi wameahidi kutangaza mafanikio yao kupitia TV na vyombo
vingine vya habari mkapiga kelele , pale makao makuu yenu kuna CHADEMA
TV hakuna mtu aliyewahi kuipigia kelele endelezeni hiyo itaweza kuleta
mafanikio na mabadiliko zaidi .

On Dec 23, 10:49 pm, nevill...@gmail.com wrote:
> Kwenye Mkutano Mkuu walijadili Chadema mwanzo mwisho. Kila aliyesimama alizungumzia Chadema. Aliyetaka kura nyingi alizungumzia chama hiki, halafu mnakibeza? Dk Kigwa hapo vp? Nilikuwa nakusabahi tu kaka, upo?
> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
>
>
>
>
>
>
>
> -----Original Message-----
> From: paul lawala <pasamila292...@gmail.com>
>
> Sender: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Sun, 23 Dec 2012 11:29:56
> To: <wanabidii@googlegroups.com>
> Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: Re: [wanabidii] RE: RAIS J.M.KIKWETE ANATAKIWA AMPISHE DR.SLAA IKULU
>
> Yona
>
> Huwa nikiwasikiliza majukwaani nyie watu wa CCM mnaongea lugha inayofanana
>
> Tukiwasoma mitandaoni mnaandika mistari inayofanana
>
> Si mtu mzima si kijana, ndiyo maana hata kwenye mkutano wa mkuu wa chama
> badala ya kujadili agenda zenye mashiko mlibakia kuongea lugha
> inayofananafanana
>
> 2012/12/23 Vincent Mhangwa <vmhan...@gmail.com>
>
> > Yawezekana kuna baadhi ya watu wanadhani wao wana michango sahihi zaidi
> > kuliko ya wengine, na kudhani kuwa wanachokiona na kuamini wao ni sahihi
> > zaidi.  Wewe ukiona hivi mwingine anaona vile. Sasa huyo JK anayecheka
> > cheka tu na kufungua ma gesti na ma bar na magorofa kila mahali ndo
> > wanamwona sahihi siyo? Mtu anaye jenga milimani na katika vyanzo vya maji
> > huku inchi ikilalamika kukumbwa na mabadiliko ya tabia inchi. Lo! hatuna
> > aibu. Bora Slaa hata kama chama chake hakina diwani katika makao makuu
> > (*ingawa hatusemi kura zake zilizochakachuliwa, badala yake tunasema eti
> > inchi ya kidemeokrasia!*)
> > Vin
>
> > 2012/12/23 Yona Maro <oldmo...@gmail.com>
>
> >> Walishindana kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 mmoja akashindwa mpaka leo
> >> amegoma kumtambua kwa kutangaza hadharani , sasa ndio aina ya viongozi
> >> tunaowataka kwenye nchi ya demokrasia kama yetu jamani ? Amekuwa mbunge kwa
> >> karibu miaka 15 na kugombea urais mara moja , wenzake wote wamejiuzuru au
> >> kuwa washauri tu hawanganganii nafasi yoyote ndani ya vyama vyao wala
> >> popote pale .
>
> >> Na hawa ndugu zetu wanaotetea dr slaa kuingia kwenye nafasi hii hawajui
> >> mengi wanajibu kutokana na maslahi yao katika chama ambacho makao makuu
> >> yake diwani wake ni wa chama tawala , mbunge ni wa chama tawala , waanze
> >> kwa kukomboa sehemu hizo mbili .
>
> >> 2012/12/23 Vincent Mhangwa <vmhan...@gmail.com>
>
> >>> Jamani, tusilete unyanyapaa na ubaguzi wa umri. Kinachotakiwa ni busara
> >>> ya uongozi si umri. Lakini mimi nimefurahishwa sana na hoja ya Kikwete
> >>> kumpisha Dr. Slaa, wala hii siyo hoja dhaifu. Hoja dhaifu ni zile
> >>> zinazolenga kuwakumbatia mafisadi hadi wengine wanataka kugombea uongozi
> >>> 2015 kupitia CCM.
> >>> Vin
>
> >>> 2012/12/23 <hkigwanga...@gmail.com>
>
> >>> **
> >>>> Kumekuwa na tabia ya watu kuleta hoja dhaifu sana na za kitoto hapa
> >>>> jukwaani, hivi Yona hawa wanachama wa hivi huwa unawatoa wapi?
>
> >>>> Slaa amechoka na hana hoja tena siku hizi, awaachie vijana makini kama
> >>>> akina Zitto wafanye kazi ya kueleweka, yeye akalee watoto wake tu na
> >>>> mchumba wake Jose.
>
> >>>> Kama hana kazi nyingine ya kufanya arudi shuleni akasome Bachelor
> >>>> degree ili ahalalishe ile Ph.D yake aliyoipata akitokea Diploma!
>
> >>>> Urais wa nchi haupewi pewi tu, unatafutwa kwa wenye nchi. Mwambieni
> >>>> Slaa akatafute walau Urais wa NGO kama anatamani sana hiyo title
> >>>> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
> >>>> ------------------------------
> >>>> *From: * GILL DAVID <gilldav...@yahoo.co.uk>
> >>>> *Sender: * wanabidii@googlegroups.com
> >>>> *Date: *Sun, 23 Dec 2012 09:29:17 +0000 (GMT)
> >>>> *To: *<h...@muhas.ac.tz>; <m...@mum.ac.tz>; <i...@mzumbe.ac.tz>; <
> >>>> i...@out.ac.tz>; <i...@ruco.ac.tz>; <mfumb...@yahoo.com>; <
> >>>> vcs...@saut.ac.tz>; <admiss...@saut.ac.tz>; <stmarksad...@sjut.ac.tz>;
> >>>> <gchel...@sjut.ac.tz>; <ad...@sjut.ac.tz>; <s...@suanet.ac.tz>; <
> >>>> v...@suanet.ac.tz>; <d...@suanet.ac.tz>; <dvcadmin...@suanet.ac.tz>; <
> >>>> f...@suanet.ac.tz>; <i...@suanet.ac.tz>; <sua...@suanet.ac.tz>; <
> >>>> sc...@suanet.ac.tz>; <pest...@suanet.ac.tz>; <p...@suanet.ac.tz>; <
> >>>> p...@suanet.ac.tz>; <supp...@suza.ac.tz>; <i...@teku.ac.tz>; <
> >>>> dpacade...@duce.ac.tz>; <elctsmm...@smmuco.ac.tz>; <
> >>>> i...@butmaninternational.com>; <sematangoto...@cybernet.co.tz>; <
> >>>> serenacarh...@habari.co.tz>; <sgres...@yahoo.com>; <s...@habari.co.tz>;
> >>>> <to...@albatros.co.tz>; <m...@albatros.co.tz>; <i...@chadema.or.tz>; <
> >>>> rassing...@pmoralg.go.tz>; <mhar...@habarileo.co.tz>; <
> >>>> advertis...@dailynews.co.tz>; <jen...@albatros.co.tz>; <
> >>>> shido...@yako.habari.co.tz>; <sssafa...@cybernet.co.tz>; <
> >>>> s-s.kol...@web.de>; <wanabidii@googlegroups.com>; <
> >>>> unasem...@radiofreeafricatz.com>; <mwananchipap...@mwananchi.co.tz>; <
> >>>> globalpublish...@dar.bol.co.tz>; <educ...@intafrica.com>; <
> >>>> cost...@costech.opc.org>; <i...@satif.or.tz>; <i...@satf.org>; <
> >>>> e...@raha.com>; <e...@cats-net.com>; <zi...@chadema.or.tz>; <
> >>>> worldtourstanza...@hotmail.com>
> >>>> *ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com
> >>>> *Subject: *[wanabidii] RE: RAIS J.M.KIKWETE ANATAKIWA AMPISHE DR.SLAA
> >>>> IKULU
>
> >>>> Kama CCM inakubali kuwa Dr. Slaa ana kadi ya CCM na ni mwanachama hai
> >>>> basi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anapaswa apumzike kipindi hiki
> >>>> kilichobaki cha uongozi ampishe Dr Slaa aingie ikulu amsaidie kumalizia mda
> >>>> huu uliobaki kusafisha uchafu uliopo ndani ya chama na Serekali kwani yeye
> >>>> mheshimiwa Kikwete ameshindwa.Kama Dr Slaa aliweza kuwataja Mafisadi  pale
> >>>> Mwembe Yanga tuna imani naye zaidi kuwa ataweza kupambana nao kuliko
> >>>> Mheshimiwa Kikwete ambaye ametajiwa kabisa Wezi wa mali za Umma lakini
> >>>> anakaa nao meza moja na kula bila kuwachukulia hatua zozote.
>
> >>>> Watanzania wengi tungelijua hilo Mapema kuwa Dr Slaa anayo kadi ya CCM
> >>>> tungeandamana mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asiingie Ikulu kwani hata
> >>>> kwenye kura za uchaguzi vyombo vingi vya kusimamia uchaguzi kutoka nje ya
> >>>> nchi vilishatamka kuwa Dr Slaaa ndiye alikuwa anaongoza kwa kuwa na kura
> >>>> nyingi lakini Serekali ikachakachua matokeo. Uwezo wa kiutawala wa Dr Slaa
> >>>> ni bora mara mia moja kuliko wa mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ndio
> >>>> maana hata midahalo anaikwepa. Dr Slaa ndiye anafaa kuiongoza nchi mara
> >>>> dufu kulikoni JK.
>
> >>>> Ukiangali sana kila Kiongozo yeyote wa Upinzani wote wametokea CCM na
> >>>> kuanzisha vyama vingine. Wote lazima walikuwa na Kadi za CCM. Sasa
> >>>> inaelekea wengine walitupa kadi zao ama kwa kuwa walikuwa hawazilipii au
> >>>> pengine wanadaiwa na CCM kuzilipia kadi hizo jambo ambalo Katibu Mkuu wa
> >>>> CCM Ndugu Nape Mnauye anatakiwa afuatilie madeni badala ya kupiga kelele
> >>>> hovyo kwa mtu aliyelipia kadi yake na hana deni kama Dr Slaa. CCM ni chama
> >>>> Mama wa vyama vyote. Hivyo mimi sioni sababu ya wao kupiga kelele eti Dr
> >>>> Slaa ana kadi ya CCM. Kadi ile inaweza kuwekwa kwenye jumba la Makumbusho
> >>>> ya chama cha CHADEMA kila mtu ajue jinsi gani Katibu wao alivyokuwa
> >>>> mwadilifu kwa kulipia kadi yake ya uanachama kwa miaka zaidi ya 20 kwa
> >>>> wakati mmoja.
>
> >>>> Serekali ya CCM ina tabia ya kuwafanya Watanzania kuwa wajinga na
> >>>> pengine wapumbafu. Nchi ina mjadala wa fedha zilizofichwa nje. Fedha ambazo
> >>>> zimeyumbisha uchumi mzima wa Taifa. Badala viongozi wa CCM na Serekali yake
> >>>> kujadili jinsi ya kuzirudisha fedha zile zisaidie kuongeza madarasa ya
> >>>> watoto wengi waliofaulu na hawana madarasa wao wanaingiza nchi kwenye
> >>>> mijadala isiyo na tija. Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM hata kwenye pochi yake
> >>>> kunamuathiri nini mkulima na mfanyakazi wa Tanzania, au mtoto wa Kitanzania
> >>>> au mfanya biashara wa Kitanzania. CCM acheni mijadala isiyo na tija.
> >>>> Tumewachoka. Porojo mingi sana. Kama mnataka mbaki madarakani jadilini
> >>>> yafuatayo mjinusuru mwaka 2015.
>
> >>>> -Fedha zilizopatikana kwenye mashirika ya umma mliyoyauza ziko wapi?
>
> >>>> -Fedha zilizopatikana kwenye viwanda vya umma mlivyouza ziko wapi?
>
> >>>> -Fedha zilizopatikana kwenye wanyama mliowawinda na kuwauza nje ziko
> >>>> wapi?
>
> >>>> -Fedha zilizopatikana kwenye shamba za umma mlizouza ziko wapi?
>
> >>>> -Fedha zilizopatikana kwenye nyumba za umma mlizouziana ziko wapi?
>
> >>>> -Fedha zilizopatikana kwenye migodi ya umma zimefanyia kazi gani?
>
> >>>> -Fedha zilizopatikana baada ya kuuza Ranch za Taifa ziko wapi?
>
> >>>> -Fedha zilizofichwa nje ya nchi mnazirudisha lini ziongeze madarasa na
> >>>> maabara ya wanafunzi?
>
> >>>> -Fedha za mapato na matumizi ya Serekali ya miaka yote 51 mliyokaa
> >>>> madarakani lini mtaziweka wazi kwenye magazeti ya umma kama Uhuru, Mzalendo
> >>>> na Daily News.
>
> >>>> -Fedha zinazopatikana kwenye Hifadhi zetu za Taifa na Milima iliyopo
> >>>> Tanzania lini mtaziweka wazi kwa Watanzania?
>
> >>>> -Fedha mlizopata baada ya kuuuza ardhi ya Tanzania kule Loliondo lini
> >>>> mtaziweka wazi?.
>
> >>>> -Fedha mlizopata baada ya kuuza Bandari ya Mtwara lini tutazijua sisi
> >>>> Watanzania?
>
> >>>> -Fedha zilizopatikana baada ya kuwekeza Viwanja vyetu vya Ndege lini
> >>>> mtaziweka hadharani tuzijue?
>
> >>>> -Vitalu mnavyowinda wanyama mtatujulisha lini mapato yake?.
>
> >>>> -Mtatutajia lini Wabunge na Mawaziri wanaofanya biashara wakiwa kwenye
> >>>> nyadhifa za umma. Tunawajua wanaojenga mahoteli, wanaofanya biashara za
> >>>> mafuta, Usafirishaji nk.
>
> >>>> Mkiweza kuweka mambo haya bayana nina uhakika mtabaki madarakani
> >>>> vinginevyo 2015 jitoeni tu wagombea wabaki ya vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR,
> >>>> TLP, SAU nk. CCM Tanzania mmepoteza uelekeo na imani kwa Wananchi. Mkiona
> >>>> mtu anawashabikia labda ni mmoja wenu, au mpambe, au ana hisa na kampuni
> >>>> zenu, au ni muwekezaji, au mkwepa kodi, au mtoto wenu, au Zuzu, au mchumia
> >>>> tumbo, au anawapa
>
> ...
>
> read more »

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment