Tuesday 18 December 2012

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Re: Serikali ya CCM kutumia ITV, Star TV na TBC1 Kueleza mafanikio ya Serikali - William Lukuvi

Haya (kwa mtazamo wangu) ni miongoni mwa yanayosababisha CCM na serikali ichukiwe. Na Mwenyezi Mungu anisamehe inastahili kuchukiwa.

Sioni sababu kama Mwakyembe amefanikisha kufungua usafiri wa reli Dar es Salaam (muujiza), alipiwe ili akatangaze! Nini? Kwa ajili ya nani?

Halafu hata wakitumia mabilioni ya Shilingi kwa matangazo, kama Nanyamba kule Mtwara wanakunywa maji yenye tope, Kojani kule Pemba hakuna vyoo na uwezo wa kiuchumi unaotegemea uvuvi ni mdogo, kama eneo kubwa la nchi lina hayo Seleman anayoyaita majengo, yawe kwa mfano wa shule zisizo na walimu na vifaa, ama zahanati zisizo na wataalamu wa afya, dawa ama vifaa vya tiba, na tamka jingine lolote, ina maana gani?

Mimi nadhani bado kuna haja kwa serikali kutafuta namna bora ya kuwajibika kwa umma. Wakibaki na fikra za ki-Lukuvi Lukuvi, kukimbilia matngazo yenye takwimu za kupikwa, watazomewa, hata kama hawatasikia kwa maana watakuwa kwenye runinga, lakini aibu itabaki kuwa juu yao.

Ni suahuri tu, waachane na mkakati huo, wafanye kazi ili Watanzania wawapime kwa matokeo ya kazi zao.


--- On Tue, 12/18/12, Selemani Rehani <srehani@hotmail.com> wrote:

From: Selemani Rehani <srehani@hotmail.com>
Subject: [Mabadiliko] Re: Serikali ya CCM kutumia ITV, Star TV na TBC1 Kueleza mafanikio ya Serikali - William Lukuvi
To: "mabadiliko Tanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, December 18, 2012, 3:25 AM

 
Ndugu zangu,
 
Jana nilikuwa mapumziko kidogo, nakapata nafasi ya kumsikiliza Waziri Lukuvi katika kipindi cha kumekucha ITV. Kwa ufupi alisema kuwa Serikali ya awamu ya nne imepata mafanikio makubwa sana ila wananchi hawayajui. Hivyo wameamua kuja na wazo la ubunifu, kuanzia siku chache zijazo, kutakuwa na vipindi maalumu kwa muda wa nusu saa ambapo Mawaziri mbalimbali watatumia muda huo kueleza mafanikio yaliyopatikana kupitia TV stations zifuatazo ITV, TBC1 na Star Tv. Hili ni zoezi endelevu mpaka 2015. Wazo hili ni moja ya maazimio yaliyotokana na Mkutano mkuu wa CCM uliofanyika hivi karibuni. Akawaomba wananchi wasikose kuangalia vipindi hivi.
 
Hivi kama kuna mambo mazuri si yanaonekana tu?? mpaka myatangaze?
 
Hivi wakati wananchi wanakabiliwa na changamoto lukuki kuwahubiria mafanikio si kuwadhihaki? watu hawana maji, hawana makazi ya mazuri, rushwa na ufisadi vimekithiri wewe unazungumza ujenzi wa barabara na majengo (wengine wanaita shule, lakini sio shule, yale ni majengo. Shule ni ile inayotoa elimu na ina mazingira ya kutoa elimu) ambayo hayana waalimu, hayana vitabu wala maabara!!! 
 
Jitayarisheni kuelemishwa juu ya mafanikio ya CCM.
 
Selemani

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group, send email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment