Friday 14 December 2012

[wanabidii] JUU YA MWENENDO WA UNDUMILAKUWILI WA BWANA WILBROD PETER SLAA KATIBU MKUU WA CHADEMA TAIFA

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, WANACHADEMA NA UMMA WA WATANZANIA JUU YA 
MWENENDO WA UNDUMILAKUWILI WA BWANA WILBROD PETER SLAA KATIBU MKUU WA 
CHADEMA TAIFA.* 

Ndugu wanahabari rangi nyeupe katika bendera chama changu ninachokipenda 
(CHADEMA) chama changu ninachokipenda inasimamia ukweli na uwazi. Rangi 
hiyo inawataka wanachadema wote kuwa wazi katika kulinda, kusimamia 
falsafa, itikadi na sera za chama chetu. 

Nimehuzunishwa sana ka kukatishwa tama na kitendo cha undimilakuwili na 
umamluki wa Katibu Mkuu Bwana Slaa kwa kitendo chake cha kuendelea kumiliki 
kadi ya Chama cha Mapinduzi wakati akitambua kuwa yeye ni Kiongozu 
anyeongoza harakati za chama Kikuu cha Upinzani hivyo kutakiwa kuwa mfano 
bora wa kuigwa kwa kuonyesha mwenendo bora kwa kuishi maisha anayohubiri. 

Katiba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sura ya tano ibara ya 
kwanza ndogo ya 5.1.6 kinachosema "Mwanachama wa CHADEMA asiwe mwanachama 
wa chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA" Akitambua kadi 
ndicho chombo kikuu kinachomtambulisha mwanachama ndani ya chama hivyo, 
kitendo cha kuendelea kumiliki na kulipia kadi *Chama cha 
Mapinduzi*kimedhihirisha kuwa yeye ni mbwa mwitu aliyejivika ngozi ya 
kondoo ndani ya 
upinzani. 

 Bwana Slaa amekuwa akiaminisha Umma kuwa yeye ni Kiongozi mzalendo safi 
huku akiendelea kuwatuhumu baadhi ya wanachama na viongozi wenzie kuwa ni 
mapandikizi,Hivyo kitendo hicho cha yeye kumiliki na kulipia ya CCM 
imeonyesha kuwa yuko CHADEMA kwa kazi maalum ya kuhujumu harakati za 
Ukombozi hivyo hana na amepoteza sifa ya kuwa Kiongozi wa Upinzani. Kwa 
mujibu wa Katiba ya CHADEMA ibara ya tano, BWANA WILBROAD PETER SLAA NI 
PANDIKIZI kutokana na sababu zifuatazo, ambazo nimejiridhisha nazo bila 
chembe ya shaka yoyote hivyo tunamuomba apishe uchunguzi dhidi yake ili 
tukiona dhamira njema tuendeleze harakati za Ukombozi yeye amepoteza sifa, 
kwa kitendo cha kuwa na Kadi ya chama ambacho kimetesa Watanzania na 
kuwanyanyasa lakini yeye bila aibu kukusanya kadi za wananchi wanaojiunga 
na CHADEMA kuzichoma moto na huku yeye akiwa amebaki na yake kibindoni hii 
imepelekea yeye kufanya kazi na umamluki na kukivuruga Chama kama 
ifuatavyo:- 

Amekuwa akitumika kugawa Mabaraza ya chama kwa kuidhinisha kumlipa mshahara 
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Ndugu JOHN HECHE kinyume cha Katiba na mwongozo 
wa baraza la Chama ilihali Viongozi wengine wa Kitaifa wa mabaraza hata 
wale wa Mikoani na Wilayani hawalipwi chochote wakati wao ndio 
wanaohangaika kukijenga Chama. 

Hii inaonyesha Bwana Slaa analipa fadhila kwa mwenyekiti huyo ambaye 
maamuzi yote ya baraza huamiliwa na Bwana Slaa, Mfano huu wakulipana 
fadhila anaoufanya Bwana Slaa ni mfumo wa CCM ambako Slaa ni mwanachama na 
baada ya kukiri kwamba ni kweli anamiliki Kadi ya CCM hadi leo hii. 

Bwana Slaa ni Kiongozi anyejihusisha na vikundi vya majungu jambo ambalo ni 
kinyume na Katiba na kanuni ya Chama kwa kudhihirisha kwamba Bwana Slaa ni 
mamluki ndani ya CHADEMA aliyekuja kutimiza kazi maalumu amekuwa akichochea 
mgogoro na kuchukua maamuzi ya kuwafukuza baadhi ya vingozi ambao 
wamekiongoza chama kwa muda mrefu. 

Bwana Slaa alifukuza viongozi wa chama Geita. Alifukuza madiwani Arusha. 
Hapa Mwanza alishinikiza kufukuzwa kwa madiwani wawili *CHAGULANI NA 
MATATA*bila kuzingatia falsafa ya Chama kuamini katika nguvu ya umma 
kwamba 
wananchi ambao ndio wapiga kura wenye maamuzi juu ya hao Madiwani 
hawakushirikishwa katika kutoa maamuzi wakati wa kuwafukuza. 

Bwana Slaa amesababisha madiwani watatu kufukuzwa hapa Mwanza kwakuwakataza 
wasihudhurie vikao vya Halmashauri. Hivyo kwasababu kupoteza kata tatu (3) 
ambazo ni Ilemela, Nyamanoro na Kirumba. Kwa madai kwamba hawamtambui *Meya 
MATATA.* 

Pia Bwana Slaa amekuwa akivunja uongozi wa chama bila kuzingatia Katiba ya 
Chama kama Geita, Nyamagana, mvomero Morogoro Lindi na Mtwara bila kufata 
Katiba kama inavyoeleza Ibara ya 6.3 (b) mamlaka ya nidhamu na uwajibikaji, 
"kwamba kingozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza kusimamishwa au 
kuachishwa Uongozi na Kikao kilichomteuwa"Lakini yeye amekuwa akifukuza na 
kuvunja Uongozi katika sehemu mbalimbali za nchi bila kuzingaita misingi ya 
Katiba, Anaongoza Chama kwa Mfumo wa Hailakia kwamba atakalosema yeye ndio 
sheria na linalotakiwa kufuatwa na haitakiwi kuhoji. Slaa amekuwa 
akiwafukuza na kuwaita kwa kuwatukana mamluki Vingozi ambao wamejenga Chama 
kwa muda mrefu bila hata ruzuku leo hii chama kinapata ruzuku ya zaidi ya 
Milioni 200 wanaonekana hawafai licha ya kutopelekewa ruzuku majimboni mwao. 

Vilele Bwana Slaa amekuwa akilazimisha Viongozi wa Chama Mikoani kumpokea 
anaedaiwa kuwa mchumb wake bibi JOSEPHINE MSHUMBISI kama Kiongozi wa chama 
Taifa,mchumba wake amekuwa chanzo pia cha migogoro ndani ya chama kwani 
amekuwa akipeleka watu majimboni na kuagiza viongozi wa Chama wamtambue 
kama mgombea wa ubunge mwaka 2015, Pia amekuwa akitumia rasiliamali za 
chama vibaya katika ziara yake. 

Amekuwa akichangisha michango kwa kisingizio cha M4C ( vuguvugu la 
mabadiliko) Huku pesa hizo akizitumia kwa ajili ya taasisi yake yake 
binafsi iitwayo JUKWAA LA WANAWAKE kwa kifupi Josephine Mshumbusi 
haifahamiki kama ni mwanachama wa CHADEMA au La:- Hivyo Bwana Slaa hatuna 
imani nae kwani vitendo hivyo vyote vinatishia usalama wa Chama. 

Jambo lingine la kusikitisha kwa wana – nyamagana na Mwanza nzima kwa 
ujumla bwana Slaa amemteua Ezekiel wenje mbunge wa Nyamagana kuwa 
mkurugenzi wa mambo ya nje makao makuu ya chama Dar es salaam hivyo 
wananchi wa Nyamagana hawana mbunge kwani kwa sasa anaishi Dar es salaam na 
kufanya kazi huko. Sasa hivi wana- nyamagana hawana tena mbunge kwani yuko 
Dar es salaam amekuwa mbunge wa makao Makuu. 

Ndugu waandishi ,katika kudhihirisha kuwa Wenje sasa hivi sio mbunge wa 
wanachi bali mbunge wa Makao Makuu, Ndugu Wenje haelewi suala lolote 
linaloendelea jimboni kwake kwani ninyi wanahabari ni mashahidi alipotoa 
tamko la Uongo mbele yenu akidai machinga wa Mwanza wamesema wanampa siku 
14 Mkurugenzi wa Jiji awe amejiuzuru , jambo ambalo lilithibitisha kuwa ni 
la uzushi kwani SHIUMA (Shirika la Umoja wa Wamachinga). Lilimjibu na 
kumtaka afute kauli yake kwani hajazungumza wala kuwahi kuonana na 
wamachinga aache kuwachonganisha na Serikali kwa manufaa yake binafsi kwani 
hao wameendelea kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo wakishirikiana bega 
begani na Mstahiki Meya na madiwani wao. 

Ndugu wanahabari katika hili bwana Slaa hawezi kukwepa lawama hivyo basi 
kama ana uso wa aibu apishe kiti akae pembeni tujenge chama chetu. 

*Ndugu wanahabari:* 
Naamini mnakumbuka mwishoni mwa mwaka huu bwana Slaa alipokuwa anafanya 
ziara ya kukagua uhai wa Chama Mkoa wa Dar es saalm na majimbo yake 
alisikika akitekeleza na kuunga mkono mfumo kandamizi na unaofinya 
Demokrasia na utumiaji mbovu rasimali za nchi hii kwakuwa na wakuu wa Mkoa 
na Wilaya cha kustaajabisha na kushangaza bila aibu wala soni Bwana Slaa 
aliwataka viongozi wa Ngazi mbalimbali katika Jimbo la Kigamboni (Chadema) 
wawe tayari kupewa ukuu wa Wilaya na Mikoa Chadema itakapo kuchukua dola. 
Kitendo cha bwana Slaa kuendeleza sera za CCM kama kuwepo kwa wakuu wa 
Wilaya na Mikoa kinapingana moja kwa moja na sera na itikadi za CHADEMA. 
Kauli tata kama hii inamuhalalisha bwana Slaa kutumikia mabwana wawlili 
yaani CCM na CHADEMA ndio maana tunamtaka arudishe kadi ya Chadema na 
aendelee na Chama chake cha CCM anachotekeleza sera na itikadi zake. 

Ndugu Nadhani mnakumbuka tarehe 28 /10/2012 tulikuwa na uchaguzi mdogo wa 
madiwani baada ya nafasi hizo kuachwa wazi kwa sababu mbalimbali. Katika 
uchanguzi ule CHADEMA iliambulia viti 5 (vitano) kati ya viti 29. Lakini 
baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa nini CHADEMA ilifanya vibaya katika 
uchanguzi mpaka kupelekea kupata viti vichache kiasi hiki wakati CHADEMA 
kwa sasa ni chama pendwa kwa Watanzania uchunguzi unaonyesha kwamba katika 
uchaguzi ule wa madiwani Bwana Slaa ambae alizunguka katika kata zote 
zilizokuwa zimeachwa wazi hakuwa na agenda ya kuhakikisha CHADEMA inashinda 
bali alibeba agenda yake binafsi na chama chake pendwa CCM NDIO maana Kanda 
ya ziwa CHADEMA tulishinda kwa asilimia 99 kwa sababu ya hujuma ya 
undumilakuwili Bwana Slaa. 

*Ndugu wanahabari:* 
Vyanzo vya mapato katika Vyama vya Siasa ni ruzuku kutoka Serikalini, 
michango mbalimbali kwa wadau, ununzi wa kadi za vyama kwa wanachama na 
kulipia ada ya uanachama katika vyama vyao. Bwana Slaa anakichangia CCM ili 
kiendelee kujiimarisha zaidi kwa kulipia ada ya uanachama . Kwa hio ujenzi 
na uimarishaji wa CCM unasaidiwa na uwepo wa Bwana Slaa na michango yake 
katika CCM. 

*HITIMISHO:-* 
Kutokana na mwenendo wa Bwana Slaa Wilbroad ninataka mwenyekiti wa Chama 
Taifa achukue maamuzi sahihi ya kutuepusha na janga hili ndani ya Chama 
maana ni bora uwe moto au baridi kuliko kuwa vugu vugu endapo akishindwa 
tutaitisha maandamo nchi nzima maana Ni watanzania wazalendo wengi 
walioumia, kifilisika, na hata kupoteza maisha wakipigania ukombozi wa nchi 
hii, leo hii mamluki kama WILBROAD PETER SLAA hatuweai kukubali waturudishe 
nyuma katika harakati za Ukombozi. Tunamtaka ajiuzuru haraka iwezekanavyo. 
Hakuna kulala mpaka kieleweke. 

*……………………………..* 

*MIMI SALVATORY MAGAFU* 

*KATIBU BAVICHA MKOA WA MWANZA.* 

*nakala:wajumbe wote wa BAVICHA TAIFA* 

Source: JF 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment