Thursday 20 December 2012

[wanabidii] Imesogewa mbele: siku ya wanataaluma ; kongamano na tuzo 2012

Wazalendo,

Napanda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha kuwa kutokana na maombi ya
wanataaluma wengi kuwa mwishoni mwa mwezi desemba wanakuwa likizo.
Hivyo basi TPN imesikiliza maoni hayo na tumeamua kuisogeza mbele siku hii
ya wanataaluma Tanzania hadi mapema mwaka 2013.

Siku na Mahali tutawajulisha hapo baadae, mambo yote yaliyopangwa
yatafanyika.

Kutokana na kusogezwa mbele nachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa bado
tunapokea maombi ya wanaotaka kutunikiwa tuzo; unaweza ukampendekeza mtu au
ukajipendekeza mwenyewe , ambatanisha CV na ueleze ni kwa nini upewe au
unayempendekeza apewe tuzo husika (soma email ya chin kwa maelezo zaidi).

Naomba tuendelee kushirikiana na kupeana ushauri kufanikisha siku hii.

Nawashukuru wote waliojitokeza kudhamini tukio hili na pia walijitokeza
kuchangia mawazo kufanikisha siku hii.

Makampuni yaliyojitokeza kudhamini ni pamopja na ya umma na binafsi.

tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaosababishwa na kuahirishwa kwa tukio
hili ,naomba tuendelee kushirikiana.

Nawatakia wote kila heri ya kipindi hiki cha siku kuu za Krismasi,
mapumziko na Mwaka mpya mwema 2013.

Wanataaluma tuna nafasi ya kutumia taaluma zetu kuleta mabadiliko chanya kwa
faida ya Taifa letu.

Mungu awabariki wote, Mungu ibariki Tanzania.

Phares Magesa
Rais- TPN
+255 784 618320

----------------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------------
-----

Wazalendo,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha kuwa siku ya wanataaluma Tanzania
itakuwa 28 Dec, 2012 kuanzia saa 8 mchana hadi usiku..

Tunatarajia itafanyika katika moja ya hotel maarufu katikati ya jiji la Dar
Es Salaam, ukumbi tutawajulisha baadae mara baada ya taratibu za awali
kukamilika .

Siku hii kutakuwa na mambo yafuatayo:

1. Mkutano wa mwaka wa wanachama wote ( wanachama wetu wote wa ndani na
walio nje ya nchi mnakaribishwa sana kushiriki maana wengi kipindi hiki
wanakuwa likizo, wale mnaopenda kujiunga na TPN pia karibuni)
2. Kongamano la wanataaluma wote kujadili mambo mbali mbali kuhusu
Taifa letu na mwaka huu mad azote zitahusu Ujasiriamali na maendeleo ya
Taifa, wasemaji watakuwa ni wafanyabiashara,
viongozi wa kijamii na kiserikali, wanataaluma walio ndani
nan je ya nchi, mnakaribishwa kama una taka kuwa msemaji.
3. Tuzo za mwaka kwa wanataaluma walio ndani na nje ya nchi waliofanya
vizuri katika fani zao (Tiba, Elimu,Sheria, Sayansi na Teknolojia, Habari,
Uchumi, Sanaa, Siasa n.k) na tuzo kuu ya
Mwanataaluma wa Mwaka (Professional of the year Award)
ambaye ataingie katika Hall of Fame ya wanataaluma wa Tanzania, mwaka Jana
2011 tuzo hii ilienda kwa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.
4. Pia kutakuwa chakula cha usiku na burudani ya kumaliza mwaka 2012
na kuukaribisha mwaka mpya 2012 wanataaluma wote tujumuike pamoja tafadhali
thibitisha ushiriki kwa kutuma ujumbe
mfupi (sms au email) wenye jina lako kwa mratibu au Rais.

Nawakaribisha wote tujumuike na kushiriki kikamilifu kwa hali na mali katika
maandalizi ili kufanikisha siku hii kubwa ya wanataaluma Tanzania.

Wale ambao mnaodhani mna sifa za kupewa tuzo mnaweza mkawasiliana na nasi
moja kwa moja au kama kuna mtu unadhani ana sifa za kupewa tuzo hizo pia
tutumie mapendekezo yako na wasifu wake. Mapendekezo haya yafike kabla ya
tarehe 15, Dec 2012 ili kamati ya utendaji ya TPN iyapitie na kutoa uamuzi
wa watakaotunikiwa tuzo hizo.

Maoni na ushauri vyote vinakaribishwa, mnaweza kuwasiliana na walitajwa hapo
chini.

Nachukua nafasi hii kuwaomba wadau wetu wote mtakaopenda kushirikiana nasi
katika kufanikisha siku hii kwa kudhamini au kufadhili matukio ya siku hii
muwasiliane nasi .

Mratibu Mkuu wa shughuli hii ni Bi. Maryam Marambo 0689 288919 , 0716 350
650 email: maryam_marambo@yahoo.com ; Maryam.marambo75@gmail.com

Nawatakia wote kila la heri.

Phares Magesa,
Rais- TPN,
+255 (0784/0713/0767) 618 320
magesa@hotmail.com

Richard Kasesera,
Makamu wa Rais- TPN
+255 767 777151
rkasesela@gmail.com

Mhe. Bi. Janet Mbene (MB),
Katibu Mkuu - TPN
+255 784 596 444
maorchid@gmail.com

Gervas Lufingo
Mhazini- TPN
+255 784 482597
nasemaasante@yahoo.com

Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN),
Url: www.tpntz.org
Email: president@tpn.co.tz


----------------------------------------------------------------------------
----------------------------------------


Disclaimer: This email and any files transmitted with it are confidential and solely intended for the use of the individual or entity to whom they are addressed. If you are not the addressee, do not disclose, copy, circulate or in any other way use or rely on the information contained therein. If received in error, notify the sender immediately and delete this email from your system. Please note that any views or opinions presented in this email are solely those of the author and do not necessarily represent those of the Tanzania Ports Authority, unless that information is subsequently confirmed in writing. The integrity and security of this email cannot be guaranteed on the internet. Therefore Tanzania Ports Authority accepts no liability for any damage caused by the contents and/or any virus transmitted by this email.

Tanzania Ports Authority, Head Office, P.O Box 9184, Dar-es-Salaam, Tanzania.
www.tanzaniaports.com

0 comments:

Post a Comment