Wednesday 12 December 2012

[wanabidii] CHADEMA inakufa? – Ripoti maalumu – Gazeti la Jamhuri - Mwanzo

Hali ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni mbaya na tayari kumeanza kuwapo hofu ya chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini, kufa.

Hofu hiyo inayokana, pamoja na mambo mengine, kuibuka kwa makundi yanayohasimiana, yanayoundwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho.

Katika fukuto hilo, JAMHURI imefanikiwa kupata habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wanachama na viongozi, zinazohusu kuwapo mkakati madhubuti wa kuwafukuza baadhi ya viongozi wa chama hicho.

Duru za uchunguzi zinaonesha kuwa walengwa wakuu kwenye mpango huo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto, na Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda. Pamoja nao, walengwa wengine ni wafuasi wa wanasiasa hao.

Moja ya sababu zinazotajwa kuchochea au kuibua makundi makuu matatu ndani ya Chadema, ni mbio za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015. Makundi yanayotajwa, na ambayo yameanza kujitokeza hadharani yamejiegemeza kwa viongozi watatu maarufu – Zitto, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa.

Zitto anatajwa kama mmoja wa vinara wa migogoro ndani ya Chadema, akidaiwa kutumia umaarufu wake kama kinga ya kufanya lolote analotaka akiamini kuwa "Chadema bila Zitto, haipo".

Pia urafiki wake wa karibu na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, na viongozi wengine waandamizi wa CCM umekuwa ukiwatia shaka baadhi ya wanachama, wafuasi na viongozi wa Chadema.

Tayari Zitto ameshatangaza hadharani nia yake ya kuiwakilisha Chadema kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015, na kwa sasa anaendesha kampeni ya umri wa wagombea urais kupunguzwa na ikiwezekana iwe miaka 35. Mwaka 2015, Zitto atakuwa anatimiza umri wa miaka 39.

Hii si mara ya kwanza kuibuka kwa makundi ndani ya Chadema, kwani miaka kadhaa iliyopita Zitto na Mbowe walisuguana kutokana na uamuzi wa Zitto wa kutangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa. Mzozo huo ulimalizwa kwa busara ya wazee na wanachama waandamizi ndani ya chama hicho, kwa Zitto kukubali kuondoa jina lake mbele ya waandishi wa habari.


http://wotepamoja.com/archives/10863#.UMh8RkX9S7I.gmail

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment