Wednesday 12 December 2012

[wanabidii] BW. MGIMWA: BASI HATA HALMASHAURI MOJA KUTOKA ZANZIBAR???

"Benki  ya Dunia (WB), imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo usio na riba wa Sh. bilioni 489.8 kwa ajili ya kuendesha miradi mitatu ya kilimo, kuendeleza serikali za mitaa na uhifadhi wa chakula nchini.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa mkopo huo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, alisema mradi wa kilimo utapatiwa Sh. bilioni 47.4 kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vocha za pembejeo, 
kuelimisha wakulima juu ya kilimo cha kisasa pamoja miundombinu katika kilimo hicho.
Dk. Mgimwa alisema mradi wa pili ni ule wa uhifadhi wa chakula ambao utatumia Sh. bilioni 39.5 na  mradi wa tatu utatumia Sh. bilioni 402.9 kwa ajili ya kuendeleza serikali za mitaa katika halmashauri 18 nchini.
Alizitaja halmashauri zitakazonufaika na fedha hizo kuwa ni Sumbawanga, Tabora, Morogoro, Iringa, Songea,  Moshi, Lindi, Bukoba, Musoma, Singida,  Babati, Korogwe, Masasi, Nyumbu, Mpanda, Bariadi na Geita.
Dk. Mgimwa alisema msaada huo ni mkopo usio na riba na utalipwa katika kipindi cha miaka 40.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa WB nchini, Philippe Dongier, alisema msaada huo ni mojawapo katika kutekeleza kuisaidia serikali kufika lengo lake la kutekeleza mradi wake wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (Mkukuta).
Pia alisema uimarishaji na utoaji wa elimu kwa wakulima utasaidia kuwasaidia wakulima hao kujua mbinu mbadala za kuzalisha zaidi mazao yao".
Chanzo: Nipashe
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/367457-bw-mgimwa-basi-hata-halmashauri-moja-kutoka-upande-wapili-wa-muungano.html#post5211480


0 comments:

Post a Comment