Saturday 15 December 2012

[wanabidii] Bia sasa hazinyweki - CTI na theory ya consumer behaviour.

Katika mlo wa matajiri wa bongo CTI kinara wao na mzee wa uwekezaji Felix Mosha alilalamika kuwa upo uwezekano wa uchumi kudorora kutokana na mauzo ya bia (nadhani ni pamoja na Nzagamba Chibuku na Balimi) kushuka kwa kasi, alidokeza kuwa TBL pekee malipo ya kodi yameshuka kwa Tshs 40bn achilia faida iliyokosekana kwa kampuni yenyewe, hata wenzao wa SBL na TDL nao hali ni ngumu pia, hivyo akapendekeza kodi zishushwe kidogo angalau walevi waongezeke. Mkuu wa kaya aliguna na kusema mbona consumers hajasikia wakilalamika! lakini akasema atalifanyia kazi.
 
Mwenyekiti wa TRBDA ndugu Gasisi Mahuti wakati wa mapitio ya badget alionya kuwa upo uwezekano wa jamii kukosa staha na utu kupungua kutokana na offa kupungua mno, alisema sasa kila mtu akifika baa ananunua bia yake na michongo nayo imekuwa migumu kwani hakuna anaepiga story na mwenzie, watu wanakunywa bia moja na kujiondokea. Naamini Gasisi anawakilisha consumers wa hii bidhaa labda anaonekana mlevi tu ndo maana mkuu anasema hajaona consumers wakilalamika.
 
Ningependa kumwambia mosha afanye zoezi la ziada kwani naamini zipo bidhaa ukipandisha bei ndo kwanza zinapendwa zaidi, mfano ni hizi shampeni tunazotumia kwenye sherehe watu hununua ile ya bei mbaya zaidi ambayo ikishazibuliwa humwagika yote chini, yaani hata toti moja kubaki ni issue. Lakini pia Mheshimiwa Kafulila alisema bungeni upo uwezekano wa consumer behaviour kubadilika kutokana na kubadilika kwa mfumo wa maisha na uchumi kubadilika. Pia kauli za wanaharakati kama "ulevi noma" na vifo vya watu maarufu hasa wasanii ambapo inasemekana pombe zemechangia kwa namna fulani inaweza badili consumer behaviour.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment