Saturday 8 December 2012

Re: [wanabidii] ZIARA YA SIKU NANE KUHAMASISHA SHUGHULI ZA KILIMO MKOANI RUKWA

Namuomba tu huyu Stella asihamasishe kilimo cha tumbaku, kama kweli anawapenda watu wake. Tumbaku ni zao linalotia sumu ardhini, kuwatia sumu wakulima, kuwatia sumu wote wanoashughulika nalo (viwandani) na wale wote wanaolivuta. LKK
 


From: Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, December 8, 2012 9:01 PM
Subject: Re: [wanabidii] ZIARA YA SIKU NANE KUHAMASISHA SHUGHULI ZA KILIMO MKOANI RUKWA

Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanafahamu wajibu wao katika kilimo, hawahitaji kuhamasishwa, wanachohitaji ni kujengewa mazingira mazuri ili kilimo chao kiwe cha tija na kuwanufaisha.

Felix

2012/12/8 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wananchi wa
kata ya Matanga leo katika ziara yake ya siku 8 kwa ajili ya
kuhamasisha shughuli za kilimo Mkoani Rukwa. Ziara hiyo itahusisha
Wilaya zote tatu za Mkoa wa Rukwa ambazo ni Sumbawanga, Kalambo na
Nkasi pamoja na Halmashauri zake. Ziara yake inabeba ujumbe huu
ufuatao:
1. Mkuu wa mkoa wa Rukwa anawatakia kila la kheri wananchi wote katika
kusherekea sikukuu ya Noeli na Mwaka Mpya. Anawaomba kudumisha amani,
Upendo na Mshikamano kwenye maeneo yetu na tupashane habari. Toa
taarifa Polisi kwa jambo lolote lisilo la kawaida. Tuwatambue wageni
wote wanaofika katika maeneo yetu wengine si watu wema.

2. Mkuu wa mkoa anawataka viongozi wote katika ngazi zote kuwajibika
na kuwa waadilifu katika kutimiza wajibu wao.

3. Kila familia ihakikishe kuwa inatumia fursa hii ya msimu wa mvua
katika kujiondoa na balaa la njaa na pia umaskini wa kipato. Viongozi
wa kata na vijiji wafuatilie ili kujua kila kaya imelima kiasi gani
katika msimu huu. Kila kijiji kiwe na Daftari la wakulima. Wakulima
watashindanishwa.

4. Kila kijiji kitenge maeneo maalum kwa ajili ya kuendeleza shughuli
maalum kama Ufugaji, kilimo na kuchague nguzo yake kuu ya uchumi.
(Mpango wa SAGCOT).

5. Watoto wote watakaofaulumwaka huu wa 2012 lazima wapelekwe shule.
Watoto wa kike wanastahili kulindwa ili wasipate ujauzito. Mzazi awe
mlinzi namba moja.

6. Akina mama wapeleke watoto wao wa chini ya miaka mitano ili kupata
chanjo ya minyoo na Vitamin A.

7. Kuanzia mwezi wa Januari 2013 watoto wa miezi 9 watapatiwa chanjo
ya kuzuia kuharisha na Kichomi. Hivyo wazazi wote tuwapeleke watoto
kupata chanjo hiyo. Malengo yetu ni kuwapa chanjo watoto wote.

8. Lishe bora ni muhimu kwa familia. Kula samaki mboga mayai, wanga na
nyama kadiri inavyowezekana.

9.Nawashukuru kwa jinsi mnavyoniunga mkono, nami nawapenda sana.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment