Sunday 9 December 2012

Re: [wanabidii] Risala ya Uhuru kwa niaba ya Afro-Shirazi Party Na A A KARUME

Kumbe kesho ni Uhuru wa Zanzibar?

Sasa mbona hatusheherekei?


Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

-----Original Message-----
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 9 Dec 2012 06:54:45
To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Risala ya Uhuru kwa niaba ya Afro-Shirazi Party Na A A KARUME

Tunachukuwa fursa hii kuwapa mkono wa furaha watu wote wa visiwa hivi
kwa jtihada yao na bidii kubwa, pamoja na misaada mikubwa katika
juhudi zetu sote za kuupinga ukoloni na utawala wa kibeberu.
Jitihada . Leo mwezi 10 Disemba, 1963, ZANZIBAR imekuwa Huru.

Hii leo sisi watu wa visiwa hivi tumepata haki ya kuchukuwa mahala
petu kuwa ni Dola sawa na nyengine katika umoja wa Nchi za Dola za
Commonwealth.

Kwa uchache, kuwa mwanachama katika umoja huo, kuna maana kwamba nchi
hii ni huru chini ya mpango wa serekali ambayo msingi wake umejengwa
juu ya kuendelea kwa ridhaa ya wanaotawaliwa. Ili kufikilia matarajio
yetu hayotunayo moja katika Katiba zenye msingi madhubuti iliohusika
na shuruti za haki za binadamu, haki za mambo ya siasa na uhuru wa
dola yoyote nyengine.

Ni wajibu wa watu wote wa dola yetu mpya, kila mmoja katika sisi bila
yakujali fikra zetu za siasa au madaraka yetu kusaidia kweli kweli
katiba yetu iweze kufanya kazi. Pamoja na manufaa, haki na uhuru
ambayo yote hayo yamepatikana baada ya nchi kuwa huru.

Vile vile yapo mambo yaliyo wajibu na lazima ambayo imebidi
yatimilizwe kwa ajili ya dola na kwa ajili yetu wenyewe kila mmoja juu
ya mwenziwe. Kwa hakika kwa ajili ya wajibati hizo na mambo yalo
lazima, kama ilivyo juu kufurahikia haki za uraia na haki za siasa na
uhuru mbali mbali basi vile vile uhuru wetu lazima utimilizwe kwa njia
hizo.

Tuliyoyapata leo mwezi 10 Disemba ni mipango ya mwanzo tu ya kuweza
kufanya juhudi kwa ukamilifu dhidi ya maadui zetu nao ni ujinga,
umasikini na maradhi na kuweza kuleta imani penye khofu na shaka na
kuleta masikilizano mahala ambapo hata hivi sasa dawa ipo, na kuleta
mapenzi mahala ambapo pana chiki, ili dola yetu mpya ichomoze katika
neema, umoja na furaha.

Kwa hivyo katika hii siku ya leo na tumwombe Mwenye Enzi Mungu,
Inshallah atuweke tuifanye na tuitimilize kazi kubwa ya kujenga taifa
ili dola yetu mpya ya ZANZIBAR ipate baraka ya matunda mema ya kazi
zetu.

Uhuru na Umoja, Uhuru na kazi!".

Jarida la MAARIFA la Serikali ya Zanzibar. Makala maalumu kwa
kufikilia Uhuru. Jumaane, 10 Disemba, 1963.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment