Monday 24 December 2012

Re: [wanabidii] RE: Mawaziri wa JK wagongana

Kama ulivyosema kua uozo tumeulea wenyewe. kwahiyo anapojitokeza mtu mmoja nakufanya jambo lakijasiri kama alivyofanya Dr.Uvisa tumtie moyo na tusimbeze maana amethubutu. Au Hilda unasemaje?




From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, December 24, 2012 4:39 PM
Subject: Re: [wanabidii] RE: Mawaziri wa JK wagongana


Nchi imeoza. Tunaangalia mengi mabovu tunayaacha yaendelee. watendaji waovu ni sisi wenyewe. Na siku hizi kumeingia kulipiziana kisasi-kukatwa vichwa, kuchomewa nyumba, kuuawa. Utekelezaji wa sheria unakuwa mgumu kuwa mtu anaogopa kufanyiziwa kutumia mitandao ya mauaji. Afisa wa NEMC mmojawapo kafanyiziwa tumesoma magazetini. Leo unaona mtaani mtu anamwaga maji machafu hovyo na ana biashara inamuingizia hela. Wananchi wanasema-Serikali ije ituondolee tatizo hili. Wakati kuna balozi wa nyumba kumi, serikali ya mtaa, afya Kata, Police Kata, kamati ya mazingira etc lakini tunaogopana wenyewe kwa wenyewe. Mtu mmoja anaweza kuweka karaha mtaa mzima ukakereka. Tutaona ktk TV eti nyumba ya kuishi imegeuka kiwanda cha mikae inatoa moshi jamii inashindwa kuishi salama. waliotoa leseni ya mikate hawaangalii kiwanda kipo wapo bali ushuru tu na mapato ya halmashauri. Ndio sasa mtu anapangisha Mchina (mgeni) anafungua kiwanda cha maplastiki uraiani au chga mazao ya chakula-kinyesi na maji machafu yametapakaa ndani na nje ya jengo. Huu uhuru ya hata wageni kuja kufanya wasiyofanya kwao inakuwaje jamani watutese na kufufanya zoba nchini kwetu? bado na sisi wenyewe garage kial mahala, viosk na mapishi kila mtaa na kila nyumba. Nyama inaning'inizwa bushani kutwa inazingirwa na mainzi hata misingi ya afya haizingatiwi. Viongozi na wahusika wengine wanaona, bucha linakioo na air conditioner lakini milango ipo wazi mainzi kibao au chakula kinauzwa kabati ni la kioo linafungika lakini halifungwi kutwa li wazi na maishi. Kisha unaona watu na suti zao wanakula hapo pa mainzi na vumbi linapulizwa na upepo linaingia humo.

Ndio tutajali kuwa na wawekezaji wanaozingatia sheria za mazingira ambapo wenyewe tuna wa ustaarabu wa paka kukalia mkia? Vijijini ndio balaa, mifugo inakunywa hapa, nasi twaoga hapa na kuchota hapo, hapo hapo tunaoshea dhahabu na madini mengine kisha tunakunywa. Mara maguduria ya kunyunyizia dawa mashambani tunakosha mtoni na kulala na madawa ndani ya nyumba. Huku baba anavuta sigara ndani ya nyumba walimolala mama na watoto. Unaona kifafa kinapanda juu katika kijiji na Mtaa unashangaa why kifafa kutibiwa watu 400 kwa mwaka kaeneo kadogo hivyo-Madawa kuala nayo na kuyapumua, kuyanywa majiji; mafundi magari na mbao kupulizia rangi na mivuke yenye madawa hewa inavutwa na watoto na watu majumbani magereji na uselemala upo majumbani makao ya mbanano, welding na irin dust twabwiwisha watu. Nenda uwakamate-wanatishia kukunyima kura au kukumaliza-mtendaji kazi unaogopa. Unachukua kasenti unalala mbele.

Ndio hayo matokeo ya kuzaa watoto wenye vilema viungo vipo nje, mara kazaliwa hana pua ila uso una jicho moja etc. Ndio vinyesi tutambavyo mama ntilie na madhara mengine kupitia maziwa na nyama za mifugo na samaki (bio-accumulation in milk, meat). Mwageni tu kinyesi, kemikali etc mitoni na maziwani, baharini matokeo ni kulimaliza taifa. matibabu-India. Krismass Njema.
 


--- On Mon, 24/12/12, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] RE: Mawaziri wa JK wagongana
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, 24 December, 2012, 15:07

Hilda,
Maelezo yako ni sawa, kua mfumo mzima umefanya uzembe. Lakini Dr. Uvisa lazima awe na mahali pakuanzia. Na asiinuke mtu mwingine na kubeza utekelezaji wa majukumu yake (Unless kama Uvisa nae anasukumwa na hila) nakuta kutushawishi kwa hoja nyepesi kua nchi itapata hasara zikishughulikiwa hotel zisizo zingatia sheria za mazingira.
Alexander



From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, December 24, 2012 3:34 PM
Subject: Re: [wanabidii] RE: Mawaziri wa JK wagongana


Ina maana Alexander hakuna horozontal na vertical integration katika upangaji na utelekezaji Sera na Sheria kiwizara. Kila mmoja hataki kuingiliwa katika nyanja zake.

Ni kama hii iliyotokea majuzi ya Mbunge Lema. Eti mshtaki hakuwa mgombea, lakini mahakama zimekubali kesi toka huko ilikotokea na mshitaki hakuwa mgombea. Kwa nini toka huko chini isikataliwe na mamlaka zote za kisheria pamoja na vyama husika kuwa haikuzingatia misingi hadi ikafika mahakama ya Rufaa? Hawakuona misingi yote ya kesi na kuyikubali hadi huko juu kupoteza muna na fedha? Gharama kubwa sasa.

Hili la Hotel usemalo hapa. Tanzania mwalimu wetu KIPOFU na Mshauri wetu KIZIWI, mkaguzi katika maswala mbali mbali ni KIWETE hana hata baiskeli ya kumsaidia movements. Ndio maana hatuoni na kujifunza kutoka mifano ya tulikotoka na wala hatuisikii tukielezwa na wengine wanapofungiwa kutokana na uchafuzi wa mazingira hatupati kujifunza maana hattuendi kuona na hata kama tulikwenda kuona hatujali.

Kwanza, environmental scientist gani wa NEMC au Ministry of Health and Social Welfare (MOHSW) na wa Town Planner gani was Mipango Miji Wizara ya Ardhi na industrial inspector gani wa MOHSW aliyepitia Mchoro wa Double Tree Hotel na kuidhinisha jinsi ilivyo bila ya mifumo itakiwayo kisheria ya afya na mazingira?.

Hapo ni signature zaidi ya moja na nibaada ya kupitia mchoro wa ujenzi wa hotel na kukagua eneo. Kisha Kibali cha ujenzi kutolewa kinachomuwezesha pia kupata leseni ya biashara. Tanzania Investment Centre haihusiki hapa na huu ni uwekezaji akakubali uwepo na kutoa mionbgozo leseni isitoke mpaka yote yamezingatiwa? Ni sahihi za watu wangapi hapa ambao hawajatajwa kwa majina na vyeo vyao ktk sakata hili?

Watajwa hapo juu wanaoupitia mchoro wanatakiwa kuangalia-water supply service hoteli itakayotumia, estimated volume of sewage na treatment or connection to the sewerage system. Hawawezi kufanya certification ya ujenzi bila kuangalia hayo. Design ya hotel itaonyesha aina ya jiko, waste collection chamber, connection za umeme, location ya generators zake kwa emergence power maana noise ni tatizo. Plot layout itaonyesha mahusiano yake na bahari-ukaribu/umbali na lazima waone kama itakuwa near or far from the highest tidal wave (60 metres) zinazotakiwa mbali toka wave ya mwisho ya bahari ziwe zimeachwa- zisiguswe. Leo land use planner anapitisha mchoro wa jengo la hoteli ambalo lipo baharini na mikoko itang'olewa; industrial health inspector anayeangalia jengo la biashara au kiwanda haangalii layout ya jengo kuangalia masuala ya afya pamoja na matumizi na umwagaji maji safi na chafu na taka nguvu na sewer connection. NEMC anbapohusishwa anafumba macho vipi kuangalia kama masuala ya mazingira yameangaliwa kabla ya hotel au kiwanda au hata mgodi kujengwa. unakuja kusikia hoteli kama hii utajayo hapa au mgodi wa dhahabu unamwaga maji machafu yenye cyanide au mercury katika Mto (mara, Ziwa victoria etc). Hiyo national environmental law inatumikaje, Industrial law imealana na inspectors wake? Kila ujenzi mijini unatakiwa kuwakilishwa kwa mamlaka husika mchoro wa jengo upitiwe uidhinishwe. Hii imekufa miaka mingi na ukipeleka file linakaa karne. Hii inatoa mwanya kwa watu kujenga hovyo watakavyo. Plot ya kutakiwa ijengwe 40 % inayobaki 60% ni outer building na fire security and waste collection services unakuta mtu amejenga 100% na ameziba feeder roads. Kisha ameawacha sewer pipe imepoita nje ya nyuma hataki kulipa sewerage connection na fee yake kwa mwezi anafanya connection ktk open or closed drainage system. Majumba mengi, lodges mjini dar  na Hotel nyingi kubwa zinafanya hivi na maji machafu yanaonekana.

Watu wamengenga maroshani kariakoo, kawe, Mbezi Beach etc wanapangisha kwa dola plot 100% with buildings uchafu wao wanaingiza mto tegeta, directly baharini. Kuzuia ni bora kuliko kutibu kubomoleana majumba. Hii michoro ya 100% full plot coverage ameidhinisha nani. makosio ya 20% growth in housing or population in a  5 year plan yanazidiwa. Mzigo mkubwa unakuwa kwa DAWASA-DAWASCO ktk Maji safi na machafu, Tanesco, solid waste collection-Halmashauri. Tuanaangalia kujaa matumbo yetu tu watumishi wa serikali hatuangalii madhara yote haya. Na hao maofisa sio wamesoma tu bongoland bali wamesoma ulaya na kupelekwa study tours kuona usimamisi wa miji, Environment and waste treatment na madhara ya nature ya waste za aina mbali mbali kwa binadamu na viumbe vingine hata samaki na mifugo na miti ya majini na nchi kavu. Keo ndio hao wanaoidhinisha Double Tree Hotel untreated sewerage and sullage imwagwe baharini. Maji mengine ni ya moto yanaingia baharini kuua viumbe.

Kamata wahusika walioidhinisha jengo lijengwe maana hawakufanya kazi yao vizuri, ikabidi watoao leseni waidhinishe kutokana na recommendation zao mbovu. NEMC aliona jengo halina waste stabilization pond na itamwaga baharini moja kwa moja. Kwa nini aliacha lijengwe aje leo hii kulisimamisha. Akamatwe huyo aliyeidhinisha lijengwe na lianze kazi bila ya own waste treatment plant. Kwa muda mrefu mfumo wa maji taka ulikuwa unakarabatiwa-Mikocheni na Gymkana pumping station, Buguruni oxidation ponds. Za urafiki ni disaster na nyingine nyingi pia DSM. Hivyo Jiji limekuwa na Direct Sea Outfall. Mabomba kumwaga moja kwa moja kutoka mambomba taka yaliounganisha majengo mbalimbali kumwaga baharini bila ya pupitia waste stabilization ponds na pumping station. Kama hili ni tatizo hadi sasa, jee unategemea kutokuwepo na treatment plant na pumping station ya City kutawafanya wenye hotel wasimwage maji moja kwa moja baharini? Wanalipa kodi ya sewerage na hakuna system ya opokeaji na usafishaji maji taka. Jee, wajenge wao wewe uchukue kodi usijenge? Kama system ipo na hazingatii-hapo hoja ipo. Funga hoteli Kagasheki hata kama hasara itaingia kwa mwekezaji na kwa nchi.

Mzungu amekuja bongo kwenye rushwa anafanya kama ule usemi-Ukienda Roma fanya kama wafanyavyo wa-Roma. Kwao ulaya atazingatia sheria. Akija hapa hazingatii maana tunamuingiza ktk rushwa, anatoa chocte unashiba, unambadilishia umeme analipa chache sana badala ya mamilioni na unamuunganishia maji taka yaingie baharini. Kila mwisho wa mwezi anakupa pension wewe yeye anaokoa gharama na kupandisha juu faida. Ujinga wetu wenyewe. Hatuipendi nchi yetu, tunakulala wewenye kwa wenyewe na kupigana wenyewe kwa wenyewe kama MAJUHA badala ya kuzingatia sheria na utawala bora plus ethics za integrated development. Inaonekana leo hapa kuwa NEMC hawezi akakaa kuwa na mpango na usimamizi wa pamoja na Maafisa wa Ministry of land na Health na TIC! kwenye uwekezaji !? Why mgongano wa Mh Kagasheki, Waziri wa Mazingiza Dr Huvisa na watu wake wa NEMC etc? DAWASA-DAWASCO yupo wapi na mabombataka yake hoteli inajiunganishia ipendavyo? hapa kuna msuriru wa`wahusikka kukamatwa Double Tree iseme ilikula na nani aliyempa kibali wakati jengo linajengwa na kuunganishia mabombataka baharini directly. Hoja ya kuwaambia warekebishe mfumo ni secondari maana mchoro wa jengo ulipitishwaje na nani alikagua kuwa ulizingatia environmental structural and health safety? Kama Dr Huvisa alitekeleza majukumu yake-ni baada ya kujengwa na kufanya beashara!! Prevention is better than cure. Wamekosea. Ingekuwa kabla ya kutoa leseni likaanza operation-ukaguzi wa awali ya yote ya michoro etc. Nao wanaweza wakalaumiwa kwa kutokutimiza wajibu Alexander.


Lastly,-Wizara husika zinaona jinsi majengo yanavyojengwa DSM kwa kupindisha shertia za ukomo wa maghoroga kwa eneo, kuziba njia zilizoachwa na serikali miaka ya nyuma mtu anaweka kiosk anaziba feeder roads. Nyumba za ghorofa kuziba zisizo za ghorofa hata zile za maeneo ya NHC houses za vyumba sita na nyinginezo. Hewa inazibwa, TB na magonjwa ya mapafu yaitaongezeka sana. Kila mwenye ghorofa anachipa borehole na kufanya pumping ya maji juu. Hii inaharibu ardhi na kutatolea madhara ya overpumping na fractures ardhini majumba yakaanguka. Hapo hapo watu wanavyoo vya shimo na septic tanks na visima virefu na vifupi vya maji wanywayo untreated, garage zisizompangilio na mauchafu ya maji ya kemikali kutoka saluni za nywele. Tumeweka pazia machoni kwa haya yote na kusubiri 'Kubomoa' majengo ya watu baadae eti kuzingatia sheria za mazingira na ujenzi badala ya kuyakabili kwa sasa. Inasikitisha sana.

--- On Mon, 24/12/12, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] RE: Mawaziri wa JK wagongana
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, 24 December, 2012, 10:34

Ndg, Wanamabadiliko,
Wiki chache zilizopita waziri wa Mazingira Dr. Theresa Uvisa alizifungia Hotel 2 za Double Tree na Girafee Ocean View baada yakugundua kua hazizingatii usalama wa mazingira zinapoendesha shughuli zake. Kabla yahapo watumishi waliochini yake walifanya ukaguzi wa kushitukiza nakubaini uchavuzi mkubwa unaofanywa na hizio hotel, hasa kutiririsha mojakwamoja baharini bila kufanyiwa treatment maji taka na vinyesi. Waliwapa maagizo kua warekebishe mifumo yao ya majitaka, lakini wamiliki wa hotel hawakufanya chochote chamaana. Kwa maneno mengine walizizarau mamlaka zilizowekwa kisheria na kikatiba. Baada ya ukaguzi mwingine waziri Uvisa akaamua kuzifungia hizo hotel.
 
Chaajabu ajabu leo waziri wa Utalii Mr. Kaghasheki amekuja juu na kuuita uamuzi wa Wairi mwenzake kua ni uamuzi hatari sana na finyu wenye haraka, nausio kua na maslahi kwa taifa. Sababu kubwa anayotoa nikwamba hiki ni kipindi cha high season. Kwamaana kua nikipindi cha sikuku nyingi na watalii wengi wankuja kuitembelea Tz, kwahiyo huo uamuzi wa Dr. Uvisa utaikosesha nchi mapoto. Nimemshangaa sana huyu waziri Kaghasheki. Inamaana yeye kwake kinacho matter ni pesa hata kama zinapatikana kwa gharama ya mazingira na afya za watu? Kitu kingine cha hatari anasema kabla Dr. Huvisa hajachukua huo uamuzi alipaswa kuwasiliana na wizara yake, kwangu naona hayo pia nimawazo hatari sana. Maana kila wizara ana mandate yake amabayo amepewa, kwahiyo chamsingi nikusimamia hayo maagizo uliyopewa kwakufuata sheria. Kama kilawaziri atafanya maamuzi baada ya consultaion na wizara nyingine hata mahala amabapo mambo yako wazi hii nchi itaenda kweli???
 
Mr. Kaghasheki pia anasema wageni wataacha kuja Tz baada ya kufungia hizo hotel, kwakua hizo habari zakufungiwa hizo hotel zimewekwa kwenye mitandao. Haya ni mawazo ya ajabu na hatari sana. Inamaana hao wageni wangependa kuishi Katika hotel zisizo zingatia sheria za mazingira? Au tushidwe kutekeleza majukumu yetu kwakuogopa watu wengine wataquetion juu ya hayo maamuzi?? Mimi nasema kama nihivyo hao watalii nawapotelee mbali na fedha zao. Wengi tulikua tunamuona huyu Waziri Kaghasheki kama mchapa kazi lakini kwa mwendo huu nihatari sana kwataifa hili na ustawi wa mazingira ambao ndio hasa msingi wa Utalii huo anaoupigia upatu. Kweli jamani tuache uchafu ukiendelea kisa ni HIGH SEASON?
 
Nafikiri tunahitaji mawaziri watakao fanya kazi kwakufuata sheria na miongozo waliyopewa, Mimi naona Dr. Uvisa ametekeleza majukumu yake na mama kaza buti. Nakushauri kama itaonekana uamuzi wako siomzuri nawakubwa zako (kitu ambacho siamini) nakushauri ujiuzuru maana watakua hawana dhamira yakulinda mazingira. Mji wa Dar es salaam umekua mchafu kwasababu ya kupindisha sheria za mazingira.
Alexander
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment