Sunday 16 December 2012

Re: [wanabidii] RAIS WANGU MPENDWA…..MTWARA KUNA TATIZO.

Tatizo la Mtwara ni tatizo la taifa zima, ni tatizo la ugavi wa matunda ya raslimali zetu kwa Watanzania kwa kuzingatia umuhimu wa wakazi wa sehemu zilizopo raslimali hizo. Tatizo la Mtwara ni tatizo la Shinyanga, Mwanza, Mara kwenye dhahabu, ni tatizo la Nantumbo na Bahi penye Yurani, ni tatizo la Kagera penye Nickel, ni tatizo la Arusha, Manyara, Mara, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Katavi na Tabora penye mbuga za wanyama, ni tatizo la Meru na Kilimanjaro penye milima mirefu, ni tatizo la Mbeya penye makaa ya mawe na chuma, ni tatizo la nyanda za juu penye misitu na vyanzo vya maji, ni tatizo la nyanda  za chini penye misitu ya miombo, ni tatizo la Tanga, Pwani, DSM, Zanzibar, Lindi na Mtwara penye fukwe, kwa kweli hili ni tatizo la taifa zima.

Tatizo hili linakuzwa zaidi na tabia ya mamlaka kupenda kujilundikia udhibiti wa mali na madaraka (control of resources and the associated power).

Nimependekeza siku nyingi kuwa ni haki na ni busara kutenga sehemu ya kutosha ya pato litokanalo na raslimali zetu kubaki na kutumiwa na walezi (custodians) wa raslimali hizo ambao ni jamii za karibu (proximal communities). Ni vyema sera zikaainisha mipaka ya ukaribu huo, kuanzia vijiji, kata, wilaya na mikoa, na hata kiwango cha ugavi kikatofautishwa kwa ngazi za ukaribu. Kumbuka kwa mfano bei za ardhi, bidhaa na huduma zinapanda zaidi pale hizi raslimali zilipo na hatuna njia rahisi ya kuwafidia wananchi ambao hawawezi tena kununua kiwanja cha kujenga.

Kwa mfano niliwahi kupendekeza mirahaba yote ya madini ibaki mikoa husika ambayo itagawiwa wilaya zake kwa viwango mbali mbali ikiongozwa na wilaya mama ya raslimali kupata tuseme 1 percent of the royalty. Serikali inaweza kubaki na kodi nyinginezo.

Najua hili ni gumu kulitekeleza (complexity) na serikali (the center) hazipendi kuachia udhibiti wa raslimali kwa walezi (the periphery) kwa kiasi kikubwa, lakini kama hatukufanya hivyo na tukiendelea na maendeleo yanayoelemea sehemu kadhaa za taifa hakuna mashaka kuwa hili litakujatuletea ghasia.

It is cheaper to maintain peace through good neighbourly relations than erecting fences and hiring security guards. Hata haya mamigodi yataacha kuwa profitable kama yamezungukwa na jamii hasimu (hostile proximal communities).

my unedited two cents.

mchilyi7.0






-----Original Message-----
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sun, Dec 16, 2012 3:43 pm
Subject: [wanabidii] RAIS WANGU MPENDWA…..MTWARA KUNA TATIZO.

SALAM KWA RAIS WANGU MPENDWA…..MTWARA KUNA TATIZO.    Na Baltazar B.komba.    Nianze kwa nukuu za jumbe kutoka kwa ndugu zangu na rafiki zangu wa  Mtwara jumbe hizi zimezagaa katika simu za mkononi huko Mtwara jumbe  hizi zinaashiria kuna jambo linahitaji kushughulikiwa kwa mstakabali  mwema wa Mtwara na Tanzania kwa ujumla    Mali za kusini zilichukuliwa wakati kuna makambi ya wapigania uhuru na  mali hizi zilitumika kuletea sifa taifa na mikoa mingine, Leo gesi  yetu inahamishwa kwenda huko huko tunaambiwa ni mali ya taifa, je  kusini ni taifa gani?Tusikubali kuondolewa gesi yetu ndio urithi wa  vizazi vyetu kama wewe ni mzalendo tuma sms hii kwa watu ishirini kama  na wewe unakubali kuwa fisadi kujidhulumu urithi wa watoto wako, basi  nyamazia kusini bila kanda zingine inawezekana amka jitambue okoa  vizazi vyako.(0652 137989)    Mikoa ya kusini ndio ilikuwa mikoa ya kimkakati katika mapigano ya  vita kusini mwa afrika,Mazao yetu kama mihogo,Mpunga,ufuta na mahindi  yalichukuliwa kwa ajili ya kuwachangia ndugu zetu walio kuwa  wanapigana vita , na mikoa hii ilikuwa kama yenye vita kwa kipindi  kirefu hali hii ilitufanye tukose fursa za maendeleo mpaka sasa,  Lakini pia tukumbuke kuwa reli iling'olewa bila sababu kuwekwa wazi na  sasa gesi inaondolewa bila sababu kuwekwa wazi ndgu wana Mtwara  tusikubali tukatae tuma ujumbe huu kwa watu wengi uwezavyo(0715616006)    Rais wangu hizi ni jumbe zilizo ingia katika simu yangu siku ya Tarehe  24/11/2012 na 25/11/2012 zikiwa zimetumwa na wananchi wakazi wa Mtwara  na siku ya tarehe 14/11/2012 nilihudhuria mkutano ulioandaliwa na TPDC  katika ukumbi wa Makonde pale Mtwara mjini mkutano huu ulikuwa na  lengo la kuchuka maoni ya wananchi juu ya utengenezaji wa rasimu ya  sera ya gesi. KIlicho tokea katika mkutano huu unaweza kumuuliza  mkurugenzi wa TPDC na najuwa hawezi kusema uongo tena kwa kuwa  aliambiwa kuwa atakuja kukudanganya kuwa wananchi wa Mtwara  wamefurahia sera hiyo ingawa haikuwa hivyo kilicho tokea ni wananchi  kumwambia mkurugenzi wa TPDC hawaihitaji maswala ya sera wakati tayali  gesi imekwisha ondoka na mikataba imekwisha ingiwa dhidi ya zao hilo  na wananchi hawakutoa mawazo yao kama ilivyo kusudiwa walikataa kutoa  maoni wakidai kuwa hawaja shirikishwa katika hatua zozote za  uchakatuaji mradi huo muhimu kwa mustakabali wa maisha yao.    Katika salam hizi sitaki kurudia kilicho wakuta mawaziri walio  ambatana na msafara wa sekretarieti mpya ya chama chetu haya najua  umeshaambiwa na katibu mpya wa chama cha CCM Mzee kinana, lakini si  mbaya nikakudokeza kuwa Yule mama aliye jitambulisha kwa jina la Rukia  Ismail Athumani ni mama mmachinga muuza samaki katika beseni usafiri  wake miguu trela yake kichwa maisha yanaenda, nafikiri umeambiwa namna  alivyo mshambulia dada yetu,mbunge wetu waziri wetu Hawa ghasia juu ya  suala hili hili la uchakatuaji mradi wa gesi na usafirishaji wa gesi  kwenda Dar salaam, Si rahisi kwa utamaduni wa wanawake wa mikoa ya  pwani wewe unajua hilo, kuwa na ujasiri mkubwa wa kuongea mbele za  watu katika hadhira kama ile tena kuongea kwa kukemea kwa jazba na  kumkemea mwanamke mwenzie zile ni dalili kuwa kuna tatizo linalo  hitaji kushughulikiwa mapema na wewe mwenyewe ,sitaki kuongea kuhusu  zile zomea zomea za wahuni…..!    Muh,Rais salam hizi sijui kama zitakufikia kwa wakati, ila kuzileta  niliapa tokea siku ile nilipo hudhuria mkutano wa kutoa maoni kuhusu  sera najua kipindi hiki muheshimiwa utakuwa unapumzika kutokana na  majukumu mazito uliyo yafanya ya kupanga safu katika chama chetu  chadema…lakini naomba unisamehe nimeoana nizitume mapema ili ratiba  yako ya majukumu itakapoanza kwa siizoni hii basi ikiwezekana uje  uongee na wananchi (si wazee wa chama chetu peke yao) wa Mtwara.    Muheshimiwa Rais wangu naomba unisikiliza kuhusu masuala mawili  makubwa yanayo zizima hapa Mtwara swala la kwanza ni suala la gesi,  wananchi hawajui chochote kuhusu gesi na unajua kama ulivyo sema siku  ile ukihutubia pale Dar salaam wakati timu yetu ya ushindi ikiwa  inapongezwa nakumbuka ulisema hivi nanukuu wao wakisema tusipo jibu  hata kama ni uongo utakuwa ni ukweli.    Mheshimiwa Rais Mtwara wananchi wana hamu ya kujua kwanini gesi  imepelekwa Dar salaam kwa bahati mbaya hakuna hata kijana wako mmoja  aliye mudu kuwaeleza wananchi kwa ufasaha juu ya suala hili na dalili  zinaonyesha kuwa hawajui, kwa bahati mbaya zaidi hata hawa wabunge  wetu maarufu kwa jina la Kaka(mjini) na Dada(vijijini) nao wapo kimya  tena hawana muda kabisa wakuongea na wapiga kura wao juu ya suala hili  na wananchi wameshindwa kuwashinikiza chochote wanadai kuwa kaka  alifanya mambo yetu yale wakati wa kumchagua naogopa kusema moja kwa  moja kwa kuwa sina evidensi ila huyu kaka anaonekana hajui chochote  juu ya wajibu wake kwa wananchi walio mchagua na wala hili ninalo  kuambia kuwa ni fukuto sijui kama hata anajua ila ukweli ni kuwa  Mtwara si shwari kuna tatizo    Muheshimiwa Rais jambo la pili ni Ardhi muheshimiwa Rais Mtwara ya leo  sisi watoto wa Kudihalika, Nammohe, Minjale, Lupanda, Namdimba na  wengine hatuna tena uwezo wa kununua ardhi hata kipande cha robo ekari  kwa matumizi yeyote ardhi katika mji huu imeshakuwa ni bidhaa adimu,  Manispaa wako kimya kupima ardhi na wakipima tayari imekwisha ombwa na  kunamaombi mengi ya muda mrefu sijui sasa kizazi hiki kitapata wapi  ardhi, na tunachoshuhudia hapa ni wanasiasa kuotesha majumba na  kuporomosha vitega uchumi na kuendelea kujilimbikizia viwanja si hivyo  tu muheshimiwa hata viongozi wa serikali yako nao wanajipatia maeneo  huku kwa kasi ya ajabu na kwa habari tulizo zichomoa zikiwa mbichi ni  pamoja na malalamiko ya madiwani eti kila wanapo kaa katika vikao vyao  wanapo taka kupima viwanja wanakutana na maombi kwa ajili ya matumizi  maalum maombi ambayo hayatakiwa kuhojiwa wala kuulizwa kwa kuwa ni  maalum mimi mwandishi wa salam hizi nakumbuka niliandika maombi kwa  njia ya barua kuomba kiwanja mwaka 2008.mpaka naandika waraka huu  kwako hata jibu sijapatiwa…!    Jambo jingine ambalo kelele zake inawezekana umezizowea ni kuhusu zao  la korosho kuna minong'ono huku mitaani kwetu kuwa wanao angusha bei  ya zao letu hili la korosho ni hawa viongozi wetu tulio waamini kuwapa  nafasi za kutuwakilisha huku katika jumba la maamuzi na kutungasheria  na kisa kikubwa kinazungumzwa huku ni kuwa hao nao ni miongoni mwa  wenye makampuni haya ya kifisadi yanayo jifanya yananunua Korosho kwa  mfumo usiotakiwa na wananchi mfumo wa stakabadhi gharani,    Muheshimiwa kama kuna vita inakuja Mtwara ni vita ya Ardhi kwa kuwa  wananchi wa kawaida wamepoteza matumaini kabisa ya umiliki Ardhi na  hakuna kiongozi wetu tuliye mchagua anaye onyesha utashi wa kisiasa wa  kuja na mbinu au mkakati wowote wa kumilikisha wananchi Ardhi.    Muheshimiwa Rais kupitia salamu hii tunaomba utusaidie haya yafuatayo  kwanza uje utuambie tusiuze tena kura mwaka 2015, Na utuambie umuhimu  wa hicho kitu kinacho itwa ARDHI katika maeneo yanayo patikana  Rasilimali kama gesi au mafuta hivyo tusiraghaiwe kwa kuwauzia  mafisadi wenye tamaa ya kuinunua nchi yote hii, na uje uwaambie  mafisadi na viongozi wa kisiasa na serikali wanao jilimbikizi a ardhi  kuwa hawataweza kuikalia kwa starehe kama hawa maskini wengi  wataendelea kuitwa wavamizi katika ardhi ya mababu zao, lakini kubwa  zaidi uje na mkakati maalumu wa kuwafanya vijana wa Mtwara walio  poteza matumaini ya kuwa wana Mtwara kwa kuwa hawana uhakika  wakuendelea kuwa Mtwara kwa kukosa ardhi uwasadie wapate ardhi,    muheshimiwa Rais yanayotokea katika nchi za wenzetu yaweza tokea kwetu  na dalili zimeanza kuonekana maana viongozi wakisiasa na serikali  wanajilimbikizia maeneo kwa kuendelea kuwalaghai wazee maskini  wawauzie bila kujali kuwa maeneo ya Ardhi hayapanuki na watu  wanaongezeka hali hii inasababishwa na uwepo wa uwekezaji wa gesi na  mafuta.    Lakini umaskini, kukosa elimu kutokana na mlimbikizo wa mkoa huu  kukosa fursa ni sababu za msingi za wakazi wake kutokuelewa umuhimu wa  masuala ya umiliki wa ardhi, sawa na sheria ya ardhi na 5 ya mwaka  1999.    Tukumbuke kuwa wajukuu zetu watahoji asili zao na wataambiwa kuwa wao  ni wana Mtwara achilia mbali wamakonde,wayao,wamakuwa,wango ni,wamwela  na wataonyeshwa makaburi ya baba,bibi,babu zao wakiwa wamezikwa katika  Ardhi ya Mtwara lakini wakati huo watakuwa hawana hata kipande cha  Ardhi na watakuwa wanaiona ardhi inayo milikiwa na Mushi, Shirima,  Mrema, Mfinanga, Mkama, Bundala katika hali kama hiyo maswali yatakuwa  mengi kuliko majibu na mwisho wake watakuwa hawana cha kupoteza na  hatua ya kukosa cha kupoteza ikifika maamuzi yeyote yanaweza kufuatwa  tusishangae kuona ya Biafra yakitokea pia hapa kwetu mungu apishe  mbali    Mimi ninaye kuandikia salaam hizi ni miongoni mwa wamachinga wenye  jina kutokana na shughuli zangu na sina tumaini la kumiliki ardhi leo  wala kesho kwa muujiza wowote zaidi yakuendelea kuitwa mvamizi tu  katika ardhi ya mababu zangu hii ni hatari sana,Naelewa muheshimiwa  Rais maandishi haya yanaweza kunibadilisha jina sijui nitaitwaje,  mwongo, mgombanishi,mpinzani au hata mchochezi au hata  vyovyote ,lakini nimeyaandika nikijua kuwa maandishi hayafutiki na  hasa maandishi kama haya yaliyo beba sauti ya kutafuta haki za watu  wengi wasio na sauti.    Muheshimiwa rais mungu amekujalia wewe binafsi kuwa na huruma hebu  tuhurumie sisi vijana wa Mtwara, hebu tumia hiyo huruma yako kuiokoa  Tanzania, hebu tumia huruma yako kuondosha balaa, na katika hili  usimuamini mtu njoo uongee na sisi wamachinga, uongee na sisi bodaboda  na wengine wengi    Muheshimiwa Rais nisikuchoshe na ujumbe huu usio na maana sana kwako  lakini kabla sija hitimisha ni vema nikakujulisha majibu nilyo wapa  wale wana Mtwara wenzangu walio nitumia ujumbe pale juu niliwajibu  hivi.    No.. No..Situmi ujumbe huu kwa mtu yeyote kwa kuwa huu ni ujinga wetu  wa kuuza kura kama chapati na sasa tunakumbuka shuka asubuhi, hivi  kweli gesi hii ingekuwa katika jimbo la Mchungaji Msigwa, Mnyika, au  January makamba, mwiguru nchemba, zitto kabwe ingesafirishwa bila  wananchi kujua au bila kuzingatiwa maslahi ya jimbo husika au mkoa  husika No situmi NO,huu ni uzembe wetu Sambaza ujumbe huu kadri  uwezavyo.  Haya ndiyo majibu yangu kwa jumbe nilizotumiwa na rafiki zangu hao  hapo juu kutoka Mtwara.  Ahsante muheshimiwa rais wewe pekee ndio tumaini letu okoa Mtwara okoa  Tanzania.  (Mtumwa wa watu)  +255 786-821744,767 821744,779 8217144.    (HAPA KUNA BANGO LENYE BENDERA MBALIMBALI LIKIWA MBELE YA OFISI YA  JIMBO MTWARA MJINI)  Bango lenye maneno ya…. Gesi kwanza vyama baadaye hakitoki kitu  hapa….. likiwa limewekwa nje ya ofisi ya Jimbo ya chama cha NCCR-  Mageuzi siku ya Tarehe 12/12/2012 siku ambayo vyama vyote vya siasa  isipokuwa CCM vimeungana na kufanya mkutano wa Pamoja wenye ajenda ya  kupinga kusafirishwa kwa gesi kutoka mnazi bay Mtwara kwenda Dar-es-  salaam    huuu ujumbe(kama ulivyo) nimetumiwa kwenye email nifikishe kwa zitto  kabwe.    --   Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com  nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com  Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com    DELL LATITUDE D 620 & D30    80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM  DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .    TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY    CALL : 0786 806028   Free Delivery in Dar es salaam    Kujiondoa Tuma Email kwenda   wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma    Disclaimer:  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal   consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be   presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to   this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.      

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment