Saturday 8 December 2012

RE: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI

Usilaumu viongozi wa dini tu kwani:
Unaona mtu amebaka akahukumiwa miaka 35 lakini keshokutwa mtaa huohuo mtu  anabaka tena kibabu (sio kijana) anakabaka katoto 5 years. Jee huyu hajuikama hilonikosa? mfano kauona ila anajiamini kuwa yeye hatopatikana au ataimaliza kwa kuhonga. Jee hao wanaokata vichwa watu na vitu vya siri Butiama hawana dini au mila? Jee hawajui ubaya wa kifo mbona wanajificha na kukimbia mkondo wa sheria?

Mila imekataza mambo mengi mno lakini watu wanafanya.Hata kuua wanaua. Ukikataa kukeketa mwanao-utaona ndugu yako anamuiba mwanao anamkeketa. Utafanya nini-ukamfunge shangazi-ukoo utakufanya outcast-unaogopa. Vipi huyo Mungu aliyembali na haonekani? Sababu za FGM ni nyingi:-
-Kukubalika ktk jamii ama mtoto male aliyetahiriwa ataingia jando la kiume kuangalia mashindano ya waliau tohara. Jibaba ambalo hajapitiatohara-haruhusiwi anaonekana mtoto. Kuna mtukuwa na umri mdogo akawa mtu mzima na mtu mzima kuwa mtotokwa kutokupitia mila-biological age na cultural age.

-Kumfurahisha mume ktk ndoa-tight vulva or vagina inayotokana na scar ya FGM. Hapa hawaangalii haki ya uzazi salama bali ndoa na raha za baba SIO Mama.
-Kuzuia maradhi-preventive health (vagina warts, genital herpes, chanroid, candida, trichomas etc. Hivyo FGC ni usafi. Au ni kutibu maradhi-curative health.Mila si yakomganga gyne kijijini atakushauri ukate ili uondoe warts. Na katika waganga wa kienyeji wapo wa aina zote-meno, maradhi ya kike (gynaecologist) na ya kiume, watoto, vijana na wazee; kisukari, figo kwa mitishamba; wa mifupa-bone setters (Muulize Dr Nyamliakung'e akueleze jinsi waganga wa mifupa wanavyo mchanganya). Mguu wa kukata mgonjwa anatoroka anakwenda kwa mganga anatengenezwa anabaki na kiguu kinaning'inia robo. Wapo wanaofanikiwa kitibu miguu ambayoingekatwa pia.

-Ulinzi-ukivuta yakiwa marefu kuna namna ya vivalo insitu kwa hedhi na kuzuia kubakwa
-Kukata na kutanua-mwemba. Husaidia ndoa za umri mdogo kurahisisha mambo yake.
-Esoto-kuboresha viungo na uzazi ambapokiukweli virutubisho hivyo husambaza ukimwina fungus diseases kuleta tubal infertility na ukimwi juu.
-Wanaotahiri wanawake baadhi hukataza ndoa na male asiyetahirimaana anaambiwa atakufa-mbona wanaoana. Watu wanaangalia kula au tumbokujaa na love.Kweli utakufa maana utaambukizwa maradhi kiurahisi panapo poor hygiene na HIV/STIs.
-Kila alichoumba Mungu kizuri lakini alimuumba shetani yupo anatujaribu daily. Ndio maana unakuta hata watu wa dini wakihusika na vitendo viovu. Haki za mtoto za kupendwa,chakula bora, kutokuonewa, Elimu, usalama wake, mavazi na malazi; haki za wanawake na za binadamu za body integrity zinakiukwa na ukeketaji,kupigwa na kukatwamkono, vidole, masikio eti kamuudhi mume. Mama mkwe anapiga mkamwana;kijukuu kimebaka bibi yake,wanafunzi kubaka walimu kuwakomoa na ukaliwao etc. Mila ipo wapi na dini ipo wapi? Bado mlolongo wa sheria kesi kuchukua miaka. Mwisho mwathirika anaamua kuchukua rushwa afute kesi. Dini ipo wanasali sana ila wanaamua kuficha kesi ya ukeketaji na ubakaji kwa ajiri ya heshima ya familia na kuogopa stigma.

Dini na mila huenda ni opium. Sheria na watendaji wake nimzigo mkubwa mwingineo. Bila ya donor money kwa NGO ndio kabisa uharakati wa msaada wakisheria utazama. Kwani serikali huwapa fungu ili watoe huduma ya kisheria bure au kwa mchango mdogo wa muhusika? Jitambue sawa lakini system ya sheria iwe fast na highly responsive.Na mila na desturi zikubali kubadilika usitengwe. Otherwise utakata tamaa na kuwa mtazamaji pia. Kihelehele kikakuua wakakuvizia kukupiga mapanga au kukunyima KURA. Ndio maana tunatazama kuogopa vyote hivi-kuvikosa KURA, kuogopa Kisasi.

-

`

--- On Fri, 7/12/12, Demetria Kalogosho <demetria.kalogosho@tgnp.org> wrote:

From: Demetria Kalogosho <demetria.kalogosho@tgnp.org>
Subject: RE: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI-Print
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 7 December, 2012, 5:20

Hapo ndipo mimi nashindwa kuelewa kazi ya viongozi wa dini wanapotuambia /wanapotusomea misahafu na kusema kwamba baada ya Mungu kumaliza kuumba mtu alisema ;"Tazama nilichokiumba ni kizuri na ni chema sana" maana yake kimekamilika bila dosari yoyote. Kwanini miaka nenda rudi, karne na karne hawa viongozi hawawezi kuhubiria watu kuacha ukeketaji wanawake unaotutesa wana wake? Mbona wanaona ni rahisi kuhubiria waumini  kukusanya pesa na kumpelekea Mungu asiyeonekana kwa macho? Kuna haja ya kujitambua na kuchukua hatua.

 

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Hildegarda Kiwasila
Sent: Thursday, December 06, 2012 8:57 AM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI-Print

`

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment