Wednesday 5 December 2012

RE: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI-Print

PRINT USOME:

Katiba inasema Haki za Binadamu. Haki za binadamu ni pamoja na haki ya mwili wako kuwa mkamilifu kama binadamu sio ukatwe. Sera ya afya ina haki ya afya kwa kila mtu na haki ya uzazi salama-safe delivery, primary health care for all. Na kimataifa kulikuwa na Health for all by year 2000 huko nyuma na sasa imeongezwa kupitia malengo ya Milenia.

Yupo Daktari miaka ya zamani nilisimuliwa na dada yangu ambaye sasa ni marehemu aliyekuwa pia mwalimu shule ya kanisa ya Lugoba. Alifika zahanati akitaka kuongea na daktari jamaa yake ambaye alikuwa busy akiingia na kutoka ofisi yake kachanganyikiwa hivi akitafuta solution. tatizo hakuelewa ule ugonjwa yule aliokuwa nao yule mama na hakuwahi kuuona maishani. Ashakum- Mama alivimba vibaya labia minora na majora (mapezi makubwa na madogo ya uke ya external genitalia. akamwambia ndio anahangaika sijui afanye kitu gani. Dada akamuuliza-muulize kama shida ni hiyo na kama hiyo imetokana na nini maana kuna watu wanamila ya kuvuta minora na majora (Kuvuta Matunya iitwavyo kwa baadhi ya makabila). Alipoingia ndani baadae kumuuliza mama huyo akasema hiyo ni mila yao ila huko ndani anajisikia hivi bila ya shaka pamoja na infection amevimba zaidi.Bila ya kuvuta ipo makabila mengi nisije nikaambiwa ninatukana hapa fika WRDP tumechora ramani ya mila za FGM kwa makabila yote. ramani hii ilitengenezeka vizuri kwa kuwauliza 'Wababa'. Wanawake ni wasiri sana sana na mila inataka hivyo.

Daktari ambaye hajawa exposed kwa mila za watu si rahisi kuzijua. Itakuwa kama yule wa Lugoba alishania mapezi yanayoning'inia ni ugonjwa kumbe yanavutwa na walitueleza yanatumikaje ktk menses na shughuli nyingine na kuzuia ubakaji!!  Eliza Muhigo afahamu hivyo.

Tulipogawa picha hizi kwa wauguzi wa MCHC Regional Hospital Morogoro na St Kizito Health Cetre Mikumi-tulipata positive response 2 kwamba zimewasaidia ktk kumzalisha mWanawake 2 wa Kisomali mmoja Morogoro na mmoja Mikumi waliokuwa safarini na waume zao enzi hizo 2002-2003. Kitini cha WHO tulitoa nakala-photocopy tukawapa baada ya semina kinaonyesha jinsi ya kumfungua na kumzalisha mwanamke akiyefanyiwa-Infibulation (Pharaonic Circumcision).  Picha niliyoweka ya infibulation ni moja tu ya type za FGC (ambayo Elisa, Muhigo anasema hajawahi kuona kitu hicho hospitali). Tuna wasomali, wa-Misri, wa-Sudan nchini. Nilisema hii TZ haifanyiki ila yapo makabila yanayoondoa external genitalia yote ila hawashoni na wapo wanaovuta labias na clitoris sikuitaja inavutwa wanafundishwa kuanzia age6-8 (nyamwezi, konongo, Bende, Kigoma, Ujiji tribal groups, mbunga, Pogoro, Nyakyusa etc); Mwemba (kupanua uke visichana-Ngindo) na sababu zake wametueleza ktk tafiti zetu tuna uhakika tuliongea na wazee ke na me. Tumechora ramani. Wengi watakataa. Usiri haufundishi. lakini clinical patiend blind investigation imeonyesha hata wasio na mila wametahiri-mchanganyiko wa ndoa, kutaka kukubalika ktk jamii hiyo, magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri ndio sababu kubwa-Vagina warts- au dole nimezionyesha za mama za baba (penile warts sikuonyesha); trichomoniasis-vaginatis; candidasis--vulvovaginitis yalionekana chango cah FGM kwa wasio mila-curative wenye mila-preventive. Sababu hizi za prevention/treatment tuliambiwa na tuliowahoji na kutaja symptoms za magonjwa wazuiayo. Wasio wa kabila linalotahili alieleza sababu na hata ule ugonjwa uliomfana atahiriwe ambapo gynaecologist tuliyemtumia (Dr Hiza wa Muhimbili) aliweza kuujua akauandika na kuwa ni preventable na treatable.

Kuna ushahidi TZ kuwa baadhi ya wazazi hutumia Nurses ili FGM iwe safe na wale watoao rushwa kukmkeketa mkamwaan ambaye hana mila hiyo na hataki kukeketwa humvisia wakati wa kuzaa. Wakati wa utafiti eneo moja la Pare-wahojiwa walisema upu unachunguza hili nurse wetu kwa sasa `kakataa kukeketa anaogopa na likizo inakwisha karibu watarudi shule nimekwama!! Wapo wafanyao kutumia wakeketaji kimila na ni sherehe kijijini. Wengine hukeketa kificho na kuwatoa nje ktk sherehe wengine hufanya in public na wanaume kushuhudia msichana jasiri aliyelia.

Sexual pleasure si sababu kwa makabila yote-kuzuia maradhi na kuboresha uzazi ndio tuliona muhimu. Doctor anajua kuna pleasure za source nyingi na ndio maana hata waliokeketwa vibaya wazee na wazazi wetu wamedumu ktk ndio na hawa wa makato ya CCM (makato kidogo kialama tu) mbona zina poromoka? 

Katika  Mkutano wa FGM Niliyohudhuria Misri miaka ya nyuma wakiwapo medical doctors wengi kama Asaad na wengineo Nahid Toubia na vingunge wengine wa FGM walieleza kero nchi zao za kiislamu za kiarabu ni FGM kufanywa hospitali-legal. Tatizo hili wakipambana nalo ikokeshwa. Pia Uk, USA wakifanya hospitali (private doctors) kuwasaidia wenye mila-dini itakayo usafi huo na wamepiga marufuku baadae bara ulaya na marekani. Soma Kitabu cha Sam A. Aldeeb Abu-Sahlieh kinakuonyesha makato na marembo mbali mbali ya Clitoris inavyofanywa na daktari-rasmi hospitali. Hapa kwetu wanapohusika NI SIRI.

Kama hujaona makato hayo ya mvuto ya external genitalia (kuvuta matunya) wengine wameona ila pia ni SIRI ya daktari kutokuongea vya watu. Tunapokuwa mikutano ya nje Ulaya-wawakilishi kutoka Africa hucharuka kupanda wazimu mila hizo zinapojadiliwa wanaona kama wanaingiliwa culture yao-inashangaza.

Anyway-FGC/FGM kabila zote pia tohara ya kiume inachukuliwa kuwa ni mila 'ndogo sana'. 'Mugua' huitwa kwa wengine-kumugua kidogo tu hata kama ni kukata labia minora zote.
Mafunzo-kufundwa mwali, au 'kueka mperi' kwa wanawake; au 'Mshitu we Nyumbae' (Pare) au mafunzo kwa wanaume ndio kiboko yao-ngoma kubwa.familia zenye uwezo Africa na Ulaya hutumia private health facilities, doctors, nurses kutibu, kuzalisha ili kuficha mambo yao ya siri (FGC, sodomy etc). Hii inajulikana, tusipotezeane muda imeandikwa.

Vitabu Nilivyotaja hapo nilipoweka attachment Elisa avisake mtandaoni na katika maktaba za Gender vitakuwepo. Nahid Toubia ameonyesha makato ya aina yote na ni Daktari. El Saadawi pia. Madatari wa Misri ndio gender activists wakubwa kiasi kwamba wengi wamepata matatizo ktk nchi zao. WHO imetoa makala mengi. Fahamu Misri FGM inafanywa na kinyozi wa nywele pia ni saehemu ya shughuli yake.

Kama tuachie watoto wakimbilie-kanisani, kwa DC, Msikitini kukimbia FGM, watalishwa na nani? Si kuteganisha watoto na wazazi? Vituo vya malezi kuna usalama iwapo ukakaji wa vitoto unaongezeka nchini na walimu etc kuhusika? kwa nini tusitumie mbinu za dialogue na kuonyesha video, picha kwa wazazi na walezi na kutumia sheria inaposhindikana? Mtoto alelewe kwao apate upendo wa wazazi. Baadhi ya watanzania na nchi nyingine wametumia FGM kupata kibali ya uhamiaji ulaya ila sasa wamewashitukia. Eti wanataka kunikeketa nipo hatarini wakaanza kujazana ulaya!

Tumehoji waliotahiriwa utoto wakadhani hivyo ndivyo ilivyo hadi alipoolewa na mume kumueleza ana mushkeri. Mmoja alithibitisha kuachwa kutokana na makato aliyokuwa nayo. Sasa doctor Elisa anasema ikikatwa na kuchimbwa huwa inakua tena-sielewi. makato ya Excision (kuondoa vyote na wanachimba na scar yake balaa) na kama ni infibulation inarudije?
 
Picha ya kufananisha male and female organs kwa rangi ni kukuonyesha kuwa kuondoa external genitalia ni sawa na kupangusa vyote vya external genitalia vya baba. Kuondoa clitoris-ondoa penis, kuondoa labia minona and majora-ondoa testis zote doctor. Jee-tutazaana tena. Kila mtenda atendewe nawe aone inavyonoga. Sitongea tena suala hili bali nitaweka another paper/mada tu yenye picha pia iliyotolewa na WRDP semina fulani ya TAMWA  ambayo inaonyesha kinachoendelea nchini ktk suala hili. Nitaisaka tuelimishane.

Please, Tafuta Daktari  Elisa vitabu:

- Dorkenoo, E (1994) Cutting the Rose. Female Genital Mutilation. The Practice and its Prevention. Minority Rights Publications. 379 Brixton Road. London. UK.
- Elworthy S and Dorkenoo, E (1992) FGM. Proposal for Change. Minority Rights International Report uone picha ya baada ya kushonwa hivyo mume alivyochana eneo hilo kwa tendo la ndoa. Ni picha sio mchoro na kina michoro pia. Dorkenoo ni Nigerian anasimulia jinsi alivyosaidia wasomi walimu wa vyuo Uk wasirudishe watoto wao kukeketwa Nigeria.
- Asaad, M-Female Circumcision in Egypt, Current Research and Social Implication. Huyu ni daktari mwanamke Mmisri.

Toubia, Nahid 1994, Female Genital Mutilation and the Responsibility of Reproductive Health Professionals. Global Action Against FGM . New York 10276. USA.

-Bewes, T.F.C 91946) Maarifa ya Uzazi. A book for Africans on Sex Hygiene. Published bythe General Secretary of the African Council. Diocese of Mombasa (wameanza kuhangaika siku nyingi huku kwetu kutusaidia usafi wa huko mahala badala ya kukata kama prevention au tiba ya sexually transmitted diseases na kuboresha uzazi.

-Cairo Family Planning International-1991. Facts about Female Circumcision

-Chell, A 1979-Nomadic Sexual Practices: A case Study of Sudan WIN NEWS, Genital and Sexual Mutilation of Females. Women's International Decade, 187 Grant St Lexington, Mass. USA

Kaisi, M 1988 (Gynaecologist wa Tanzania) Adverse Effects of FGM. Dept of Obsetric and Gynaecology, Muhimbili Medical Centre (jee huyu naye anadanganya uwepo wa mikato mbali mbali?).

-Mbunda, D 1988, The adverse effects of FGC, its history and Ideology. Institute of Adult Education Tanzania.

-Cowans, J and Graham, T 1989-Traditional Health Practitioners and the Spread of HIV in Sub-Saharan Africa. A research study prepared for ODA. University of Swansea UK

-Cory Hans 1956 na Beildelman, T.O 1967 wameandika kuhusu mila na desturi za makabila mbali mbali Tanzania-File zipo UDSM east Africana Section.

-Koso-Tomas, O 1987 (mnigeria) The Circumcision of Women-A Strategy for Eradication. Zed Book Publishers Ltd. London, New Jersey.

-Kenyata, J 1961-Facing mount Kenya. The Tribal Life of the Gikuyu (-Anatetea iendelee ni MILA, wazungu tuacheni, hujakamilika bila mila kama FGM). Fahamu. kuna makabila hayakati au kutahiri wanaume bali yanakata ngozi pembeni, kuvuta chini ngovu (kuipurura) na kuifunga vingofya paende 2. hawa wanaume wanaumia sana sana. Watu wengine wana myths kwamba wanazo mbili. Ni mateso kama wanavyoteza wanawake wao kwa kuondoa kila kitu bali hawawashoni kama hao wa Sudan, Somalia, Misri, Ethiopia etc.

-Mitzlaff, Ulrick 1994 (aliolewa na Mmasai kisha akaandika kitabu-ndoa ya research!!)-Maasai Women. Life in a Patriarchal Society. Field Research among the Parakuyo Tanzania. Tanzania Publishing House
-Omari, C.K (1971) Lawalawa na Nkiiri: Matumizi mabaya ya utamaduni huko Singida. UDSM (singida waliua watoto wengi kutokana na tohara ya dharura ya watoto wengi kutokana na ugongwa wa lawalawa (kuwashwa sehemu za chini ambao ni uchafuzi kutokana na mazingira, nduo chafu etc). Professor Omari (Marehemu) alitumwa na GVT kuangalia suala hilo.
-Mwisho, list ni kubwa ni mwandishi kutoka Ulaya pande za Norway nafikiri-aliyefanya kazi ya udaktari nchi za africa-Skramstad, H 1990-The Fluid meaning of circumcision in a multiethnic context in Gambia. Distribution of knowledge and linkage to sexuality. Derap Working papers D 12. Michelsen Institute. Dept of Social Science and Development.

--- On Wed, 5/12/12, Demetria Kalogosho <demetria.kalogosho@tgnp.org> wrote:

From: Demetria Kalogosho <demetria.kalogosho@tgnp.org>
Subject: RE: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, 5 December, 2012, 14:50

Je, katiba mpya isemeje kuhusu ukatili wa kijinsia, hususani UKEKETAJI WANAWAKE NA WASICHANA????????????????

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of ELISA MUHINGO
Sent: Wednesday, December 05, 2012 2:50 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI

Nafikiri kuambizana ukweli ni vizuri zaidi.

Mimi nimefanya kazi kama tabibu kwa muda fulani katika mikoa wanayotaili wanawake.

Najua na nimeona mateso wanayopata wanawake waliotahiriwa hasa wakati wa kujifungua.

Lakini sikuwahi kukutana na hali inayoonekana katika picha anayotuletea hapa Hilder.

Mimi ni Mhaya na kwetu hakuna kutahiri wanawake. nakiri kuwa ni kitendo cha ikatili. Nilipoulizia wazee katika maeneo wanayotahili wanawake, wanasema sababu ni kumfanya msichana asiwe 'malaya'. Wanafanya hivyo ili vile viungo vinavyochochea 'hamu ya mwanaume viwe havipo'.

Siamini kama hata kusudi lao linatimia kwani kumuondolea binti kiungo (Clitoris) akiwa mdogo, hadi anavunja ungo huwa kimerudi cha kutosha kumfanya ajisikie.

Ninachotaka kujua na kuhakikisha ni kabila gani la tanzania linafanya tohara inayoonekana kwenye picha ya Hilder? Maana katika picha hii nakuwa na wasi wasi kana kwamba ni 'procedure' iliyofanyika hospitali.

Ni mila gani ya watu wa mkayani walioweza kuondoa viungo hivi na kumshona huyu mhusika hivi bila kuwa hospitali na akapona bila uambukizo (Infection) kuzunguka eneo lote. Lingepata uambukizo kovu lisingekuwa hivi.

Nataka kujua?

Elisa

--- On Tue, 12/4/12, Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: wlac@wlac.or.tz, wildaf_tanzania@yahoo.com, tpfnet2007@yahoo.com, info@wat.or.tz, akaruwes@futuresgroup.com, lhrc@humanrights.or.tz, stella.mwambeja@yahoo.com, emajani@engenderhealth.org, haitz@helpagetz.org, tawla_tawla@yahoo.co.uk, mewataa@yahoo.com, envirocare@bol.co.tz, envirocare_2000@yahoo.com, wrdp@udsm.ac.tz, fabia_shundi@yahoo.com, sherrykassim@yahoo.com, kivamwo@yahoo.com
Date: Tuesday, December 4, 2012, 7:26 AM

Wadau wa Utokomezaji wa Ukatili wa kijinsia- kwa maoni yangu hakuna kuficha kitu hapa.Demetria Kalogosho ametufundisha kitu muhimu kwa kutuwekea picha sisi watu wazima tuone watoto wetu watakavyoteswa wakati mwingine bila ya ridhaa yetu. Ndygu anaweza akakuibia akamkeketa kwa kukuona wewe eti unajifanya msomi au umeokoka huzingatii mila. Ninaona kuficha ukweli kama aonavyo Nd Kailima Kombwey si sawa. Heshinda iwepo lakini tujadiliane na tuonyeshane ukweli. Ama sivyo hatutoweza kuelimisha jamii na sisi wenyewe kujua kinachoendelea nchini ambavyo ni kinyume cha haki za binadamu.

Tena hii picha ni ya mtoto mdogo. Watu wamejitoa ktk TV wakionyesha matende ya kutisha pamoja na kutitoa ktk gazeti akionyesha hydrocele lilivyomzidi ili apate msaada. Hii ni toto/sio ya maana kwa hizo.

Wapo watu wazima wanaokamatwa ukweni na kukeketwa kwa nguvu au anaviziwa wakati wa kujifungua nurse anapewa kaposho au akizalia kwa mkunga wa jadi mpango unafanywa. Wakati wa civil war uganda yupo mama alisimuliwa alivyokatwa kisha akabakwa kwa kuchangiwa, akatumbukizwa kwenye mto wenye mamba bahati akaweza kusota na kutoka, akatembea kilometa kadhaa. Hizi aibu za kutazama na kuongelea yanayotokea ktk mila na destruri zetu ndizo zinazofanya baadhi ya maovu yaendelee.

Vita vya congo, imetoka radioni na ktk TV wanaume wakilalamika kutendewa uchafu ktk vita lakini hawapati msaada wa ushauri na matibabu kwa kutokana na mila zetu na vizuizi vyake. Wanahitaji msaada na matibabu ya kuzuia na kutibu maambukizo lakini wanashindwa pa kuanzia aseme-nimebakwa (mwanaume amekabwa na wanaume). Inawanyima watu jinsi ya kupata misaada tunapoona kuficha ndio tija. Haipendezi.

 Kwani hata viongozi wa Siasa huogopa kwenda katika makabila yao kwenye majimbo yao walikochaguliwa (kwa wale waliochaguliwa kwao) kuongea na watu wao na wazee wa mila masuala ya kutokomeza mila potofu na tabia mbaya zinazoleta madhara. Hadi leo hii kabila linaweza likasimama na kusema-tutakeketa na tuna wasichana elfu 5 wa kufanya hivyo tuone wa kufanya kitu!!
Yanini tuwe na wanasiasa, wanasheria, makanisa, misikiti na viongozi wa dini maeneo hayo? Kwa nini tuwe na police, JWTZ na mahakama, wanaharakati, SOSPA, katiba na mahakama? Raia atawale na kusema yupo above wote hawa na tumtezame akikeketa? Tuyaongee, tuongee nao na taifa na vijana wao ambao pamoja na vyombo vya serikali na wanasiasa wa eneo hilo ni wengi kuliko hao wazee wachache.

Kuna la kujibu hapa. Tuyaongee, tuonyeshe ili kujenga ufahamu wa matatizo ili tusaidiane kuyatatua.  Ndio hivi kwa kutokuyaongea na kuonyesha wengi hudhania Matende na mabusha ni ugonjwa tu wa pwani unaotokana na nazi na madafu. Kumbe ni ugonjwa unaotokana na uchafu wa mazingira na joto na kuwepo mbu wa kusambaza vimelea.

Climate change inaleta mabadiliko na joto na ukame unazagaa, uchafu wa mazingira na uwepo wa kinyesi cha mifugo na vyoo vya shimo vitapeleka tende na hydrocele (busha) hadi juu Iringa na Kilimanjaro. si wanakuja DSM kuleta bidhaa na kufanya biashara, mabus yanakuja na yanarudi huko na mbu culex na vimelea vyake tunawapelekea culex wa milimani kwenye joto wanavibeba na kuvisambaza. Tuwaonyeshe picha ya tende na hilo lingine waone-maana hatuoni tunaona vimetuna ndani ya nguo unadhania ni dafu hilo. Kumbe ni kitu ambacho nawe unacho kinaweza kuharibika hivyo. Kuona kunasaidia kumbukumbu na ufahamu kwa asilimia 80%. Tukificha pseudo science ya kusingizia visababishi vya uongo kwa maradhi itaendelea.

Zipo video za wasichana na wavulana wakitahiriwa na zinatumika hapa nchini ktk kufundishia mangariba. Mimi ni mmojawapo niliyezitumia tuliagiza kutoka nje na kupata baadhi kutoka Wizara ya Maendeleo Secretariat ya kutokomeza Ukeketaji. Video hizo za Kenya, Somali, Uganda, ethiopia za wasichana na wavulana zilifunua watu akili na Ngariba au wakeketaji walishindwa kuangalia. Waliona ni ukatili ulioje hawajui kama nao huumiza na kuathiri watu kama walichokuwa wakiangalia.

Wapo wasichana waliotahiriwa lakini hawajui kama wametahiriwa kwani wamekua wakubwa wamejikuta hivyo walidhania ndio inavyokuwa hivyo. Baadhi imewaathiri kindoa baada ya kuolewa mume hamtaki anarudisha mke kwa wazazi kwani alichokiona hakubaliani nacho.

Wapo wanaopata madhara ya Fistula kutokana na FGC/FGM na akiwa na Fistula mume anamuacha maana(Ashakum)  msamba umeunganika na vagina kinyesi kinapitia mbele (ukeni) au anavuja mikojo mfululizo kibofu kimeunganika na vagina mikojo inatoka mfululizo kupitia mbele na hauna kizuizi kama hicho kinyesi. CCBRT imekuja imewafanyia akina mama na dada hawa wenye Fistula miujiza na kuwarudishia utu wao. Kijijini wanawaona watu hawa wenye fistula lakini wanasema-wamelogwa na watu kushikana uchawi. Mke mdoko kumshuku mkubwa etc. Kumbe ni Female Genital Cutting (FGC) kama kisababishi kimojawapo na kwa sehemu kubwa pia.

Tuwaonyeshe na tuonyeshe aina mbali mbali za makato (see mojawapo attached na ntaongeza kuwaonyesha nina vitabu vyake nivisake nibandike zaidi).

Tulionyesha Video tarafa ya Mikumi kwa makundi mbali mbali, tukajadiliana FGM.FGC na madhara yake. Tulipotembeza vipeperushi vya maelezo ya Fistula baada ya mafunzo hayo  tulipata wanawake wengi wenye Fistula (VVF na RVF) bila ya kutegemea tukawasafirisha kwenda CCBRT. Kama si mafunzo ya kuonyesha picha na video za FGM na madhara yake-na vipeperushi vya fistula tulivyopata Women Dignity Project na ikatuunganisha CCBRT tusingepata hao wagonjwa wa fistula ambao walikuwa ni wasichana wanaopendeza umri mdogo. Waliowengi wanaachwa na waume zao kutokana na hali zao za kinyesi na mikojo. Inataka moyo kuwasafirisha, kukaa nao kwako ili kesho umpeleke CCBRT au kama clinic imejaa ghafla umeambiwa asubiri a day or two. Bado hao ambao makato yamefanya ametunga usaha mbele, amefishwa kuogopa gvt, anaoza anaharibikiwa.

Tukubali kuzijadili na kuzionyesha na kuzitokomeza zile mbaya zenye madhara. Tusione aibu maana leo mwingine kesho ni mwanao au dadako, mjukuu wako anapata madhara haya ya kuepukika. Kupanua uke watoto wadogo (mwemba) na kuingilia visichana vidogo sexually (esoto) kama mila, kuoza vichanga etc vyote tuviongee na madhara yake na picha tusizifumbie macho. Heshima ya Mila na uafrika wetu viwepo inategemea unaangalia na nani-mtandao huu ni wa watu wazima. Yet utakuta vijijini watu wazima wanaangalia picha za matusi na watoto wadogo ktk vibanda vya nyazi kwenye video za kulipa. Pia kuna vibanda kwenye machimbo vya shutashuta (chapu chapu) tumejipanga foleni na vyangudoa na watoto wanatuona. Mitaani kila baada ya nyumba tatu kuna bar na watu wanakwenda haja hovyo watoto wanawaona. Ama wakati mwingine tu nduma kuwili.

Ikitokea ajali ya gari watu wapo hovyo kundi kubwa utaliona la watoto linaangalia, watu wamekatika vichwa n.k bado hizo dansi za matusi ya nguoni tunazoziona daima ktk TV watoto wanaangalia mama zao na baba, kaka zao wanavyocheza kwa kupekecha maeneo ya utupu. Tunashindwa kutokomeza haya ya wazi (utandawazi kama excuse). Kufundishana humu sisi watu wazima sio kosa hata. Ieleweke tunafunguka.

--- On Mon, 3/12/12, Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com> wrote:

From: Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, 3 December, 2012, 8:02

Ni ukatili usiokubalika. Ni vizuri kwamba picha inatupa hisis ya jambo lenyewe na kuguswa sana. Lakini pia ni nudhalilishaji kwa watoto kuonesha picha kama hii. Napendekeza iondolewe kwenye mtandao.

Vin

On Mon, Dec 3, 2012 at 10:47 AM, kailima kombwey <kailima.kombwey@googlemail.com> wrote:

Kwa hiyo hata picha ya kichwa cha mtu kilichochinjwa na kutenganishwa au watu wanaopigwa picha wakiwa wanazini nazo ziwekwe hapa ili watu wajifunze? Hujuwi Desturi za Mwafrika Mtanzania? Unadhani picha hizo kuwa hadharani kutasaidia? Suala la kusaidia ni kuelimisha kwa kadri inavyowezekana na vyombo vinavyosimamia sheria kutumiza wajibu wao kwa wote wanaofanya haya na siyo kuweka picha hizi hapa. Tudhani ni ndugu yako wa kike utajisikiaje?

On Dec 3, 2012 10:21 AM, "Lutgard Kagaruki" <lutgardk@yahoo.com> wrote:

Nadhani si vibaya; hata ambao hatujawahi kuona tushuhudie. Kuficha hakusaidii.  Hata hivyo desturi zetu zipi?? Hii ni kwa ajiri ya kuwasaidia hata wengine. Mwili wangu umesisimka kwa woga na uchungu!! LKK

From: kailima kombwey <kailima.kombwey@googlemail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: sophiawambura@yahoo.com; eneeso@pathfind.org; nathanielissa@ymail.com; tawla2000@yahoo.com; icnictz@gmail.com; envirocare_2000@yahoo.com; chesociety@yahoo.com; piastellah@yahoo.co.uk; info@hdt.or.tz; katri@kiwohede.org; markwambura@yahoo.com; mghambagrace@cdftz.org; envirocare@bol.co.tz; fchilimo@pactworld.org; netwo2002@yahoo.com; mewataa@yahoo.com; msangilaura@hotmail.com; Zumuni2008@yahoo.com; childrenwidows@yahoo.co.in; stella.mwambenja@yahoo.com; tomkiwala@yahoo.com; peacetanzania@yahoo.com; tahurifo1@yahoo.com; wofatatz@yahoo.com; adolfkissima@yahoo.com; fawetz@posta.co.tz; shivyawata@yahoo.com; mosesgasana@yahoo.com; Jansgar2002@yahoo.com; lrmbise@ywcatanzania.or.tz; MBetron@engenderhealth.org; elipunda@yahoo.co.uk; mwajey2003@yahoo.co.uk; berthaney@yahoo.com; mhinablandina@yahoo.com; mcharolydia@yahoo.co.uk; fnzema@hotmail.com; wlac@wlac.or.tz; info@tcib.or.tz; holmstrom@unfpa.org; lucy.merere@dfa.ie; eliza@yahoo.com; wildaf_tanzania@yahoo.com; tpfnet2007@yahoo.com; info@wat.or.tz; lucy.chamwi@yahoo.com; siltanmziray@yahoo.com; m.mshana@yahoo.com; laseha@gmail.com; murio@mst.org.tz; mawazochanya@gmail.com; children_widows@yahoo.com; judieus@yahoo.com; akaruwes@futuresgroup.com; merykessi@gmail.com; gearoid.loibhead@concern.net; mpungulez@yahoo.com; tawla_tawla@yahoo.co.uk; janethkeha@yahoo.com; mpangulez@yahoo.com; neemaduma@yahoo.com; deus.kibamba@tgnp.org; lhrc@humanrights.or.tz; gmtenga@unicef.org; khamar.kashoro@co.care.org; haitz@helpagetz.org; edacha2002@yahoo.com; gmunuo@yahoo.com; drkatanta@yahoo.com; b.ench@yahoo.com; ksimwanza@engenderhealth.org; floramasue@yahoo.com; merykessi@yahoo.com; stella.mwambeja@yahoo.com; fmakoye@yahoo.com; emajani@engenderhealth.org; lrmbise@ymcatanzania.or.tz
Sent: Monday, December 3, 2012 10:03 AM
Subject: Re: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI

Sidhani kama ilikuwa busara na kwa desturi zetu kuweka picha hii hapa.

Tuwe tunatumia busara walau kwa 23%  kabla ya ku uproad picha

On Dec 3, 2012 9:56 AM, "Demetria Kalogosho" <demetria.kalogosho@tgnp.org> wrote:

JAMANI WADAU WA GBV JIONEE UKATILI HUU

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment