Monday 17 December 2012

Re: [wanabidii] NHC na changamoto ya makazi Nchini

Zamani nilifurahi kusikia stori za kutiana moyo na zilinifanya kuunga mkono hata kama zilikuwa za kipuuzi. Hebu fikiria mtu anakuambia sement mfuko itakuwa elfu 5 badala ya tshs elfu 25 then unampigia makofi real?@#$%%&&"""""""!@@!

Napenda kusikia kauli za kutnitia matumani  but si kauli za kujazana ujinga hata kwenye impossibles najua mkubwa Slaa anasoma jumbe zetu kama kweli alisema hivyo mie ni mmoja wa watanzania tunaoipinga kauli hiyo na anaweza kutupa majibu hiyo yawezekana vipi.

Tatizo nilionalo kwa watanzania tulio wengi tunataka kukaaa na neema ishuke hali haiko hivyo na haitakaa iwe hivyo. Mwanasisa ninayemtaka mie kwa sasa awe ni yule atakae weka mazingira ya kila anayetumia akili yake kufaidikia na bongo yake. Naamini katika usawa lakini haimanishi tutakuwa na uweza sawa kwa kila kitu watakuwepo masikini matajiri na mafukara lkini so long as national bread any how inagawanyika kwa kila mtu hiyo ni poa.

Tuna uweza wa kuwaonyesha wanasiasa kuwa sie si kilaza tufanye mambo na si kusuburi kupigiwa makofi kwenye majukwaa ya kisiasa na wanasisa cheap popularity inatuuua mno

2012/12/15 Gikaro Ryoba <rgikaro@yahoo.com>
Tatizo hawa wanasiasa wanamuona kila mtu ni kilaza. Eti wanajenga nyumba kwa mlalahoi halafu wanamuuzia kwa milion 140! Wananchi hawana uwezo wa kununua nyumba ya milion 50, hiyo ya milion 140 wataiwezea wapi? Huu nimchezo wa kuigiza.

From: Hosea Ndaki <hosea.ndaki@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, December 15, 2012 7:41 PM
Subject: [wanabidii] NHC na changamoto ya makazi Nchini

Katika mambo ya msingi kwa binadamu ni pamoja na Chakula, mavazi na malazi. Watu wakipatwa na njaa serikali iko tayari kuwapa watu hawa chakula na ikiwezekana bure kwani ni haki yao ya msingi kama watanzania na binadamu, niliwahi shuhudia pia misaada ya nguo kwa familia masikini, hii yote kuwa utu wa mtu ni pamoja na nguo na ni haki ya msingi kwa kila mwananchi.
 
Malazi yakiwemo makazi ni huduma ya msingi kwa binadamu pia kama ilivyo chakula na mavazi ndo maana ukifika hotelini wanakukaribisha "karibu jisikie uko nyumbani", sote tulishuhudia mafuriko yalivyo haribu makazi ya watu na hata waliokuwa wakiishi maeneo hatarishi kupatiwa makazi mapya kule Magwepande. Heshima ya mtu pia inajengeka katika makazi ndo maana ukipeleka hati ya nyumba benki unaweza pata mkopo bila shida.
 
Mwaka 2006 kiongozi mmoja wa juu aliulizwa na wananchi wa sengerema kumetokea nini siku chache tu baada ya uchaguzi cement imepaanda bei kutoka 12,500. hadi 25,000, kiongozi huyo hakuwa na jibu la uhakika zaidi ya kusema watanzania wanakaa vijiweni bila kufanya kazi na kukalia majungu.
 
Katika uchaguzi wa 2010 Dr.Slaa alikuja na kauli mbiu kuwa kama atatwaa hatamu za uongozi basi atahakikisha bei ya cement inashuka kutoka 25,000 hadi elfu tano kwa mfuko, na atahakikisha hakuna mtanzania aneishi kwenye nyumba ya tembe. Jambo hili lilimfanya awe maarufu kwa maeneo mengi ya nchi kwani hakuna anaependa kuishi katika nyumba mbovu kama mtu asivyopenda kushinda njaa au kukosa nguo.
 
Juzi niliona kituko kipya, nao nimzozano katika uzinduzi wa nyumba za NHC, nasema hivyo kwani viongozi wote walikuwa wanalalamika, yaani huwezi jua bosi ni yupi hasa maana kila mtu analalamika tu! wakati mkuu wa kaya akilalamika kuwa serikali za mitaa zimegeuka kuwa madalali wa viwanja, alitoa mfano ambao umenisukuma pia kujenga mada hii, yaani mdengereko anapewa mil 6 wao wanauza ardhi ileile kwa mil 600! Lakini afadhali hao viwanja vinapatikana pesa yako tu, huku kwetu hata hivyo vya kulanguliwa hakuna.
 
Mkurugenzi wa NHC alisema kama nyumba ya mil 45 ikiondolewa vat basi nyumba ile ingeuzwa 38.9m tu, pia akasema 36% ya gharama ya ujenzi ni miundombinu kwa maana ya umeme maji na barabara ambavyo vilitakiwa viletwe na serikali! kwa maana hiyo nyumba ileile ingeuzwa 22mil, na kwa kauli ya Dr.Slaa kuwa uwezekano wa kushusha bei ya vifaa vya ujenzi kwa 75% upo basi nyumba hiyo ingeuzwa 12m, kwa bei hii alhamdulilah kila mtanzania angemudu. Boss wa NHC alishangazwa na urasimu na utozaji kodi makazi ambao haupo popote duniani isipokuwa Tanzania tu. Lakini kilio cha Boss huyu anakisikia nani? Ukitaka kiwanja cha Hotel utapewa chapchap na msamaha wa kodi juu, inashindikana nini kwa makazi ya watu?
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment