Wednesday 19 December 2012

Re: [wanabidii] Neno La Leo: Kitendawili Cha Embe Dodo Na Tunakokwenda....

Bwana Maggid
asante kushirikisha uliyoona huko Bagamoyo kuhusu Maembe. Nami kwa upande huu wa LIndi na Mtwara ni msimu haswaa wa embe. Kwa sasa watoto muda wote wameshiba maembe yanapatika kila mahali.

Ukienda kwa wauzao Ndoo moja ni sh. 5,000/- bei ya kuanzia. Waweza kununua Ndoo hata kwa sh 2,000/-. Inategemea tu ukarimu wa mnunuzi, kama ulivyofanya wewe.

Tafakari yangu ni kwamba nikiangalia sehemu yetu hii, maembe yanayotumika ni asimimia 40 (40%)tu. Asilimia 60 yanaozea chini. Swali ni kwamba kweli viwanda vyetu vimeshindwa kutumia msimu huu wa maembe na kuyasindika kiasi kwamba yanaweza kutumika mwaka mzima na hata kusafirisha nje?

Zao la Korosho wakulima wamekwisha kopwa. Wamebaki na stakabadhi tu. Mmoja aliniambia halali usingizi sawa sawa maana anaogopa panya kutatuna stakabadhi yake maana atapoteza haki yake yote.

Kwa hali hii KILIMO KWANZA ni maneno tu au kuna nia ya dhati ya utekelezaji wa kumsaidia na kumwinua mkulima. Utawashawishije vijana wapenda kilimo. Duu inauma kweli yaani.

kessy



From: jabir yunus <jabirgood@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, December 19, 2012 1:51 PM
Subject: Re: [wanabidii] Neno La Leo: Kitendawili Cha Embe Dodo Na Tunakokwenda....

Mhh, Maggid, hili NENO.
 
Na ndio hali ilivyo kwa wakulima (wavuvi, wafugaji, warinda asali) wa Tz. Wanatumia nguvu nyingi, muda mwingi, gharama kubwa kazini lakini wanachokipata hakizingatii hayo. Hapa si tu wanakula hasara, bali pia wanazidi umasikini.
 
Tutahadhari sana na mwenendo huu mbaya.
 
Jabir+


--- On Tue, 12/18/12, maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Neno La Leo: Kitendawili Cha Embe Dodo Na Tunakokwenda....
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Tuesday, December 18, 2012, 10:06 PM

Ndugu zangu,

Jana alasiri pale Bagamoyo nilisimama kununua embe dodo. Akina mama wale wakarimu walinipokea kama mwenzao. Bei ya dodo niliyotajiwa ilinifanya pia nitafakari sana, niingiwe na huzuni pia.

Maana, ni ukweli, kuwa mama yule anaanza kuzitafuta dodo zinakotoka, kisha anazipanga pale chini mchangani. Bei ya dodo kubwa kabisa ni shilingi mia sita!

Nilinunua dodo saba. Na hesabu ya dodo saba ikampa tabu sana mama yule. Akaniomba nimsaidie hesabu ya haraka. Nikamwambia ni shilingi 4,200. Kwenye noti ya elfu tano niliyompa alihitaji kunirudishia shilingi mia nane. Nikamwambia aitunze chenji hiyo.

Akashukuru , lakini, wakati akinifungia dodo zangu akaniongeza dodo mbili! Hivyo, kimsingi ameniongeza dodo za thamnani ya 1200! Hivyo, ile mia nane niliyomwachia haina faida kwake. Unafanyaje?

Njiani niliwaza juu ya tunakokwenda kama nchi.Tujiulize; hivi rasilimali zetu za nchi ikiwamo madini, gesi na mafuta tunayoambiwa tunayo kwa wingi yatamsaidia vipi mama yule wa Bagamoyo mwuza embe dodo ambaye yumkini hajui kusoma, kuandika na kuhesabu?

Na idadi yao inazidi kuongezeka. Takwimu zinasema; asilimia 39 ya Watanzania milioni 45 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu. Na hawa wanawaririthisha nini watoto wao?

Kila kizazi na Jukumu Lake; Tafakari,Chukua Jukumu La Kizazi Chako.... Na hilo Ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,

Morogoro
http://mjengwablog.com/

 0788 111 765
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment