Thursday 13 December 2012

Re: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA

Hildegarda,

Jitahidi usifanane na hao unaowatuhumu!!! LKK
 



From: "matinyi@hotmail.com" <matinyi@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, December 13, 2012 7:55 PM
Subject: Re: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA

Hildegarda,
Ushaolewa bibiye? Niwie radhi.
Matinyi.



T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network

----- Reply message -----
From: "Hildegarda Kiwasila" <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA
Date: Thu, Dec 13, 2012 5:54 am


Waswahili husema-'Nyani haoni kundule'' Kama mkuu wa wilaya kaacha maeneo wilaya si zina kamati za kumshauri? labda wameona huko mapambano ndio yameanza ya wizi wa mifugo na vinginevyo hakupitiki kwa usalama wa kamati kaona wakuache kupoe. Anayetukana kinyume na maadili ndiye tu si pumba ubongo bali mpira uliojaa upepeo kichwani. Wajichorao si wale wenye kucheza utupu majukwaani hata wale watukanao hovyo au kutoa lugha chafu siziso maadili-Mtu mzima hovyo. Hao ndio wanaonyesha pumba na ubongo wao ulivyo na tope na wakiwa viongozi si wepesi kupokea mawazo ya watu mbali mbali huwa dictators.  Pengine mtu hakusoma email zote kuona hiyo katiba amesoma kichwa cha habari akaona -kata hazitotoa maoni' akaona labda wamekataa. Kupayuka na lugha chafu inasaidia nini katika karne ya demokrasia na ya kujifunza kutoka kwa wengine hata wenye mawazo usiyo yapenda? Mwenye ila yake haachi !! Hongera kwa matusi-ubarikiwe.Kristmas njema.Nimekaa mara hakuna kijiji
nisichofika-ninawaelewa.


--- On Thu, 13/12/12, Chacha Mairi <chachamairi@gmail.com> wrote:

From: Chacha Mairi <chachamairi@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 13 December, 2012, 8:10

Wewe Kiwasila!

Hujui ama unafanya makusudi kutimiza azma yako! Soma chanzo cha
habari, mimi ndiye niliyetoa habari hii baada ya kupata nakala ya
Ratiba iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Serengeti, kuonesha ni
kwa kiasi gani ratiba hiyo imepangwa kwa kuacha eneo moja la upande wa
mashariki mwa Wilaya yetu ya Serengeti. Rejea attachment ya ratiba
hiyo mwanzo wa habari hii.                Kwa kawaida ratiba hutolewa
na Wilaya husika, siyo Tume ya Kuratibu Maoni Katiba Mpya.

Hakuna mtu aliyekataa au kugoma kutoa maoni hapa Serengeti. Inaonesha
wewe ni mmoja wa wale wanaohujumu wana Serengeti kwa maslahi binafsi!
Mbona ya kabila lako hujayasema hapa, ambayo huenda yakawa pumba kama
maelezo yako yalivyo pumba tupu?

Fanya utafiti, upate haki ya kuzungumza mbele ya watu, vinginevyo
unajichora na kuthibitisha ni jinsi gani ulivyojaa pumba na tope tupu!
Pole sana.

Chacha Mairi
MWANA SERENGETI


On 12/13/12, Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk> wrote:
>
> Ahsante kwa somo hili la Wakurya Matinyi. Lakini, kama wakazi wa kata 7
> Serengeti wamekataa kutoa maoni kwenye Katiba, viongozi wao ambao ni
> wanasiasa (diwani, wabunge) na wa utawala (DC, na extension staff wa DED)
> wawaelimishe ni kwa manufaa yao. Ni mangapi watendayo kinyume na sheria
> wanadamu huko serikali imewavumilia, kuwasaidia? Tatizo ni kutoa maoni au
> utawala mbaya wa hata waliowachagua wenyewe?
>
> Kila kabila lina historia yake na serikali inajua why wapo hivyo. Kila
> wakazi wa eneo fulani wana mambo yao mazuri na mabaya halafu lawama ni GVT
> tu.
>
> Kwa kuongezea niliyojifunza ktk hitoria na kuyaona nilipoishi Mara na
> kutembea vijiji vya Mkoa huo:
> Waingereza na wakoloni wengine waliangalia mambo mengi-hata desturi na tabia
> za kabila hilo. Mfano-wafugaji kama wakurya kupigana vita za wizi wa mifugo
> ambyao ni sehemu ya culture yao. Ambapo, vijijini kwao wakati wa ngoma za
> jadi wanaume hucheza na kujisifu ujasiri wao. Hii ni tosha kumpatia mtu
> heshima na mchumba. Kujisifu jinsi alivyofuatilia kupigana na kurejesha
> mifugo iliyoibiwa. Au, kuiba na kuleta mifugo lishe na mali kwa familia.
> Kama ana mke, naye hujisifu jinsi na wenzake walivyofuatilia mrejesho huo wa
> mifugo wakiwa na chakula, maji kuwapelekea waume zao au wapiganaji wao
> mbugani kwenye hatari. Nao wao ni mama jasiri. Hata tohara za kike ni
> mkeketo mbele za both sexes wakitazama nani halii na kisha kukaribia kupona
> wanapakwa unga, wanavaa lubega na kushika fimbo wanatembea kijijini,
> wanapita maendeo mtaani watu kuwatunza fedha. Nimeiona kwa macho
> Musoma-Ujasiri huu ukionekana ni muhimu. Na wazee wa mila ujasiri wao
> kuiambia Kamati ya
>  Sekretariat ya Wizara ya Maendeleo miaka ya nyuma kuwa 'wataendelea
> kukeketa iwe na liwe ni mila yao' watapambana ya GOT. Huu ni
> ujasiri-unakiambia chombo cha dola!?
>
> Mwingereza kuwaingiza jeshi waliangalia production. waliona wamasai na
> wakurya wakorofi mapigano ya wizi wa ng'ombe hayaishi uzalishaji mali
> unavurugwa. Hivyo-kuwapeleka jeshini ni kutumia uhodari wao wa vita, kimo
> kirefu muhimu kulimko kibushuti kutoka Morogoro (Mluguru). Wakaingiza coffee
> Tarime walime angalau kupunguza makali ya mifugo tu na mapigano. Kwa wamazai
> akawaona wameingia  mapaka ugogo, Iringa kupora mifugo eti ng'ombe zote ni
> zao. Ngo'mbe ankole type zikahamisha Iringa wakabaki kulima tu na wenye
> mifugo wachache ambapo baadhi yao kwa sasa huiwacha msituni inakaa kama
> mifugo pori. Nyingine zinatolewa asubuhi zinajichunga na kurudi zenyewe
> jioni.
>
> Kwa Wamasai Waingereza wakaona bora waweke kwenye Maasai Reserve kuliko
> kuwaacha wavuruge agric production na vurugu za wizi wa mifugo kutoka
> makabila mingine. Hii ikawa created na ipo ktk ramani za ukoloni za nchii..
> Kutoka humo kwa kibali. Jee umelipa kodi, jee unatoka kwenda wapi kwa kibali
> cha nani? DC/Mkuu wa Jimbo etc  katia sahihi kibali hicho na unarudi lini.
> Tanzania National Archive ina file na barua vibali hivyo na malumbano kati
> ya Chiefs wa maeneo megine kuhusu wafugaji na maeneo yao ya haki toka
> kuzaliwa baba zao wakiishi.
>
> Yale magomvi ya serengeti mapambano makubwa ya makabila yahusianayo na wizi
> wa mifugo, silaha kuwa mikononi mwa wananchi kiasi kwamba GOT ilibidi
> ipeleke jeshi ambalo ni la Wa ZNZ kutokana na JWTZ-Bongo (Tanganyika) kuwa
> majority ni toka Mara. Utampeleka Mkurya akakamate watu wa ukoo wake ambao
> walivamia mpaka Mheshimiwa Mkuu mmojawapo wa nchi alipolala kambi kuu
> mojawapo (1993 hivi). Hapo mila na desturi za makabila za huko zikatumika
> kiasi kwamba boma hadi boma kulipita msako mkali na kwa kupitia mila hiyo
> (sitoitaja) baba au bibi kizee alitoa mwenyewe bunduki au risasi
> zilikofichwa. Bibi kizee usimlambie moto-akitumika kuficha risasi/silaha
> maana hutomdhania.
>
> Mafunzo ya Mgambo-yakifanikiwa asilimia 100% kuandikisha wanaume mkoa wa
> Mara. Kila kijana akitaka aingie ajifunze silaha kwa mapigano ya wizi wa
> mifugo. pamoja na matumizi ya silaha za jadi za mishale ya sumu bado silaha
> za bunduki muhimu. Watakaporudi na mifugo iliyoibiwa ni sherehe, ng'oma,
> nyama choma. Ubaya-kila kijiji ni kikabila kimojawapo-Nata wanata,
> isenye-waisenye, robanda-waikoma (sonjo) etc wote ni wapiganaji na mafunzo
> ni toka umri mdogo. Hawa ni wababe, wanafikia kuvamia kituo cha polisi na
> silaha za jadi kumtoa mwenzao/wenzaop aliyekamatwa. Jamani si utaona heri
> wajiunge na JWTZ au polisi?
>
> Zamani tukiwa watoto tukiamini kuwa hawa Jaluo-Kurya wanaua na kula nyama za
> watu-hii ni jinsi utoto wetu tukiambiwa haya na wazee (ethnocentrism) biases
> za ukabila na kuolewa nao Jaluo, Kurya ni shughuli kwa makabila mengine ni
> pevu wazazi kukubali. Ukitakiwa upite mbali nao-wanakula watu.  Kila police
> tuliyemjua miaka hiyo-Jaluo mwanajeshi JWTZ Kurya. JKT wakituhenyesha-Kurya
> (majina ya maafande wengi ni Chacha, Mwita, Marwa)  labda wachache Wahaya na
> kabila nyingine-Meru, Arusha wote hawa wakali-  "Marshal Tribes" !!. lakini
> pia urefu nao uliwapa favours kuwa jeshini.
>
> Rais Nyerere-alipenda makabila yachanganyike. Utakuta shule ya secondary
> Mtwara imejaa wanafunzi wachaga na Tabora wanyakyusa. Unatoka Coast JTK
> unapelekwa Nachingwea sio Ruvu.Kikazi unapelekwa mikoa mbali na ya kanila
> lako. Hii imesaidia kujenga utaifa tunaoubomoa kwa sasa. Baba wataifa
> alijifunza na kuijua Historia. Akauchukua mfumo wa Wafumwa wa Upare akauweka
> ktk mfumo wa Ujamaa. yeye na Mzee Mwinyi wametuomba mara nyingi twende Upare
> tukajifunze mfumo wa kazi, ujenzi wa mabarabara milimani, conservation ya
> ardhi na ulinzi misitu, mazingira, conservation agriculture na utawala bora.
> Tupo tupo tu. Yapo makabila mengi yana mambo mazuri ya kuboresha utanzania
> na utaifa. Utaona watu wanaingia katika bandwagon ya kulitangaza moja tuu
> ili wapate hela za wahisani walipendalo hilo hata kama hilo lin mila nyingi
> mbaya za uonevu na moja tu ndio zuri na kuna makabila mengi yana mabaya
> machache na mengi ya mila zao ni mazuri na ya maendeleo watu wanaangalia
>  tumboni street tu. Yapo makabila kwa ukali wao waliuawa asilimia 90 (90%)
> kwa kufungiwa na kuchoma mapangoni kwa kukataa kulimishwa manamba ili
> wajifanyie kazi zao na wakapigana kiume (wakachomwa mapangoni) wakabaki
> kusali na kuwa watumishi wa Mungu hawaonekani ktk utawala, jeshi, siasa.
>
> Tuwaombe tena akina Mzee Kimambo wafufue chama chao cha Historia, waandike
> tena ya toka enzi hizo hadi sasa kwa kioo cha utaifa sio kile cha Ukoloni
> ili watuachie urithi mzuri maana vijana tupo ktk easynet kutafiti na
> kuandika ni ndoto ila download copy and paste. Hii historia atoayo Matinyi
> hapa itaweza ikawa kwa wengine ni kupoteza muda na maandishi ya maneno
> mengi-hawapendi kusoma vitu virefu. Tuandike vitabu tokana na makala hizi
> kama afanyavyo Shigongo vitawapa urithi vijana kuelewa tulikotoka.
>
> --- On Wed, 12/12/12, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:
>
> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
> Subject: RE: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA
> To: "Wanabidii googlegroups" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Wednesday, 12 December, 2012, 16:25
>
>
>
>
>
> Kivuyo na LKK,
>
>
>
> Naomba niwapatie ukweli ninaoujua kwa kutafiti na kufuatilia kuhusu uwepo wa
> Wakurya wengi jeshini na madai kwamba Nyerere aliwapeleka jeshini - si kwa
> kuwa mimi ni mkurya! La hasha!
>
>
>
> Kwanza niseme hivi, ni kweli kwamba Wakurya ni wengi sana jeshini
> kulinganisha na makabila mengine ya Tanzania ingawa katika miaka ya karibuni
> wamekuwa wakipungua kutokana na sababu nyingi ambazo hapa si mjadala wake.
>
>
>
> NANI ALIWAINGIZA JESHINI
>
>
>
> 1. Wakurya waliingizwa jeshini kwa mara ya kwanza na Waingereza wakati wa
> kuandaa jeshi la kikoloni ambapo ilipotokea vita ya pili ya dunia,
> Waingereza walikwenda vijijini kwa Wakurya na kuwakamata ama kuwahamasisha
> vijana wao waingie jeshini ili kwenda kupigana. Baadhi yao waliporejea,
> akiwemo Marehemu babu yangu mzaa mama na baba yangu mkubwa, walikataa
> kuingia jeshini wakisema wana mali nyingi na wakaenda kuangalia ng'ombe zao.
> Hawa walipigania nchini Burma huko Asia. Utamaduni huu wa kuingia jeshini
> ukaanzia hapo na kuendelea.
>
>
>
> 2. Kwa nini Waingereza waliwachukua Wakurya wengi kwenda jeshini? Ni kwa
> sababu ya dhana kwamba makabila ya Waafrika yana vipaji tofauti na kwamba
> ili kuwatawala Waafrika kwa urahisi, inabidi kuvitumia vipaji hivyo. Mfano,
> Waingereza walisema kwamba ukitaka madaktari wengi watiifu na wapole
> wachukue Wasukuma kwa sababu ya upole wao na utiifu na kweli tunao wengi
> sana. Waingereza wakasema tena, wafanyakazi wazuri wa ndani ni Wanyasa -
> kweli, wafanyakazi wa ndani wa balozi na maofisa ubalozi wa Uingereza hata
> sasa hivi ni Wanyasa kwa sababu ya uaminifu wao. Walisema pia kwenye elimu
> weka Wachaga na Wahaya na ni kweli hadi leo waliobobea shuleni zaidi nchini
> na nani? Tunajua wote! Wakasema, kule Kenya, ukitaka wasomi chukua Wajaluo
> na Uganda wakasema ukitaka wasomi chukua Waganda. Kwenye uaskari walisema
> kwamba kwa Uganda chukua Walango, Waacholi na ikibidi sana Wakakwa (kabila
> la Idi Amin). Nchini Kenya walisema kwamba kwa askari bora uchukue
>  Wakamba. Kwa Tanganyika wakasema chukua Wakurya na ongeza Wangoni na
> Wahehe. Wakaongeza zaidi na zaidi kwenye mpangilio wao. Ipo orodha ndefu.
> Waingereza walifanya utafiti mzuri na walipoondoka walimwachia kila kiongozi
> wa Afrika (makolonini) matokeo ya utafiti wao ingawa akina Nyerere
> hawakuzifuata.
>
>
>
> MATOKEO YA SERA YA WAINGEREZA
>
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> DELL LATITUDE D 620 & D30
>
> 80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
> DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
>
> TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
>
> CALL : 0786 806028
> Free Delivery in Dar es salaam
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment