Wednesday 12 December 2012

RE: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA


Ahsante kwa somo hili la Wakurya feshini. Lakini, kama wakazi wa kata 7 Serengeti wamekataa kutoa maoni kwenye Katiba, viongozi wao ambao ni wanasiaza (diwani, wabunge) na wa utawala (DC, na extension staff wa DED) wawaelimishe ni kwa manufaa yao. Ni mangapi watendayo kinyume na sheria wanadamu huko serikali imewavumilia, kuwasaidia? Tatizo ni kutoa maoni au utawala mbaya wa hata waliowachagua wenyewe?
 
Kila kabila lina historia yake na serikali inajua why wapo hivyo. Kila wakazi wa eneo fulani wana mambo yao mazuri na mabaya halafu lawama ni GVT tu.

Kwa kuongezea niliyojifunza ktk hitoria na kuyaona nilipoishi Mara na kutembea vijiji vya Mkoa huo:
Waingereza na wakoloni wengine waliangalia mambo mengi-hata desturi na tabia za kabila hilo. Mfano-wafugaji kama wakurya kupigana vita za wizi wa mifugo ambyao ni sehemu ya culture yao. Ambapo, vijijini kwao wakati wa ngoma za jadi wanaume hucheza na kujisifu ujasiri wao. Hii ni tosha kumpatia mtu heshima na mchumba. Kujisifu jinsi alivyofuatilia kupigana na kurejesha mifugo iliyoibiwa. Au, kuiba na kuleta mifugo lishe na mali kwa familia. Kama ana mke, naye hujisifu jinsi na wenzake walivyofuatilia mrejesho huo wa mifugo wakiwa na chakula, maji kuwapelekea waume zao au wapiganaji wao mbugani kwenye hatari. Nao wao ni mama jasiri. Hata tohara za kike ni mkeketo mbele za both sexes wakitazama nani halii na kisha kukaribia kupona wanapakwa unga, wanavaa lubega na kushika fimbo wanatembea kijijini, wanapita maendeo mtaani watu kuwatunza fedha. Nimeiona kwa macho Musoma-Ujasiri huu ukionekana ni muhimu. Na wazee wa mila ujasiri wao kuiambia Kamati ya Sekretariat ya Wizara ya Maendeleo miaka ya nyuma kuwa 'wataendelea kukeketa iwe na liwe ni mila yao' watapambana ya GOT. Huu ni ujasiri-unakiambia chombo cha dola!?

Mwingereza kuwaingiza jeshi waliangalia production. waliona wamasai na wakurya wakorofi mapigano ya wizi wa ng'ombe hayaishi uzalishaji mali unavurugwa. Hivyo-kuwapeleka jeshini ni kutumia uhodari wao wa vita, kimo kirefu muhimu kulimko kibushuti kutoka Morogoro (Mluguru). Wakaingiza coffee Tarime walime angalau kupunguza makali ya mifugo tu na mapigano. Kwa wamazai akawaona wameingia  mapaka ugogo, Iringa kupora mifugo eti ng'ombe zote ni zao. Ngo'mbe ankole type zikahamisha Iringa wakabaki kulima tu na wenye mifugo wachache ambapo baadhi yao kwa sasa huiwacha msituni inakaa kama mifugo pori. Nyingine zinatolewa asubuhi zinajichunga na kurudi zenyewe jioni.

Kwa Wamasai Waingereza wakaona bora waweke kwenye Maasai Reserve kuliko kuwaacha wavuruge agric production na vurugu za wizi wa mifugo kutoka makabila mingine. Hii ikawa created na ipo ktk ramani za ukoloni za nchii. Kutoka humo kwa kibali. Jee umelipa kodi, jee unatoka kwenda wapi kwa kibali cha nani? DC/Mkuu wa Jimbo etc  katia sahihi kibali hicho na unarudi lini. Tanzania National Archive ina file na barua vibali hivyo na malumbano kati ya Chiefs wa maeneo megine kuhusu wafugaji na maeneo yao ya haki toka kuzaliwa baba zao wakiishi.

Yale magomvi ya serengeti mapambano makubwa ya makabila yahusianayo na wizi wa mifugo, silaha kuwa mikononi mwa wananchi kiasi kwamba GOT ilibidi ipeleke jeshi ambalo ni la Wa ZNZ kutokana na JWTZ-Bongo (Tanganyika) kuwa majority ni toka Mara. Utampeleka Mkurya akakamate watu wa ukoo wake ambao walivamia mpaka Mheshimiwa Mkuu mmojawapo wa nchi alipolala kambi kuu mojawapo (1993 hivi). Hapo mila na desturi za makabila za huko zikatumika kiasi kwamba boma hadi boma kulipita msako mkali na kwa kupitia mila hiyo (sitoitaja) baba au bibi kizee alitoa mwenyewe bunduki au risasi zilikofichwa. Bibi kizee usimlambie moto-akitumika kuficha risasi/silaha maana hutomdhania.

Mafunzo ya Mgambo-yakifanikiwa asilimia 100% kuandikisha wanaume mkoa wa Mara. Kila kijana akitaka aingie ajifunze silaha kwa mapigano ya wizi wa mifugo. pamoja na matumizi ya silaha za jadi za mishale ya sumu bado silaha za bunduki muhimu. Watakaporudi na mifugo iliyoibiwa ni sherehe, ng'oma, nyama choma. Ubaya-kila kijiji ni kikabila kimojawapo-Nata wanata, isenye-waisenye, robanda-waikoma (sonjo) etc wote ni wapiganaji na mafunzo ni toka umri mdogo. Hawa ni wababe, wanafikia kuvamia kituo cha polisi na silaha za jadi kumtoa mwenzao/wenzaop aliyekamatwa. Jamani si utaona heri wajiunge na JWTZ au polisi?

Zamani tukiwa watoto tukiamini kuwa hawa Jaluo-Kurya wanaua na kula nyama za watu-hii ni jinsi utoto wetu tukiambiwa haya na wazee (ethnocentrism) biases za ukabila na kuolewa nao Jaluo, Kurya ni shughuli kwa makabila mengine ni pevu wazazi kukubali. Ukitakiwa upite mbali nao-wanakula watu.  Kila police tuliyemjua miaka hiyo-Jaluo mwanajeshi JWTZ Kurya. JKT wakituhenyesha-Kurya (majina ya maafande wengi ni Chacha, Mwita, Marwa)  labda wachache Wahaya na kabila nyingine-Meru, Arusha wote hawa wakali- "Marshal Tribes" !!. lakini pia urefu nao uliwapa favours kuwa jeshini.

Rais Nyerere-alipenda makabila yachanganyike. Utakuta shule ya secondary Mtwara imejaa wanafunzi wachaga na Tabora wanyakyusa. Unatoka Coast JTK unapelekwa Nachingwea sio Ruvu.Kikazi unapelekwa mikoa mbali na ya kanila lako. Hii imesaidia kujenga utaifa tunaoubomoa kwa sasa. Baba wataifa alijifunza na kuijua Historia. Akauchukua mfumo wa Wafumwa wa Upare akauweka ktk mfumo wa Ujamaa. yeye na Mzee Mwinyi wametuomba mara nyingi twende Upare tukajifunze mfumo wa kazi, ujenzi wa mabarabara milimani, conservation ya ardhi na ulinzi misitu, mazingira, conservation agriculture na utawala bora. Tupo tupo tu. Yapo makabila mengi yana mambo mazuri ya kuboresha utanzania na utaifa. Utaona watu wanaingia katika bandwagon ya kulitangaza moja tuu ili wapate hela za wahisani walipendalo hilo hata kama hilo lin mila nyingi mbaya za uonevu na moja tu ndio zuri na kuna makabila mengi yana mabaya machache na mengi ya mila zao ni mazuri na ya maendeleo watu wanaangalia tumboni street tu. Yapo makabila kwa ukali wao waliuawa asilimia 90 (90%) kwa kufungiwa na kuchoma mapangoni kwa kukataa kulimishwa manamba ili wajifanyie kazi zao na wakapigana kiume (wakachomwa mapangoni) wakabaki kusali na kuwa watumishi wa Mungu hawaonekani ktk utawala, jeshi, siasa.

Tuwaombe tena akina Mzee Kimambo wafufue chama chao cha Historia, waandike tena ya toka enzi hizo hadi sasa kwa kioo cha utaifa sio kile cha Ukoloni ili watuachie urithi mzuri maana vijana tupo ktk easynet kutafiti na kuandika ni ndoto ila download copy and paste. Hii historia atoayo Matinyi hapa itaweza ikawa kwa wengine ni kupoteza muda na maandishi ya maneno mengi-hawapendi kusoma vitu virefu. Tuandike vitabu tokana na makala hizi kama afanyavyo Shigongo vitawapa urithi vijana kuelewa tulikotoka.

--- On Wed, 12/12/12, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Subject: RE: [wanabidii] KATA 7 SERENGETI HAZITATOA MAONI KATIBA MPYA
To: "Wanabidii googlegroups" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 12 December, 2012, 16:25

Kivuyo na LKK,
 
Naomba niwapatie ukweli ninaoujua kwa kutafiti na kufuatilia kuhusu uwepo wa Wakurya wengi jeshini na madai kwamba Nyerere aliwapeleka jeshini - si kwa kuwa mimi ni mkurya! La hasha!
 
Kwanza niseme hivi, ni kweli kwamba Wakurya ni wengi sana jeshini kulinganisha na makabila mengine ya Tanzania ingawa katika miaka ya karibuni wamekuwa wakipungua kutokana na sababu nyingi ambazo hapa si mjadala wake.
 
NANI ALIWAINGIZA JESHINI
 
1. Wakurya waliingizwa jeshini kwa mara ya kwanza na Waingereza wakati wa kuandaa jeshi la kikoloni ambapo ilipotokea vita ya pili ya dunia, Waingereza walikwenda vijijini kwa Wakurya na kuwakamata ama kuwahamasisha vijana wao waingie jeshini ili kwenda kupigana. Baadhi yao waliporejea, akiwemo Marehemu babu yangu mzaa mama na baba yangu mkubwa, walikataa kuingia jeshini wakisema wana mali nyingi na wakaenda kuangalia ng'ombe zao. Hawa walipigania nchini Burma huko Asia. Utamaduni huu wa kuingia jeshini ukaanzia hapo na kuendelea.
 
2. Kwa nini Waingereza waliwachukua Wakurya wengi kwenda jeshini? Ni kwa sababu ya dhana kwamba makabila ya Waafrika yana vipaji tofauti na kwamba ili kuwatawala Waafrika kwa urahisi, inabidi kuvitumia vipaji hivyo. Mfano, Waingereza walisema kwamba ukitaka madaktari wengi watiifu na wapole wachukue Wasukuma kwa sababu ya upole wao na utiifu na kweli tunao wengi sana. Waingereza wakasema tena, wafanyakazi wazuri wa ndani ni Wanyasa - kweli, wafanyakazi wa ndani wa balozi na maofisa ubalozi wa Uingereza hata sasa hivi ni Wanyasa kwa sababu ya uaminifu wao. Walisema pia kwenye elimu weka Wachaga na Wahaya na ni kweli hadi leo waliobobea shuleni zaidi nchini na nani? Tunajua wote! Wakasema, kule Kenya, ukitaka wasomi chukua Wajaluo na Uganda wakasema ukitaka wasomi chukua Waganda. Kwenye uaskari walisema kwamba kwa Uganda chukua Walango, Waacholi na ikibidi sana Wakakwa (kabila la Idi Amin). Nchini Kenya walisema kwamba kwa askari bora uchukue Wakamba. Kwa Tanganyika wakasema chukua Wakurya na ongeza Wangoni na Wahehe. Wakaongeza zaidi na zaidi kwenye mpangilio wao. Ipo orodha ndefu. Waingereza walifanya utafiti mzuri na walipoondoka walimwachia kila kiongozi wa Afrika (makolonini) matokeo ya utafiti wao ingawa akina Nyerere hawakuzifuata. 
 
MATOKEO YA SERA YA WAINGEREZA

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment