Wednesday 12 December 2012

Re: [wanabidii] CHADEMA inakufa? – Ripoti maalumu – Gazeti la Jamhuri - Mwanzo

Mbona ktk maelezo yako sioni kifo cha CDM? Huu si mgogoro tu wa kuisha!

----------
Sent from my Nokia Phone

------Original message------
From: Magiri paul <kiganyi@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, December 12, 2012 1:45:22 PM GMT+0100
Subject: [wanabidii] CHADEMA inakufa? – Ripoti maalumu – Gazeti la Jamhuri - Mwanzo

Hali ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni
mbaya na tayari kumeanza kuwapo hofu ya chama hicho kikuu cha upinzani hapa
nchini, kufa.

Hofu hiyo inayokana, pamoja na mambo mengine, kuibuka kwa makundi
yanayohasimiana, yanayoundwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama
hicho.

Katika fukuto hilo, JAMHURI imefanikiwa kupata habari za uhakika kutoka kwa
baadhi ya wanachama na viongozi, zinazohusu kuwapo mkakati madhubuti wa
kuwafukuza baadhi ya viongozi wa chama hicho.

Duru za uchunguzi zinaonesha kuwa walengwa wakuu kwenye mpango huo ni
pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto, na Mbunge wa Maswa
Magharibi, John Shibuda. Pamoja nao, walengwa wengine ni wafuasi wa
wanasiasa hao.

Moja ya sababu zinazotajwa kuchochea au kuibua makundi makuu matatu ndani
ya Chadema, ni mbio za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mwaka 2015. Makundi yanayotajwa, na ambayo yameanza kujitokeza hadharani
yamejiegemeza kwa viongozi watatu maarufu – Zitto, Mwenyekiti wa Chadema
Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa.

Zitto anatajwa kama mmoja wa vinara wa migogoro ndani ya Chadema, akidaiwa
kutumia umaarufu wake kama kinga ya kufanya lolote analotaka akiamini kuwa
"Chadema bila Zitto, haipo".

Pia urafiki wake wa karibu na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, na
viongozi wengine waandamizi wa CCM umekuwa ukiwatia shaka baadhi ya
wanachama, wafuasi na viongozi wa Chadema.

Tayari Zitto ameshatangaza hadharani nia yake ya kuiwakilisha Chadema
kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015, na kwa sasa anaendesha kampeni
ya umri wa wagombea urais kupunguzwa na ikiwezekana iwe miaka 35. Mwaka
2015, Zitto atakuwa anatimiza umri wa miaka 39.

Hii si mara ya kwanza kuibuka kwa makundi ndani ya Chadema, kwani miaka
kadhaa iliyopita Zitto na Mbowe walisuguana kutokana na uamuzi wa Zitto wa
kutangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa. Mzozo huo
ulimalizwa kwa busara ya wazee na wanachama waandamizi ndani ya chama
hicho, kwa Zitto kukubali kuondoa jina lake mbele ya waandishi wa habari.

http://wotepamoja.com/archives/10863#.UMh8RkX9S7I.gmail

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment