Thursday 13 December 2012

Re: [wanabidii] BW. MGIMWA: BASI HATA HALMASHAURI MOJA KUTOKA ZANZIBAR???

Dear Kaka Matinyi,
 
>kwamba MKUKUZA wakiomba fedha mahali na kupata, kama za Korea Kusini ambazo zinakuja,
>watakuwa tayari kuigawia Bara?
 
 
 
Kwanza, kama MKUZA wameomba kama Tanzania basi itabidi waigawie Bara. Kama wameomba kama Zanzibar basi Bara hawana sehemu hapo. Kwa bahati mbaya hivyo ndivyo alivyotaka Baba yetu wa Taifa - yaani chetu ni chetu na chenu ni chetu (what a kind man he was!). Sifikirii kama unaweza kupinga hapo. Nini alikusudia Mwalimu hakuna anaejua. Karume halaumiki, kwasababu tunajua sote kuwa kwa wakati ule (1964) angelikubali Muungano wa aina yoyote ule ambao Mwalimu angeliutaka. Nia yake Karume haikuwa kuunda Muungano bali kupata hifadhi tu kutokana na chokochoko za mapinduzi mengine ambayo bila ya shaka yangelitokea Visiwani bila ya kuwepo kwa Muungano na Bara!
Pili, Kaka Matinyi, tusiende mbali sana mpaka tukafika Korea ya Kusini. Let's look at things in our own backyard. Ikiwa faida ya BoT Zanzibar hawapewi kama inavyostahiki kutokana na share yao, hivyo unadhania pesa za kutoka nje watapewa?
Hivyo kuna mtu hapa ukumbini anaefanana na yule Finance and Economic Affairs deputy minister Janeth Mbene ambae hajui Tanganyika, Zanzibar na Tanzania kila moja ilitoa kiasi gani kuianzisha BoT? Kama tunaujua ukweli ulivyo kwanini Zanzibar hawapewi haki yao na wanakuwa shortchanged mwaka hadi mwaka? Bila ya shaka matatizo yote haya yanaletwa kwa makusudi ili kuwavunja moyo Wazanzibari.
Kwa kweli ni jambo la aibu tena ni aibu kubwa sana sana sana kuliko ulivyoielezea Kaka Matinyi, kuwa tunashindwa kuendesha nchi yetu kwa serikali mbili. Ukweli ni kuwa, matatizo ya Muungano wetu ni madogo sana na tungeliweza kuyamaliza wenyewe kwa wenyewe bila ya Muungano wetu kutetereka. Hatuhitaji mtu atoke nje ili aje kutupatanisha, lakini shida ni kuwa wengi wetu kwa makusudi tunakorofisha mambo, kwani tunafaidika na hii migongano inayotokea. But, if we are not careful Tanzania itakuwa marehemu karibuni - if not tomorrow, then day after tomorrow na wakulaumiwa tutakuwa sisi wenyewe - yaani mimi na wewe Kaka Matinyi.
Wazee wanatueleza kila siku kuwa, "asieziba ufa atajenga ukuta". Wazanzibari mwisho watachoka kila siku kuja Dodoma kupiga magoti kulilia haki zao.Tumekuja kupiga magoti kwa masuala ya gesi na mafuta, sidhani kama tutakuja kupiga tena magoti kwa jambo jengine isipokuwa kutangaza kuzaliwa tena kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar (JWZ)!
 
 
 
 
...bin Issa.
 
 
 
 
(Zanzibar Ni Kwetu)
 
 

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, December 12, 2012 8:17:00 PM
Subject: RE: [wanabidii] BW. MGIMWA: BASI HATA HALMASHAURI MOJA KUTOKA ZANZIBAR???

Issa,
 
Ni kweli ila sasa tatizo linaanzia hapa, kwamba MKUKUTA ni mpango wa Tanzania na kule Zanzibar kuna MKUKUZA na inaelekea hakuna mfumo wa kushirikiana katika kuomba pesa ama kukopa na iwapo mtu wa serikali ya Muungano ataulizia kitu kule MKUKUZA ataambiwa hili si suala la Muungano. Swali pia linakuja hivi, kwamba MKUKUZA wakiomba fedha mahali na kupata, kama za Korea Kusini ambazo zinakuja, watakuwa tayari kuigawia Bara? Hapana, watasema si suala la Muungano.
 
Hii shida ingekwisha kirahisi sana kama tungekuwa na ama serikali moja tu au serikali tatu lakini ile ya Muungano iwe kamili yenye wizara zote na ikishaomba hela huko kwa wajomba zetu inakuja kufanya mgawo - lakini kwa hii akili ya eti wizara za muungano ni nne au tano tu, hatutaweza hata kueleweka huko duniani; tutaonekana kama wajinga tu.
 
Kushindwa kuendesha nchi kwa serikali mbili pia ni jambo la aibu kubwa.
 
Matinyi.
 
Date: Wed, 12 Dec 2012 14:58:51 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: [wanabidii] BW. MGIMWA: BASI HATA HALMASHAURI MOJA KUTOKA ZANZIBAR???
To: wanabidii@googlegroups.com

"Benki  ya Dunia (WB), imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo usio na riba wa Sh. bilioni 489.8 kwa ajili ya kuendesha miradi mitatu ya kilimo, kuendeleza serikali za mitaa na uhifadhi wa chakula nchini.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa mkopo huo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, alisema mradi wa kilimo utapatiwa Sh. bilioni 47.4 kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vocha za pembejeo, 
kuelimisha wakulima juu ya kilimo cha kisasa pamoja miundombinu katika kilimo hicho.
Dk. Mgimwa alisema mradi wa pili ni ule wa uhifadhi wa chakula ambao utatumia Sh. bilioni 39.5 na  mradi wa tatu utatumia Sh. bilioni 402.9 kwa ajili ya kuendeleza serikali za mitaa katika halmashauri 18 nchini.
Alizitaja halmashauri zitakazonufaika na fedha hizo kuwa ni Sumbawanga, Tabora, Morogoro, Iringa, Songea,  Moshi, Lindi, Bukoba, Musoma, Singida,  Babati, Korogwe, Masasi, Nyumbu, Mpanda, Bariadi na Geita.
Dk. Mgimwa alisema msaada huo ni mkopo usio na riba na utalipwa katika kipindi cha miaka 40.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa WB nchini, Philippe Dongier, alisema msaada huo ni mojawapo katika kutekeleza kuisaidia serikali kufika lengo lake la kutekeleza mradi wake wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (Mkukuta).
Pia alisema uimarishaji na utoaji wa elimu kwa wakulima utasaidia kuwasaidia wakulima hao kujua mbinu mbadala za kuzalisha zaidi mazao yao".
Chanzo: Nipashe

-- 
 

0 comments:

Post a Comment