Monday 22 October 2012

[wanabidii] VIONGOZI WAPYA WA IDARA YA IDARA YA WANYAMAPORI

Profesa Alexander Nyangero Songorwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori (Wildlife Division ) kuziba nafasi iliyokuwa wazi.Kabla ya kuteuliwa Profesa Nyangoro alikuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa Wanyamapori, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro. Pia ndiye aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo ya Usimamizi wa Wanyamapori SUA.

Wakati huohuo, Profesa Jafari Ramadhani Kideghesho ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi, kuiongoza Sehemu ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori (Sustainable Utilisation of Wildlife Section). Kabla ya uteuzi huo Profesa Ramadhani alikuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa Wanyamapori katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.
Uteuzi huo umetekelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarishi kwa mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa kifungu cha 6 (1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002. Utekelezaji wa
uteuzi huo ni kuanzia tarehe 24 Septemba 2012.
 
Mkurugenzi mpya wa wanyamapori, Profesa. Songorwa, ni msomi katika fani ya Wanyamapori. Anayo shahada ya kwanza (B.Sc.) ya Sayansi katika Zoolojia na Ekolojia ya Wanyamapori ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (mwaka 1987), Shahada ya uzamili (MSc) katika Mipango na Maendeleo Vijijini ya ChuoKikuu cha Guelph, Ontario, Canada (1994) na shahada ya uzamivu (PhD) katika Uhifadhi Maliasili ya Chuo Kikuu cha Lincoln, New Zealand (1999).
 
Kabla ya kujiunga na SUA mwaka 2001, Prof. Songorwa alikuwa mwajiriwa wa Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii kuanzia mwaka 1982.
 
Akiwa Wizarani Profesa Songorwa alihudumu katka nafasi mbali mbali zikiwemo Askari Wanyamapori, Mkuu wa Kanda na Msaidizi wa Mkuu wa Mradi katika Pori la Akiba la Selous. Pia alihudumu kama Afisa Mwandamizi katika Mradi wa Uhifadhi Shirikishi wa Wanyamapori, Makao Makuu, Dar es salaam.

Naye Profesa Kideghesho siyo mgeni katika Idara ya Wanyamapori. Kabla ya kujiunga na na SUA mwaka 1999 Prof. Kideghesho alikuwa mwalimu katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (CAWM-Mweka), Moshi kuanzia 1993.

Kitaaluma Prof. Kideghesho ana shahada ya kwaza (B.Sc.) katika Kilimo ya SUA (1993), Shahada ya Uzamili (MSc) katika Biolojia ya Uhifadhi ya Chuo Kikuu cha Kent, Uingereza (1996), na Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Norway kilichopo mjini Trondheim (2006).

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Simu 0784 468047
22 Oktoba 2012 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment