Sunday 28 October 2012

[wanabidii] UJINGA WA OIC NA MAHAKAMA YA KADHI


UJINGA MTUPU KAMA KUNA MTU ANATAKA KUJIUNGA NA OIC AANZE KUUNGA MKONO HOJA YA URAIA WA NCHI MBILI TANZANIA, ILI IKIPITA HIYO NA KUWA SHERIA WAKAHAMIE NCHI YOYOTE DUNIANI ILIYO MWANACHAMA WA OIC WAKAKAE HUKO, KWENYE NCHI YOYOTE  YENYE UANACHAMA WA OIC, SIO KULAZIMISHA NCHI NZIMA YA TANZANIA KUWA MWANACHAMA WA OIC AU KUNDI FLANI KUTAKA TANZANIA NZIMA KUWA WANACHAMA WA OIC? NA OIC NI NINI? 

HIVI UNATEGEMEA NCHI MOJA MIRENGO MIWILI YA SHERIA INAWEZEKANA WAPI? NIKUTOKUWA NA FIKIRA NDIO KUNA LETA YOTE HAYO
.
IKIANZA MAHAKAMA YA KADHI, BASI PIA MAHAKAMA YA KIRUMI IWEPO, sbb taratibu za usimamizi wa sheria wa tanzania utakuwa hauna maana tena.

A SPADE CALL IT BY ITS NAME, NOT A BIG SPOON

From: Ellay Mnyamoga <mnyamoga@live.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com " <wanabidii@googlegroups.com>; "ngupula@yahoo.co.uk " <ngupula@yahoo.co.uk>
Sent: Sunday, October 28, 2012 4:49 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA WAISLAMU : KUHUSU KUJIUNGA NA OIC NA KUREJESHWA KWA MAHAKAMA ZA KADHI


Tusijadili ujinga wa oic
----------
Sent from my Nokia phone


-----Original Message-----
From: Godfrey Ngupula
Sent: 10/28/2012 3:46:25 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA WAISLAMU : KUHUSU KUJIUNGA NA OIC NA KUREJESHWA KWA MAHAKAMA ZA KADHI

kiukweli ni kuwa Tanzania haiwez ikajiunga na OIC shirika ambalo haliamini uwepo wa taifa jingine ktk ramani ya dunia.Kujiunga na shirika au chama fulani ni lazima uamini shirika au chama hicho inachoamini.Na kama ni lazima Tanzania kufanya hivyo basi OIC iondoe kipengele cha kulaani na kutolitambua taifa la Israeli.Hakuna mkristo yeyote anayetambua uhalali wa kuwepo taifa la israeli kisha akaafiki Tz kujiunga na shirika la OIC,ni labda awe mkristo jina kama Membe ambaye yupoyupo tu ari mradi mkono unaenda kinywani.
pili,wakristo hawaping hata kidogo uanzishwaji wa mahakama za kadhi nchini.Wanachopinga ni kuingiza vipengere suppotive kwenye katiba yetu which in fact vitaifanya katiba yetu neutral kuwa sensitive.Jambo hili wakristo hawatalikubali hata kidogo. Ni kwa nini wakristo wanapinga mambo hayo mawili kuwemo ndani ya katiba?jawabu rahisi kupita yote ni kwa sababu jamii ya kiislam kihistoria na kimatendo imejihidhirisha kuwa sio jamii ya watu waliostaarabika.All the time handle them with care.Huu ndio ukweli,and that is cost waislam have to bare.Nina imani kwa 100% wakristo wako tayari ubaloz wa vatican uondolewa Tz kuliko nchi kujiunga na Oic au mahakama za kadhi kuanzishwa tz chini ya mfumo wa serikali. wakristo wanaamini kuwa upotevu mwelekeo wa nchi kama n4eria,ivorycost,benin ni laana ya kimaandiko kwa sababu ya kutokuwa na tahadhali ktk kufanya maamuzi.Hivyo,hiyo mifano ya nch zenye wakristo weng zilizojiunga na oic in fact stand as the negative
 example,the side effect of the decision towards...

Godfrey Ngupula
------------------------------
On Sun, Oct 28, 2012 4:58 PM EET Ellay Mnyamoga wrote:

>Acha kuandika ujinga usio na maana kwani wewe ukiishi katika uislam mi inanisaidia nini? Umeambiwa hizi ni mahakama za kikristo?
>
>
>-----Original Message-----
>From: Abdalah Hamis
>Sent: 10/28/2012 2:01:10 PM
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Subject: [wanabidii] TAMKO LA WAISLAMU : KUHUSU KUJIUNGA NA OIC NA KUREJESHWA KWA MAHAKAMA ZA KADHI
>BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA
>
>TAMKO LA WAISLAMU TANZANIA
>
>KUHUSU KADHIA YA TANZANIA KUJIUNGA NA OIC NA KUREJESHWA KWA MAHAKAMA ZA KADHI
>
>BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA
>
>I. UTANGULIZI
>
>Tanzania inapita katika kipindi cha mivutano mikubwa kati ya Waislamu kwa upande mmoja, na serikali na Wakiristo kwa upande mwingine.
>
>Tafauti hizo ni juu ya uhalalali wa urejeshwaji wa Taasisi ya Waislamu ya Mahakama za Kadhi na mchakato wa Tanzania kujiunga na Jumuiya ya misaada ya Waislamu duniani Organization of the Islamic Conference OIC.
>Historia inaonesha kuwa kufutwa kwa Mahakama ya Kadhi mwaka 1963 kunatokana na maamuzi ya Bunge kupitia The Magistrates Courts Act, 1963.
>
>Suala jingine ni uhalali na ubora kwa Jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibari (Tanzania) kujiunga na Shirika la misaada la Waislamu duniani OIC.
>
>Kutokana na madai ya muda mrefu ya Waislamu ya kutaka kurejeshwa Mahakama ya Kadhi nchini, Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa jukumu kwa Kamati ya Katiba na Sheria kushughulikia suala hilo chini ya uongozi wa Muheshimiwa Arcado Ntagazwa mwaka 1994. Mwaka 2004 kamati iliendelea na jukumu hilo chini ya uongozi wa Muheshimiwa Athumani Janguo.
>
>Suala hili pia lilijitokeza katika Ilani ya Chama tawala CCM kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2005.
>
>Kamati hiyo chini ya uongozi wa awamu zote mbili ilikutana na Jumuiya za Kiislamu kwa uelewa halisi wa suala husika na vilevile wadau wengine kwa faida za kiutendaji.
>
>Taarifa tulizonazo ni kwamba waraka wa kamati hiyo uliwasilishwa kwa Spika wa Bunge (wa wakati huo) Mh. Pius Msekwa.
>
>Novemba 11, 2007 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya 'kusimikwa' Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Alex Malasusa aliwataarifu watanzania kuwa mapitio ya vyombo husika juu suala la Mahakama ya
>Kadhi yamekamilika, akaongeza kuwa wananchi watapatiwa jawabu ya suala hili Februari mwakani, yaani 2008.
>
>Tokea mchakato wa suala hili uanze, na mpaka Rais Kikwete alipotoa tarehe ya kutoa jawabu katika hafla iliyotajwa hapo juu, ni zaidi ya miaka 13 sasa.  Aidha, suala la OIC nalo limepewa urasimu wa aina yake.
>
>Mwaka 1993 Zanzibar ambayo ni moja ya nchi zilizounda serikali ya muungano inayoitwa Tanzania, iliamua kujiunga na OIC kama Zanzibar.  Tanzania bara ilipinga kwa hoja kuwa ni vema ufanyike utafiti wa kina ili maamuzi ya kujiunga au kutojiunga yawe ya pamoja.
>
>Baada ya utafiti wa miaka 15 serikali ya Tanzania kupitia Waziri wake wa mambo ya nje imetamka hadharani kuridhika kwake na sababu zote za kujiunga OIC zikiwemo za kisheria na kiusalama.
>
>Nchi ambazo kwa muda mrefu raia wake wamekuwa wakifaidika kwa misaada ya OIC ni pamoja na Benin, Cameroon, Cote d'Ivoire,  Gabon, Guinea, Guinea Bissau, Msumbiji, Nigeria, Sierra leone, Uganda, Urusi. Nchi hizi ni sehemu ya nchi 57 wanachama wa OIC zikiwemo zenye idadi kubwa ya raia Wakiristo.
>
>Tarehe 24 Oktoba 2008 Maaskofu Tanzania walitoa tamko kali kupinga Mahakama ya Kadhi na OIC. Wameionya serikali kuwa endapo itaridhia kurejeshwa kwa Mahakama ya Kadhi na nchi kujiunga na OIC, mahusiano kati ya Wakristo na Waislamu yatavunjika na uwezekano mkubwa wa kutokea umwagikaji wa damu.
>
>Katika masuala haya, Waislamu wameendelea kusimama kwenye rejea za Sheria, Sharia, Mantiki na Historia. Wakristo wameendelea kusimama katika wasiwasi wa kuwepo kwa itikadi yao na madai ya 'uvunjwaji wa katiba' ya nchi. Serikali inaendelea kusuasua katika ahadi za muda mrefu na sura isiyoeleweka.
>
>Waraka huu ambao unakamilika kwa Tamko la Waislamu, unapitia hoja zote tegemezi kwa Wakiristo, Waislamu na mtazamo wa sheria za nchi ili kuitanabahisha serikali itekeleze ahadi zote kama ilivyoahidi, kwa maslahi ya wananchi wote.
>
>II. HOJA ZA MAASKOFU
>
>1. Udini
>
>
>Miongoni mwa hoja za Maaskofu ni kuwa suala la Kadhi kutambuliwa na katiba ya nchi ni kuleta udini miongoni mwa watanzania. Rejea gazeti la Msema Kweli, na. 578 Jumapili, Septemba 28-Oktoba, 2008, uk. 5.
>
>'Akitoa tamko hilo Jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Maaskofu wa Kipentekoste nchini, Mwenyekiti wa PCT mkoani hapa Askofu David Mwasota alisema katika awamu nne za uongozi wa nchi, kumekuwapo na juhudi za makusudi kwa baadhi ya viongozi wa serikali, Wabunge na Viongozi wa Dini ya Kiislamu kujaribu kushinikiza udini.'
>
>'Aliutaja udini huo kuwa ni kutaka kuiingiza Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na pia Tanzania kujiunga na OIC.'
>
>2. Ukiukwaji wa Katiba
>
>Ukiukwaji wa katiba ni moja ya madai ya Maaskofu katika kupinga kurejeshwa kwa Mahakama ya Kadhi na Tanzania kujiunga na OIC. Rejea gazeti la Jibu la Maisha, na.37, Jumapili, Septemba 28 Oktoba 4, 2008, uk. 2.
>
>'Na wala hatutaki kabisa kuona kinaingizwa kipengele cha kuwa na Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba, maana kwa kufanya hivyo ni kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la Novemba 1, 2000, Sehemu ya Pili Ibara ya 9 kifungu 'a' na Ibara ya 20 (2) a. Kukiuka vifungu hivyo, kutasababisha uvunjifu wa amani na kubomoa mihimili mikuu ya utulivu iliyosimamishwa ndani ya nchi yetu.'
>
>3. Uvunjifu wa Amani
>
>Maaskofu pia wametowa hoja ya uvunjifu wa amani, rejea gazeti la Utatu, Na 044, Jumapili, Septemba 28 - Okotoba 4, 2008 uk. 5.
>
>'Kwa kuwa Katiba ya nchi yetu hairuhusu serikali ya kidini hatujui linalotafutwa ni nini hasa na serikali kuendelea kuachilia jambo kurudia rudia bungeni, inaashiria nini, hata kama jambo limekubaliwa na chama tawala katika ilani yake, lakini suala hili si la kichama, bali ni la kitaifa na halina maslahi kitaifa maana lina malengo ya kuwagawa Watanzania kidini, hivyo kuchafua amani tunayojivunia muda mrefu.'
>
>4. Kunajisi Katiba
>
>Maaskofu pia wamefika mbali zaidi kwa kutowa hoja kuwa kuingizwa OIC na Mahakama ya Kadhi ni kunajisi katiba ya nchi. Rejea gazeti la Utatu - Na 044, Jumapili, Septemba 28 - Oktoba 4, 2008, uk. 5.
>
>'Akionyesha wazi msimamo usioyumba wa baraza hilo, Mwenyekiti wa PCT, Dar es Salaam, Askofu David Mwasota aliwaambia waandishi wa habari kuwa uvumilivu wa Wakristo umefikia mwisho na sasa wanasema hapana, hawataki Katiba ya nchi itiwe unajisi na sheria za dini.'
>
>Aidha, kwenye Tahariri ya gazeti hilo Uk. 4. imeeleza kama ifuatavyo.
>
>'Tusikubali kutia unajisi katiba ya nchi, iachwe ikibaki kama katiba na dini zetu zibaki kama zilivyo, kwani kucheza na eneo hilo ni kuchezea aliyeumba mbingu na nchi ambaye ana mamlaka juu ya yeyote na chochote.'
>
>5. Kujitafutia laana ya Biblia, Tanzania
>
>Imeelezwa kuwa 'Yabainika Tanzania kujiunga na OIC ni kujitafutia laana ya biblia.' Rejea gazeti la Msema Kweli Na. 579 Jumapili, Oktoba 5-11, 2008, Ukurasa wa mbele na Uk. 5,
>
>'Imebainika kuwa malengo ya Shirika la Umoja wa Kiislamu (OIC) yatailetea laana kubwa Tanzania iwapo itajiunga nalo, kutokana na moja ya malengo yake kupinga uwepo wa taifa la Kiyahudi la Israeli katika eneo la Mashariki ya Kati, huku tayari Biblia Tukufu ikiwa imetahadharisha kuwa yeyote atakayekwenda kinyume na taifa hilo atakuwa amejipatia laana.'
>
>'Ukweli wa laana ambayo Tanzania itajipatia ikiwa itajiunga na OIC inaelezwa vyema katika Biblia kwenye Kitabu cha Mwanzo 12:3 ambapo baada ya Mungu kumwahidi baraka kuu Nabii Abrahamu ambaye ni chimbuko la taifa la Israeli, alisisitiza ahadi zake kwa kuweka Agano kwamba atawabariki wote watakaombariki na kuwalaani wote watakaomlaani.'
>
>6. Kuisilimisha nchi
>
>Rejea gazeti la Msema Kweli - Na. 578, Jumapili, Septemba 28 Oktoba 4, 2008, Ukurasa wa mbele na Uk 5, chini ya kichwa cha habari:
>
>'Katiba ya OIC kuibadilisha Tanzania kuwa dola ya kiislamu.'
>
>'Juhudi zinazoendelea hivi sasa za kutaka Tanzania ijiunge na Shirika la Umoja wa Kiislamu maarufu kama Organization of the Islamic Conference (OIC), hu

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment