Friday 12 October 2012

[wanabidii] TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TAARIFA YA KAMATI NDOGO YA HAKI, KINGA NA MADARAKA YA BUNGE

Itakumbukwa kuwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge uliofanyika kuanzia Juni – Agosti, 2012, Spika wa Bunge aliunda Kamati Ndogo ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma zilizokuwepo kuwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wabunge walijihusisha na Vitendo vya rushwa wakati wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (2012/2013).

       Hivyo, Tangazo hili linatolewa kuuarifu Umma kwamba Kamati hiyo Ndogo imekamilisha kazi yake kama ilivyoelekezwa kwenye Hadidu za Rejea na kukabidhi Taarifa ya Uchunguzi huo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano tarehe 27 Septemba, 2012.
      
       Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika atatoa muongozo kuhusu utaratibu wa kufuata kuhusu uwasilishaji wa Taarifa hii Bungeni ambapo yaweza kuwa Spika akatoa uamuzi ama Kamati kuwasilisha Taaarifa hiyo Bungeni.

       Spika atatoa taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi huo Bungeni wakati wa Mkutano wa Tisa wa Bunge unaotarajia kuanza tarehe 30 Oktoba, 2012.

Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge
S.L.P. 9133
DAR ES SALAAM

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment