Tuesday 9 October 2012

[wanabidii] Ripoti ya Kifo cha Mwandishi Daudi Mwangosi, Iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) - Mwanzo

Ripoti hii ni ya wa uchunguzi mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa
Mwandishi wa Channel Ten Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi katika
kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa Septemba 2, 2012.
Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
kwa pamoja waliunda timu ya uhunguzi.
Mchakato wenyewe ulihusisha mbinu za uchunguzi za kiuandishi wa habari
ambazo si kama za uchunguzi wa kipolisi na wa kimahakama.
Methodolojia za uchunguzi zilijumuisha mahojiano, kutembelea maeneo
husika na uchambuzi mahsusi wa nyaraka kwa kuzingatia adidu za rejea
zilizopo. Waandishi wa Habari waliokuwepo Nyololo na ambao
hawakuwepo katika eneo la mauaji wametoa mchango muhimu.
Mashahidi walioshuhudia katika kijiji cha Nyololo, wakiwemo watoto
walikuwa vyanzo muhimu. Habari zilizochapishwa katika vyombo vya
habari kutokana taarifa rasmi kuhusu baa hilo pia zilichambuliwa kwa
umakini.
Uchambuzi mpana ulifanywa kuhusu hali ya mahusiano ya Uongozi wa
Mkoa wa Iringa( ikiwemo polisi) na wanahabari wa Iringa kabla ya mauaji
ya Mwangosi.Mahusiano yalikuwa si mazuri na ya shaka kati ya pande hizo
mbili tangu katika robo ya mwisho ya mwaka 2011.
Hii ilisaidia kupata picha pana ya tatizo pamoja na kuweza kufahamu kwa
undani tatizo lenyewe na kuweza kupanga mwelekeo wa uchunguzi
wenyewe na hatimaye kuwezesha timu kuweza kuunganisha mambo na
kuandaa ripoti hii.
http://wotepamoja.com/archives/8304#.UHQYoYlSQ5g.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment