Sunday 21 October 2012

[wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam @MohamediMtoi - Mwanzo

Ndugu zangu.

Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani
wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande
wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya
ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita
unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda
kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati
wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye
mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.

Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu
wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii
dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo
kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu,
wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia
watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo
ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na ndugu
zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu
lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na makamu wake, si uoni
mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi sheini na sharif
hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman yule jaji mkuu
na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si uoni hata
nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.

Wanao ongela mfumo kristo hawana udhibitisho wa kutosha kuhalalisha
madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na
ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinacho piga macho pazia mchana
wa jua kali.

Kwa waislamu na wasio kuwa waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa
waislamu sio wakristo, wapagani, wahindu,au dini nyingine
zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.

Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na
kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia
za amani kupata suluhu.
Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.

1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi
vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande
wa pili wanaokuja kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana
lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa
mashahidi hata shule tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani
ya kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa
masheikh walio iva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza
harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri
walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanao
endana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya
ushindani na pia viongozi bora wa dini.

2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya ccm kupata uhalali wa kutawala kwa
kura za waislamu. Lazima tujue kuwa ccm wametutumia vya kutosha na
kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano:~ Wametudanganya
swala la mahakama ya kadhi wakati wa kampeni 2010 waislamu waliotaka
tuwe na kadhi kwa kauli hadaa ya ccm wakapiga kura za kuhadaiwa lakini
baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa
kudanganywa, tuunge mkono chama ambacho hakita tugawa lakini pia
ambacho hakita tugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.

3.Bakwata imekuwa ni kama taasisi ya ccm, wanamuweka wanaye taka wao.
Lazima tupiganie bakwata kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke
viongozi wenye maono mapana tunao taka sisi sio ccm hii itasaidia
kurejesha imani kwa bakwata. Napendekeza Qualification ya kuongoza
Bakwata iwe ni pdh kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia
lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu
cha mum kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji
wengine wa bakwata ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe
shahada moja na kuendelea.

4.Kutokufuata mafundisho ya mtume. Mtume wetu Muhammad S. A. W alikuwa
mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na
kukumbushana mema na kukatazana mabaya, uislamu haujajengwa kwenye
misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya.
Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha
Mungu, ukarimu, na kuhurumia na kuwajali wengine. Tukiyafanya haya
tutawaepuka wale wanao utumia uislamu wetu kama daraja ambalo baadae
hutuchafua wote. Mfano wale walio ingia kuchoma na kuvunja kanisa na
kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya kanisa na mikate.

"Uislamu ni unadhifu" hii ni moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu
kipenzi Muhammad S. W. A. Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili
tumuenzi kipenzi chetu.

Wakatabahu.

On Oct 21, 1:46 pm, Magiri paul <kiga...@gmail.com> wrote:
> Ndugu zangu.
>
> Tunapokuwa tunajiuliza mhemuko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha
> na kuuasisi, si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu Waislamu.
> Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya
> kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au
> mfumo kristo kama wengine wanavyopenda kuita (Mimi sio muumini wa
> dhana ya *mfumo
> Kristo*) maana nimeona wakati wote Waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa
> Serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>
> Siuoni *mfumo Kristo* kama unavyoitwa au kama baadhi ya Waislamu wenzangu
> wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa Kiislamu juu ya hii dhana.
>
> http://wotepamoja.com/archives/9392#.UIPSVsPwbyY.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment