Thursday 11 October 2012

[wanabidii] HUU ULIKUWA MKATABA WA SHIRIKISHO NA SIO MUUNGANO

"Imeelezwa na Balozi wa Marekani kwamba aliporudi kutoka Dar es Salaam, Mzee Karume alikuwa anaamini kwamba amesaini Mkataba wa Ushirikiano baina ya nchi mbili hizi, kama alivyokuwa anaifahamu. Alipoulizwa Mzee Karume kwa nini haipo serikali ya Tanganyika kama ya Zanzibar, alijibu kwamba hilo lilikuwa shauri lao wenyewe".
 
Nyerere alikuwa fanatic kwa kutaka Umoja wa Afrika kama alivyokuwa Dr Kwame Nkurumah. Karume alivyomueleza waungane kwani akiogopa waarabu wasijekumpindua, inasemekana Nyerere alisimama na kuenda chumba cha nyuma alikokuwa ameketi mama Maria na Nyerere huko akapiga vigelegele. Karume akamuuliza Shk Thabit Kombo kuwa hizo ghasia ni za nini? Hanga akaingilia kati baada ya kuona Shk Thabit anasitasita kujibu na akajibu kuwa Mzanaki akifurahi hivyo ndivyo inavyokuwa.
Nyerere aliekuwa tayari kuuchelewesha Uhuru wa Tanganyika ili kuzingojea Kenya na Uganda zipate Uhuru pamoja ili ziungaane, hakuweza kuficha furaha yake, kwani hakutegemea kuwa his dream would one day turn into truth!
Siku za mwanzo Karume akimsikiliza sana Nyerere, kwani akiona uwezekano wa waarabu kuichukua Zanzibar bado ulikuwepo. Baadae Karume akawa hamsikilizi tena Nyerere, kwani alijua kuwa Zanzibar isingeliweza kupinduliwa na ndio maana hata Azimio la Arusha alithubutu kusema limalizikie Chumbe na lisiingie Zanzibar. Pia, aliweza kumwita CHORI yule marehemu Waziri wa Fedha Amir Jamal wakati alipotaka kuunganisha foreign reserves za Bara na za Visiwani. Bw. Jamal aliwahi kuwa declared kama ni 'persoana non-grata' pale alipotaka kuenda Unguja kuzungumzia juu ya pesa za kigeni na ikabidi arejee airport bila ya kushuka kwenye ndege pale Zanzibar Airport. Pia Karume aliwahi kuwafukuzia Bara Wazanzibari tele.
Suala ni kuwa, hivyo Karume kama angelikuwepo mpaka leo angelikubali hapa ulipotufikisha huu Muungano?

/Geo Kimbi 

 

0 comments:

Post a Comment