Tuesday 9 October 2012

RE: [wanabidii] TEMA MATE TUMCHAPE

Hildegarda,

Asante kwa kusema mengi yanayotokea mitaani kwetu. Suluhisho ya kwanza kwa mambo haya ilikuwa ni malezi katika familia na bado inabaki hapo tukijirudi. Kumomonyoka kote kumeanzia hapo, nikianza kubadilika mimi, wewe, kisha wengine inawezekana.

Suluhisho la pili laweza kuletwa na serikali kama tutapata watu wanaochukua mambo hayo kwa dhati. TV zisingeweza ruhusu mambo yanayomomonyoa maadili kama wenye mamlaka wangekuwa hawashabikii mambo hayo. Wakiaacha kushabikia mambo hayo au kuwa na hisa kwenye vyombo vinavyorusha itasaidia sana kupiga vita.

Jamii kwa upande mwingine inamchango mkubwa sana kujenga au kubomo maadili. Ikipaza sauti kuyakataa mambo haya iwe yanarushwa kwenye TV au yanafanyika maeneo yeyote yale. Umoja ni nguvu hakuna lisilowezekana. Tupaze sauti ya umoja itasikika tu.

-----Original message-----
From: Hildegarda Kiwasila
Sent: 09/10/2012, 16:47
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TEMA MATE TUMCHAPE


 
Tukiambiwa mtoto akipatikana sokoni. Hii inategemea na mazingira mliyokuwa mkiishi. Wengine tukiambiwa Mtoto akipatikana mtoni au ziwani au baharini. Inategemea pia unaishi kando ya aina gani ya water resource. Au aina ya miti mikubwa, milima, vichuguu vigumu kufikiwa na mtu asije jabari ambako baba na mama watakwenda kufungua vyungu ambacho kimoja hakitolia booo!! (hakuna kitu. Kingine kitalia 'ng'aa, ng'aa!! hapo kuna katoto. Hadithi hizi zilitaka kumfanya mtoto wa dadangu amtupe mdogo wake ambaye alikuwa anamkera kwa kulia sana. Akataka kumtumbukiza katika pipa la takataka akasema baba akija akalete mwingine baharini huyu analia sana mimi nimechoka ninamtupa. Budi tuwafundishe watoto kufa ni nini ama sivyo wataua bila ya kutegemea na kujua ubaya wa tendo lao.
 
Na sehemu ya siri ya mtoto ikiitwa 'dudu' au tumbaku na babu au bibi akiomba mjukuu utoe tumbaku anuse. Hapo kama inanuka, anasema 'chafu, chafu!' anapiga chafya anakuambia ukaoge au kunawa. Mafunzo ya hygiene. Inapokuwa inaitwa dudu kuna baadhi ya watoto kuambiwa chafu chafu akaona bora aondoe ngozi iliingia matope. Mwenzie akachukua wembe akamkata. Kelele zikatoa wazazi na jirani nje akakimbizwa hospitali Sinza maana walikuwa jirani. maneno tutumiayo yanaweza kuleta madhara kwa watoto. Twaita 'dudu' wakati ni mwili. Hivi sasa kitoto hicho kimeshakua jitu zima.
 
Zamani mtoto  haangalii maiti. Kwa sasa mtu anapigwa mawe, anauawa wao wakwanza  mstari wa mbele wanamkodolea. Wakina mama wanacheza dansi ya matusi ya nguoni mtaani kipindi cha uswazi nao wapo wanaangalia hiyo tikisa dansi. Maadili hakuna, ukimwambia 'dudu'atasema si dudu au atacheka maana anaona ktk mitandao, mtaani hapo jirani penye nyumba za makazi kuna bar na zipo mtaa wote jioni viti nje na wakilewa wababa wanatoa miili yao wanakwenda haja katika mfereji hapo bila kujali mazingira kuwa kuna nyumba na watoto nje au madirishani wanaweza kumuona. Tunaona hatukemei maana nyumba hizo ni zetu na serikali za mtaa zinakusanya ushuru wanaokula wao wala haziingii ktk maendeleo ya usafi ya mtaa.
 
Tuna mengi ya kujirekebisha kama jamii ili watoto wetu wawe na maadili. Hata katika taasisi za elimu ya juu, tukataze waingiao madarasani chupi juu suruali inaning'inia chini ya matako na wadada matiti yamebenjuliwa na kupandishwa juu yapo wazi. Wamama wanacheza dansi wamevaa vichumi wana familia, watoto, wazazi na wanacheza matusi ya nguoni ktk TV wanaonekana. Bar  kila baada ya nyumba moja mtaani, walevi wanatukana matusi makubwa, barmaid kaguo kafupi na anapapaswa hapo watoto wanaona, hiyo 'tema mate tumchape' itajenga maadili kweli kwa sasa ambapo wakubwa tunaonyesha mfano mbaya mbele yao? Bado hizo video za matusi majumbani sebure ndio pahala pa video kuongeza kipato. Vyumba vya kulala watoto ndio madangulo ya short-time hadi saa 6 ndio waingie wakalale.
Maadili yamekwisha, nasi wazazi na wananchi ni wakosa. Ukimfuatilia mtu kisheria-utaokotwa maiti mtaroni umeuawa. Tutabadilika lini tukubali maadili ya jamii, ya dini na utii wa sheria? Mungu atusaidie.


________________________________
From: masedon Bagile <bagilem@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, 9 October 2012, 13:22
Subject: Re: [wanabidii] TEMA MATE TUMCHAPE

Mbona unajiuliza 'Tema mate tumchape' tu wakati zipo nyingi zilizotumika katika kuwajengea watoto wa zamani maadili mema. Kuliko sasa hivi mtoto mmoja akikosa mama/ mzazi anakuja juu na mzazi mwenziwe wakati watoto husika wanaendelea kujichezea zao. Kumbuka tulikuwa tuambiwa mtoto anapatikana sokoni.... n.k

Masedon B Bagile
P O Box 1280 Dar es Salaam
Mobile: +255 718 31 41 58
+255 762 95 49 21

--- On Tue, 10/9/12, Emmanueley Mgongo <emmanueley@gmail.com> wrote:


>From: Emmanueley Mgongo <emmanueley@gmail.com>
>Subject: [wanabidii] TEMA MATE TUMCHAPE
>To:
>Date: Tuesday, October 9, 2012, 3:01 AM
>
>
>Hivi ile tabia ya kumwambia mtoto TEMA MATE TUMCHAPE ilianzanje?
>
>
>manake naona kila mtoto aliyeudhiwa akiwa analia ukamwambia TEMA TUMCHAPE ananyamaza.
>
>
>sijapata kujua hii ilianzaje anzaje naomba msaada kwa anayejua 
>-- "No matter how far down the wrong road you've gone, TURN BACK."
>
>"I would like to live as POOR MAN with lots of MONEY"
>
>"By the the time a MAN is wise enough to watch his step, he is too old to go anywhere"
>
>"TODAY IS TOMORROW YOU WORRIED ABOUT YESTERDAY"
>
>
>
>
>MGONGO EMMANUELEY P. 
>P.O.BOX 3746
>DAR  ES SALAAM
>MOBILE:0784-740487
>             0715-388883
>             0755-388883
>             
>http://us.mc1646.mail.yahoo.com/mc/compose?to=emmanueley@iwayafrica.com
>http://us.mc1646.mail.yahoo.com/mc/compose?to=emmanueley@in.com
>http://us.mc1646.mail.yahoo.com/mc/compose?to=emmanueley@ecommtz.com
>http://us.mc1646.mail.yahoo.com/mc/compose?to=chandling@ecommtz.com
>http://us.mc1646.mail.yahoo.com/mc/compose?to=sales@ecommtz.com
>WEB: http://www.ecommtz.com/-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.   -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and
hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment