Monday 22 October 2012

Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA

Naomba nikuulize swali ndugu Peter hivi si kawaida ukivaa nguo ikachafuka na ukafua? utajisikiaje mtu akipita akakupaka uchafu? Bila shaka utakasirika, japo uzito wa hasira unaweza kupunguzwa kama utagundua hakukupaka makusudi na aliyekupaka uchafu atakwambia maneno mazuri ya kukupoza kama vile samahani nk. Lakini pia itategemea kama tangu jana au asubuhi ni mabaya mangapi umekwishafanyiwa na yeye au mtu mwingine (marejeo katika ubongo wako). Kitu kinachoweza kukunyima busara ata ya kusikiliza samahani ya aliyekuchafua na badala yake ukaanza kumzaba makofi.

Maswali yako naweza kuyajibu kwa mfano kama huo, kwamba kitabu kinapochakaa ni kawaida kukitupa, kukichoma au kukisahau store. Acha kuchakaa ukikiacha hovyo mtoto anaweza kukikojolea, kukinyea, kukichana au kukimwagia mchuzi kikaharibika na kutupwa. Kitabu kama kitabu hakiendi kwa Mungu kinachoenda kwa Mungu ni ujumbe uliomo. Tendo lolote linalohusu namna ya kukidispose kitabu halina tatizo tatizo ni association ambayo mtu anaamua kuijenga, mfano kama kuna visa utasikia ndiyo maana umefanya hivi au vile, wewe umeniona mtu wa chini na kunidharau ndo maana umefanya na hili nk.

Pamoja na yote kama tukio la kuchafua nguo aliyelifanya ni mtoto si kawaida kwa mtu mzima mwenye busara zake aanze kurusha makofi kwa mtoto badala yake atasamehe kwa sababu si rahisi kuassociate hasira ya aina yoyote na mtoto. ukifanya hivyo lazima kuna tatizo katika busara zako.  Kuchana au kukojolea kitabu au karatasi zake si tatizo, tatizo ni nani amefanya hivyo na nani amefanyiwa hivyo, yuko katika hali gani na historia yenu ikoje, historia yaweza kuwa ya kweli au dhaniwa

2012/10/22 Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
Wanabidii,

Naomba mnielimishe.

Najaribu kujiuliza kwamba si ni ukweli kuwa hivi vitabu vitakatifu tulivyonavyo majumbani kwetu huwa vinachakaa? Kama vinachakaa sasa ni nani kati yetu anazo nakara zote za vitabu hivi vilivyochakaa nyumbani kwake? Nadhani ni wachache wenye nakara hizo kama wapo. Sasa nakara za vitabu hivi zilizochakaa huwa tunaziweka wapi? Tunazitupa? Tunazichoma moto? Tunazikojolea? Tunazipeleka mbinguni? Ziko wapi hizi??!! Ukichunguza kwa makini utakuta kwamba nakala hizi zilizochakaa hatujui zilipo. Zimetupwa majalalani na kuoza, kuchomwa moto, kukojolewa na kadhalika. Kama huu ndiyo ukweli basi sote tunafahamu (bila kujifahamu) kwamba kilicho cha muhimu katika vitabu vitakatifu ni ujumbe na siyo makaratasi. Tusidanganyike.

Lwega

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, October 22, 2012 12:41 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
Wahuni wameziba masikio
Hawataki kusikia hilo.
Na wanadai wanalishughulikia.
Nitalia kama kijana aliyekojolea kuruani ataadhibiwa peke yake. Sitakuwa namlilia aliyeadhibiwa. Nitakuwa nalililia taifa letu kukosa umakini wa kutafuta vyanzo vya matatizo yetu, badala yake kutibu dalili kama unavyosema.
Panadol inatuliza maumivu haitibu Malaria. Ezekiel-Tufanye nini?

--- On Sun, 10/21/12, ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> wrote:

From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, October 21, 2012, 11:55 PM

ELISA MUHINGO
 
Nadhani na mimi nikubaliane na wewe kwamba atafutwe huyo kijana aliyemshawishi mwenzie kukojolea hicho kitabu kwa udanganyifu wa kugeuka kuwa mjusi. Huyu ndiye mtuhumiwa namba moja katika sakata hili kwa mtizamo wangu. Kuachwa huyu ni sawa na kutibu Malaria kwa kunywa PANADOL ambayo inapunguza joto tu lakini haitibu maradhi yenyewe.
 
Atafutwe yule kijana aeleze alikuwa na kusudi gani. Kama alitumwa atasema tu.
 
K.E.M.S.
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, 21 October 2012, 13:35
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
Erick.
Tumeandika humu kuulizia hili lakini hakuna anayejibu. Si haki kumuacha huru yule kijana aliyemshawishi mwenzake akojolee kitabu hicho. Na Polisi wangelifanyia kazi wangegundua huyo kijana alikuwa katumwa. --- On Sat, 10/20/12, Erick Mathew <mathewerick@yahoo.com> wrote:

From: Erick Mathew <mathewerick@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "eric.rushiho@gmail.com" <eric.rushiho@gmail.com>
Date: Saturday, October 20, 2012, 11:20 AM

Habari wapendwa na watanzania wenzangu.
Pamoja na yote mlio changia kwa kuitakia mema nchi yetu, mimi nataka mnijuze!  hivi yule mtoto aliyekua  na masahafu hiyo na kumpa kijana
mwenzie na kumwambia kojolea uone kama hutageuka nyoka nae amekamatwa? maana yeye ndiye chanzo cha kushawishi mwenzie akojolee!au siku hizi sheria siyo msumeno tena kama tunavyo jua?
From: Amos Malongo <amos_772002@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, October 20, 2012 1:46 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA

Wapendwa wanabidii,

Kwa mara hii ya kwanza naandika humu ndani, huwa nafuatilia sana hoja na majadiliano mbalimbali. Nimeona niungane na Salamu za Maaskofu wa KKKT, lakini pia nikushukuruni William, Monica, Kunyaranyara kwa kumjibu ndugu Salumu. Nami naongezea nukuu kutoka kitabu kitakatifu Biblia hapo chini, labda itasaidia kujipima ustaarabu na kuelimika kwetu katika ku-address issues za msingi.

Luke 18:9-14
New International Version (NIV)

The Parable of the Pharisee and the Tax Collector

To some who were confident of their own righteousness and looked down on everyone else, Jesus told this parable: 10 "Two men went up to the temple to pray, one a Pharisee and the other a tax collector. 11 The Pharisee stood by himself and prayed: 'God, I thank you that I am not like other people—robbers, evildoers, adulterers—or even like this tax collector. 12 I fast twice a week and give a tenth of all I get.'
13 "But the tax collector stood at a distance. He would not even look up to heaven, but beat his breast and said, 'God, have mercy on me, a sinner.'
14 "I tell you that this man, rather than the other, went home justified before God. For all those who exalt themselves will be humbled, and those who humble themselves will be exalted."

Nitaeleza wakati mwingine kwa nini nimeleta mfano huu au kusema hayo niliyoandika hapo juu.

"Do nothing from selfishness or empty conceit, but with humility of mind, regard one another as more important than yourselves;do not merely look out for your personal interests,but also for the interest of others.""So then, while we have opportunity,let us do good to all people,and especially to those who are of the household of the faith."
Philippians 2:3;Galatians 6:10

--- On Sat, 10/20/12, josta mwampamba <jostamwampamba@yahoo.com> wrote:

From: josta mwampamba <jostamwampamba@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, October 20, 2012, 2:24 AM

UCHOMAJI WA MAKANISA HAUWEZI KUVUMILIKA, KWASABABU HAYA MAKANISA YANAJENGWA KWA GHARAMA KUBWA SANA. NA HII SIYO MARA YA KWANZA WANACHOMA.KWELI SISI WAKRISTO TUMECHOKA NA HUU UNYANYASAJI.TUMEKUWA WAPOLE KUPITA KIASI.

From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, October 19, 2012 4:02 PM
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
Salumu,
Mchango chini unaonekana kubeba maana kubwa sana. Je unaweza kufafanua kidogo ili na sisi wenye uelewa mdogo wa mambo tupate picha ya mambo haya kaka. Yanatuumiza sana.
 
K.E.M.S.
From: William Kihigwa <wkihigwa@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, 18 October 2012, 8:17
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
Salum,
 
Mi nikuombe labda utusaidie kutupa au kutoa suluhisho ili maaskofu wetu waweze kujipanga vizuri.
 
William
From: salum mkango <salumkango@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, October 18, 2012 5:17 PM
Subject: RE: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
 
Baada ya kusoma hili tamko kwa makini nimegundua watanzania bado hatuna amani mioyoni mwetu. Na busara za viongozi wetu wa dini bado kabisa. Si wakiislamu wala Wakikristo. Misamaha ya kweli mioyoni mwetu haipo. Tunasamehe mdomoni lkn mioyoni mwetu tunavisasi vilivyojificha. Hatuangalii tulipojikwalia bali tunaangalia tulipoangukia. Hatutatui chanzo cha tatizo bali ni matokeo yake. Tunachanganya vyanzo vingi kwa matokeo ya chanzo kimoja cha tatizo. Mafundisho yetu ya dini yamejaa kasoro nyingi ikiwemo visasi na chuki badala ya busara na amani. Kwa mwenendo huu BADO SANA KUFIKA KWENYE SULUHU. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
SM.
--- On Thu, 10/18/12, Monica Malle <moninaike@hotmail.com> wrote:

From: Monica Malle <moninaike@hotmail.com>
Subject: RE: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
To: "Wanabidii googlegroup" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, October 18, 2012, 6:49 AM

Wewe ulitaka wawapongeze wachomaji haoooooo?
 
Date: Thu, 18 Oct 2012 16:34:36 +0300 Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA From: oldmoshi@gmail.com To: wanabidii@googlegroups.com Maaskofu nao wanajiingiza kwenye siasa kutetea maslahi ya kanisa wakati uhalifu hauna dini wala rangi na uhalifu ni uhalifu tu na watuhumiwa wenyewe wako mahakamani kwahiyo wanataka kulazimisha nini ?
2012/10/18 Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM.

Wapendwa Katika Bwana,
Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla.

Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina.

Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu:
  1. Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33).
  2. Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini.
  3. Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya. Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini.
Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:
  1. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe.
  2. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini.
  3. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake.
Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga.

Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo:
  • Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa "mfumo Kristo", na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili.
  • Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa.
  • Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania
  • Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi.
  • Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama:

  1. Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi?
  2. Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini.
  3. Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini
  4. Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria.
  5. Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma,
  6. Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini
Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni "wana harakati", tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii.

Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema "sasa basi" pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo.

Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu?

Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.

Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine.

Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).

Daima tukumbuke kuwa, "KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO" (Waefeso 6: 12).

Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu,
  1. Askofu Dr. Alex G. Malasusa – Mkuu, KKKT na D/Mashariki na Pwani
  2. Askofu Dr. Stephen Munga –Mkuu, D/Kaskazini Mashariki
  3. Askofu Dr. Martin Shao – Mkuu, D/Kaskazini
  4. Askofu Dr. Thomas Laizer – Mkuu- D/Kaskazini Kati
  5. Askofu Dr. Benson Bagonza- Mkuu, D/Karagwe
  6. Askofu Isaya J. Mengele – Mkuu, D/Kusini
  7. Askofu Levis Sanga – Mkuu- D/Kusini Kati
  8. Askofu Elisa Buberwa – Mkuu –D/Kaskazini Magharibi
  9. Askofu Andrew Gulle – Mkuu, D/Mashariki ya Ziwa Victoria
  10. Askofu Michael Adam –Mkuu, D/Mkoani Mara
  11. Askofu Renard Mtenji – Mkuu, D/Ulanga-Kilombero
  12. Askofu Dr. Israel-Peter Mwakyolile – Mkuu, D/Konde
  13. Askofu Job Mbwilo – Mkuu, D/Kusini Magharibi
  14. Askofu Dr. Owdenburg Mdegella- Mkuu, D/Iringa
  15. Askofu Jacob Ole Mameo- Mkuu, D/Morogoro
  16. Askofu Zebedayo Daudi – Mkuu, D/Mbulu
  17. Askofu Paulo Akyoo – Mkuu, D/Meru
  18. Askofu Charles Mjema – Mkuu, D/Pare
  19. Askofu Mteule Amon Kinyunyu- Mkuu, D/Dodoma
  20. Askofu Mteule Dr. Alex Mkumbo- Mkuu, D/Kati
Bart

--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment