Wednesday 10 October 2012

Re: [wanabidii] Ripoti ya Baraza la Habari ya Kifo cha Mwangosi

Matinyi
Nafikiri watu wameshindwa kujadili kwa sababu Ripoti ya Nchimbi
inashangaza na kuonyesha udanganya toto mwingi. Ripoti ya Baraza la
habari imekuwa kamilifu haichi shaka lolote kulitia jeshi la polisi
hatiani. Wameeleza methodology waliyotumia na kila kitu kipo wazi data
zao ni valid and reliable huwezi kufananisha na ya hao waheshimiwa.

Ndugu zangu wakati mwingine tusikubali kudhalilisha professions zetu
kwa sababu ya vijisenti au kuiogopa serikali. Inawezekana waheshimiwa
si wataalamu katika kufanya tafiti ukifananisha na wanahabari ila
ripoti yao imeandikwa kinamna kwa kuonyesha kwamba walikuwa
wanaongozwa na adidu za rejea zaidi bila kucrosscheck ukweli.

Kama waziri aliwapa adidu za rejea zenye upungufu basi upungufu huo
huko wazi kwenye ripoti hiyo. Janja ya kusingizia kwamba kesi iko
mahakamani tumekwishaigundua. kama kulikuwa na kesi mahakamani na
mahakama ndo sehemu ya kutujulisha nani ana makosa mheshimiwa Nchimbi
aliunda tume ya nini? Kama si kupotezeana muda na fedha za walalahoi?
Je kama walijua kuna hilo ya nini kukurupuka na kumfungulia Simon
Kesi?

Kwa janja hizi kweli tutafika?

2012/10/10 Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>:
> Jamani,
>
> Sijaona hii ripoti ya pili kutoka Baraza la Habari la Tanzania ikijadiliwa
> au kuwekwa humu.
>
> Naomba basi kwa heshima na taadhima niiweke humu ingawa mwenyewe sijapata
> muda wa kuisoma. Pamoja nayo, naomba niiweke na ile ya Kamati ambayo kidogo
> jana inipe homa nilipoidonyoadonyoa kidogo dakika chache baada ya kuwekwa
> humu.
>
> Matinyi.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment