Sunday 21 October 2012

Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

Amour,
Unataka kujifanya hujaelewa point ya Matinyi, siyo kweli, ni kwa vile unataka kuleta ubishi tu, nitaomba msamaha nikitereza kwa machache hapo chini, Amour ukubali usikubali sehemu kubwa ya watu wenye msimamo unaopelekea vurugu zinaziotokea wengi wao wana lack elimu dunia, wamejazwa elimu ya kiimani + uongo ndani ya taarifa hizo, uongo hautoki kwenye mifaafu ya hizo imani bali wale wanaohubiri wanatia chumvi kwenye mafundisho yao.
Mifano uliyopewa ya nchi zenye 99%ya waumini wa dini ya kiislam lakini vurugu bado haziishi, umeulizwa tatizo la waislam wa nchi hizo ni nini, wanaonewa na mfumo gani? Umeambiwa I ndia yenye idadi kubwa ya waumini wa kiislam lakini husikii muislam analalamika eti kaonewa kwa ajili ya dini yake, na nchi hiyo ina imani nyingi kuliko tulizo nazo hapa Tanzania na bado hawana mifarakano, kutaka kukana mfano eti hauna uhusiano na haya ya Tanzania ni kukuta kubisha tu bila kuwa na swala la kimsingi.
Unapodanganya una elimu ya madrasa  uongo huo utamsaidia nani, itakuwa ni kwa faida yako wewe mwenyewe unayefahamu kiwango chako cha elimu, Matinyi ameuliza swali kwa nia nzuri tu.


From: amour chamani <abachamani@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, 21 October 2012, 18:33
Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

Matinyi,
Aya ya kwanza sijakuelewa.Nadhani kuna tyiping error.
Elimu yangu niya Madrasa.Kusaidia kashindwa poti kwa miaka yake 24 nitaweza mie.
Mfano wako wa India unahusiana vipi na tunachosema? Kwahiyo tatizo la Waislam wa Tanzania ni nini? maana sasa wewe unakuja na doctrine mpya kabisa au ndiyo tunatoana kwenye mada ndugu yangu.


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, October 21, 2012 8:11 PM
Subject: RE: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

Chamani,
 
Hata kwenye nchi zenye Waislamu 99% au zaidi malalamiko huwa ni haya haya - tunataka serikali ya kiislamu. Na ikiwepo ya kiislamu yanazuka malalamiko mengine kwamba haina uislamu wa kweli. Kuna mahali nimeona watu wakidai kwamba hata marais watano wa Tanzania wote ni waislamu na kisha wakataja vyeo vingine kibao - je, ulitaka na wewe upewe? 
 
Dawa ya yote haya ni elimu - watu wakiwa na elimu hawatakimbilia kazi za serikali ambazo mishahara yake ni midogo mno ukilinganisha na kwenye kampuni binafsi. Chamani unafahamu kuwa mtu mwenye shahada moja ya uhandisi akiajiriwa kwenye sekta binafsi anamzunguka mhandisi wa serikali karibu mara tano? Hivi wewe mwenyewe Chamani hebu tueleze, una utaalamu na elimu kiasi gani na unafanya nini na umehawahi kuwasaidia wangapi na wao wapate elimu dunia?
 
Unajua kwamba India ni taifa la pili duniani kwa kuwa na Waislamu wengi baada ya Indonesia? Unajua kwa nini wao hawana matatizo na hawalalamiki? Hebu tafuta uone. Huko Indonesia mwaka 2000 Waislamu waliwaua Wachina maelfu kwa madai kama yako kwenye upande wa uchumi (siyo siasa kama Tanzania) lakini ukweli ukabaki pale pale, kwamba wenzao wanachapa kazi na wao wanalalamika tu isipokuwa familia ya rais na washikaji zake ndio waliokuwa na ukwasi wa kutisha. Ipo mifano mingi ila wasiwasi ni kwamba Chamani husomi habari za dunia wala vitabu vya utafiti, kazi kulalama tu na kujenga chuki.
 
Matinyi.
 

Date: Sun, 21 Oct 2012 09:28:44 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
To: wanabidii@googlegroups.com

Peter,
Tunataka serikali isiyoegemea upande wowote wa dini kwani hii nchi si ya dini yoyote.


Walewale.


From: Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, October 21, 2012 6:35 PM
Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam


Mfumo wowote una malengo, viongozi na sifa zake. Waacheni watwambie malengo, viongozi na sifa za mfumo kristo ni zipi? Msiwalishe maneno. Badala yake watwambie wanataka mfumo gani?
Lwega.


------------------------------
On Sun, Oct 21, 2012 7:41 AM PDT Willy Makundi wrote:

>Jee tunaweza kusema serikali ni ya mfumo Nabii Issa unayoongozwa na Dr Jakaya Mrisho Kikwete, Dr Mohamed Bilal, Dr Ali Mohamed Shein, Chief Justice Mohamed Chande Othman, Mkurugenzi Usalama wa Taifa Rashid Othman, IGP Said Mwema, Minister of Defense Shamsi Vuai Nahodha, Chief of Staff Abrahamani Shimbo, ambao kwa wanaojua mamlaka za serikali, hawa ndicho kiini, ndio moyo, ndio uti wa mgongo wa serikali. Hawa Waislamu wote hawana maslahi ya Waislamu moyoni ila kulelea mfumo Nabii Issa?
>
>Binafsi sipendi kuona majina ya miungu na manabii wetu yanatumika kurahisisha maelezo magumu ya mapungufu yetu ya kijamii. Kuna ugumu gani kueleza mapungufu ya mfumo wetu wa utawala bila kuyaficha kwa nabii Issa? Mifumo ya utawala ya magharibi haiwezi kurahisishwa kiasi cha kuipa jina la nabii Issa. Fikiria Israel, India, Japan, Russia nk uone urahisishaji huu unavyopotosha na kutoheshimu miungu na manabii wetu.
>
>
>mchilyi7.0
>
>
>
>
>-----Original Message-----
>From: mngonge <mngonge@gmail.com>
>To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
>Sent: Sun, Oct 21, 2012 5:05 pm
>Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>
>
>Naungana na mchambuzi wa maadui wa uislamu, kwa mtiririko kwamba adui
>namba moja inawezekana kabisa ikawa ni elimu. Mimi naongeza kwa kuiita
>elimu bora na sahihi. Wapo wachangiaji wengi wetu ambao nawajua kwamba
>wamesoma na wana shahada moja au zaidi lakini bado ndo kwanza kabisa
>wanaeneza dhana ya mfumo kristo na hivyo kuwapotosha wale wasiokuwa na
>elimu.
>
>Kweli kabisa wakisoma na kuelimika vizuri hawataendlea kupotoshwa
>maana watakuwa na uwezo wa kuchambua mbichi na mbivu. Kwa upande wa
>wakristu haswa kwa madhebu ya katoliki na KKT si rahisi wahumini
>kufuata na kutekeleza atakayowaambia padri bila kwanza kulipima na
>kuona kama lina mashiko au la. Anaweza kusema na wasimjibu kanisani
>lakini wakishatoka kanisani watayaacha hapo hapo bila kumuunga mkono.
>
>Pamoja na ushauri mzuri kwa waislamu juu ya kuongeza na kuboresha
>shule na vyuo. Nataka niseme kwamba pia wanaokosa elimu bora si
>waislamu tu ni watanzania kwa ujumla wao. Shule nzuri ata kama ni ya
>wakristu au waislamu mlalahoi hawezi kupeleka mtoto wake uko. Ukienda
>Uingereza utawakuta watoto wengi wa kiislamu hasa toka Pemba wakisoma
>huko katika shule nzuri.  Kama shule na vyuo vya serikali vingekuwa
>vinatoa elimu bora mbona watu wengi wangekuwa wameelimika vilivyo,
>kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa elimu tunayoitoa kwa vijana
>wetu. Iwe ni elimu ya kuwasaidia kuchambua jambo kwa akili zao wenyewe
>na kuweza kupambana na mazingira yanayowazunguka
>
>Mwisho ninaomba wale wanaosema seriakli ni ya mfumo kristo
>watufafanulie zaidi pengine kuna ukweli. Wakitaja tu kwamba serikali
>ni ya mfumo kristo bila kufafanua si rahisi kuelewa wanchokilalamikia
>
>2012/10/21 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>:
>> Katika Tanzania hakuna adui wa muislamu wala adui wa dini yoyote ,
>> Sisi wote ni wamoja , tuendeleze umoja wetu .
>>
>> On Oct 21, 4:31 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
>> Ndugu zangu.
>>
>> Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani
>> wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande
>> wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya
>> ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita
>> unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda
>> kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati
>> wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye
>> mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>>
>> Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu
>> wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii
>> dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo
>> kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu,
>> wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia
>> watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo
>> ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na ndugu
>> zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu
>> lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na makamu wake, si uoni
>> mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi sheini na sharif
>> hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman yule jaji mkuu
>> na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si uoni hata
>> nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.
>>
>> Wanao ongela mfumo kristo hawana udhibitisho wa kutosha kuhalalisha
>> madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na
>> ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinacho piga macho pazia mchana
>> wa jua kali.
>>
>> Kwa waislamu na wasio kuwa waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa
>> waislamu sio wakristo, wapagani, wahindu,au dini nyingine
>> zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.
>>
>> Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na
>> kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia
>> za amani kupata suluhu.
>> Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.
>>
>> 1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi
>> vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande
>> wa pili wanaokuja kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana
>> lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa
>> mashahidi hata shule tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani
>> ya kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa
>> masheikh walio iva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza
>> harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri
>> walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanao
>> endana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya
>> ushindani na pia viongozi bora wa dini.
>>
>> 2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya ccm kupata uhalali wa kutawala kwa
>> kura za waislamu. Lazima tujue kuwa ccm wametutumia vya kutosha na
>> kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano:~ Wametudanganya
>> swala la mahakama ya kadhi wakati wa kampeni 2010 waislamu waliotaka
>> tuwe na kadhi kwa kauli hadaa ya ccm wakapiga kura za kuhadaiwa lakini
>> baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa
>> kudanganywa, tuunge mkono chama ambacho hakita tugawa lakini pia
>> ambacho hakita tugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.
>>
>> 3.Bakwata imekuwa ni kama taasisi ya ccm, wanamuweka wanaye taka wao.
>> Lazima tupiganie bakwata kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke
>> viongozi wenye maono mapana tunao taka sisi sio ccm hii itasaidia
>> kurejesha imani kwa bakwata. Napendekeza Qualification ya kuongoza
>> Bakwata iwe ni pdh kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia
>> lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu
>> cha mum kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji
>> wengine wa bakwata ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe
>> shahada moja na kuendelea.
>>
>> 4.Kutokufuata mafundisho ya mtume. Mtume wetu Muhammad S. A. W alikuwa
>> mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na
>> kukumbushana mema na kukatazana mabaya, uislamu haujajengwa kwenye
>> misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya.
>> Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha
>> Mungu, ukarimu, na kuhurumia na kuwajali wengine. Tukiyafanya haya
>> tutawaepuka wale wanao utumia uislamu wetu kama daraja ambalo baadae
>> hutuchafua wote. Mfano wale walio ingia kuchoma na kuvunja kanisa na
>> kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya kanisa na mikate.
>>
>> "Uislamu ni unadhifu" hii ni moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu
>> kipenzi Muhammad S. W. A. Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili
>> tumuenzi kipenzi chetu.
>>
>> Wakatabahu.
>>
>> On Oct 21, 1:46 pm, Magiri paul <kiga...@gmail.com> wrote:
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>> > Ndugu zangu.
>>
>> > Tunapokuwa tunajiuliza mhemuko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha
>> > na kuuasisi, si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu Waislamu.
>> > Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya
>> > kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au
>> > mfumo kristo kama wengine wanavyopenda kuita (Mimi sio muumini wa
>> > dhana ya *mfumo
>> > Kristo*) maana nimeona wakati wote Waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa
>> > Serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>>
>> > Siuoni *mfumo Kristo* kama unavyoitwa au kama baadhi ya Waislamu wenzangu
>> > wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa Kiislamu juu ya hii dhana.
>>
>> >http://wotepamoja.com/archives/9392#.UIPSVsPwbyY.gmail
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
>ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
>--
>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
>
>--
>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.





--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment