Monday 22 October 2012

Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

Matinyi,
Mimi nilisema nakaa mbali na mambo ya Imani sana, maana utaumwa kichwa ukibishana na mtu anatoa hoja kwa Imani. Lakini kwa mjadala huu nimeguswa, ngoja nitoe mawazo yangu.

Yaani tuna tatizo kubwa hata kama hatutaki kukubali. Sisi watanzania wengi wetu kwa ujumla na ndani ya mioyo yetu na kwa kificho ni wadini, wabaguzi, wakabila, tunaogopa kusema hadharani.

Ndo maana sayansi na Imani haviendani.  Kwa sababu ya udini, mtu anajificha kwenye imani, sio kwamba hajui analoliteda. Wengi wao wanajua, ni wasomi wazuri tu.

Wakati mwingine unasema basi bwana acha waseme tu mambo ya imani lakini tunalishana sumu, tunawalisha sumu watoto wetu. Wakatoliki kabla ya kuwa padre unasoma kwa miaka miwili falsafa, na  kwa ujumla  falsafa inaamini kuwa hakuna Mungu! Utawashangaa kwanjni mtu anaandaliwa kuwa padre anafundishwa kutokuwepo mungu? Wana sababu na ndiyo hizo na baadhi ya sababu ziko wazi. Hii elimu inwasaidia sana kuueleza vizuri uwepomwa Mungu hata mtu akisema Yesu alikuwa na mke au alikuwa Shoga hawamkati mtu Shingo au kumchoma  moto au kumchinja Kama Kuku. Na kuna hadi sinema za kashfa juu ya Yesu. Wendawazimu ni wengi, ukiamka kila siku unataka kumchinja anayemmkashifu Yesu wewe ndo utaonekana mwehu na mwendawazimu!

Nimesoma waraka  wa waislamu japo uko anonymous unasambazwa sehemu mbalimbali. Wao wanatoa hoja a za ajabu sana, wanatukana, wanazusha mambo, hisia wanazifanya zinakuwa ukweli.  Wanasambaza chuki na ukiusoma kwa makini, unakuta hauna tofauti na zile kanda za matusi na  mihadhara ya kutukana raia wema na wananchi wenzao bila sababu.
Nikitumia msemo wa Chamani, ni wale wale, hoja za kuita wenzao kafiri.


Heri Ndugu yangu Chamani  anatoa mawazo yake humu, bila kificho, ni mjasiri. Napenda kusoma michango yake, ni muwakilishi wa mawazo ya wengi, tujue hilo, na msimkasirikie, yeye anawazidi wanaotoa anuani za makazi ya wanaharakati kwa waraka na kwa kujificha. Hawa wanaleta ghasia, watasababisha vurumai za kidini Kama Nigeria.

Hizo shule ambao umezitaja waislamu marafiki zetu wanasomesha na kusoma ha watoto wao huko kwenye st.thereza, st.Mary's, shule za st.Francis.

Nina rafiki yangu muislamu na Alhaj kwa sasa ni Afisa wa idara nyeti  ya  serikali aliomba udhamini wa jimbo katoliki la Rulenge akiwa mtumishi wa serikali akasome st.Augustine maaskofu wakampa.

Kuna shida ya ajira Hapa nchini, na vijana wanasubiri mtu awawekee kiberiti na kusema hauna kazi kwa sababu mkristo ndo anasababisha, hiyo inatosha kulipua nchi.

Hii  habari ya ubaguzi ni agenda ya kutaka kutugawa, tusiibubali hata akija nayo Shehe, padri au mchungaji. Ubaguzi ni mbaya sana. Ukiona unaonewa fanya  bidii ongeza nguvu uondoe huo ubaguzi na hiyo ni elimu tu. Lakini cha msingi, njoo na hoja sio kutugawa na kutukana.

Usiku Mwema,
From LR

On 22 Okt 2012, at 5:50, "Mobhare Matinyi" <matinyi@hotmail.com> wrote:


 

Chamani,

Kwanza niseme hivi: Jitahidi sana kuwapenda watu wote wa Tanzania bila kuhisi haya unayoyahisi. Hayana ukweli.


Aya yangu ya kwanza ilitaja vitu kwa usahihi labda sikufafanua. Sijui lipi limekutia shaka kama ni hili la kusema kwamba marais watano wote ni Waislamu – maana yake ni kwamba Kikwete, Bilal, Shein, Maalim Seif na Balozi Idd wote ni Waislamu. Nikasema pia kuna wengine wamewataja wengine kwenye nafasi zingine. Unazijua. Hoja ni kwamba, kama kungekuwa na ubaguzi hawa wasingekuwepo hapo. Kumbuka hata huo muungano uliletwa na Nyerere huku akijua kwamba anaungana na nchi ambayo watu wake kwa 98% ni waislamu. Nyerere alikaa na makamu wake mwislamu siku zote na muda mrefu akiwa na waziri mkuu mwislamu. Ni kweli kwamba alipenda Sokoine amrithi lakini alipofariki chaguo la Nyerere lilikuwa Salim Ahmed Salim. Akaja Mwinyi hata hivyo na alipomaliza Nyerere tea akamwomba Salim lakini akakataa kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa nchini. Ndiyo Nyerere unayemsema huyo.


Kuhusu swali kwamba wewe kama mwislamu uliyekwenda shule japo hutaki kuiweka wazi, kwamba umeshasaidia wangapi? Naona umekwepa na hivyo kuniachia jibu kwamba hujafanya lolote ila unalalamika tu. Sasa nitakupa dodoso kidogo, kwamba haya madhehebu ya Kikristo yana utaratibu mmoja wa kutoa zaka na sadaka kila wiki. Hebu fikiria zinakusanywa pesa ngapi kwa mwaka. Ndiyo kisa na mkasa ukienda vijijini na mijini unakuta hospitali na mashule na sasa vyuo vikuu vinavyoibuka kama uyoga. Wewe ungeweza kuwashawishi waumini wengine waanzishe mfuko na wawe wanauchangia kila Ijumaa ili baada ya mwaka ijengwe shule, chuo, hospitali, n.k. Hebu jaribu hivyo kwanza. Hii itasaidia sana; wewe hutatoa pesa zako, bali mawazo tu. Ndugu yangu elimu dunia ndiyo inayoendesha dunia hii na elimu ahera ni ya imani tu – haina nafasi katika maendeleo. Ni kweli hata huko Magharibi nako elimu ahera ilichukua sana nafasi hapo kale lakini walistuka. Vyuo vikubwa vya Ulaya kama Bologna, Paris Oxford na Cambridge vilivyoanza miaka 900 iliyopita vilikuwa na msisitizo katika thiolojia lakini kaone leo. Harvard na Yale vya Marekani navyo vilianza hivyo hivyo lakini sogea leo uone walivyoiweka kando elimu ahera. Dunia haiendeshwi na elimu ya dini bali elimu ya maarifa mengine.


Uliuliza kuhusu Ufaransa. Ndiyo, nilipokwenda mara ya pili mwaka 2001 nilikutana na mwajamvi mmoja, Finnigan wa Simbeye na kila jioni tulikuwa tukienda kula kwenye migahawa ya waislamu wenyeji wa Moroko, Algeria na Tunisia. Walikuwa huru na watu wenye furaha na wengine wakisema wazi kwamba wamekukimbia kwao. Nilipokwenda mwaka 1999 nilikutana na watu wa Afrika Magharibi waislamu wakiwa na maisha yao raha mstarehe na wakienda masjid bila bughudha. Ila ni juzi tu ndiyo Wafaransa walikataa katu kata kuruhusu vazi la hijabu kwa maelezo kwamba huo siyo utamaduni wao. Walisema kwamba wanaong'ang'ania hijabu warudi kwao kwa kuwa hakuombwa kuja Ufaransa. Kimsingi walikuwa wakionesha hasira zao kufuatia uadui uliozuka kati ya makundi haya mawili yenye ustaarabu unaotofautiana – watu wa Ulaya na watu wa Uarabuni kwenye uislamu. Kuna mgongano wa kimaslahi ya kimataduni. Lakini kinyume chake, waislamu wanakiri kwamba wako safi huko ugenini barani Ulaya. Nadhani unafahamu kwamba wakristo hawapewi fursa hiyo kwenye nchi za kiislamu. Sizitaji.


Kuhusu Tanzania – ni hatari kubwa kwamba vijana wa kiislamu wa leo wanalishwa uongo kwamba eti waislamu wamekuwa wakionewa na kubaguliwa Tanzania tangu uhuru. Siku moja niliandika makala kwenye gazeti la JAMHURI kuhusu mambo ambayo yako wazi kabisa. Nitakutumia barua pepe ya kijana mmoja ambaye alikiri kwamba maisha yake yote amekuwa akilishwa imani kwamba serikali hii na wakristo ni watu wabaya na kwamba alifuta imani hiyo wakati akiwa UDSM baada ya kupangwa chumba kimoja na mlokole. Alikiri kwamba mengi hakuwa hakiyajua na kwamba makala ile ilimfunua. Nitakutumia kama hukuisoma na ilisema kwamba: Adui wa Waislamu wa Tanzania si serikali wala wakristo bali ni utamaduni wa Ghuba.


Nyerere alifanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba waislamu wanavuna matunda ya uhuru na hadi leo hajatokea kiongozi yeyote aliyemfikia – hata Mzee Mwinyi na JK wetu. Hakuna. Endeleeni kuchochea chuki dhidi ya Marehemu huyu lakini hamuwezi kuufuta ukweli. Ukitaka kuelewa vema kabisa, kwamba sera za elimu za Nyerere ziliwabeba waislamu, basi angalia hali ilivyo leo ambapo kuna mfumo huria wa elimu nchini. Nyerere aliwazuia wakristo kujenga vyuo vikuu mathalani, kimojawapo kikaenda Kenya (University of East Africa), lakini leo nenda kwenye tovuti ya TCU uone vilivyojaa vya wakristo na huku waislamu wakiwa na kimoja tu walichopewa na rais mkristo Mkapa. Sasa njoo kwenye shule za chekechea za Kiingereza, za msingi na nenda kwenye sekondari. Hali ni mbaya kulinganisha na enzi za Nyerere ambaye aliyazuia haya. Serikali ilichofanya ni kufungua tu milango – wote wanaruhusiwa kujenga lakini kwa nini waislamu hawajengi??? Halafu unataka kumlaumu Nyerere?


Hakuna haja ya kumwita Mwenye Heri kwa kuwa hilo ni shauri la wakatoliki, tena siyo wote. Mwanaye alipohojiwa na Daily News siku moja alisema baba yake asingekubali hadhi hii kama angejua. Yeye mwenyewe alisema New Delhi mwaka 1996 kwamba hakustahili Tuzo ya Amani ya Gandhi kwa kuwa alishiriki kwenye mapambano ya bunduki. Hakupenda utukufu huu unaozushwa ambao binafsi yangu naamini hastahili pamoja na kwamba alifanya mema (na makosa alifanya pia lakini halimo hili unalotaka kumsingizia).


Tanzania haina ubaguzi wa dini ila ina watu wanaoukariri huo ubaguzi. Tanzania haina chuki ya dini ila watu wanaoipandikiza. Sisi tuliokulia mitaani kwenye dini zote na kisha tukasoma na waislamu na wakristo na kufanya nao kazi na hadi huku Majuu tunaishi nao, sisi Watanzania, hatuyaamini maneno yako Chamani.


Matinyi.



Date: Sun, 21 Oct 2012 10:33:02 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi,
Aya ya kwanza sijakuelewa.Nadhani kuna tyiping error.
Elimu yangu niya Madrasa.Kusaidia kashindwa poti kwa miaka yake 24 nitaweza mie.
Mfano wako wa India unahusiana vipi na tunachosema? Kwahiyo tatizo la Waislam wa Tanzania ni nini? maana sasa wewe unakuja na doctrine mpya kabisa au ndiyo tunatoana kwenye mada ndugu yangu.


From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, October 21, 2012 8:11 PM
Subject: RE: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam

Chamani,
 
Hata kwenye nchi zenye Waislamu 99% au zaidi malalamiko huwa ni haya haya - tunataka serikali ya kiislamu. Na ikiwepo ya kiislamu yanazuka malalamiko mengine kwamba haina uislamu wa kweli. Kuna mahali nimeona watu wakidai kwamba hata marais watano wa Tanzania wote ni waislamu na kisha wakataja vyeo vingine kibao - je, ulitaka na wewe upewe? 
 
Dawa ya yote haya ni elimu - watu wakiwa na elimu hawatakimbilia kazi za serikali ambazo mishahara yake ni midogo mno ukilinganisha na kwenye kampuni binafsi. Chamani unafahamu kuwa mtu mwenye shahada moja ya uhandisi akiajiriwa kwenye sekta binafsi anamzunguka mhandisi wa serikali karibu mara tano? Hivi wewe mwenyewe Chamani hebu tueleze, una utaalamu na elimu kiasi gani na unafanya nini na umehawahi kuwasaidia wangapi na wao wapate elimu dunia?
 
Unajua kwamba India ni taifa la pili duniani kwa kuwa na Waislamu wengi baada ya Indonesia? Unajua kwa nini wao hawana matatizo na hawalalamiki? Hebu tafuta uone. Huko Indonesia mwaka 2000 Waislamu waliwaua Wachina maelfu kwa madai kama yako kwenye upande wa uchumi (siyo siasa kama Tanzania) lakini ukweli ukabaki pale pale, kwamba wenzao wanachapa kazi na wao wanalalamika tu isipokuwa familia ya rais na washikaji zake ndio waliokuwa na ukwasi wa kutisha. Ipo mifano mingi ila wasiwasi ni kwamba Chamani husomi habari za dunia wala vitabu vya utafiti, kazi kulalama tu na kujenga chuki.
 
Matinyi.
 

Date: Sun, 21 Oct 2012 09:28:44 -0700
From: abachamani@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
To: wanabidii@googlegroups.com

Peter,
Tunataka serikali isiyoegemea upande wowote wa dini kwani hii nchi si ya dini yoyote.


Walewale.


From: Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, October 21, 2012 6:35 PM
Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam


Mfumo wowote una malengo, viongozi na sifa zake. Waacheni watwambie malengo, viongozi na sifa za mfumo kristo ni zipi? Msiwalishe maneno. Badala yake watwambie wanataka mfumo gani?
Lwega.


------------------------------
On Sun, Oct 21, 2012 7:41 AM PDT Willy Makundi wrote:

>Jee tunaweza kusema serikali ni ya mfumo Nabii Issa unayoongozwa na Dr Jakaya Mrisho Kikwete, Dr Mohamed Bilal, Dr Ali Mohamed Shein, Chief Justice Mohamed Chande Othman, Mkurugenzi Usalama wa Taifa Rashid Othman, IGP Said Mwema, Minister of Defense Shamsi Vuai Nahodha, Chief of Staff Abrahamani Shimbo, ambao kwa wanaojua mamlaka za serikali, hawa ndicho kiini, ndio moyo, ndio uti wa mgongo wa serikali. Hawa Waislamu wote hawana maslahi ya Waislamu moyoni ila kulelea mfumo Nabii Issa?
>
>Binafsi sipendi kuona majina ya miungu na manabii wetu yanatumika kurahisisha maelezo magumu ya mapungufu yetu ya kijamii. Kuna ugumu gani kueleza mapungufu ya mfumo wetu wa utawala bila kuyaficha kwa nabii Issa? Mifumo ya utawala ya magharibi haiwezi kurahisishwa kiasi cha kuipa jina la nabii Issa. Fikiria Israel, India, Japan, Russia nk uone urahisishaji huu unavyopotosha na kutoheshimu miungu na manabii wetu.
>
>
>mchilyi7.0
>
>
>
>
>-----Original Message-----
>From: mngonge <mngonge@gmail.com>
>To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
>Sent: Sun, Oct 21, 2012 5:05 pm
>Subject: Re: [wanabidii] Re: Hawa ndiyo maadui wa Waisalam na Uislam
>
>
>Naungana na mchambuzi wa maadui wa uislamu, kwa mtiririko kwamba adui
>namba moja inawezekana kabisa ikawa ni elimu. Mimi naongeza kwa kuiita
>elimu bora na sahihi. Wapo wachangiaji wengi wetu ambao nawajua kwamba
>wamesoma na wana shahada moja au zaidi lakini bado ndo kwanza kabisa
>wanaeneza dhana ya mfumo kristo na hivyo kuwapotosha wale wasiokuwa na
>elimu.
>
>Kweli kabisa wakisoma na kuelimika vizuri hawataendlea kupotoshwa
>maana watakuwa na uwezo wa kuchambua mbichi na mbivu. Kwa upande wa
>wakristu haswa kwa madhebu ya katoliki na KKT si rahisi wahumini
>kufuata na kutekeleza atakayowaambia padri bila kwanza kulipima na
>kuona kama lina mashiko au la. Anaweza kusema na wasimjibu kanisani
>lakini wakishatoka kanisani watayaacha hapo hapo bila kumuunga mkono.
>
>Pamoja na ushauri mzuri kwa waislamu juu ya kuongeza na kuboresha
>shule na vyuo. Nataka niseme kwamba pia wanaokosa elimu bora si
>waislamu tu ni watanzania kwa ujumla wao. Shule nzuri ata kama ni ya
>wakristu au waislamu mlalahoi hawezi kupeleka mtoto wake uko. Ukienda
>Uingereza utawakuta watoto wengi wa kiislamu hasa toka Pemba wakisoma
>huko katika shule nzuri.  Kama shule na vyuo vya serikali vingekuwa
>vinatoa elimu bora mbona watu wengi wangekuwa wameelimika vilivyo,
>kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa elimu tunayoitoa kwa vijana
>wetu. Iwe ni elimu ya kuwasaidia kuchambua jambo kwa akili zao wenyewe
>na kuweza kupambana na mazingira yanayowazunguka
>
>Mwisho ninaomba wale wanaosema seriakli ni ya mfumo kristo
>watufafanulie zaidi pengine kuna ukweli. Wakitaja tu kwamba serikali
>ni ya mfumo kristo bila kufafanua si rahisi kuelewa wanchokilalamikia
>
>2012/10/21 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>:
>> Katika Tanzania hakuna adui wa muislamu wala adui wa dini yoyote ,
>> Sisi wote ni wamoja , tuendeleze umoja wetu .
>>
>> On Oct 21, 4:31 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
>> Ndugu zangu.
>>
>> Tunapo kuwa tunajiuliza mhemko wa udini unatoka wapi au nani
>> wameusababisha na kuuasisi si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande
>> wetu waislamu. Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya
>> ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita
>> unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyo penda
>> kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo kristo) maana nimeona wakati
>> wote waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa serikalini, kwenye
>> mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>>
>> Siuoni mfumo kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya waislamu
>> wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa kiislamu juu ya hii
>> dhana. Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo
>> kristo, si uoni kwa kuwa hii nchi niya wakristo, wapagani, waislamu,
>> wahindu na dini nyingine. Si uoni mfumo kristo kwa kuwa nimeshuhudia
>> watu kama kina omari mahita, na said mwema wakiwa viongozi wa vyombo
>> ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauwaji ya waislamu wenzetu na ndugu
>> zetu wakristo pia. Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu
>> lakini siuoni mfumo kristo nikimuangalia jk na makamu wake, si uoni
>> mfumo kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi sheini na sharif
>> hamad, si uoni mfumo kristo nikimuangalia Chande othman yule jaji mkuu
>> na Othamani Rashidi mkurugenzi wa usalama wa taifa, si uoni hata
>> nikiungalia kwenye wizara na taasisi nyingine za serikali.
>>
>> Wanao ongela mfumo kristo hawana udhibitisho wa kutosha kuhalalisha
>> madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na
>> ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinacho piga macho pazia mchana
>> wa jua kali.
>>
>> Kwa waislamu na wasio kuwa waislamu, Lazima tutambue kuwa adui wa
>> waislamu sio wakristo, wapagani, wahindu,au dini nyingine
>> zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.
>>
>> Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na
>> kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia
>> za amani kupata suluhu.
>> Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.
>>
>> 1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi
>> vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande
>> wa pili wanaokuja kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana
>> lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa
>> mashahidi hata shule tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani
>> ya kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa
>> masheikh walio iva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza
>> harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri
>> walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanao
>> endana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya
>> ushindani na pia viongozi bora wa dini.
>>
>> 2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya ccm kupata uhalali wa kutawala kwa
>> kura za waislamu. Lazima tujue kuwa ccm wametutumia vya kutosha na
>> kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano:~ Wametudanganya
>> swala la mahakama ya kadhi wakati wa kampeni 2010 waislamu waliotaka
>> tuwe na kadhi kwa kauli hadaa ya ccm wakapiga kura za kuhadaiwa lakini
>> baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa
>> kudanganywa, tuunge mkono chama ambacho hakita tugawa lakini pia
>> ambacho hakita tugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.
>>
>> 3.Bakwata imekuwa ni kama taasisi ya ccm, wanamuweka wanaye taka wao.
>> Lazima tupiganie bakwata kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke
>> viongozi wenye maono mapana tunao taka sisi sio ccm hii itasaidia
>> kurejesha imani kwa bakwata. Napendekeza Qualification ya kuongoza
>> Bakwata iwe ni pdh kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia
>> lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu
>> cha mum kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji
>> wengine wa bakwata ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe
>> shahada moja na kuendelea.
>>
>> 4.Kutokufuata mafundisho ya mtume. Mtume wetu Muhammad S. A. W alikuwa
>> mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na
>> kukumbushana mema na kukatazana mabaya, uislamu haujajengwa kwenye
>> misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya.
>> Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha
>> Mungu, ukarimu, na kuhurumia na kuwajali wengine. Tukiyafanya haya
>> tutawaepuka wale wanao utumia uislamu wetu kama daraja ambalo baadae
>> hutuchafua wote. Mfano wale walio ingia kuchoma na kuvunja kanisa na
>> kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya kanisa na mikate.
>>
>> "Uislamu ni unadhifu" hii ni moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu
>> kipenzi Muhammad S. W. A. Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili
>> tumuenzi kipenzi chetu.
>>
>> Wakatabahu.
>>
>> On Oct 21, 1:46 pm, Magiri paul <kiga...@gmail.com> wrote:
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>> > Ndugu zangu.
>>
>> > Tunapokuwa tunajiuliza mhemuko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha
>> > na kuuasisi, si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu Waislamu.
>> > Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya
>> > kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au
>> > mfumo kristo kama wengine wanavyopenda kuita (Mimi sio muumini wa
>> > dhana ya *mfumo
>> > Kristo*) maana nimeona wakati wote Waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa
>> > Serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.
>>
>> > Siuoni *mfumo Kristo* kama unavyoitwa au kama baadhi ya Waislamu wenzangu
>> > wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa Kiislamu juu ya hii dhana.
>>
>> >http://wotepamoja.com/archives/9392#.UIPSVsPwbyY.gmail
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
>ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
>--
>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
>
>--
>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.





--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment